Category Archives: politics

American people have spoken……..! Congratulations to President-elect Donald Trump!

screenshot_2016-11-09-07-43-42-1Whether you like him or not, he is the President of United States of America for the next 4 years! Congrats Mr President, Donald John Trump. Wishing you the best in “making America great again”!! ..,…..The American people have spoken let everyone say Amen!

Happy election day America! #I’m with her!

screenshot_2016-11-08-13-25-45-1 fb_img_1478632082658SHE VOTED ALREADY! What about you! Go out and vote! Every vote counts!………..and ?fb_img_1478632096859screenshot_2016-11-08-12-55-40-1….and let everybody say Amen! ??

3 more days! Vote for Hillary Clinton!

fb_img_1478388634428“It was an honor to meet and network with Senator Thomas Carper and our next Awesome, Exceptional New Castle County Executive Matt Meyer . Please go out on Tuesday and Vote . YES WE CAN #VOTEDEMOCRAT #MATTMEYER #VOTEMATTMEYER Meyer For New Castle County”~~~~~Faith MboriĀ fb_img_1478388620107Faith Mbori owner of Authentic Kenyan Dishes with Mayor Matt Meyer
fb_img_1478388614611Faith Mbori and Mr Senator Thomas Carper …..nice pictures!… and please vote for Hillary Clinton ?

“HILI ALILOSEMA MBOWE BUNGENI JUU YA UTAWALA NA WABUNGE WA CCM LINAHITAJI KUTHIBITISHWA UKWELI WAKE.”-Peter Sarungi

Katika kipindi cha maswali na majibu ya hapo kwa hapo kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Chini ya mwamvuli wa UKAWA Mh. Freeman Mbowe alitaka kujua ukweli wa taarifa ya kufanyika kwa kikao cha wabunge wa CCM chini ya mwenyekiti wao Mh. Kassim Majaliwa Ambaye pia ni Waziri Mkuu. Katika kikao hicho kulikuwa na ajenda ikiwemo kujadili Mswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari na upashaji wa habari pamoja kujadili mpango wa bajeti ya mwaka ujao ambazo kwa pamoja zinakwenda kujadiliwa katika bunge la sasa na ikiaezekana kupitishwa. Lakini Mh. Mbowe amekwenda mbali zaidi katika taarifa alizopata na kusema kwamba ” Wabunge wa CCM wamepewa Zawadi ya sh. milioni kumi (10M) kila mmoja na shuguli hiyo ikiratibiwa katika ofisi za CCM Lumumba.

Taarifa hizi zina mshitua mwananchi yoyote ambaye ni mzalendo na makini na nchi yake bila kujali itikadi za kisiasa na mwenye imani na utawala huu wa JPM kwa juhudi zake za kubana matumizi na kutumbua majipu kama njia ya kupambana na Rushwa. kwa taarifa hizi zisipo elezwa ukweli wake basi wananchi watabaki njia panda juu ya imani kwa serikali yao pendwa.

Kama Taarifa hizi ni za kweli basi zitakuwa zina tafsiri yafuatayo:…..

1. Serikali ya awamu hii imezidiwa katika kuibua, kusimamia na kutetea hoja hadi kufikia kutoa zawadi ya 10M ambayo ni rushwa kwa wabunge ili kuweka mazingira mazuri katika ajenda zake bungeni

2. Kuna dalili za serikali ya JPM kutoungwa mkono na wabunge hadi wa chama kinacho tawala. Na inaonesha hata wabunge wa ccm wanasoma namba za kisiasa na za utawala huu.

3. Ile kauli ya kupambana na rushwa ina ubaguzi katika utekelezaji maana haiwezekani ukatumbua majipu kwingine halafu kwako ukatekeleza ufugaji wa majipu.

4. Inawezekana huu Mswada wa sheria ya vyombo vya Habari una matatizo ya mbeleni ama una nia ovu ya kukandamiza uhuru wa habari kama wahariri wengi wanavyo lalamika na ndio maana Waziri Mkuu ameamua kutumia nguvu ya pesa katika kulainisha koo za wabunge na kupata kuungwa mkono

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

#Mytake
Kuna haja ya Waziri Mkuu kujitathimini kama kweli kikao hicho kilifanyika na mlungura ukatolewa kwa wabunge ili kama hana uwezo wa kuongoza baraza la mawaziri katika kutetea hoja na mipango inayotazamiwa kufanywa na serikali. Kama hawezi basi akae pembeni kupisha nguvu mpya yenye kuendana na kasi ya JPM na wenye ushawishi wa hoja bila kutumia Zawadi.
JPM akilifumbia macho taarifa hii na matendo kama haya yanayo fanywa na watendaji na viongozi wasaidizi alio wateua, atakuwa anafifisha juhudi alizo anzisha za kupambana na Rushwa na tutakuwa na tafsiri mbaya juu ya ndoto alizo nazo kwa nchi.

Tunaiomba serikali isikae kimya kwa tuhuma hizi na ikiwezekana itoe maelezo ya kina na kueleweka juu ya kikao hicho kama kilifanyika kwa kubagua wabunge tu na posho nono kama zawadi.

asanteni sana

“Kenya tatizo ni moja tu! Ukabila”- Rais JP Magufuli

fb_img_1478139802483

“VYAMA VYA SIASA VINADUMAZA FIKRA ZA WAFUASI WAO NA WANASIASA WAO?”- Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

Wakati fulani naonaga hakuna haja ya kuangaika kusoma mpaka hata PHD na Uprofesa ikiwa haisaidii kutatua matatizo ya jamii hasa ukizingatia jamii inakuchukulia kama kioo cha kujifunza. Aibu hizi za wasomi kutumia akili za kushikishwa zinazowakumba wengi hasa wasomi wa kiwango cha juu sio Tanzania tu bali ni karibia Afrika nzima, madudu haya yanasababishwa na uwepo wa mifumo kandamizi na mibovu ya uendeshaji wa siasa ndani na nje ya vyama vya siasa. Katika nchi za Afrika, Mwanasiasa ndiye mtu anaye ogopeka zaidi, kuheshimika zaidi, kuthaminiwa zaidi, mwenye nguvu ya kuishi maisha ya Mungu Mtu, siasa ndiyo kazi iliyo karibu sana na fursa mbalimbali za uchumi hivyo katika nchi zetu basi ni wengi wanao tamani kufanya siasa ili tu waishi maisha mazuri.

