*KESHA LA ASUBUHI* _JUMANNE MEI 08, 2018_ _Kando ya Akina Mama Akiwaongoza Watoto Wao_ _Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko. 1 Sam 1:27, 28._ ? Akina mama Wakristo wanapaswa kutambua kuwa wao ni watendakazi pamoja na Mungu wakati wanapowafundisha na kuwaadabisha watoto wao katika namna ambayo itawawezesha kuakisi tabia ya Kristo. Katika kazi hii watakuwa na ushirikiano wa malaika wa mbinguni; lakini ni kazi ambayo kwa masikitiko imepuuzwa, na kwa sababu hii Kristo ananyang’anywa urithi wake-washiriki walio wadogo wa familia yake. Lakini kupitia kwa ukaaji ndani wa Roho Mtakatifu, ubinadamu unaweza kutenda kazi pamoja na uungu. ? Somo la Kristo wakati wa kuwapokea watoto, linapaswa kuacha alama yenye kina juu ya mioyo na akili zetu. Maneno ya Kristo yanawahimiza wazazi kuwaleta watoto wao kwa Yesu. Wanaweza kuwa wakaidi, na kuwa na hisia kali kama zile za kibinadamu, lakini hii haipasi kutukatisha tamaa ya kuwaleta kwa Kristo. Aliwabariki watoto waliopagawa na hisia kali kama yake mwenyewe. ? Mara nyingi tunakosea kuwafundisha watoto. Mara nyingi wazazi wanawaendekeza watoto katika kile kilicho cha kibinafsi na chenye kuharibu maadili, na, badala ya kuwa na uchungu wa roho kwa ajili ya wokovu wao, wanawaacha kuzurura bila malengo wala mwelekeo, na kukua wakiwa na tabia potovu na mienendo isiyopendeza. Hawakubali wajibu wao waliopewa na Mungu kuwaelimisha na kuwafundisha watoto wao kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Hawaridhishwi na tabia za watoto wao, na kuvunjwa moyo wanapotambua kuwa makosa yao ni matokeo ya uzembe wao wenyewe, na kisha wanakatishwa tamaa. ? Lakini ikiwa wazazi wangelihisi kwamba kamwe hawawekwi huru kutokana na mzigo wao wa kuwaelimisha na kuwafundisha watoto wao kwa ajili ya Mungu, iwapo wangelifanya kazi yao kwa imani, wakishirikiana na Mungu kwa maombi na kazi ya dhati wangelifanikiwa katika kuwaleta watoto wao kwa Mwokozi. Hebu akina baba na akina mama wajitoe wao wenyewe, roho, mwili, na nafsi kwa Mungu kabla ya kuzaliwa kwa watoto wao. - Signs of the Times, Apr. 9, *TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*
Category Archives: Spirituality
Kesha la asubuhi: Mwenye Wazazi Wanaojali
*KESHA LA ASUBUHI* _JUMATATU MEI 07, 2018_ *Mwenye Wazazi Wanaojali* _Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usini-ondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Zaburi 51:11-13._ ?Ni ombi la namna gani hili! Ni dhahiri kiasi gani kuwa wenye dhambi walioko nyumbani hawapaswi kutendewa kwa kutokujali, bali kwamba Bwana anawaangalia kama walionunuliwa kwa damu yake. Katika kila kaya ambamo ndani yake wamo ambao hawajaongoka, inapaswa kuwa kazi ya wale ambao wanamjua Bwana kutenda kwa hekima kwa ajili ya wongofu wao. Bwana kwa hakika atabariki juhudi za wazazi, wakati ambapo kwa kicho na upendo watajitahidi kuokoa roho za walio katika kaya zao. Bwana Yesu anasubiri kuonesha neema. ? Kwamba kazi ingelianza moyoni! “Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” (Zaburi 51:16, 17). Basi hebu na ifahamike na wanakaya wote kwamba kazi hii lazima ianze moyoni. Moyo lazima utiishwe na kufanywa kuwa na toba kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu unaoumba, na kufufua. Kwa kutambua msaada wa wakala huyu mwenye nguvu, je wazazi hawawezi kufanya kazi kwa ari na upendo zaidi kwa ajili ya wongofu wa watoto wao kuliko walivyowahi kufanya hapo nyuma? ?Ahadi ya Bwana ni kwamba “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.” (Ezekieli 36:25-27). ? Roho