Category Archives: Parenthood

Mother and daughter moment: Mama Essy na Essy

Ain’t they cute! Lawyer Janeth Igogo and her beautiful daughter Essy looking beautiful in a custom made African print dress! Wamependeza sana ??

Mother and son moment: Mama Zion na King Zion

Ni picha ya muda kidogo lakini nimependa! Dina Marios na mtoto wake #King Zion handsome boy wa nguvu!…….Nimependa sana muonekano wao na maneno ya kwenye Tshirt! Wamependeza sana!……..Kuna video fulani inaonyesha Dina akimfundisha Zion kukaanga Kuku, nimependa sana! Dunia ya sasa maswala ya kupika siyo kazi ya Mwanamke peke yake! Hapana! Hata wanaume nao wanahitajika kujua kupika ili waweze saidiana na mke ndani ya nyumba 🙂 Dunia imebadilika! …..Mbarikiwe sana mama Zion na King Zion!

Father and son moment: The Teshas’

Manhood! What an amazing picture of JT and his son! Just lovely!……mbarikiwe sana!

Don’t miss, the Mother and Child Gala April 22, 2017!

o.k.

Mother and daughter moment

Katika wazazi ambao nawahurumia pia na mu-admire sana ni mama yake Wema Sepetu! Ni mmoja wa wazazi ambao wanapitia changamoto nyingi sana katika maisha ya kila siku kutokana na maisha ambayo binti yake ameamua kuishi; hivyo kahilo namuhurumia sana! Lakini kama nilivyowai kusema huko nyuma (somahapa) kuwa ni mama ambaye ananifurahisha sana na jinsi anavyo simama bega kwa bega na binti yake, katika mabaya na mazuri! Kwa wazazi wa Kiafrika ni ngumu sana! Wachache mno wanaweza fanya afanyavyo mama Sepetu! Na kwasababu hiyo anakua mfano mzuri sana wa kuigwa! Mtoto wako ni mzigo wako mpaka kifo. Huwezi mkana au mkataa mtoto wako eti kwasababu tu haendani na maisha utakayo! Big up mama Wema!

 

Mother and son moment

Penny na kijana wake wakifurahia weekend. Wamependeza sana! Mwaju na first born wake. Wamependeza sana! The smile tells it all!

TAIFA LA JANA, LEO NA KESHO…. na Peter Sarungi

Imeandikwa….

1. Baba bora ni yule anayelinda na kutetea familia yake, anaye tengeneza urithi mzuri kwa watoto, wajukuu hadi vitukuu na anaye hashimu familia yake.

2. Mke mwema ni yule anaye jenga familia yake bila kuharibu kwa mikono yake, anaye lea watoto katika maadili mema na anaye simama imara na mumewe katika hali ya hatari, dhiki, shida, raha, hofu, furaha, matatizo kama ya siasa, umasikini, chuki, wakati wa ujana na uzee, wakati wa afya na magonjwa.

3. Mtoto bora ni yule anaye heshimu wazazi wake na kujifunza maadili na maarifa kutoka kwa walio mtangulia. Ambaye anapenda kuwa kichwa na si mkia. 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

#MyTake.

Vijana ambao wamefika umri wa kujenga familia wachukue hatua kufanya hivyo, wasisubiri harusi na madoido ya kifahari maana kuna maisha ya ndoa baada ya kupata sifa za harusi.

??Fidel Pilato alikuwa akiangalia post zangu  za nyuma huku akijaribu kuuliza maswali katika lugha nisiyo tambua.???…Hao ndio watu wazima wadogo, Taifa la kesho. NIWATAKIE MWANZO MZURI WA WIKI………MUNGU BARIKI KAZI YA MIKONO/AKILI ZENU.

Mother and daughter moment!

Mimi hapa na mommy angu ? hapa ni siku ya Juma Mosi iliyopita tukiwa nyumbani Keko Juu teyari kwa mtoko wa harusi ya mtoto wa jirani yetu and a good friend to mama…….Jamani sasa hivi tunaishi mbali hivyo tukitaka kwenda kwenye sherehe za maeneo ya Tabata, Mbezi n.k inatubidi tulale kwenye mji wetu wa zamani (Keko Juu) kwani wakati wakurudi kuna kuwa mbali na kabla ya kufika home kuna pori fulani hivi huwa hatupendi kupita usiku sana….Sasa hivi nafikiri itabidi kuangalia sana sherehe za kwenda kwani usalama wetu ni muhimu sana japo so far hatujawahi sikia kitu chochote kile ambacho ni cha kutishia amani au usalama wa eneo hilo!

Malezi ya watoto na changamoto zake!