Kutokana na mfumo wa vyama vingi nchini, ina mlazimu kila mwenye ndoto ya kuwa kiongozi basi apitie kwenye chama cha siasa ili aweze kufanya siasa. Unapo amua kuchagua chama ni lazima uangalie kile chama kitakacho saidia kufikia malengo yako yawe ya karibu ama ya mbali. Kwa Tanzania yetu, unaweza kujiunga na chama tawala, umoja wa Ukawa ama ACT na vyama vingine vingi vinavyofika 25+. Watu wazima wengi na wazee wengi hupendelea kujiunga na chama tawala kwa lengo lakufanya siasa ya malengo ya karibu maana wana amini kwa umri waliofikia hawana ndoto za miaka mingi mbele, Lakini pia hawana nguvu na hari ya kufanya harakati na siaaa za vuguvugu. Vijana wengi wanapendelea kujiunga na vyama vya upinzani kwa sababu ya ndoto walizonazo, nguvu pamoja na utayari wa kufanya siasa za vuguvugu na harakati, lakini pia wanakuwa wapo katika umri wa kutafuta maisha mazuri hivyo wapo tayari kuthubutu na kujaribu mambo mbalimbali katika utafutaji wao. Na kinyume cha hapo basi kijana anayejiunga na chama tawala huwa na fikra kwamba chama tawala kitashikilia dola kwa miaka mingi itakayoweza ku cover miaka aliyo nayo hadi uzeeni…??? , vivyo hivyo kwa mtu mzima ama mzee kujiunga na upinzani huwa na imani kwamba chama tawala hakina miaka mingi katika kushikilia dola ama ana amini kuwa uchaguzi ujao ndio chama chake cha upinzani kitachukua dola…???

Hivyo unapojiunga na vyama hivyo utasajiliwa na kupewa katiba kama muongozo wa taratibu zote za chama husika, ndani ya katiba utakuta kuna itikadi, taratibu za wewe kufanya siasa na kuwa kiongozi, taratibu za kukuadhibu, haki na wajibu wako pamoja na maelezo mengi yanayokueleza kipi cha kufanya na kipi usifanye. Ā Katiba hizi zinakuwa zinatengenezwa kwaajili ya kulinda maslahi mapana ya chama ya muda wote bila kujali maslahi ya Taifa na ya mwanachama husika, na hichi ndicho chanzo za wasomi wetu kuwa watumwa na vikra na matendo, yaani na usomi wao wote wanajikuta maarifa yao yamebanwa kwenye katiba za vyama. Mtaka cha Uvunguni Sharti Akunje goti na kuinama..???. Ukitaka kula tamu ya siasa na uongozi basi sharti uiname kwenye fikra zetu hata kama ni mbovu, ovu, duni, zenye uongo, propaganda, fitna, unafiki, ghiliba, chuki, uhasama, kinyongo, vurugu, umbea, ushirikina, uuaji, mateso, rushwa, udini, ukabila, ukanda na mambo mengi sharti ukubaliane nayo na uwe tayari kuyatetea na kujitoa muhanga maana chama siku zote huwa akikosei. Daaaah, inapofika hapa ndipo akili za kisomi zinawekwa pembeni na kuvikwa sharti la kupiga magoti na kuinama maana anaaminishwa kuwa hizo ndizo mbinu za ushindi katika siasa. Huu mfumo umedumaza akili na fikra za wafuasi na wana siasa wa vyama husika kiasi kwamba wapo tayari kubadili nyekundu kuwa nyeusi kwa njia zozote na kuhalalisha, wapo tayari kudhalilisha utu na elimu yao kwa maslahi yake na ya chama chake, wapo tayari kupinga kila kitu kinachofanywa na mpinzani wake hata kama ni kizuri na jema na wapo tayari kukubali kila kitu kinachosemwa na chama chake hata kama ni baya na ovu. Hizi ndizo akili ninazozipinga maana hazina maslahi ya kweli na mapana ya Taifa, wapo tayari taifa liangamie ili walinde maslahi yao na wapo tayari kuchafua hali ya hewa kwa maslahi yao. Alafu wanajiita majina ya kondoo kama Wazalendo, Wakombozi na Wanaharakati wakati ni mbwa mwitu wasio kuwa na maslahi na Taifa na watu wake.

Kila mtu amepewa akili na utashi wa kuamua jambo na kutumia fikra na maono yake, hivyo kuwa tofauti au kuwa pekee ni jambo linalojitokeza mara nyingi,ila tatizo ni nani mwenye uwezo wa kusimamia na kueleza fikra zake zilizo tofauti na mifumo ya vyama vyetu? ni nani anayeweza kukosoa na kupinga maamuzi na mambo mengine yaliyopo kwenye vyama vyetu? ni nani anayeweza kumkosoa Mkuu wa kaya katika chama tawala na akaendelea kuwa mwanachama? ni nani anayeweza kumkosoa Mtu huru katika chama chake na akawndelea kuwa mwanachama? Ukiweza kufanya tofauti na mifumo ilivyo basi jiandae kutapikwa na mifumo husika, Ndio maana tunaimba CCM ni ile ile na CDM ni ile ile. Prof. Lipumba pamoja na kukimbia vita vya mwaka jana lakini bado ana wafuasi waliopenda stayle yake ya kukimbia, JPM pamoja na kuapa kutoshirikisha mpinzani katika serikali yake lakini ameweza kumchagua Agustino Mrema katika serikali yake.