wa Bwana anapofanya kazi katika mioyo ya wazazi, maombi na machozi yao yatakuja mbele za Mungu, watasihi kwa bidii, na watapokea neema na hekima kutoka mbinguni, na watakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ajili ya watoto wao ambao hawajaongoka. Kadiri Roho huyu anapodhihirishwa nyumbani, ataletwa kanisani, na wale ambao ni wamisionari wa nyumbani nao pia watakuwa mawakala wa Mungu kanisani na katika dunia. Taasisi ambazo Mungu amezipandikiza zitabeba tabia tofauti kabisa. - Review and Herald, March 14, 1893. *TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI MTOTO WA MFALME*
Kesha la asubuhi: Bado tunapendwa ijapokuwa tunakosea
*KESHA LA ASUBUHI* _JUMAMOSI MAY 5, 2018_ *Bado Tunapendwa Ijapokuwa Tunakosea* _Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. 1 Yoh. 2:1._ ✍? Wale ambao wako katika muunganiko na Mungu ni mifereji kwa ajili ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Iwapo mtu ambaye kila siku anawasiliana na Mungu atakosea njiani, iwapo atageuka hata kidogo na kuacha kumtazama Yesu kwa uaminifu, hiyo si kwa sababu anatenda dhambi kwa makusudi; kwa kuwa anapoona kosa lake, anarejea tena, na kukaza macho yake kwa Yesu, na ukweli kwamba amekosea haumfanyi kuwa na thamani pungufu moyoni mwa Mungu. ✍? Anafahamu kuwa ana mawasiliano na Mwokozi; na anapokemewa kwa ajili ya kosa lake katika jambo fulani la hukumu, hatembei kwa kinyongo, na kumlalamikia Mungu, bali huligeuza kosa lile kuwa ushindi. Anajifunza somo kutoka katika maneno ya Bwana, na kuchukua tahadhari asije akadanganyika tena. ✍? Wale ambao wanampenda Mungu kwa kweli wanao ushahidi wa ndani kuwa wao ni wapendwa wa Mungu, kwamba wana mawasiliano na Kristo, kwamba mioyo yao inachochewa kwa upendo motomoto kwake. Ukweli kwa ajili ya wakati huu unaaminiwa kwa imani hai. Wanaweza kusema kwa uhakika wote, “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. … ✍? Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” (2 Petro 1:16-19). Maisha ya ndani ya roho yatajidhihirisha yenyewe katika mwenendo wa nje. Hebu acha Neno la Mungu libebe ushuhuda wake badala ya mjumbe ambaye kupitia kwake Mungu ametuma ujumbe katika siku hizi za mwisho ili kuwaandaa watu waweze kusimama katika siku ya Bwana. ✍? “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!” (Isaya 52:7). Hekima ya wale wanaoitwa wasomi haiwezi kutegemewa, isipokuwa wamejifunza na kila siku wanajifunza masomo kutoka katika shule ya Kristo. Wanadamu, katika hekima yao ya kudhaniwa, wanaweza kupanga na kubuni nadharia na mifumo ya falsafa, lakini Bwana anawaita bure na wapumbavu. Bwana anasema, “Upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.”(1 Wakorintho 1:25). - Review and Herald, May 12, 1896. *MUNGU AKUBARIKI MTOTO WA MFALME*
Kesha la asubuhi: Kuzungukwa na ngao ya Mungu
*KESHA LA ASUBUHI*
*Alhamisi 03/05/2018*
*Kuzungukwa na Ngao ya Mungu*
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza. Zaburi 50:15.
?Majaribio yanapoinuka ambayo yanaoelekea kutoku-elezeka, hatupaswi kuruhusu amani yetu kuharibiwa. Hata tutendewe isivyo haki kiasi gani, hebu hasira kali isiinuke. Kwa kuendekeza roho ya kulipiza kisasi tunajidhuru sisi wenyewe. Tunaharibu imani yetu wenyewe kwa Mungu, na kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Kando yetu yuko Shahidi, Mjumbe wa mbinguni, ambaye atainua kwa ajili yetu bendera dhidi ya adui. Atatufungia ndani kwa miale angavu ya Jua la Haki. Shetani hawezi kupenya ndani ya miale hii. Hawezi kuipita ngao hii ya nuru takatifu.
