Category Archives: Michezo

SIMBA ANAPO LAZIMISHWA KULA MIWA. -Peter Sarungi

Utani wa jadi huwa una raha na karaha zake. Ushindi wa timu yangu Yanga jana haukunishawishi kuandika chochoye juu yao maana naijua timu yangu hasa katika dakika za lala salama kama hizi. Lakini kufungwa kwa watani zangu Simba kumenishawishi kuandika post hii japo kuwasabahi kwa ushindani wao. Moja ya uchawi katika soka ni historia. Hata makampuni ya bahati nasibu (kubeti) huwa wanatumia historia katika kuweka rate, mara nyingi wanaweka rate ndogo kwa timu iliyopata ushindi kwa wingi huku wakiweka rate kubwa kwa timu iliyopata kushindwa mara nyingi pale timu hizo zinapo kutana. Lakini pia wanaangalia historia ya michezo hiyi ugenini na nyumbani.

Historia inaonesha timu ya simba imekuwa ikipata taabu sana wanapo kutana na Kagera Fc hasa wanapo safiri hadi bukoba. Simba imekuwa ikipata matokeo ya ovyo sana kama ya leo ya kufungwa bila huruma. Hawa wakulima wa miwa wamekuwa wakiwalisha Simba miwa bila kupenda huku mabingwa watetezi tukianza kuwasha taa za hatari kwa watani zetu juu ya Ubingwa wa mwaka huu 2017. 

Peter Sarungi (The next time)

Matokeo ya watani zangu yawe dedication kwa marafiki zangu wa zaidi ya miaka 20 iliyopita ambao ni watani zangu akiwemo Godlove Mpandiko, Nelly Peter Namasambillo na Swaleh Madjapa.

Lakini pia matokeo haya yakwende kwa ndugu zangu wa damu waliokuwa kwenye kikao wakiongozwa na mwenyekiti Mzee Busara, Sabasaba Sarungi, Daniel Sarungi, Nyakwar Omwami Bonnie Sarungi, Mourice Leonard Sarungi, Hamisi Sarungi na wengine wanao shabikia Simba.

Niwakumbushe kuwa kilele kinamilikiwa na Yanga. Asanteni sana.