Kuna watu walio jaribu kuvunja tabia za kutumia akili za mfumo badala ya kutumia zake, walikataa kukubali kila kitu cha chama chake ama kukataa kila kitu cha mpinzani wake, waliamua kupaza sauti zao kuu zilizotoa fikra kinzani na chama chake. Pamoja na mfumo kuwatema na wakaitwa majina ya kudhiaki, majina ya matusi, wakazushiwa kashfa nyingi, wakalaaniwa kwa maneno, wakaombewa na kutabiriwa vifo, lakini waliweza kusimama na kusema kwa kutumia akili zao. Watu hao ni pamoja na Mh. Edward Lowassa, MSaid Arfito Zuberi, Said Arfi, Marehemu Deo Filikunjombe, Mh. Raila Odinga, Mh. Ababu namwamba, Mh. Kiiza Besige, Mh. Donald Trump na wengine walio itwa WASALITI kwa kusema fikra zao zilizo tofauti na mifumo ya vyama vyao. Wengi wetu tunaendelea kuwa wafuasi, wananchama na wakereketwa wa vyama bila hata kushirikisha akili zetu na mwisho wa siku tunakubali kila kitu kinachosemwa na kamati kuu isiyozidi hata watu 50 wanaotuamulia sisi tulio zaidi ya milioni kadhaaa.. (80/20 rule) kisha tunafuata maamuzi hayo kwa nguvu zote hata kama ni mabovu. Na tunapinga kila jambo lilifanywa na mpinzani wako hata kama ni la maendeleo na hapo ndipo unapoweka pembeni maslahi ya Taifa hili.fb_img_1477677488775#Mytake
1. Tuanhitaji vyama vya siasa visizo na kikwazo katika fikra, vyama vyenye kuruhusu fikra mbadala, fikra huru zisikilizwe, vyama vyenye kuwa na ajenda yenye masalhi makubwa kwa taifa, vyama vyenye kutengeneza wafuasi, wanachama na wakereketwa huru wenye kuhoji maamuzi ya kamati kuu.
2. Tunahitaji wanachama wasomi wanao tumia akili na elimu zao katika kufanya siasa, wanaojali maslahi ya taifa.
3. Tunahitaji upekee, maana upekee unaleta utofauti, utofauti unaleta mabadiliko na mabadiliko huleta Maendeleo

Please Vote for Dr. Magufuli

screenshot_2016-10-25-22-22-12-1

Haya twende sasa tuka VOTE! Mimi nimesha vote kama inavyo onekana hapo chini ? Na mpaka sasa Dr. John Pombe Magufuli anaongoza kwa 81% ……….haya basi tufanye kazi ya kupiga kura tulete ushindi nyumbani ?img_20161025_231937

“TIT FOR TAT” YA LEMA YAWEZA SAIDIA UPINZANI KUWA IMARA? – Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

Andiko langu lililopita nilijaribu kuwatahadharisha Upinzani juu ya kupooza kwao katika siasa za sasa. Niliwakumbusha na kuwa sihii wabadili mbinu na mikakati yao juu ya kuendesha siasa zao na hata kuleta maendeleo kwa wananchi walio wachagua.

Leo nimeona video inayomuonesha G.Lema (MB) mbunge wa Arusha akitoa msimamo juu ya kadhia aliyoipata kutoka kwa Mkuu wake wa mkoa RC M.Gambo akisema:

“kuanzia leo ikitokea kiongozi wa upinzani amedhalilishwa na ikiwa protocal na itifaki za serikali haikufuatwa kwao hata ikiwa ni mbele ya Raisi basi watafanya TIT FOR TAT hapo hapo.”

Kwa maana yangu binafsi nilivyo ielewa kauli hii ni kwamba Mbunge wa Arusha anakuja na mkakati mpya wa kujibu mapigo ya papo kwa papo hata kama itakuwa ni mbele ya Raisi as long itifaki na protocal za serikali hazikufuatwa kwa viongozi wa upinzani kama alikuwa anastahili.

Hasara za mkakati huu..
1. Ikiwa itafanyika hivi mbele ya wageni kama ilivyofanyika Arusha basi huu utakuwa ni Uhuni wa kulaani.
2. Mkakati huu bado hauoneshi nidhamu ya viongozi wetu na inaweza kuwachukiza wananchi ambao ni wastaarabu.
3. Yaweza kusababisha serikali kukwepa kushirikisha viongozi wa upinzani katika hafla mbalimbali kwa hofu ya kutokea vurugu na aibu kwa jamii.

Faida za Mkakati huu.
1. Ikiwa itafanywa kwa ustadi mkubwa na matokeo yakawa ni makubwa kwa jamii basi yaweza kuwa ni moja ya mkakati mzuri wa kuondoa kadhia hii ya kutengwa na kubezwa kwa upinzani. Maana serikali zetu mara nyingi hutatua tatizo baada ya kuona matokeo ya tatizo.
2. Ikiwa itafanywa vizuri basi yaweza kuwa ni “KIK” ya kisiasa na inaweza kuteka vyombo vingi vya habari. ukweli ni kwamba chakula cha mwanasiasa yoyote ni kutoka kwa habari zake nzuri na za harakati kuonesha ana tetea wananchi wake kama serikali ya sasa inavyofanya.

#Mytake.
Ni vizuri kubadilika kila mara ili adui yako asikufahamu vizuri lakini tumia mbinu zenye matokeo makubwa kwa wakati mmoja ili kulinda nyakati zingine. Mbinu hii ni ndogo sana ukilinganisha na tatizo la demokrasia na siasa zilizopo sasa, kuna haja ya kuja na mbinu nyingi zaidi mipya itakayo shitua ulevi wa madaraka mnao ulalamikia. Endeleeni kufikirisha vichwa vyenu maana kuchagua kuwa Mpinzani katika nchi yetu sio raha hata kidogo, Ni Mzigo mkubwa wenye kuhitaji mapambano ya ziada ili kufikia malengo.

asanteni.

Kauli / Maneno yana ishi -Peter Sarungi

Hii ni kauli na maneno ya Mh. JPM alipokuwa anajinadi na kuomba kura kwa wananchi wa Tanzania.Ā fb_img_1477415913995“Nasema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu, kwenye serikali yangu hamna mwanafunzi atakaye kosa mkopo eti ashindwe kuendelea na elimu ya chuo kikuu”Ā inaendelea……..Ā “Hii nchi ni Tajiri kweli kweli, kwenye serikali yangu nita hakikisha kila mwanafunzi ananufaika na mkopo. Haiwezekani nchi kama Tanzania wanafunzi waanze kuandamana kisa mkopo, huyo waziri niliye mteua ajiandae kuondoka”

Naomba kauli na maneno haya yaendane na matendo ya sasa kwa wanafunzi wa vyuo.Ā Lakini kwa utaratibu mpya sasa wa Mikopo kwa wanafunzi, naona kuna walakini katika kutimiza Ahadi ya JPM.

Najaribu kutafakari, tusaidiane kutafakari kwa pamoja kabla ya maafa.

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

asanteni sana.

