Category Archives: politics

“Ningekuwa mimi Mbowe” na Peter Sarungi

FB_IMG_1471977078685
Peter Sarungi

**Sehemu ya Kwanza**

WAKATI NI UKUTA: Katika Dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano, WAKATI(Time) ni jambo la kuwekewa umakini mkubwa kupitia tafiti na uchunguzi wa jambo lolote lile unalotaka kulifanya. Wakati una tabia mbilimbili. Wakati haurudi nyuma wala hauna haraka, Wakati hunena na kuamua jambo, Wakati hutibu na kuzalisha vidonda, Wakati huishi na kufa, Wakati huelezea historia na kutunza, Wakati hutabiri yajayo na kutimiliza, wakati ni kipimo cha udhaifu na uimara, Wakati hutenganisha watu na kuunganisha, Wakati ni kiungo kwa mambo makubwa na madogo.

Wakati una nyakati nyingi na kila nyakati una zama zake na kila zama zina mambo yake. Leo naomba nivae viatu vya Mtu Huru kumwambia Mbowe kama Mkuu wa Chama mbadala (CHADEMA), Ni kweli kazi mliyoifanya kwa miaka zaidi ya 20 ya kujenga fikra mbadala katika siasa za Tanzania ni kubwa na yenye kuhitaji kupongezwa kwa moyo wa dhati kabisa (Hongereni sana). Lakini nasikitika kusema kuwa kazi yote hii ni kama 30% kati ya 100% ya wajibu wenu mlioamua kuutimiza juu ya siasa za nchi. Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda vitu, matendo na fikra tofauti zenye kubadili mitizamo, imani na mienendo ya jamii maana naamini kuwa “FIKRA Tofauti Huzaa UBUNIFU na Ubunifu ndiyo chanzo na chachu ya MAENDELEO katika jamii”. Nchi yetu ipo katika nchi zinazofanya siasa za kuigiza, Siasa za majukwaa, siasa za propaganda, siasa za Ukweli kugeuka Uongo na Uongo kugeuka Ukweli, Siasa yenye kibwagizo cha Demokrasia, Siasa ya matabaka ya uelewa na vimelea vya Ubaguzi, Siasa ambayo mpinzani anatumia Chuki na vugurgu kutafuta madaraka na Mtawala akitumia vyombo vya Dola kulinda Madaraka yake, Siasa ambayo vyama vyake hutegemea Umasikini na Ujinga wa wananchi kama Mtaji wao, Siasa mabazo mifumo ya nchi huegemea upande mmoja, Siasa ambazo mwanasiasa anawekeza katika chama kuliko waliomchagua, Siasa zisizo na mabadiliko ya mbinu, Siasa za kungojea Marekani na Uingereza wamefanya nini ndipo nasi tuige, Siasa zisizo zungumzia ISSUES na badala yake zinazungumzia MATUKIO, Siasa zenye kulenga kizazi kilichopo tu badala ya kwenda zaidi kwa vizazi vijavyo, Siasa zenye kunukuu Fikra za Mwl Nyerere kama kikomo cha Fikra badala ya kuja na Fikra pevu zaidi, Siasa iliyoacha kutilia mkazo masomo ya siasa na uraia kwa vijana, Siasa ya UBEPARI katika nchi ya UJAMAA yenye mifumo ya utendaji ya URIBALELI…

Mtu huru anawezaje kufanya siasa katika nchi kama hii na ategemee kupata matunda huru? Nchi ambayo wananchi (wapiga kura wake) hawana uelewa juu ya HAKI na WAJIBU wao katika nchi, Hawajui kutofautisha ukweli na propaganda, Hawajui kutofautisha ushabiki wa vyama vya michezo na siasa, Hawajui mipaka yao wala ya watawala wao, Nchi ambayo mfumo wake kwa mwananchi tangu anazaliwa mpaka anazeeka ni Mtegemezi tu, Nchi ambayo walinzi wake ni wale ambao hawakufanya vizuri shuleni na wale ambao walikuwa ni wakorofi, majasiri na watukutu shuleni.