?Wakati dunia ikisonga mbele katika uovu, asiwepo hata mmoja kati yetu atakayejidanganya kwamba hatutakuwa na magumu. Bali ni magumu haya haya ndiyo yanayotufikisha katika chumba cha uwapo wa Mungu. Tunaweza kutafuta ushauri wa Yeye asiye na kikomo katika hekima.
?Bwana anasema, “Ukaniite siku ya mateso” (Zaburi 50:15). Anatualika kumpelekea matatizo yetu pamoja na mahitaji ya lazima, pamoja na hitaji letu la msaada wa Mungu. Anatuambia omba haraka. Mara tu tatizo linapoinuka, tunapaswa kumtolea maombi yetu ya uaminifu na ya dhati. Kwa kuombaomba sana kwetu tunatoa ushahidi wa imani yetu kubwa kwa Mungu. Hisi ya uhitaji wetu hutuongoza kuomba kwa bidii, na Baba yetu wa Mbinguni anaguswa na kusihi kwetu. Mara nyingi wale wanaoshutumiwa au kuteswa kwa ajili ya imani yao wanajaribiwa kufikiri kwamba wameachwa na Mungu. Katika macho ya wanadamu wako upande wa wachache. Katika mwonekano wote adui zao wanaonekana kushinda juu yao. Lakini hebu na wasikiuke dhamiri yao. Yeye aliyeteseka kwa niaba yao, na kubeba huzuni na mateso yao, hajawaacha.
?Watoto wa Mungu hawajaachwa peke yao na kuwa bila ulinzi. Maombi hugusa mkono wa Mwenyezi. Maombi “hushinda milki za wafalme, kufunga vinywa vya simba, kuzima nguvu ya moto” – Tutaelewa kinachomaanishwa pale tutakaposikia taarifa za wafia dini ambao walikufa kwa ajili ya imani yao- “walikimbiza majeshi ya wageni” (Waebrania 11:33, 34). – Christ’s Object Lessons, uk. 171, 172.
*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI*
Kesha la asubuhi: Kuweka msingi thabiti
*KESHA LA ASUBUHI*
_JUMAPILI APRILI 29, 2018_
? Sauti ya Mungu inanena nasi kupitia katika Neno lake na zipo sauti nyingi tutakazozisikia; lakini Kristo amesema tuwe macho dhidi ya wale watakaosema, Kristo yupo hapa au Kristo yuko kule. Sasa, tutajuaje kwamba hawana ukweli, kama tusipoleta kila kitu kwenye Maandiko? Kristo ametuonya kuwa macho na manabii wa uongo ambao watatujia katika jina lake, wakisema kwamba wao ni Kristo.
? Sasa, ikiwa utakuwa katika mtazamo kwamba sio muhimu kwenu kuelewa Maandiko ninyi wenyewe, mtakuwa hatarini kupotezwa na mafundisho haya. Kristo amesema kwamba kutakuwa na kundi ambalo siku ile ya malipo hukumuni litasema, “Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Lakini Kristo atasema, “Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:22, 23)…
? Muda unakuja ambapo Shetani atafanya miujiza mbele za macho yenu, akidai kwamba ndiye Kristo; na kama miguu yako siyo imara kwenye ukweli wa Mungu, utapelekwa mbali kutoka kwenye msingi wako. Usalama wako pekee ni kuchunguza ukweli ili kupata hazina zilizofichwa. Chimbua ukweli kama mtu achimbaye hazina ardhini nawe wasilisha Neno la Mungu, Biblia, mbele za Baba wa mbinguni, na kusema, Niangazie; nifundishe kile kilicho kweli.