“UPINZANI TANZANIA UMEPOOZA, BADILISHENI MBINU ZA MAPAMBANO. MSIPO BADILIKA MTAZAA UASI WA NCHI.”-Peter Sarungi

fb_img_1477317177774Nchi yoyote inayofuata utawala na siasa za kidemokrasia ni lazima kuwe na upinzani imara kwa manufaa ya utawala bora kwa nchi. Tanzania ni moja ya nchi yenye siasa za kidemokrasia kupitia vyama vingi. Moja ya Upinzani Imara kuwahi kutokea Tanzania ni pale vyama vinne vya siasa vilivyoamua kujiunga pamoja na kuunda muungano uitwao UKAWA. Ni Ukweli kuwa nguvu kubwa ya UKAWA inatokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hii imetokana na mbinu nyingi za siasa zilizotumiwa na CHADEMA kwa kipindi cha miaka 10 ya utawala wa Mh. J. Kikwete ambayo iliweza kuimarisha Upinzani nchini. Tulishuhudia mbinu mbalimbali zilizo teka fikra za watanzania pamoja na vyombo vya habari Mfano Operation Sangara iliyofanyika kanda ya ziwa iliyovuna wafuasi kwa wingi kama Sangara anavyovuliwa baharini, Kulikuwepo na vuguvugu la kutaka mabadiliko M4C iliyorindima kwa wananchi kupitia makundi mbalimbali ya vijana, wanavyuo, wafanyakazi, wanawake na kada mabalimbali na matokeo yake tulishuhudia migomo na maandamano ya kudai haki na kutaka kusikilizwa kutoka kwa makundi hayo kama vile migomo ya waalimu nchi nzima, migomo ya wanavyuo, migomo ya wananchi kama kule Mtwara na migomo ya wafanyakazi nchi nzima. Tulishuhudia Sera na kelele za kupambana na Rushwa ziliyoibua madudu mengi yaliyokuwa yakifanywa na watawala pamoja na watumishi wa Umma kama vile Scandal za Richmond, EPA, Meremeta, Tegeta Escrow, IPL, Kagoda na nyingi zilizo ibuliwa na kuiacha Serikali na Chama tawala ikiwa uchi kisiasa na hapo ndipo neno FISADI na Ufisadi lilipopata umaarufu. pamoja na hayo Upinzania uliweza kubadili fikra ya wananchi juu ya rasilimali zao, kufuatilia mapato na matumizi ya Serikali pamoja na kujua Haki za binadamu na haki za kikatiba kama vile Uhuru wa kujieleza, kutoa maoni yako na kusikilizwa. Kwa jitihada hizi za Upinzani Imara tuliweza kuona Serikali ikitoa maelezo ya kujitetea, ikichukua hatua mbalimbali ikiwa ni njia ya kurespond malalamiko ya wananchi. Yote haya yalifanyika kwa sababu ya Upinzani Imara.

Leo tupo katika utawala wa tano, utawala unaojinasibu kwa maneno ya HAPA KAZI TU, Utawala uliojiapiza kutetea wanachi wanyonge walio wengi na walio teseka kwa mda mrefu, Utawala uliojiapiza kupambana na Mafisadi, Utawala uliojiapiza kurudisha nidhamu ya watumishi wa umma juu ya rasilimali za nchi, Utawala usio hitaji siasa wakati wa kazi, Utawala usio taka kugaramia garama za demokrasia kama kuonesha Bunge Live, Utawala unaochukua maamuzi kwa maslahi ya nchi, Utawala uliojiapiza kupita katika njia za ahadi za Raisi na kuzitimiza kama vile kufufua shirika la ndege ATC, Utawala usio hitaji kupelekeshwa wala kujaribiwa, Utawala ulio amua kwenda kinyume na utawala uliopita wa JK yaani utawala ulio amua kufanya mengi yaliyo lalamikiwa na wapinzani wa JK na kutofanya yale mema yaliyofurahiwa na wapinzani wa JK kama vile kulinda na kuheshimu demokrasia.

Kwa zama hizi za JPM, Upinzani unaonekana kupooza sana nchini. Kupooza kwa Upinzani kunatokana na matokeo hasi ya mikakati yao ya kisiasa wanayofanya dhidi ya mikakati ya kisiasa inayofanywa na serikali ya JPM kwa wapinzani. Mikakati inayofanywa na serikali ya JPM ni ya makusudi na yenye ufundi wa hali ya juu na yenye kufuata udhaifu wa sheria zetu zinazotungwa bungeni. JPM amesoma tabia na desturi za wapinzani, amesoma njia zao na mbinu zao, amesoma uwezo wa watu muhimu katika upinzani (key people) na mwisho akasoma udhaifu uliopo katika kila idara ya uendeshaji wa Upinzani. Matokeo yake ni JPM kuja na mbinu tofauti na zile zilizo zoeleka na Upinzani kipindi cha JK, ndio maana ameweza kudhibiti vyanzo vyote vya kuimarisha Upinzani kama vile Bunge, Siasa za majukwaa, Maandamano, Migomo, vyanzo vya mapato, demokrasia katika chaguzi za sasa na mengine mengi yanayoweza kififisha demokrasia na vyama vya Upinzani.

Kwa Bahati mbaya sana, Upinzani bado haujashitukia mchezo unavyochezwa, bado wana mikakati, njia, tabia, desturi na mbinu zilezile na key people walewale waliodumu kwa miaka 10 ya JK. Bado wapinzani hawajabadilika kwa fikra na mienendo, Mfano: Bado wanaamini katika maandamano na migomo, Bado wanaamini katika matamko yasiyo fanyiwa kazi na bado wanaamini katika kususia vikao hata vile muhimu kisa tu wanatendewa ndivyo sivyo. Kwa muundo huu wa Upinzani usiobadilika na kwa mikakati hii JPM kuna uwezekano Upinzani ukafifia na kudorora ifikapo 2020, kuna haja ya Upinzani kubadilika tena haraka ili kutopoteza imani waliyoijenga kwa muda mrefu kwa wananchi.