Kuna jambo Mtu huru amelisahau ambalo ni la muhimu sana kwa nchi kuwa huru. Apo ndipo WAKATI unapobadilika na kuwa UKUTA, Wakati wa siasa za chuki kwa vyombo vya Dola umepitwa, Wakati wa kuwaandamanisha wananchi wanyonge umeshapita, Wakati wa siasa za matukio umepita, Wakati wa siasa za migomo umepita. Kama Mbowe na timu nzima ya upinzani bado wana siasa za namna hii basi wajue kuwa wamefikia UKUTA na wana haja ya kubadilika.

Ningekuwa mimi ninkiongozi wa Upinzani kama alivyo Mtu Huru MBOWE basi ningefanya yafuatayo….

1. Ningewekeza na kuanzisha operation kwa wananchi za kutoa ukungu wa kuelewa haki na wajibu, siasa na uraia na kuwapa uelewa zaidi wa kijamii ili wawe huru na waweze kuja na fikra huru na mbadala katika nchi. Kwa sasa bado watanzania wengi hawajui mambo mengi ya siasa na hivyo maamuzi yao mengi yamekuwa ni ya kuiga na kufuata mkumbo.

2. Ningewekeza katika kurudisha mahusiano ya karibu sana na vyombo vya ulinzi na usalama. MBOWE, Huu sio Wakati wa kushindana na vyombo vya usalama ambavyo hata wao wengi hawana elimu ya uraia na ni vyombo vinavyoendeshwa kwa oder za wakubwa. Ni muhimu sana kwa chama mbadala kama Chadema Tanzania kuwa na watu kila idara kwa idadi kubwa katika vyombo vya usalama maana hivyo vyombo ndivyo vinavyotumika kulinda maslahi ya siasa za nchi.

#Mytake Tunahitaji Siasa Huru kutoka kwa wanasiasa Huru kwenda kwa Wananchi Huru wanaoweza kufanya maamuzi Huru katika nchi Huru ndio maana tunahitaji kutengeneza vyama Huru.

Asanteni sana

Baadhi ya maoni ya Watanzania kuelekea Sept. Mosi #UKUTA

Screenshot_2016-08-30-21-22-33-1Screenshot_2016-08-30-21-23-05-1Screenshot_2016-08-30-21-23-23-1-1Screenshot_2016-08-30-21-23-40-1Screenshot_2016-08-30-21-24-09-1Screenshot_2016-08-30-21-24-44-1Screenshot_2016-08-30-21-24-56-1Screenshot_2016-08-30-21-25-44-1Screenshot_2016-08-30-21-25-54-1Screenshot_2016-08-30-21-26-03-1Screenshot_2016-08-30-21-26-23-1Screenshot_2016-08-30-21-26-34-1Screenshot_2016-08-30-21-26-44-1Screenshot_2016-08-30-21-27-10-1Screenshot_2016-08-30-21-27-22-1FB_IMG_1472436063790Haya, hayo ni baadhi tu ya maoni ya Watanzania kuhusiana na kile kinachotakiwa kutendeka tarehe Moja September, 2016 #UKUTA ……….! Naomba usome kwa faida yako mwenyewe na ufanye maamuzi yaliyo sahihi …..!!! Mungu ibariki Africa. Mungu ibariki Tanzania……..??

“USHABIKI WA VYAMA VYA SIASA NI TOFAUTI NA USHABIKI WA VILABU VYA MICHEZO.” – Peter Sarungi

FB_IMG_1471977078685Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Nakumbuka tangu nilipoanza kufuatilia mchezo wa mpira wa miguu nikiwa darasa la kwanza katika shule ya walemavu (Salvation Army) sijawahi kuhama Yanga pale nilijikuta nafurahia timu ya Yanga chini ya wacheza nyota kipindi hicho kama lunyamila, chambua, mohamed machinga na wengine wengi. Desturi ya ushabiki wa vilabu vya michezo katka historia ya soka inaonesha kuwepo kwa uvumulivu wa hali ya juu kutoka kwa mashabiki wa vilabu hasa pale wanapo boronga au hata kushuka daraja (mfano kwa sasa Arsenal na Liverpool). Mashabiki hushangilia timu husika iwe kwa shida ama kwa raha yaani wafungwe ama washinde bado ataendelea kuwa mshabiki wa timu husika. Hivyo ushabiki wa vilabu una lengo moja la kupata burudani pale timu inaposhinda.

