Regrann from @dinamarious - Nilipopata mtoto Feb 2014 wakati nahangaika kutafuta mafuta mazuri ya mtoto nikashauriwa ya nazi.
Nikazunguka kila kona nisiyaone ndio nikakata shauri la kutengeneza mwenyewe sababu najua kutengeneza.
Lakini wakati natengeneza ndio likaja wazo la biashara nakumbuka kabisa nikishauriana na Da Husna mmiliki wa @zero2twelve maduka ya nguo za watoto akanishauri fanya.
Nilipoanza nakumbuka alikuwa mteja wangu wa kwanza alinunua carton 24
But ninachokumbuka nilipopata wazo sikulaza damu nikaanza mdogo mdogo kwa ugumu wake nikijaribu kujifunza na Mimi niwe na bidhaa yangu yenye jina langu.
Michakato ya kufungua kampuni Mimi ni mlipa kodi TRA kila mwezi sina malimbikizo ya madeni.
Kuyasajili TFDA yakaguliwe na kupata kibali yanafaa kwa watoto na watu wazima.
Kupata barcode pale GS1 ambapo Mimi ni mwanachama
Na mambo mengi mengi.
Kwa sasa unaenda mwaka wa nne lakini ya milima na mabonde,kurudi nyuma kujifunza na kujipanga upya.
Kubwa nilichokuwa nataka ni kukuza Brand yangu ya mafuta ya nazi Dina Marios Baby Coconut Oil itambulike na iaminike sikuwaza pesa hata kidogo.
Nilipofikia sasa naweza Kufanya Official Launch ya product hii hapa Tanzania. - #regrann
Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Dina Marious a.k.a Mama King Zion kwa ubunifu na kuleta bidhaa bora! Natamani mama yetu Mh. Samia Suluhu ndio awe mgeni rasmi siku hii au baba yangu Dr Magufuli ili ajionee kuwa Wanawake tunaweza na azidi kutuunguka mkono kuwapa wanaume wengine motisha ya kuwanyanyua wanawake kwenda kwenye uchumi wa viwanda.
Jamani mafuta haya ya Dina Marious coconut oil ndio mambo yote kwa ngozi nyororo yenye afya kwa mtoto wako. Ni mazuri sana sio tu kwa watoto hata watu wazima. Mimi niliyatumia sana nilipokuwa Bongo bahati mbaya sikubeba kuja nayo hivyo huku natumia Coconut oil ya Wamexico au Jamaica. Mimi natumia pure coconut oil wakati wote labda wakati wa baridi ndio natumia Nevea lotion kwasababu nataka kitu cha kuongeza joto. Nunua mafuta haya bila wasiwasi utunze ngozi ya mwanzo. Simmeona yamethibitishwa basi usiwe na hofu. Tumuunge mkono Mwanamke wa shoka halafu simnajua 10% inakwenda kwenye ile charity yake ya Dada Dina Marious kusaidia watoto, wamama, na watoto yatima. Tumuunge mkono, tujenge jamii zetu.