Kuna hasara kubwa kama upinzani hautabadilika kutoka sasa. Tabia ya kususa vikao mbalimbali halali vya kuwasemea wananchi walio wachagua hauna tija kwa sasa maana una nyima haki ya wananchi kuwakilishwa na mwisho wa siku yanapatikana maamuzi yasiyojali wananchi walio wengi,
mfano: upinzani ulisusia Bunge la katiba na matokeo yake ikapatikana katiba yenye maslahi ya chama kimoja, Wamesusia Bunge la bajeti na matokeo yake ikapatikana bajeti iliyokuwa na mapungufu mengi ya sera za uchumi, wamesusia uchaguzi wa meya wa kinondoni na matokeo yake amepatikana meya kwa kura 18 za ccm. Hii tabia inakera sana na inawagarimu wananchi walio wapigia kura katika mazingira magumu na wengine walipata ulemavu wa kudumu katika kutimiza na kulinda haki zao. Kwanini msipambane kwa njia zote katika kupata haki zenu? kwanini mkimbilie kususa na kutoka nje? kwa nini mnafanya siasa ya maneno badala ya kufanya siasa ya matendo?
Mmeitisha maandamano ya nchi nzima, mmekuja na UKUTA na mwisho mka airisha kwa sababu ya uimara wa JPM.

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

#Mytake
Upinzani ukiendelea kufanya siasa za maneno na kuacha matendo nyuma, Upinzani ukiendelea kung’ang’ania mbinu na mikakati ya kipindi cha JK bila kubadilika, watajikuta wanapandikiza mbegu za chuki, hasira, vurugu na uhasama dhidi ya Serikali na itafika kipindi watazaa WAASI wa nchi watao sababisha Machafuko ya nchi. Upinzani hauna chaguo mbadala zaidi ya kubadili mbinu na miakakati ya siasa zao maana ni kweli bado tunahitaji uimara wa upinzani nchini katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya wananchi. Siasa zina Ishi na zitaendelwa kuwepo hata aje malaika kutoka mbinguni kuja kutawala bado siasa itazaa wapinzani kwa hoja na kwa kupingana katika fikra na ndio maana hata katika utawala wa mbinguni bado siasa ilijitokeza na malaika mkuu akahasi na akawa mpinzani mkuu wa Mungu. pamoja na hayo bado Mungu alimpa Shetani Uhuru wa kufanya siasa ili apate wafuasi ingawa Mungu alikuwa na sababu na uwezo wote wa kuangamiza upinzani wa Shetani kwa watu wake.

asanteni.

“Hivi, watu wote wanaoenda kusoma kwenye vyuo vikuu hesabu zao zote ni kuja kuajiriwa serikalini?”- Mimi Mwanakijiji

Swali la Jumapili: Nimesoma malalamiko na hata manung’uniko ya watu mbalimbali kuhusiana na kusitishwa kwa ajira serikalini hadi wakati fulani mwakani. Wapo wanaolalamika kuwa kusitisha huku kwa ajira mpya na kupanda vyeo kumesababisha watu waliohitimu vyuo na wengine kukkosa kazi na hivyo “kukaa nyumbani”. Hivi, watu wote wanaoenda kusoma kwenye vyuo vikuu hesabu zao zote ni kuja kuajiriwa serikalini? Inawezekana elimu ambayo vijana wetu wanapatiwa haiwaandai kuwa wabunifu na wavumbuzi (rejea mada yangu ya juzi) kiasi kwamba nje ya serikali au utumishi wa umma hawawezi kufanya lolote na hivyo kweli “wanakaa nyumbani”?fb_img_1477237341357

ARUSHA ACHENI SIASA NA UTAWALA WA KIHUNI~~~Peter Sarungi

Nimeshawahi kuandika kuwa kuna tofauti katika kushabikia club za mpira na vyama vya siasa. Siasa inagusa maisha ya kila siku ya mwanadamu, ukiingiza ushabiki usio kuwa na tija kama wa club za mpira katika siasa ni wazi utakuwa una cheza na maisha ya watu na inawezekana uka angamiza ndoto za wananchi. Kilichotokea katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha afya ya mama na mtoto jijini Arusha ni dhairi kuwa bado tuna safari ndefu sana ya kutoa elimu ya kujitambua sio kwa wananchi pekee bali hadi kwa viongozi tunao wachagua na wale wanao teuliwa na mamlaka za juu. Haya matukio ndio yanayo akisi ukweli wa kauli ya Donald Trump aliposema “Afrika bado inahitaji kutawaliwa kwa mda mrefu zaidi” akimaanisha bado viongozi wetu tunao wachagua ili kutuongoza na kututawala hawajitambui, hawana weledi na utashi mzuri wa siasa na utawala, wana ubinafsi na sifa zilizopitiliza, hawajui kutofautisha siasa na harakati, wengi wana akili na tabia za kitoto katika kufanya maamuzi, wengi wana angukia kwenye utafiti wa Twaweza hasa kundi la Vichaa, wengi wana ongoza na kutawala kwa kutumia propaganda chafu kwa maslai yao na ya vyama vyao. Ukweli ni kwamba tunao pata Hasara ni sisi wananchi tunao kaa pembeni kusubiria utashi wa wana siasa kama hawa.Ā fb_img_1476910893576Huu ni UHUNI wa kulaani bila kupepesa macho, haiwezekani tukakubali kupata aibu tena aibu inayotokana na Ufinyu wa Busara kutoka kwa viongozi wetu tunao waamini watuongoze, Uhuni unaoletwa kwa maslahi binafsi ya watu wawili, Uhuni unaoletwa na Akili ndogo ambazo hazipaswi kupewa dhamana, Uhuni wa kutengeneza kwa makusudi kabisa wa kutaka sifa bila kujali athari za akina mama na watoto, Uhuni wa mwisho kabisa kuvumilika.

Mrisho Gambo (RC) na Godbles Lema (MP) hamtutendei haki hata kidogo na kamwe siwezi kusapoti UHUNI huu, yaani jambo dogo linawafanya mnakosa busara mbele ya wageni tena wafadhili walio kubali kuweka mabilioni ya pesa kwaajili ya kutatua matatizo ya wananchi wenu, sasa umuhimu wa nyinyi kuwa viongozi wakati hamtaki maendeleo ni upi? Mnataka sifa kwa kutumia Propaganda ili iweje? Hopeless kabisa na vizuri mkajichunguza akili zenu kupitia Twaweza.

Matokeo ya Tukio hili……..

1. Tukio linaonesha kutokuwepo kwa uhusiano kati ya Mbunge na Mkuu wa Mkoa, hii inamaanisha maendeleo ya jiji la Arusha yapo njia panda.

