Wahenga walisema kulea mimba si kazi kazi kulea mwana! Ukiwa mjamzito kike kiumbe ulichobeba hata kama hutaki kikuwe kitakuwa tu! Sasa ni hiyari yako kula vizuri na kujijali ili uzae kiumbe chenye afya bora na salama. Mama uliyebeba hicho kiumbe ni jukumu lako kutafakari matendo na tabia zako wakati wa ujauzito huo kwani huyo mtoto anauwezekano mkubwa sana wa kuhakisi tabia zako akiwa tumboni mwako! Huo ni mtihani wa kwanza katika malezi ya mtoto! Jana nilisoma post ya Jackie ikanikumbusha mtihani wa pili katika malezi ya mtoto ambapo wazazi wengi huwa wanafeli! Pia ikanikumbusha kuhusu wazazi fulani ambao wapo kwenye reality show fulani inaitwa “Married to Medicine” wote ni madaktari na mama anaumizwa na kitendo cha wao kuwa busy na kazi kiasi kwamba wanakuwa hawana nafasi ya kukaa na watoto zao! Napia ikanikumbusha interview ya Naomi Campbell aliyofanyaga na Oprah Winfrey mwaka 2010 ambapo Naomi alisema kuwa siku zote amejisikia mpweke toka akiwa mdogo kwani wazazi wake wahakuwa nae karibu. Mama yake Naomi yeye aliamini kuwa anafanya kitu kizuri kufanya kazi sana ili kuweza kumpatia mtoto wake vitu vizuri, kusoma shule za private n.k ………. Soma na tazama video hapo chini ?@Regranned from @j_n_mengi – Dear parents, I know you’re busy working hard to feed and raise your kids but please remember that your physical presence is very important to your child. You need to invest more than money to your child, they need to talk to you, they need your hugs and reassurance and most importantly they need you to teach them to be good human beings.”
Pesa na mali ni vizuri kama ukiwawekea watoto wakawa navyo kwani hilo ni jukumu lako kama mzazi! Kumbuka “Pesa na mali ni urithi mtu apataye kutoka kwa babaye” hayo ni maandiko ya Biblia siyo mimi! Lakini kabla ya kuwapa hizo pesa na mali ni vyema ukawafundisha jinsi ya kupata hizo pesa na mali ili nao waweze fundisha watoto zao! Hata hivyo, kabla ya kuwafundisha jinsi ya kutafuta pesa na mali watoto wanatakiwa kufundiswa maadili!
Watoto wanatakiwa kuonyeshwa upendo iliwajifunze kwa matendo, watoto wanatakiwa kufundishwa elimu ya Mbingu kabla hujampa elimu ya duniani! Kwamfano, kabla ya kumfundisha mtoto wako kuhesabu embu hakikisha anajua kusali au kusema sala ya Bwana kwanza! Mfano mwingine, kabla hujamfundisha mtoto wako kusema “naomba” mfundishe kushukuru kwa kila kitu anachopewa, hakikisha anajua kusema “asante” kwanza kabla ya kusema “naomba”!
Kumvalisha mtoto wako nguo za designer maharufu siyo malezi! Surely, itamfanya aonekane vizuri lakini haita msaidia kuwa kiumbe bora! Kumlaza mtoto wako kwenye nyumba ya mamilioni ni vizuri lakini haita mpa confidence au kuacha kuwa muongo na mwizi! Watoto wanahitaji malezi ya wazazi! Pesa na mali siyo malezi!!