Category Archives: Mother’s Day celebration

Safari ya mama Washington DC

 Siku iliyofuata, tuliamka na kupata breakfast, kisha tukaendelea na mizunguko yetu.     Nilitaka mama aone Washington DC yote kila jengo la office na majumba ya matajiri wa huko. Bahati mbaya au nzuri mama alikataa kutembea alidai amechoka kwasababu ya mizunguko ya jana yake. Hivyo, ikabidi tuchukue tour bus ambayo ilituonyesha sehemu zote tulizopenda kuona. Of course, nimuhimu kusalimiana na wapendwa wako pale unapopata nafasi. Basi hapa tutakutana na cousin yangu (mtoto wa mama yangu mkubwa, mama yake ni wapili kuzaliwa katika familia ya mama yangu) Dr. Joseph Obure yeye anafanya kazi hapo Washington DC. Mama na wanae Mama na kijana wake  wakisogoa story za miaka mingi ? 

Mama na binti yake katika pozi ?


Siku ilyofuata, tulianza kwa kununua green tea na pumpkin bread (my all time favorite breakfast) katika cafe ya Starbucks, tuliungana na aunt yangu aitwaye Sophie au mama AnnaD na baadaye kuanza safari ya kuelekea Makao Makuu duniani ya kanisa la Wasabato.  

Hili eneo ni kubwa sana kama utabahatika kutembelea basi panga angalau masaa azidi ya matatu ili uweze kufaidi na kujifunza kidogo. Mama yangu alifurahia sana. 

  

Basi safari yetu kwa siku hii ikaishia napa, tukaenda kula na kufanya mizunguko kidogo ya dakika za mwisho kwani muda wetu ulikuwa unatupa mkono.    
Nawatakieni maandalizi mema ya Sabato na Sabato njema kwa waumini wote wa dhehebu la Wasabato duniani ?

NITABAKI NA MAMA YANGU

         NITABAKI NA MAMA YANGUKijana mmoja daktari alikwenda kuposa kwa familia moja yenye uwezo wa kifedha na Mali zao .

Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Baada ya kujua kwamba daktari alimchukua mama yake aishi naye kwake baada ya kuona mama yake amekuwa ni mzee Sana.

Yule Binti Akamwambia chagua mawili kunioa mimi au kukaa na mama yako pale kwako ?? ,

kwa sababu ukinioa mimi sitokubali kukaa na mama yako pale kwako maana itakuwa ni kwangu sasa mama yako akae pale ili iweje?? !

Yule kijana daktari alimuelemewa. Hakujua la kufanya Kuhusu maisha yake na yeye yule Binti , Mke mtalajiwa , Uku akitafakari Binti anampenda Sana lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu kwakuwa alikuwa wanatoka wote kijiji kimoja pia Ndio kiongozi wake wa maisha yake.

Daktari alimwambia mwalimu :- 
Mwalimu kama nilivyokueleza awali kwamba nitaenda kuposa kwa yule kwa wazazi wa yule binti niliyekuambia yaani kwa Kweli moyo wangu unampenda mno yule binti siwezi Fikiria Mwanamke mwingine zaidi yake ,

lakini masharti aliyonipa ya yule Binti mke mtalajiwa ni kwamba nimfukuze mama yangu pale nyumbani kwangu ,,

kitendo ambacho kinaniumiza Sana Kichwa, mimi siwezi kuishi mbali na mama yangu maana amekuwa mzee.

Mwalimu sasa Nifanye nini na yule Binti nampenda vibaya mno ?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa yule kijana daktari , alimjibu kwa kumwambia:

Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao wa kukaa naye nyumbani kwako fanya mambo yafuatayo ,

Kwanza kabisa rudi nyumbani kwako , na leo usifanye chochote, ila Ukifika tu kosha mikono ya mama yako.

Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake.

Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya wasiwasi wowote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa, mikono kama mgongo wa kenge sasa ya kufanya kazi za sulubu wakati wa ujana wake.. ,

mama yake akamwambia mwanangu mikono yangu imegutaa kwasababu ya kufanya vibarua Ya kulima viazi na kupalilia mipunga ktk Mashamba Ya watu , Kwaajili Ya kutafuta Ada yako ya shule na uniform , 
Baba yako alifariki ukiwa mdogo Sana... 
Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kufanya kazi ngumu kwa ajili ya mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, mashambani, kulima viazi, kukosha nguo, kufyeka barabarani na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea fedha ya halali bila ya kujali ugumu hiyo Kwaajili Ya kumtunza Mwanae .

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana maendeleo mzuri.

Yule kijana Daktari alilia sana akamwangalia viganja vya mama yake, akasema nakupenda mama yangu, nitakutunza kwa hali yoyote. .

Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia,

Mwalimu siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya huyo Binti msomi asiyejua thamani ya mama yangu.

Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi Mwalimu !

Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya Mwanamke msomi ambaye hajali thamani Ya mama yangu .. wakati mama yangu ameteseka maisha yake yote kwa ajili ya yangu.

Mwacheni aende tu akaolewe na mwanaume yeyote ampendaye mimi nitabaki na mama yangu

**Hadithi hii nimesoma kwa Ayo TV Facebook page**

Mother’s Day 2018: Je, ungependa ku-share nasi hadithi / shukrani ya mama yako mpenzi?

Mother and daughter moment: Mother's Day inakuja ni jumapili ijayo, je umepanga kufanya nini au kumfanyia nini mama yako? Mimi binafsi nitakuwa Washington, DC niki enjoy kidogo na mama yangu! Kwani hii itakuwa Mother's Day ya kwanza kabisa kwa mama yangu kuwa hapa Marekani pamoja nami; hivyo nitaitumia nafasi hii vyema. Sasa basi tuambie kuhusu wewe. Je, ungependa kuShare nasi stori ya mama yako au kutoa shukrani zako kwa mama ukiambatanisha na picha ya mama yako? Basi wasiliana na alphaigogo.com kwa kutuma ujumbe kwa njia ya blog, Instagram DM, au Facebook nasi tutaweka ujumbe wako. 

**Zoezi hili linaanza rasmi leo hii mpaka JumaMosi.**
Asanteni 
Pichani ni mdogo wangu Janeth na binti yake Essy. #TBS 2017

 

Nilipenda hii…..!

Unajua zawadi sio lazima iwe material things au kitu cha bei kubwa eti ndio iwe na thamani! Kitu chochote kinachoweza mfanya mtu ajione kuwa unamthamini na kujali uwepo wake basi kinafaa kuwa zawadi! Basi hii ndio ilikuwa Mother’s Day gift / msg ya mdogo wangu Magreth kwa mama! Was just a simple msg ambayo inaleta kumbukumbu nzuri ya mambo yaliotekea katika hisia tofauti na ya furaha zaidi! Yote haya aliosema ni kweli kabisa!

Mimi (kushoto), Mama, na Magreth. …..Kalamazoo, Michigan 2012

Katika picha hii ni mama na mdogo wangu Magreth walipokuja U.S.A pamoja na baba mzazi mwaka 2012! Ni moja ya tukio la furaha sana kwangu, kwani kutembelewa na wazazi wangu pamoja na mdogo wangu kwa wakati mmoja was something very special, was really big deal to me! ………..Haya Father’s Day inakuja June 17 tafakari nini cha kumwambia au kumfanyia mzee wako!

Motherhood!

Mama na mwana! Pendeza sana mama yetu so beautiful!  Happy belated Mother’s Day to you mama yetu we love you ? Btw, Dinnah na mimi tulisoma wote CBE Marketing major natulikuwa roommates.  Dinnah ni ana akili usipime hata waliosoma naye UD watashuhudia! Plus msafi sana kama mimi vile ??