2. Mbunge hana busara za uongozi hasa baada ya kuhamaki kwa jazba mbele ya wageni.

3. Mbunge hana nidhamu kwa mkuu wa mkoa na hajali itifaki /protocal na hivyo kuzidisha mgororo kati yao.

4. RC hana busara za utawala hasa baasa ya kudharau na kubeza jitiada za Mbunge katika project husika.

5. RC yupo kwa malengo tofauti na mendeleo ya wananchi anao waongoza na anatumia uongozi wake kufanikisha hayo malengo yake.

6. Wafadhili watamini maneno ya Trump na watakuwa wamefadhaishwa sana na kitendo hicho.

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

#Mytake.
1. Ni kweli tunahitaji viongozi wabunifu, wachapakazi na wanao tafuta maendeleo kama G.Lema lakini ni kweli pia kwamba hatuhitaji viongozi wasio na nidhamu na wasioweza kulinda maendeleo waliyo yatafuta kama G.Lema. Acha jazba za kihuni katika ku handle issues za maendeleo. Mchezo huu hautaki Hasira kaka..

2. Mrisho Gambo, usitafute sifa zinazo kuzidi uwezo. Kasi ya JPM ni ya kupongeza yetote yule anaye leta maendeleo katika nchi anayo iongoza. Usiwe kikwazo katika hili na wala usitake sifa ya kuwa RC anaye ponda kila kitu cha upinzani, hao wapinzani nao wamepewa dhamana ya kuongoza Arusha tena na wanachi. Usipo badilika basi unafaa kutumbuliwa na JPM.

Asanteni sana

BAADHI YA MAONI:Ā screenshot_2016-10-19-16-00-35-1 screenshot_2016-10-19-16-00-42-1

 

“Rais Kabila na Rais Magufuli ondoeni visa”-Zitto Kabwe

Rais Kabila Na Rais Magufuli ondoeni visa kwa wananchi wetu wanaoingia kwenye Nchi zetu za Jamhuri ya KiDemokrasia ya Kongo Na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kurahisisha Biashara miongoni mwa Nchi zetu.

Hivi sasa raia ya Kongo anayeingia Tanzania analipa $50 za visa. Vile vile raia wa Tanznaia anayeingia Kongo. Hiki ni kikwazo kikubwa sana cha Biashara hasa Mpakani mkoani Kigoma, Katavi Na Rukwa.

NIMEOTA NDOTO YA MATUMAINI KWA WALEMAVU-Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

Nimekuwa nikikosa usingizi kwa wiki nzima tangu Pilato aje duniani na hii inatokana na huduma ya mama na baba kwa mtoto mchanga mda wote hasa usiku maana pilato bado hajajua majira ya duniani yakoje. Lakini leo majira ya saa tisa usiku nilikamatwa na usingizi mzito ulionichukua na kuniburudisha na ndoto ya matumaini kwa watu wenye ulemavu. Hii ni ndoto ya pili inayotaka kufanana ila hii ya sasa imejumuisha kundi kubwa la watu wenye ulemavu. Kwa waafrika ndoto zina maana sana na hasa kwa kabila letu la kimataifa la LUO. Hata maandiko na adithi za mitume inaonesha jinsi ndoto ilivyotumika kutoa taarifa kutoka kwa Mungu kwenda kwa mitume wake.

NDOTO yenyewe iko hivi…
“Nimejikuta nipo shule ya Pugu Secondary nikiwa kama mwanafunzi, (kwa historia fupi hii ndio shule yenye mazingira na baadhi ya miundombinu inayo support wanafunzi wenye ulemavu wa kiume jijini Dar, na ndio shule ambayo nimepata elimu yangu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita mchepuo wa Sayansi PCB). Ndoto inaonesha Mh. Raisi JPM anatembelea shule hiyo gafla tena alfajiri ya saa 12 tukiwa tunaamka. Pugu sekondary ina mabweni mawili ambayo ni maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu, hivyo ndoto inaonesha Mh.JPM alifikia moja kwa moja katika mabweni yetu na wanafunzi wote tuliokuwemo tukapatwa na mshangao huku tukiwa na furaha sana ya kutembelewa na Mh.JPM. Kama kawaida ya JPM alianza na maswali yake ya kutaka kujua hali halisi ya Elimu tuayopata hapo shule, tulimueleza mengi yaliyogusa changamoto za mifumo ya elimu kwa watu wenye ulemavu na tukatoa na mapendekezo ya jinsi ya kupunguza changamoto hizo kama sio kuzimaliza kabisa. Mh.JPM alikuwa msikivu na alionesha sura ya kuguswa sana na maelezo yetu watu wenye ulemavu juu ya umuhimu wa Elimu kwa watu wenye ulemavu.

fb_img_1475607460628
Peter Sarungi (kulia) na Spika wa Bunge Job Ndungai

Baada ya hapo Mh.JPM alinigeukia na kutaka mazungumzo na mimi, (Oooh May God) nilishituka nikupatwa na wasiwasi na fikra ya kutumbuliwa lakini nikajipa moyo na kujikaza kisabuni kisha nikasema moyoni (sina makosa ngoja nimsikilize).Mh. JPM alianza kwa kunipongeza juu ya makala zangu ninazozitoa katika mitandao ya kijamii akisema kuwa na yeye huwa anazisoma na kuzifurahia. Baada ya pongezi Mh.JPM akanipa jukumu moja la kuandika makala za kueleza changamoto za watu wenye ulemavu Tanzania, Mh.JPM akaenda mbee zaidi kwa kusema niwashirikishe waandishi wengine kama Yericko Nyerere, Magoiga SN, Binti Tanzania, na Malisa katika kuibua changamoto zinazowapata watu wenye ulemavu bila kujali itikadi maana Mh.JPM alisema hata wao wanaguswa na kundi hili. Baada ya agizo hilo Mh. JPM na wasaidizi wake walituaga na kurudi kwenye magari yao tayari kwa safari ya kwenda Ikulu, gafla nikapata wazo la kupiga picha na Mh. JPM lakini nikiwa najiandaa kuvaa nguo nzuri kwa ajili ya picha nikasiki muungurumo wa magari yake meusi kuashiria Mh.JPM alikuwa anondoka. Moyoni niliumia sana kukosa kupiga picha na JPM na ndio maana nikaona niweke picha ya ndoto yangu ya kwanza iliyofanikiwa kutimia na kupiga picha.Ā Baada ya hapo nilishitushwa na kelele za mwanagu Pilato akiwa analia kuashiria tatizo.Ā fb_img_1474834072101Tafsiri ya Ndoto…(kwa maoni yangu

1. Ndoto imebeba ujumbe na taarifa mahususi kwa watu wenye ulemavu juu ya utayari wa JPM katika kutatua matatizo ya walemavu. Inabidi tuamke na kueleza.

