Tabia ya mtu utaijua vizuri pale anapo kuwa hana kitu na pale anapokuwa ana pesa! Je binadamu wote kwake ni sawa? Au? ……..Jamani ipo siku nitawasimulia story yangu na experience yangu ya Watanzania hapa Marekani na pia na ndugu ambao hawaoni thamani ya undugu wako kwao mpaka pale wanapoona kuna kitu “kinang’aa” kwako!…….Ee Mungu endelea kumbariki huyu baba!
Category Archives: Leadership
Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima~~~~~Zitto Kabwe
Nakasirishwa sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa mkoa wa Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo una dhamana zaidi Kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi. Kaa Na Mbunge Godbless Lema mnywe kahawa pale New Arusha Na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi. Nakushauri kaa chini Na Mkuu wa Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya Kwa pamoja.
Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima.
“Ukiambiwa unielezee mimi #Paul_Makonda unadhani utaandika nini?”
Wewe ni binadamu haukosi mapungufu yako kama binadamu yoyote yule. Lakini wewe ni kiongozi shupavu usiye ogopa kusema ukweli, mwenye mtazamo chanya wa maendeleo ya vijana wa taifa la leo na kesho. Ni kiongozi mwenye uzalendo na moyo wa imani kwa watu wote hauna unafiki. Nakutakia maisha marefu yaliyojaa amani na upendo mwingi ili Tanzania ifaidike na kujivunia kuwa na mtu kama wewe ?