? Roho wake Mtakatifu atakapowajia mioyoni mwenu, ili kuweka mguso wa ukweli nafsini mwenu, haitakuwa rahisi kwenu kuuachia. Mmepata uzoefu huo katika kuyachunguza Maandiko, kiasi kwamba kila sehemu imethibitishwa. Na ni muhimu kwamba mdumu kuchunguza Maandiko. Inakupasa uhifadhi Neno la Mungu moyoni; kwani mnaweza kutenganishwa na kuwekwa mahali ambapo hutakuwa na fursa nzuri ya kukutana na watoto wa Mungu. Hapo ndipo mtakapohitaji hazina za Neno la Mungu mioyoni mwenu na wakati upinzani utakapowajia ukiwazingira, mtahitaji kuleta kila kitu kwenye Maandiko. Review and Herald, Aprili 3, 1888.
*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*
Kesha la asubuhi: Kuweza Kubainisha Ukweli Kutoka Katika Uongo
*Kesha la Asubuhi* *Ijumaa : Tarehe 27/4/2018* *Kuweza Kubainisha Ukweli Kutoka Katika Uongo* ?Maana watu kama hao ni mitume wawawe uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 2 Wakorintho 11:13, 14.* ?Ukweli ni madhubuti na kupitia katika utii uwezo wake huwa unaubadili moyo uwe na sura ya Yesu. Ni ukweli kama ulivyo katika Yesu ambao unahuisha dhamiri na kubadilisha moyo; kwani moyoni huwa unaambatana na Roho Mtakatifu. Wapo wengi ambao, huku wakipungukiwa utambuzi wa kiroho, huchukua tu herufi za Neno, na kukuta kwamba haliambatani na Roho wa Mungu, kwamba halihuishi nafsi, halitakasi moyo. Mtu anaweza kunukuu kutoka Agano la Kale na Jipya, anaweza kujua amri na ahadi za Neno la Mungu; lakini Roho Mtakatifu asipouweka ukweli moyoni, akiangazia akili kwa nuru ya kimbingu, hakuna nafsi itakayouangukia Mwamba na kuvunjika; kwani ni wakala huyu wa kimbingu anayeunganisha nafsi na Mungu. ?Bila kuangaziwa na Roho wa Mungu, hatutaweza kuutambua ukweli toka katika uongo nasi tutaanguka chini ya majaribu stadi na udanganyifu ambao Shetani atauleta duniani. Tumekaribia kufungwa kwa pambano kati ya Mfalme wa nuru na mfalme wa giza na muda sio mrefu udanganyifu wa adui utazijaribu imani zetu, zionekane ni za namna gani. Shetani atafanya miujiza machoni pa mnyama na kudanganya “wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama” (Ufunuo 13:14). ?Lakini japo mfalme wa giza atafanya kazi kuifunika dunia kwa giza, na kwa giza nene kabila za watu, Bwana atadhihirisha uwezo wake wa kuongoa. Sharti kazi ikamilishwe duniani inayofanana na ile iliyofanyika wakati wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika siku zile za wanafunzi wa awali, walipomhubiri Yesu, Yeye aliyesulubiwa. Wengi wataongolewa kwa siku; kwani ujumbe utaenda kwa nguvu. Ndipo itakaposemwa: “Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu” (1 Wathesalonike 1:5). Ni Roho Mtakatifu anayewavuta watu kwa Kristo; kwani huwa anachukua mambo ya Mungu na kumwonesha mwenye dhambi. Yesu alisema: “Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari” (Yohana 16:14). – Review and Herald, Nov. 29, 1892.