Pole sana mpendwa, tunamuombea uponyaji wa haraka! …….tukio hili limenikumbusha jinsi my cousin brother alivyo “piga pasi” tumbo lake!  kaka yangu alikuwa na tabia ya kunyoosha sehemu za shati lake ambazo zimejikunja huku akiwa teyari amevaa!! Kumbe mtoto anamuangalia na siku moja akachukua pasi iliyokuwa yamoto Akanyoosha tumbo lake! It was an awful experience! He was  2.5 yrs old by then sasa hivi anakwenda miaka 30 na sidhani kama anakumbuka hilo tukio!…….Anyway, malezi ya watoto yana changamoto nyingi sana. Wewe mzazi unaweza kuwa makini lakini watu unao ishi nao wakawa ni majanga! Nikuomba Mungu tu kama una amini kuwa Mungu yupo!…..Juzi nilisimuliwa kisa cha mtoto wa cousi-sister wangu ambaye house girl alimfungia ndani ya nyumba akiwa amelala halafu yeye akaenda shule kumfata mtoto mkubwa, with a assumption kuwa “atawahi kurudi”! Too bad alipofika shule, siku hiyo walikuwa wamekwenda picnic picnic wakawa wamechelewa kurudi ikabidi dada wa kazi amsubiri! Mtoto aliye achwa nyumbani he is barely 3 yrs old!! Aliamka usingizini haoni mtu ndani ya nyumba! Mtoto kalia mpaka kachoka ma njaa juu! Mama mtu anarudi nyumbani anakutana na hayo majanga! Yani ni alimfukuza house girl siku hiyo hiyo!…..Sasa can you imagine kama moto ungewaka ndani ya nyumba na mtoto kachwa mwenyewe? Au mtoto angechezea jiko la gas ambalo wanalo hapo ndani! Hivi ingekuwaje?! . ……Malezi ya watoto yanahitaji maombi ya ziada kwani bila Mungu hatuwezi!

mother and daughter moment!

Foster na mama yake wakiwa Dubai wakati wa family holidays vacation ya 2016! Wamependeza sana

What a lovely picture of Nambua na mama yake, beautiful and inspiring! ……by the way ushawahi kusikia Cassandra Lingerie?! Wanakwambia “Mwanamke vazi la ndani”! Yani huko ndipo mambo iko kwa wasichana na wanawake wanaojijali na kujithamini fika Cassandra Lingerie ukajionee mwenyewe!

Mama Foster na binti zake waki enjoy vacation yao, so cute!

If you want your children to turn out well………!

screenshot_2016-12-14-14-53-26-1Mama Zion na Zion  wake…..so lovely!fb_img_1481749068942Wifi yangu mama Fidel na Fidel-Pilato Sarungi…….nice one!  screenshot_2016-12-14-14-52-45-1 Mama Miran na Miran wake ndani ya jiji la Italyscreenshot_2016-12-12-13-21-51-1fb_img_1481607023189

Mama na binti yake!

screenshot_2016-12-11-10-38-11-1-1 Mwamvita na binti yake wakifurahiya weekend! Nivizuri sana na ndivyo inavotakiwa kwa wazazi kutenga muda wa kukaa na watoto wao kwani inaimarisha uhusiano mzuri wa watoto na wazazi wao!screenshot_2016-12-11-11-32-22-1screenshot_2016-12-11-11-32-47-1

Congratulations to Zari and Diamond……Please call him Mh. Jakaya Kikwete

screenshot_2016-12-06-08-18-41-1Awiiiii! What a day, what a joy! Congratulations to  both of you Zari and Diamond for your new  bundle of joy!! Mungu awakuzie jamani! Amen ! fb_img_1481033748075 fb_img_1481033739511Queen Latifah kapata kaka ?? mimi naona huyu aitwe Mh. Jakaya Kikwete kwani amekuwa kama baba mlezi kwako. Just honor mzee wetu bwana!……. anyway hongereni sana! Btw, do we still need a DNA test? ?????

Mother and son moment

screenshot_2016-11-25-16-14-50-1 screenshot_2016-11-25-16-15-10-1 screenshot_2016-11-25-16-15-56-1Zion! Zion! Mbona huu mzuri hivyo jamani? Ee Mwenyezi Mungu mlinde huyu mtoto umfunike kwa damu yako. Amen! I can imagine Dina anajisikia furaha ya nmna gani moyoni mwake! Najua hilo kwani hata mie saa nyingine nikimwangalia binti yangu nasikia furaha sana moyoni nasema Asante Mungu kwani umenibariki sana!……..Ubarikiwe sana Dina na famili yako! Japo sikupata jina la aliyempiga picha naombeni mtembelee Instagram page ya DinaMarious mkajiionee picha nzuri sana. Halafu kuna mtu alisifia sana mafuta ya Dina Marious yale ya nazi. Kama unataka kupendeza kwa ngozi yako na ya mtoto wako paka mafuta ya nazi ya Dina Marious. Mimi huwa wakati wa summer sipaki lotion kwasababu ya joto hivyo siku zote natumia mafuta ya pure coconut oil during the summer. Soon nitakuwa mteja wa Dina ?? #UzalendoKwanza #WomanSupportWoman