Kwenye siasa hali iko tofauti kabisa. Siasa inagusa maisha ya kila siku ya mwananchi katika nchi. Siasa inawagusa watoto, vijana, wazee, wakulima, wavuvi, wachimba migodi, wafanyakazi, wafanyabiashara, walimu, masikini, matajiri, wanasiasa na makundi yote katika jamii. Kila mwananchi na kila jamii inaguswa na maamuzi ya kisiasa katika nchi kwa namna fulani yaani kila unachokifanya kinawezekana kwa sababu ya mazingira ya kisiasa. Lengo la siasa sio kupata burudani kama ilivyo kwa timu za michezo bali ni kuboresha maisha ya kila siku ya mwananchi.

Kwa utafiti wangu nimegundua watanzania wengi wanafananisha ushabiki wa vilabu nya michezo na ushabiki wa vyama vya siasa. Hali hii ni hatari sana kwa ustawi wa siasa na demokrasia katika nchi. Mara nyingi unamkuta mtu ana kuwa mfuasi wa chama cha siasa mpaka anapata upofu wa fikra yaani hata kama chama chake kinaboronga katika kuboresha maisha yake bado atakuwa mkaidi na mwenye kutetea chama. Hii hali imefanya watu wasomi na wenye heshima zao kuweka usomi wao mfukoni ili kutetea maslahi ya chama, hata haki ya kuhamia chama fulani inakuwa ni fedhea kwa mtu mpaka anaitwa majina mengi kama msaliti, mroho, malaya wa siasa. Yaani unapohama ni shida na unapohamia napo shida ipo, huu ni ushabiki wa Vilabu vya mpira, sio wa vyama vya siasa. Aina hii ya ushabiki wa vilabu katika siasa ndio sababu ya kuwepo kwa uadui kwa mashabiki na unagawa taifa kwa majina ya kejeli kama vile ndugu yangu Magoiga SN anavyowaita upande wa pili NYUMBU na Ben sanane anvyowaita upande wa pili FISIEMU. Ushabiki huu ndio sababu ya kupata baadhi ya wabunge ambao hawana sifa, uwezo wala weledi ya kuwa viongozi lakini wanachaguliwa kwa sababu ya ushabiki huu wa ovyo kabisa.

#Mytake. Unapokuwa mfuasi wa chama fulani ni vizuri ukaangalia maslahi yako na ya wapendwa wako kama yanapatikana kabla ya kutetea maslahi ya chama lakini vilevile tusishangae tunapo mwona mwanasiasa anahama kutoka chama kimoja na kwenda kingine jua anatafuta falsafa inayomfaa. Tusitukanane wala kuitana majina ya ajabu kwa kwenda upande fulani.

Asanteni sana

Amani! Amani! Amani! Ndiyo nguzo ya Tanzania!

FB_IMG_1472404915202FB_IMG_1469659269564Watu walio starabika utawajua tu kwa matendo yao! Yana ng’aa hata gizani!! Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!! Kwakweli mzee Lowassa na mke wake ni watu wastarabu sanaaaaaa! Hawa ni watu ambao hawajazoea “drama” hata kidogo! Ni watu wa kujishusha. Haya mambo mengine ni watu tu wanataka kuwalazimisha lakini sio asili yao! Unajua kuna watu  ni wastarabu wa mavazi tu! Yani ukiwaona utafikiri tabia na roho zao zinaendana na mavazi yao ya kitanashati!! Kumbe ovyo kabisa!! ……….anyway I love this picture a lot! Siasa sio uwadui na wala sio chuki zisizokuwa na kichwa wala mguu!! Tunataka democracy ndani ya Tanzania lakini hatuwezi kuvunja nguzo yetu kuu (amani) halafu mkafikiri tutakua salama baada ya hapo!! Nope! Pindi tutakapo jaribu vunja amani ya nchi yetu basi tuhesabu maumivu! Haitokaa irudi tena! Niambie nchi gani ambayo imechezea amani ya nchi yao nawakaweza irudisha???!! Amani! Amani! Amani! Ndiyo nguzo na msingi wa Tanzania!!