Kesha la asubuhi: Kuweza kutambua nadharia za uongo
KESHA LA ASUBUHI ALHAMISI 26/04/2018 *_KUWEZA KUTAMBUA NADHARIA ZA UONGO_* ? *Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Yuda 3.* ✍?Yuda analeta ujumbe huu ili kulinda waumini dhidi ya mivuto inayodanganya ya walimu wa uongo, watu wenye mfano wa utauwa lakini wasio viongozi salama. Katika siku hizi za mwisho, walimu wa uongo watainuka na kuwa watendaji wenye ari. ✍?Nadharia za naomba zote zitawasilishwa ili kupotosha akili za wanaume na wanawake kutoka kwenye ukweli unaoonesha kile tunachoweza kukisimamia bila wasiwasi wakati huu, huku Shetani akifanyia kazi kwa nguvu washika dini, akiwaongoza kuwa na mfano wa kuwa wenye haki, lakini wakishindwa kujiweka chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. ✍?Mafundisho ya uongo yatachanganywa na kila hatua ya uzoefu na kutetewa na bidii ya kishetani ili kushikilia akili ya kila mtu ambaye hana mzizi na msimamo katika ujuzi kamili wa kanuni takatifu za Neno. ✍?Katikati yetu kabisa watainuka walimu wa uongo, watakaosikiliza roho zinazodanganya ambazo chanzo cha mafundisho yake ni Shetani. Walimu hawa watavuta wanafunzi wawafuate. Wakijipenyeza bila kuonekana, watatumia maneno ya kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa na kufanya mawasilisho yasiyo sahihi kwa ustadi huku wakitumia mbinu za udanganyifu. ✍?Tumaini la pekee la makanisa yetu ni kudumu kuwa macho. Wale wenye msimamo mzuri kwenye ukweli wa Neno, wale wanaojaribu kila kitu kwa “BWANA asema hivi” wako salama. Roho Mtakatifu atawaongoza wale wanaothamini hekima ya Mungu kuliko mafumbo yanayodanganya ya mawakala wa kishetani. ✍?Hebu na pawepo kuomba kwingi, sio katika mtazamo wa kibinadamu bali chini ya uvuvio wa upendo wa ile kweli kama ilivyo katika Kristo Yesu. Familia zinazoamini ukweli yapasa zinene maneno ya hekima na akili – maneno yatakayowajia kama matokeo ya kuyachunguza Maandiko. ??♂ ```Huu ndio muda wetu wa kutahiniwa na kujaribiwa. Sasa ndio wakati ambapo washiriki wa kila familia inayoamini ni lazima wafunge midomo dhidi ya kunena maneno ya kushtaki ndugu zao. Hebu na wanene maneno yanayoleta ujasiri na kuimarisha imani itendayo kazi kwa upendo na kusafisha mioyo. – Kress Collection, uk. 5.``` *MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*
Kesha la asubuhi: Kutotumainia Maono Yetu
*KESHA LA ASUBUHI* _JUMATATU APRILI 23, 2018_ *Kutotumainia Maono Yetu* _Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako. Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako. Zaburi 119:15, 16._ ✍? Mungu amewapa watu ujuzi ulio muhimu kwa ajili ya wokovu kwenye Neno lake. Maandiko Matakatifu yapasa yakubaliwe kama udhihirisho wa mapenzi yake wenye mamlaka, usiokosea. Maandiko Matakatifu ni kiwango cha kupimia tabia, mdhihirishaji wa mafundisho, na kipimo cha uzoefu. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2 Timotheo 3:16, 17). ✍? Hata hivyo, ukweli kwamba Mungu amedhihirisha mapenzi yake kwa watu kupitia kwa Neno lake hakujaondoa umuhimu wa kuwepo kwa Roho Mtakatifu na uongozi wake. Kinyume chake, ahadi ya Roho ilitolewa na Mwokozi wetu, ili afungue Neno kwa watumishi wake, aangaze na kuweka mafundisho yake katika matumizi. Na kwa sababu ni Roho wa Mungu aliyevuvia Biblia, haiwezekani kwamba mafundisho ya Roho wakati wowote yawe kinyume na yale ya Neno. ✍? Roho hakuletwa – wala kamwe hawezi kutolewa – ili kuizidi Biblia; kwani