Mother and daughters moment

screenshot_2016-11-22-13-16-52-1fb_img_1479842379658Raha sana pale watoto au mtoto wako ndio anakuwa rafiki na shabiki wako number moja! Yani ni mbaraka wa pekee kwani kuna wamama wengine mmmh! Wamama wa DotCom yani hata watoto zao wanawakimbia! ??? Yani LB namfananisha na Kris Jenner mama yao Kim Kardashian jinsi alivyo karibu na watoto wake hadi raha!
fb_img_1479842349202
Wamenoga eeh! Wanavutia sana! Hata kama huwafahamu lakini lazima utakuwa unajisikia furaha kuwatizama!…….. Mbarikiwe sana LB na familia yako!

Mother and daughters moment #TheMcClureTwins

screenshot_2016-11-20-18-42-20-1OMg! How do I love the McClure twins! Such adorable funny girls! Just too sweet to watch them ?? by the way I always ❤❤  and a big fan of any identical twins ?? …….. May God continue to protect them!

Mothers and daughters moment

screenshot_2016-10-29-20-59-19-1Siwafahamu nimekutana na picha zao huko Instagram nikazipenda. Wamependeza sana
screenshot_2016-10-29-21-10-55-1Beautiful Emelda Mwamanga owner of Bang Magazine and her gorgeous daughter Gabriel………. Naona hapa walikuwa kwenye mother and children gala…….. Wamependeza sana. fb_img_1477847340782Siwafahamu, nimekutana na picha zao kwa Facebook nikazipenda. Wamependeza sana………. Mbarikiwe wote

Mother and sons moment: the Mengis

fb_img_1477847233465Jackline na wanajeshi wake!…… Can you imagine sikuwahi kufikira kuwa watoto wa Jackline wanaweza tembea peku peku ??Naomba msinifikirie vibaya I mean it well! Yani achilia mbali kuwa ni watoto wa Billionaire Mengi hivyo uwezo wa kununua viatu wanao ila kweli kabisa nilikuwa na muona Jackline ni  “germophobe” fulani hivi. Na hivi uwezo wa kuishi that life (germ free) anao  basi nikadhani watoto wake hata hawawezi kanyaga sakafu bila viatu au socks fulani hivi ?? Masikini kumbe dada wa watu yupo very-very simple! Kha!…………. Anyway wamependeza sana. Pia wazazi wengine muige mfano wa Jackline money doesn’t define who she is! Big up! Nakupenda zaidi ya jana ?? Mbarikiwe

Wewe ni mwanaume / mume / baba wa aina gani?

fb_img_1475669607547fb_img_1475895366588Kama wewe ni baba au unategemea kuwa baba basi haya ni maneno ya kutafakari sana. Je mambo unayo yafanya kwa mwanamke uliye naye akitendewa binti yako utajisikiaje?! Kama haufurahii basi huna budi kubadilika! Na hii si tu kwa wale wenye watoto wa kike, hata kama una watoto wa kiume jiulize! Je, ungependa wafate nyayo zako au! Je, unawafundisha na kuwaandaa kuwa wanaume na baba wa aina gani! Badilika sasa!

Mother and daughter moment

screenshot_2016-10-25-12-13-57-1 fb_img_1472436063790Isn’t that lovely! Too cute to say the least!!…… Sina mpango wala nia ya kuzaa tena mtoto mwingine. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa mtoto wangu mmoja aliyenipa bila kuangaika kama wanawake wengine wanavyo angaika! Nampenda sana mtoto wangu, and always I feel proud to say “she is my only biological child / daughter”!! She’s just PERFECT the way she is (only child)! Nasikiaga na kusoma wanawake wengine wanasema kuwa “he completed me” wakimaanisha WAUME zao. But ma’am! To me is definitely different MY DAUGHTER COMPLETED ME!………Lakini pamoja na kuwa sina mpango wa kuzaa tena haimaanishi siwezi furahiya wanawake wenzangu ambao wapo kwenye ‘parenthood’! Mie sinaga hizo! Furaha ya mtu mwingine naona sawa na furaha yangu! Hivyo sipatagi shida kumsifia mtu au kufurahiya kizuri cha mtu mwingine hata kama anijui!…………. Anyway, napenda sana huu muamko ambao watu wamekuwa nao siku hizi wa kuvaa SARE na watoto zao! Inapendeza sana. screenshot_2016-10-25-12-14-33-1Niliona hiyo picha ya juu kwa Wema Sepetu nika Click link ya Aunt Ezekiel nakukutana na picha zaidi……,…Wamependeza sana. Mungu awabariki siku zote!