EALA has passed a motion to make Swahili an official language to the EA Community!: by Hon. Shy-Rose Bhanji

FB_IMG_1472401262385
Hon. Shy-Rose Bhanji, EALA MP

EALA in Arusha: it gives me great pleasure to inform you that EALA has passed a motion to make Kiswahili an official language of the East African Community.

This motion was undertaken thru the collaboration of 3 EALA MPs: Hon. Aboubakar Zein from Kenya, Hon. Shy-Rose Bhanji and Hon. Abdullah Mwinyi from Tanzania. It has been my long outstanding desire, dream and ambition to promote Kiswahili as one of the official languages of the EAC. For its polularity among East Africans and extensive impact in various fields of daily life, Kiswahili is core and integral to the EAC integration and a big asset to make it people centred and market driven integration. FB_IMG_1472401262385I feel more than happy to have been part of this important Team to canvas and lobby for the promotion of this historical motion. Special thanks go to the Speaker of Eala Rt Hon. Dan Kidega for his his approval and the leadership on this noble agenda which we owe to the people….This motion won the hearts and minds of Eala members overwhelmgly. We owe them a lot of gratitude and appreciation.

It is our strong conviction that the Heads of State of EAC will endorse this motion to enable the amendment of the EAC Treaty which has only English as the official language. #EAC #OnePeopleOneDestiny #UmojaWetuNiNguzoYetu

FB_IMG_1469659269564Hongereni wabunge wa Africa Mashariki kwa uwamuzi huu! Ni jambo la kujivunia sana. Natumaini wengi wetu sasa tutahamasika kujifunza Kiswahili fasaha kwa faida ya jumuiya yetu na hatimae kiwe ndio lugha kuu ya bara la Africa!

“Inahitajika busara kubwa ili kuvunja ukuta”-Peter Sarungi

FB_IMG_1471977078685Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Kila mtu hapa duniani ana mapungufu yake, inawezekana mtu akayajua hayo mapungufu ama laa asiyajue mpaka aambiwe. Kuwa na mapungufu ni sehemu ya uumbaji wa Mungu maana Mungu hakupi vyote vilivyokamilika na ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kibinadamu wa kukosoana, kuelekezana, kusifiana na hata kupingana katika maswala mbalimbali. Sio jambo la ajabu kukubali unapoambiwa mapungufu yako maana huo ndio mwanzo wa kutibu udhaifu unasababishwa na mapungufu yako, lakini ni jambo la ajabu na lililokosa busara na hekima kukataa kushauriwa ama kupinga uwepo wa mapungufu yako pale unapo ambiwa.

Kuna tukio linalozungumzwa sana na makundi mengi ya kijamii Tanzania, UKUTA. UKUTA inaratibiwa na chama cha upinzani Chadema Tanzania katika kufikisha ujumbe ya madai yao, lakini pia serikali ya awamu ya tano kupitia Chama cha Mapinduzi nao wanaratibu operation ya KUVUNJA UKUTA chini ya idara ya ulinzi n usalama wa nchi. Pande zote mbili zimekuwa na matamko mbalimbali yenye kuonesha ubabe, vitisho, dhihaka, chuki, na hali ya kutokubali kurudi nyuma. Kwa historia za mambo ya kisiasa hali hii ya sasa ni hatari sana kwa usatawi wa nchi ki uchumi, siasa na jamii nzima.