2. Ndoto inakumbusha jamii kushiriki katika kupaza sauti za watu wenye ulemavu bila kujali itikadi ili kuibua matatizo yanatukumba watu wenye ulemavu

3. Ndoto pia inaonesha kuwepo kwa ziara ya gafla ya JPM kwa shule zenye mazingira na miundombinu inayokidhi watu wenye ulemavu. (Hivyo walimu wakuu wajiandae ???)

#Mytake.
Jamii ya watu wenye ulemavu inakuwa kwa haraka kutoka na majanga ya ajali na magonjwa, na nina hakika kila mtu anaguswa na jamii hii maana tumefika 4M, hivyo natoa wito kwa jamii kupaza sauti kwa ku comment na ku share ili imfikie Mh.JPM na serikali aliyoiunda na kumpa taarifa kuwa watu wenye ulemavu tuna imani na yeye na tumeona nia yake ya kutuinua juu.

Asanteni sana

#TanzaniaDisabilityEmpire, #JukwaaLaWalemavuTanzania
#ElimuKwaWalemavu

“Tanzania haijawahi kuwa naye mtu wa namna hii”-Zitto Kabwe

Dikteta ( Kwa lugha nyepesi ) Ni mtu ambaye anaongoza Nchi Kwa faida yake yeye na kundi lake la utawala. Tanzania haijawahi kuwa naye mtu wa namna hii. Mfano wa Huyu Ni Mobutu, Bokasa, Idi Amin nk.

Dikteta Uchwara ( Kwa tafsiri yangu ) Ni mtawala ambaye anaelekea kuwa Dikteta Kwa tafsiri hiyo hapo juu. Tanzania haina kabisa Huyu maana hawezi kutokana na misingi ya Nchi kuwa imara.

Dikteta Mamboleo Ni mtawala ambaye analeta Maendeleo bila kutaka kuhojiwa. Maji mtapata. Barabara mtapata na Hata ndege mtapata lakini msihoji amepataje. Mifano ya madikteta mamboleo Ni Mingi sana duniani na ndio madikteta wa kisasa hao. Mfano maarufu Ni Vladimir Putin.screenshot_2016-09-30-09-25-35-1Haya ni baadhi ya maoni ya watu ?screenshot_2016-09-30-09-30-03-1screenshot_2016-09-30-09-30-47-1screenshot_2016-09-30-09-32-16-1

“NCHI HAINA DAWA MAHOSPITALINI, SERIKALI NA PAP WANAHAHA KUFUJA MABILIONI YA WATANZANIA” Zitto Kabwe

NCHI HAINA DAWA MAHOSPITALINI, SERIKALI NA PAP WANAHAHA KUFUJA MABILIONI YA WATANZANIA

Gazeti la The Citizen limeandika Juu ya Suala la Ukosefu wa Madawa Katika Hospitali zote Nchini. Hii ni Habari Mbaya na Kuogopesha Kwa Watanzania Wote.

Sababu Kubwa ya Kukosekana Kwa Madawa kwenye Mahospitali nchi Nzima ni Serikali kukosa Fedha. Serikali imeipa Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) 32% Tu ya Fedha ambazo ilipaswa kutoa Kwa MSD. Serikali ilipaswa kutoa Shilingi Bilioni 62.5 Kwa MSD Katika Kipindi cha Mwezi Julai mpaka Septemba 30. Lakini mpaka Leo imeipa MSD Kiasi Cha Bilioni 20 tu.

Uchunguzi Umeonyesha mpaka Septemba 16 MSD walikuwa na Tembe za Vidonge vya Paracetamol 170,000 Tu Katika Bohari Yao ya Mbeya. Huku Nchi Hospitali zikiwa hazina Kabisa Tembe Hizo. Hali ikiwa Ni Hivyo Hivyo Hivyo Katika Dawa za Ukimwi (ARVs), Vifaa Tiba kwaajili ya Mama Na Mtoto, Dawa za kipindupindu nk.

Katika Wakati ambao imegundulika tumelipa Kampuni ya Kitapeli ya PAP kwenye Sakata la Escrow zaidi ya Dola Milioni 245 Sawa Na Shilingi Bilioni 530 – Kiasi hiki Cha Fedha Ni zaidi ya Mara Mbili ya Bajeti ya Shilingi Bilioni 251 ya MSD Kwa Mwaka. Na tukilipa Bilioni 320 tunazodaiwa Baada ya Hukumu ya ICSID tutakuwa tumelipa zaidi ya Mara Tatu ya Bajeti ya MSD Kwa Mwaka.

Serikali ya CCM ionyeshe kuwa inawajali Wananchi wake Kuliko inavyowapenda Mafisadi wa PAP.Ā fb_img_1475084993950Zitto Kabwe Ruyagwa
Septemba 26, 2016

“Adui wa taifa hapaswi kuwa sehemu ya taifa letu”-Abdul Mohamed

fb_img_1475071899850 Miaka kadhaa nyuma, tulikuwa safarini kwenda Msumbiji, nakumbuka brother Zitto Kabwe pia tulikuwa naye kwenye msafara ule. Tulipanda ndege ya Shirika la ndege la Kenya kupitia Nairobi kisha Maputo.

Tukiwa njiani wakati wa kurudi nilipanda ndege nikiwa nafanya utani wenye kufanana na ukweli, “Hivi yaani sisi taifa kubwa tunashindwa na Kenya kumiliki ndege zetu kuja nchi jirani ya Msumbiji tu?”

Mhudumu wa ndege ile ya KQ alinijibu kwa kucheka “Ahh, Nyie Watanzania mko na maneno mengi, mnapiga siasa sana, hamwezi kuwa na ndege ka hizi”

Majibu haya yalifanya nijisikie aibu na kunyamaza, Licha ya ukweli kuwa Tanzania tulipoteza ndege nyingi baada ya kuvunjika kwa Shirikisho la Afrika Mashariki mwaka 1977. Lakini bado kama Taifa tusingepaswa kuwa katika hali ya kukosa hata ndege moja ya kuimiliki mpaka kufikia leo.