Maandiko yanasema wazi kabisa kwamba Neno la Mungu ni kipimo ambacho kwa hicho mafundisho yote na uzoefu ni lazima yajaribiwe. Mtume Yohana anasema, “Msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani” (1 Yohana 4:1). Naye Isaya anatamka, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi” (Isaya 8:20). ✍? Kazi ya Roho Mtakatifu imetupiwa lawama kubwa kutokana na maovu ya kundi la watu ambao, huku wakidai kuwa na ujuzi juu yake, wanadai kutokuwa na hitaji zaidi la uongozi kutoka kwenye Neno la Mungu. Hawa wanaongozwa na fikra ambazo wanadai kuwa ni sauti ya Mungu moyoni. Lakini roho anayewatawala siyo Roho wa Mungu. Hali hii ya kufuatilia fikra hizi, huku Maandiko yakipuuziwa, inaweza tu kufikisha katika machafuko, udanganyifu na uharibifu. Hii inaendeleza tu mipango ya yule mwovu. ✍? Kwa sababu huduma ya Roho Mtakatifu ina umuhimu mkubwa kwa kanisa la Kristo, ni mbinu ya Shetani, kupitia kwa makosa ya wenye itikadi kali na misimamo mikali, kutweza kazi ya Roho na kusababisha watu wa Mungu kupuuzia chanzo hiki cha uwezo ambacho Bwana wetu mwenyewe ametupatia. – The Great Controversy, uk. vii, viii. *MUNGU AWABARIKI MNAPOTAFAKARI NENO*
ULAFI NA KUTOKUWA NA KIASI
ULAFI NA KUTOKUWA NA KIASI: Ulafi na kutokuwa na kiasi ndiyo msingi wa anguko kuu la upotovu wa maadili katika ulimwengu wetu. Shetani analifahamu hili na daima huwajaribu wanaume na wanawake waendeleze ladha ya kionjo kwa gharama ya afya nahai wenyewe. Kula, kunywa na kuvaa yamefanywa kuwa lengo la maisha kwa ulimwengu. Hali ya mambo imekuwa sawa naile iliyokuwa kabla ya gharika, na hali hii ya ubadhirifu ni moja ya ushahidi bayana Wa ukaribu Wa kufungwa kwa historian ya Dunia hii. Tunajua kwamba Bwana anakuja mapema sana. Ulimwengu unaharakisha kuwa kama ulivyokuwa katika siku za Nuhu. Umejikita kwenye kuendekeza ubinafsi. Kula na kunywa hufanywa kupita kiasi. Watu wanakunywa Vileo vyenye sumu ambayo huwafanya kuwa wehu. Kitabu cha matukio ya siku za mwisho, UK, 21. **Nimeitowa kwa rafiki yangu Facebook**
Kesha la asubuhi: Kutokuongozwa kwa hisia
KESHA LA ASUBUHI JUMAPILI 22/04/2018 *_KUTOKUONGOZWA KWA HISIA_* ? *Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu. Zaburi 119:105.* ✍?Utakaso sio hali ya hisia ya furaha inayotawala kwa muda mfupi, sio kazi ya mara moja, bali kazi ya maisha yote. Yeyote akidai kwamba Bwana amemtakasa na kumfanya kuwa mtakatifu, uthibitisho wa dai lake la kuwa na hiyo baraka utaonekana kwenye matunda ya upole, subira, uvumilivu, ukweli na upendo. ✍? Ikiwa baraka ambayo wale wanaodai kuwa wametakaswa inawaongoza kutegemea namna fulani ya mhemko, nao wanasema kwamba hakuna hitaji la kuchunguza Maandiko ili wapate kujua mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa, basi, hiyo baraka inayotajwa ni ya bandia, kwani inawaongoza wale walio nayo kuthamini mihemko na matamanio yasiyo takaswa na kufunga masikio yao dhidi ya sauti ya Mungu katika Neno lake. ✍?Kwa nini wale wanaodai kuwa wamekuwa na udhihirisho wa pekee wa Roho, na ushuhuda kwamba dhambi zao zimesamehewa zote, wahitimishe kwamba wanaweza kuiweka Biblia pembeni na kuanzia hapo watembee peke yao? Tunapowauliza wale wanaodai kupata utakaso wa ghafla, ikiwa wanayachunguza Maandiko kama Yesu alivyowaambia wafanye, ✍?kuona kama hakuna ukweli wa ziada kwa ajili yao kuukubali, huwa wanajibu, “Mungu huwa anatufahamisha mapenzi yake moja kwa moja katika ishara maalum na mafunuo nasi