UKUTA na VUNJA UKUTA ni majina tu ya operation zinazoratibiwa lakini utekelezaji wake unabeba matendo na matukio makubwa yanayozaa mbegu ya chuki itakayopandikizwa kwa wananchi na serikali yao kwa vizazi vya sasa na vinavyokuja. Hali kama hii ilianza miaka ya 90+ nchini burundi na watawala wakashindwa kisoma alama za nyakati kwa kujivunia dola wanayo miliki bila kujua kuwa dola huletwa na wananchi, matokeo yake nchi ilipata hasara na pigo kubwa linalosumbua mpaka leo.

Viongozi wetu wanahitaji kutumia meza ya mazungumzo zaidi katika kufikia makubaliano mbalimbali kuliko kutumia operation za UKUTA na VUNJA UKUTA. Mazungumzo ni busara yenye nguvu ya Mungu kuliko operation za kibinadamu zinazotumia mabomu, mawe na vurugu. Hivyo nawaomba viongozi wa pande zote mbili kujadili kwa kutumia meza badala ya nguvu. Hii ndio busara na hekima zinazohitajika kutoka kwa viongozi wetu. Mfano: video hii ya chini

inatafsiri hali halisi ya viongozi wetu wengi tunaowapa dhamani ya kulinda maslahi ya nchi na wananchi wake wanavyokosa lugha yenye matamshi ya kuleta nchi pamoja na badala yake wanatoa matamshi ya kugawanya wananchi na kushauri wajenge UKUTA mwingine maana huu wamesha ubomoa tayari, matamko kama haya yanaishi vichwani mwa wananchi kwa muda mrefu na wengine hufika mbele zaidi katika kufikiri jinsi ya kukabiliana na VUNJA UKUTA zingine zitakazo kuja mbeleni.

#My_Take Tutumie taratibu za kisiasa katika kutatua migogoro ya kisiasa balada ya nguvu za dola, migomo na maandamano.
Naipenda Tanzania kuliko chama na mwanasiasa.

Kutoka Facebook

FB_IMG_1471582160781Ni zamu ya vijana kushika hatamu! Pongezi kwa Rais Dr. Magufuli kwa kuona umuhimu wa vijana kuanza kuiliongoza taifa hili kwani dunia imebadilika, tunahitaji vijana ambao wataweza kwenda na kasi ya mabadiliko hayo…………Hongera sana Mh. Mrisho Gambo Mkuu wa mkoa wa Arusha mpya!FB_IMG_1471582147172“Hongera sana Mheshimiwa Mrisho Gambo kwa kuteuliwa Mkuu wa mkoa Arusha. Ninakutakia Kila Heri, Baraka na Mafaniko ktk nafasi hii ya kuwatumikia wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla. #ArushaNiYetuSote” hayo ni maneno yake Mh. ShyRose Bhanji Mbunge wa East Africa-Tanzania………..picha nzuri sana

Tanzania Vs Marekani

FB_IMG_1469659269564Nilikutana na huu ? mjadala huko Facebook nikaona ni share nanyi……………Kitu ambacho huwa sielewagi ni kwanini baadhi ya Watanzania wanapenda kuilinganisha Tanzania na Marekani inapofika kwenye swala la maendeleo ya miundo mbinu na siasa? Hivi hamjui kuwa Marekani hawakutumia jasho lao kuijenga hii nch?! Marekani ilijengwa kwa nguvu ya watumwa! Watumwa walimwaga damu na jasho lao lilibubujika kuijenga hii Marekani ambayo mnataka kufananisha na Tanzania. Tanzania inajengwa kwa au itajengwa kwa jasho lako wewe na mimi!! Sasa sijui kwanini wewe unayelalamika usikubali kutoa jasho lako kwa maendeleo ya nchi yako? Kulalamika kwako hakuijengi Tanzania bali linajenga a “whining. Nation”!! Jiulize wewe kama Mtanzania mzalendo unachangia kitu gani katika maendeleo ya nchi yako? Au unaongezea watu stress zisizokuwa na ulazima!! Tafakari! Screenshot_2016-08-12-12-34-07-1Screenshot_2016-08-12-12-34-00-1Screenshot_2016-08-12-12-32-44-1Screenshot_2016-08-12-12-32-07-1Screenshot_2016-08-12-12-30-31-1Screenshot_2016-08-12-12-29-38-1