 

“How amazing are we, we fly even though we don’t have wings…..!” Jacqueline Mengi

“How amazing are we, we fly even though we don’t have wings, we go faster than our legs can carry us, we communicate further than the eye can see, we create organs, animals, plants, we outside our given, in space, we invent the unimaginable the imaginable and we have just started. Yes we are pretty amazing but as for our creator I can’t even find words worthy or even good enough to praise Him and thank Him. Oh how grateful I am to be born human and all the amazing things I know I can do. You should be too” ~~~~~~~JNM

“Kupata mtu wa kuzaa nae inaweza isiwe tabu sana ila…..!” Diamond

“Kupata mtu wa kuzaa nae inaweza isiwe tabu sana ila kupata mwanamke atakaye kubali kuacha starehe zote za dunia na kukulelea watoto ipasavyo siyo kitu rahisi………….kazi yangu imejawa na vishawishi sana, wakati mwingine napatia wakati mwingine nakukosea lakini siku zote umekuwa mwenye kunanielekeza pale nikoseapo na sio kunihukumu……..na ndiomaana siku zote chochote ukitakacho nikiwa nacho lazima nikupe pengine itanisaidia kukueleza ni kiasi gani nakupenda na kukuthamini………Happy Mother’s Day @Zaribosslady”~~~~~~Diamond

Happy Mother’s Day to all mothers around the world!

Mdogo wangu Magreth, mimi mwenyewe, na mama, March 2017, Segerea, Tz….nyumbani kwa mdogo wangu mzee William Igogo

Nawatakieni kheri ya siku ya wakina mama wa mama wote katika dunia hii! Mungu awabariki sana na azidi kutupa khekima ya kuwalea watoto wetu katika njia mpasayo! Wale ambao wanategemea kuwa mama, basi Mungu akawatangulie mjifungue salama. Nao wanao tamani kuitwa mama basi Mungu akawajaze mibaraka hiyo kulingana na mapenzi yake!………..Tunapokuwa tukifurahia Siku hii kuu duniani tusisahau kuwaombea wamama wote ambao watoto wao wamelala usingizi wa mauti! Mungu awaponye na awape sababu ya kuwapa nguvu ya kuendelea na maisha. Na wale wamama ambao watoto zao ni wagonjwa Mungu awaponye upesi. Nawale  ambao kwanamna moja ama nyingine watoto wao wapo kwenye matatizo yoyote yale basi Mungu akafungue njia, awapiganie na shetani asipate nafasi kamwe!

Mimi mwenyewe na mama yangu, December 2016, Dar, Tz…..makazi yetu ya zamani

Nawasii wamama wenzangu tuwalee watoto katika upendo wa dhati na hofu ya Mungu! Watoto ambao hawajalele katika upendo wanakuwa tatizo kubwa si tu kwenye familia zao bali hata kwa jamii husika. Kumfundisha  mtoto kuwa strong katika maisha haimaanishi kuwa unfundishe mtoto wako roho mbaya, ukatili, kuwa bully, muongo, mnafiki, mchonganishi n.k! Hapana! Kama ni mtoto wakike mleee kama ndio the next queen! Nakama ni mtoto wa kiume mfunze kuwa a gentleman! There are too many evil men in this world let us save the world by raising our children in a Godly loving manner! ……..Happy Mother’s Day to all mothers! ❤❤

Mother and daughter moment

What a beautiful picture of Hoyce Temu and her beautiful lovely daughter Rubby! Priceless! Happy Mother’s to Hoyce Temu

Mother and daughter moment

Nimependa sana hii picha ya Nambua Cassandra na mama yake mzazi mama Mlaki. Hii ilikuwa wiki iliyopita kwenye babyshower ya Nambua. Mmh! So touchy, lovely, and priceless moment. Happy Mother’s Day to both of them!

Happy Mother’s Day!

Samahani wapendwa as much as I wish ningewekeza post picha za watu mbalimbali na mama zao, lakini inakuwa ngumu kwani nina commitments zingine! Naomba nichague chache ambazo zitawakilisha wa mama zetu wote. ……Hivyo nawatakieni kheri ya siku ya wakina mama wa mama wote bila kusahau mama Kimati na Mama Double G (George na Georgina) wenye picha hii! ??