Kwa vyovyote vile, atakayejitokeza kupinga au kubeza juhudi hizi za dhati za Mh Rais JPM katika kufufua Shirika letu la ndege ambalo ndicho kiungo muhimu katika kukuza Utalii na kutangaza nchi yetu katika kuongeza mapato ya kigeni, lazima atakuwa ni adui wa taifa na adui wa taifa hapaswi kuwa sehemu ya taifa letu.

Najua tumeanza na ndege ndogo mbili, lakini kufika tatu lazima moja na mbili tuzivuke. Tujivunie hichi chetu na tuendelee kuamini tupo katika wakati mzuri zaidi kama taifa kufikia malengo ya kuwa taifa la watu wa kipato cha kati.

Shime, viongozi wa Shirika la ndege Tanzania na Watanzania wote, tuwe mabalozi wazuri wa ndege zetu na tuzitunze na kuzithamini ndege hizi.Ā fb_img_1475071831955Ndege hizi ni Fahari ya nchi yetu, Na ni Fahari yetu sote.

Van.

Rais Magufuli aonyeshe hasira zake dhidi ya Ufisadi kwenye huu ufisadi mkongwe wa IPTL- Zitto Kabwe

fb_img_1474302356894Nimesoma ‘ arbitral award ‘ ambayo Benki ya Standard chartered wametunukiwa na ICSID ( case no. ARB/10/20 ) na kuumizwa sana kutokana na kwamba hoja zote ambazo zimetumika kuwapa ushindi SCB ndizo Kamati ya PAC ilizijenga kwenye Taarifa yake Maalumu iliyopitishwa na Bunge na kutolewa maazimio 8. Ndio hoja hizo hizo zilibezwa na Serikali chini ya Waziri Sospeter Mwijarubi Muhongo na umma kuambiwa kuwa TANESCO hawatakuwa na madai dhidi Yao.

Mahakama hii ( tribunal ) ya ICSID imethibitisha maonyo ya PAC kwamba hasara Kwa Nchi kwenye kashfa ya #TegetaEscrow itakuwa Ni mara mbili ya Fedha zilizochotwa kwani mwenye Mali akijulikana tutapaswa kumlipa tena. Tulimpa Harbinder Singh Seth tshs 306 bilioni na tunapaswa kuwalipa SCB tshs 320 bilioni. Jumla tshs 626 bilioni. Na bado tunamlipa Seth kila Mwezi $4m Kwa umeme wa mtambo alioupata kitapeli.

ICSID imesema IPTL Ni Mali ya Standard Chartered Bank.

Rais John Magufuli ana fursa ya kihistoria kumaliza kabisa huu mtandao wa wizi na utapeli uliodumu toka mwaka 1995.

“ESCROW INAENDELEA KULITAFUNA TAIFA”-Zitto Kabwe

Kwanini Rais Magufuli hafanyii Kazi suala la IPTL? Matapeli hawa wataendelea kuipa hasara Nchi yetu mpaka lini? Sasa mahakama ya ICSID imeamua kuwa Benki ya Standard Chartered ilipwe Shilingi Bilioni 300 na riba. Kiwango Hicho Ni zaidi ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda.

TANESCO wanaingia Hasara hii Kwa sababu ya wizi wa Fedha za TEGETA Escrow na Rais bado anavuta miguu kuchukua hatua dhidi ya suala hili. Nini kimemkuta Rais Magufuli? Rais Kwanini hashughulikii Ufisadi huu wa IPTL/PAP? Nini Kinamzuia Rais Kuchukua Hatua dhidi ya Wizi huu wa Dhahiri Kwa Taifa

Tanzania Tunapata Hasara mno, Na Hizi zote Ni Fedha za Wananchi zitakazopotea.

ā€¢ Watanzania mmelipa matapeli Fedha zilizokuwa kwenye “TEGETA escrow account”, Fedha ambazo ziligaiwa Kwa Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri.

ā€¢ Watanzania Mmewapa Mtambo wa kuzalisha umeme matapeli hao na mnaendelea kuwalipa “capacity charges” mpaka sasa – Kinyume Kabisa na Maazimio ya Bunge yanayotaka Mitambo Husika itaifishwe.

ā€¢ Baada ya Hukumu hii Watanzania tutawalipa Standard Chartered Fedha zao kwa mtambo ambao sio wenu na Kwa Fedha ambazo (Kama tungelazimika Kulipa) tungezitoa kwenye Akaunti ya Escrow – Lakini sasa tutazitoa Hazina zikiwa ni Kodi za Watanzania.

Ushauri Wangu – Rais achukue Hatua Zifuatazo

ā€¢ Awafikishe Mahakamani watu wote waliohusika na kuitia Nchi hasara katika sakata la TEGETA Escrow.

ā€¢ Aitwae mitambo ya IPTL kisheria na kuimilikisha Kwa TANESCO (Kama ilivyoazimiwa Na Bunge).

ā€¢ Amkamate Bwana Harbinder Singh Seth na wafuasi wake wote na kuwafikisha Mahakamani Kwa makosa ya Utapeli, Wizi, Uhujumu Uchumi, Utakatishaji wa Fedha nk.

ā€¢ Ahakikishe Taifa halilipi Fedha Hizi Kwa Standard Chartered. Benki iliyotumika Kupitisha Fedha za TEGETA escrow ndio ilipe Hilo deni tunalotakiwa kulipa.

MUHIMU: Rais AAMUE Kusimama na WATANZANIA au kusimama na “Matapeli wa TEGETA escrow”.Ā fb_img_1474302356894Zitto Kabwe Ruyagwa
Sept 19, 2016

Maoni ya baadhi ya Watanzania baada ya #UKUTA kuhairishwa

Screenshot_2016-08-31-23-38-29-1 Screenshot_2016-08-31-23-39-44-1Screenshot_2016-08-31-23-45-36-1 Screenshot_2016-08-31-23-44-35-1 Screenshot_2016-08-31-23-44-45-1 Screenshot_2016-08-31-23-44-53-1 Screenshot_2016-08-31-23-45-07-1 Screenshot_2016-08-31-23-45-15-1 Screenshot_2016-08-31-23-45-20-1