“Tusikubali mama yetu Tanzania kusambaratika”- James Mbatia

Screenshot_2016-08-13-18-35-02-1FB_IMG_1469659269564Tanzania kwanza, vyama nyuma! Tunahitaji democracy ndani ya Tanzania lakini amani yetu ni kipaumbele number moja! Simtetei Rais Magufuli hapana, lakini lazima tukubali kumpa nafasi ya kufanya kazi! Mfumo wa nchi ulikuwa umeoza, na yeye anataka kuubadilisha kwa kuanzia na nidhamu ya kazi na ufisadi. Basi haya mambo ya siasa kila kukicha yanazidi kuturudisha nyuma!  ……… Mimi na Tanzania, wewe je? Tafakari!

Kifo cha Nyani miti yote huteleza- Mkandara Ebbie

2016-06-30 09.17.03Naomba iyelewe kuwa Siasa isn’t my cup of ‘protein smoothie’! and my knowledge is very limited kwenye maswala ya siasa. Hivyo naogopanga sana kuongelea vitu ambavyo siwezi kutolea ufafanuzi. Ila nachoweza kusema hawa wanasiasa wote haijalishi wa inchi gani, wote wana “personal” interest in everything they do or say. Hivyo kabla ya kushabikia mtu sana Jaribu kukaa pembeni na utafakari kama kweli hakuna any hidden agenda kwani usipende kuwa Nyumbu! With that being said; mimi binafsi sitokaa niongelee Siasa hapa kwa hii blog! Lakini nikipata mjadala mzuri uliopangiliwa vizuri with point za kuelimisha, nita share nanyi humu! Na ninaomba mtu asiniulize msimamo wangu au maoni yangu kwani sitakuwa nayo! I hope mtanielewa!………haya nimekutana na huu mjadala hapa by Mkandara Ebbie Screenshot_2016-07-01-13-21-38-1Screenshot_2016-07-01-13-22-05-1Screenshot_2016-07-01-13-23-15-1Screenshot_2016-07-01-13-20-43-1Screenshot_2016-07-01-13-24-21-1

Makamba ashtukia “Manabii, Mitume” wapya

Screenshot_2016-06-27-10-02-51-1Haya, Mh. Makamba kashtuka! Nafikiri kama juma moja sasa limepita tangu niulize swali la “kizushi” kuhusu hawa manabii / mitume wanaojitokeza siku hizi (soma ? Siku za mwisho! Just thinking out of the box!) Kuwa je ni waukweli au “wakichina”? Na Mr January Makamba. Yeye katupatia mtazamo wake kama unavyo someka hapo juu ?. Je wewe unawaonaje? Toa mtanzamo wako. Kusoma zaidi bonyeza ? Makamba ashtuka

Nchi yoyote iliyoendelea imeendelezwa kwa kodi- Stephen Mndalila

Screenshot_2016-06-24-10-16-21-1Screenshot_2016-06-24-10-16-49-1Screenshot_2016-06-24-10-17-07-1Screenshot_2016-06-24-10-17-35-1

THANKS TO OUR EXCELLENCE PRESIDENT DR, JPM!!- Richard Mbilinyi

THANKS TO OUR EXCELLENCE PRESIDENT DR, JPM!!!!!!!,

Nianze kumshukuru mheshiimiwa Rais Dr John Magufuli kwakuweza kuonyesha misimamo ya wazi kabisa katika kusimamia kile anachokiamini katika kuongoza nchi. Mambo muhimu Mheshimiwa rais kayaamua katika kufikia malengo yake na ambayo binafsi yamenifurahisha na imani yangu hata watanzania ni haya yafuatayo;-

1. Kuamua Kodi ya Majengo ikusanywe na mamlaka ya mapato (TRA)

Msimamo dhabiti wa mheshimiwa rais katika eneo hili la kodi za majengo kukusanywa na TRA kwasasa na kuachana na mpango wa kuziachia halmashauri zetu ambazo zimekuwa zikishindwa kukusanya pesa na zikitumia vibaya pesa za nchi vibaya. Katika eneo hili niombe sana serikali itumie teknolojia ya mifumo ya ki geografia (Geographic Information System (GIS)) katika kuhakikisha kila mmiliki wa nyumba na eneo nyumba liliko limeainishwa katika mfumo huu. Kwenye eneo hili binafsi naweza hata kutoa ushauri bure kwa serikali yangu namna gani mfumo dhabiti uanzishwe maana ni sehemu ya taaluma yangu.

2. Kodi ya Kiinua Mgongo cha viongozi wote.

Katika eneo hili hakika mheshimiwa raisi kanifurahisha sana maana hata baadhi ya bunge wa chama chake hawakutaka kabisa wakatwe pesa hii, lakini mheshimiwa rais kaonesha mfano tayari kwa yeye kuamua pesa yake iikatwe na kuruhusu viongozi wote wa kisiasa wakatwe kodi. Hakika tunae rais mzalendo maana ni kwa nadra sana kuona kiongozi yupo tayari kukatwa kiinua mgongo vyao. Hii nadhani iende mbali kabisa hata kwa kupunguza posho zisizo na msingi, maana hii inajenga tabia watu kufanya kazi kwakutegemea posho.

3. Kukusanya kodi za makampuni ya simu kwenye utoaji na upokeaji wa pesa.

Hili eneo makampuni ya simu yamekuwa yakiibia serikali pesa kwa muda mrefu maana serikali ilikuwa inalipwa na makampuni ya simu pesa ya kupokea tu na sio ile ya kutuma wakati wao walikuwa wanajikusanyia mapato kwa mtumiaji wa mwisho ambae ni mwananchi. Hapa niendelee kuishauri serikali ihakikisha inakuwa na mifumo ya kuweza kujua gharama halisi ya mzunguko wa mpesa, aitel money, tigo pesa, na z-pesa ambazo zinakadiliwa karibu trillioni 50.

4. Kuruhusu makampuni yote ya simu kuuza hisa zake katika soko la hisa ndani ya nchi.

Katika eneo hili ndio naona hapa serikali imecheza heko maana katika eneo hili makampuni mengi ya simu yalikuwa yanauza hisa zake nje ya nchi kitu ambacho watanzania walikuwa sio sehemu ya umiliki wa makampuni ukiachilia mbali vodacom ambayo wameliki wachache tu na ambao walikuwa viongozi pekee ndio walikuwa wamiliki wahisa hizo. Iende mbali zaidi kutoa adhabu kwahaya makampuni yatakayo kaidi kutokuweka hisa zake ndani ya miezi sita ili watanzania waweze kupata haki ya kuwa wamiliki wahaya makampuni.

5. Kuongeza kodi kwa vitu vya nje ambavyo vinazalishwa ndani ya nchi.

Hapa pia niendelee kuipongeza serikali kuhakikisha inalinda viwanda vya ndani kwakuongeza kodi kwa baadhi ya bidhaa ambazo ndani ya nchi tunazalisha lengo likiwa ni kulinda viwanda vya ndani. Pia katika eneo hili serikali imepandisha mitumba ambayo imekuwa ni haibu kwa nchi yetu kuendeleea kuagiza mitumba (nguo za ndani, sindilia) kutoka nje ya nchi. Ifeke mahali kwenye eneo hili serikali ijikomit kuleta mashine za kisasa nakuwapatia vijana na kuwapatia baadhi ya magodown yaliyokuwa hayatumiki kufungua kiwanda cha nguo hasa kwenye maeneo ya pamba inalimwa kama bariadi ilituachane kabisa nauagizaji nje bidhaa ambazo kama taifa tunaweza kuzalisha. Tunatumia pesa nyingi za kigeni na hii pia ndio sababu pesa yetu inakuwa haina dhamani na ajira nayo kuwa ngumu kupata.

6. Kutokuongeza bei ya Mafuta

Eneo hili niishukuru serikali iliyo chini ya mheshimiwa JPM, kwakukataa mapendekezo ya baadhi ya wabunge waliotaka bei ya mafuta kuongezwa ili serikali ikusanye kodi. Lengo ni zuri lakini ukipandisha bei ya mafuta unakuwa umeongeza bei ya kila kitu, na serikali hii tayari imehakikisha bei inakuwa haibadiliki badiliki (Stable price). Naishauri serikali iendelee kusimamia zaidi eneo hili la mafuta kwakuwapata waagizaji waaminifu na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaojaribu kuhujumu mafuta kama kipindi cha nyuma.

7. Kusimamia watu wafanye kazi na kutoruhusu kuigiza siasa kwenye mambo ya maendeleo.

Hapa binafsi nimshukuru sana raisi kwakuamua watu wajielekeze kwenye maendeleo na kupunguza muda mwingi katika kufanya siasa wakati tayari mshindi kashapatika na uchaguzi ushaisha. Tumezoea katika nchi yetu kuendekeza siasa kila mara na kusahau kufanya maendeleo na kisababishia nchi yetu ishindwe kusonga mbele. Nipongeze misimamo hii ya mheshimiwa rais kukataza watu kuendeleza malumbano ya kisiasa badala ya kuwatumikia wananchi ambao wana hali ngumu sana kimaisha. Misimamo muda mwingine inahitajika…..kwahili tunakushukuru umeliona anaetaka siasa za kiharakati akafanye yeye na familia yake awaache watanzania wafanye kazi kujiletea maendeleo.

8. Kuweka adhabu ya wale wanaonunua vitu bila kupewa risit na muuzaji wa bidhaa.

Serikali yoyote inaendeshwa kwa kodi za wananchi hasa walipa kodi. Kwahiyo kuweka adhabu ya miaka mitatu jela au faini ya millioni tatu itajenga heshima kwa wafanya biashara na wananchi. Nchi zilizo endelea ukwepaji kodi ni criminal offence na haijalishi weye ni rais au unaumaarufu.

9. Kodi za pikipiki na magari.

Pikipiki na magari imefika wakati eneo hili serikali ikusanye mapato maana uingizwaji wake ni mkubwa sana na licha ya kutokuwepo kwa kodi kwenye pikipiki lakini bei zimekuwa sikipanda siku ya siku …kutoka laki tisa miaka ya 2009 sasa ni milioni mbili. Hii isibaki kuwa ni ajila pekee kwa vijana kama serikali ibuni ajira mpya zitakozo toa fursa kwa vijana wengi.

10. Kuendelea kuaminiwa na mataifa ya nje.

serikali mpaka sasa inaendelea kusaini makunaliano na jumuiya mbalimbali, nchi zilizo endelea, mashirika mbalimbali. mfano tayari (Benki ya Dunia) World bank ambayo tayari ishaadi trillion 3, serikali ya Amerika tayari imeahidi kutoa trillion 1…….kwahiyo neema inaendelea kuja zaidi maana wahisani wanaimani na serikali hii kwa hatua zinazochukuliwa.

Kwa leo niishie hapa, hivi ni baadhi tu ya mengi ambayo serikali ya JPM imeyafanya na wanaendelea kuyafanya maana sijaongelea hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa kwa wafanya kazi hewa na mafisadi ambao wamelitafuna nchi. hatua ni nzuri sana na tuendelee kuchukua hatua zaidi na zaidi hadi mtu wa mwisho aliechukua hata dhumuni kwa lengo tu la kuifisadi nchi wachukuliwe hatua na kuwafikisha mahakamani ikiwezekana hata mali zao zitaifishwe………….. SHARE FB_IMG_1466781294961

Asanteni!!!!!!!!!!………………….
RRM
MR. RICHARD MBILINYI
MSc in GIS – University of Manchester (UK)
MSc in Economics and Finance for Development – University of Bradford (UK)
PGT in Economic Diplomacy – Centre Foreign Relation – CFR (TZ)
BSc. in Geomatics – UDSM (TZ)
Phone: +447909249556
Email: [email protected]

***soma baadhi ya comments za watu kuhusu hii post kwenye post inayofuata***