tunaweza kuiweka Biblia pembeni.” ✍?Wapo maelfu wanaodanganywa kwa kutumainia mihemko fulani maalum na kutupilia mbali Neno la Mungu. Hawa hawajengi kwenye msingi ambao ndio pekee ulio salama na wa hakika – Neno la Mungu. Dini inayoelekezwa kwa viumbe wenye akili itaonesha vithibitisho vya kimantiki vinavyoonesha uhalisia wake, kwani kutakuwa na matokeo dhahiri moyoni na kwenye tabia. Neema ya Kristo itadhihirishwa kwenye mwenendo wao wa kila siku. ✍?Bila wasiwasi tunaweza kuwahoji wale wanaodai kutakaswa, “Matunda ya Roho yanaonekana maishani mwako? Je, unadhihirisha upole na unyenyekevu wa Kristo na kufunua ukweli kwamba unajifunza kila siku kwenye shule ya Kristo, ukijenga maisha yako kulingana na mfano wa maisha yake yasiyo na ubinafsi? ??♂```Ushuhuda bora zaidi ambao yeyote kati yetu anaweza kuwa nao juu ya uhusiano wetu na Mungu wa mbinguni ni kwamba tunazishika amri zake. ??♂ Uthibitisho bora zaidi wa imani katika Kristo ni hali ya kutojitumainia nafsi na kumtegemea Mungu. Uthibitisho pekee wa kuaminika wa sisi kuwa katika Kristo ni kuiakisi sura yake. Kadiri tunavyofanya hivi, tunathibitisha kwamba tunatakaswa kwa njia ya ukweli, kwani ukweli unaoneshwa katika maisha yetu ya kila siku. – Signs of the Times, Feb. 28, 1895.``` *MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI*
Kesha la asubuhi: Kuongozwa kwa Njia ya Ushuhuda Ulioandikwa
*Kesha la Asubuhi* *Alhamisi, Tarehe 19/4/2018* *Kuongozwa kwa Njia ya Ushuhuda Ulioandikwa* ▶Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi. Isaya 8:20. ▶Daima Roho Mtakatifu anaongoza kwenye Neno lililoandikwa na huwa anavuta usikivu katika suala la kiwango kikuu cha maadili cha uadilifu. Kuheshimiwa na Mungu kwa namna hiyo kwa kupata fursa hii ya pekee kushuhudia ukweli ni jambo la ajabu. Kristo aliwaambia wanafunzi wake mara kabla ya kupaa juu na wingu la malaika kumpokea na kumwondoa machoni pao, “Mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Matendo 1:8). Walifanywa wafae kumshuhudia Kristo kutokana na karama ya kimbingu ya Roho Mtakatifu. ▶Natamani kuwasisitizia ukweli kwamba wale ambao Yesu anakaa mioyoni mwao kwa imani kwa kweli wamempokea Roho Mtakatifu. Kila mtu anayempokea Yesu kama Mwokozi wake binafsi kwa uhakika pia anampokea Roho Mtakatifu kuwa Mshauri, Mtakasaji, Kiongozi na Shahidi wake. Kadiri muumini anavyotembea kwa karibu na Mungu, ndivyo ushuhuda wake unavyozidi kuwa wazi na kama matokeo yaliyo ya hakika, ndivyo mvuto wa ushuhuda wake utakavyokuwa wenye nguvu zaidi kwa wengine kuhusu upendo wa Mwokozi; ndivyo atakavyozidi kuonesha uthibitisho kwamba anathamini Neno la Mungu. Hiki ndicho chakula chake, ndicho kinywaji chake, kwa ajili ya kuridhisha nafsi iliyo na kiu. Anathamini fursa hii ya pekee ya kujifunza mapenzi ya Mungu kutoka katika Neno lake. ?Baadhi ya watu wanaodai kuwa waumini wameweka pembeni, wamegeukia mbali na Neno la Mungu. Wameipuuzia Biblia, Mwongozo ulio wa ajabu, kipimo cha kweli cha mawazo yote na wanadai kwamba wanaye Roho anayewafundisha, kwamba hili linafanya suala la kuchunguza Maandiko lisiwe la muhimu. Wote wa namna hii wanasikiliza hila za Shetani, kwani Roho na Neno wanakubaliana. Maandiko yanasema, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Yeye ambaye ukweli unamweka huru ndiye mtu ambaye yuko huru kweli. – Manuscript Releases, vol. 14, uk. 70, 71.
Kesha la asubuhi: KUTAKASWA KWA NJIA YA NENO
KESHA LA ASUBUHI JUMATANO 18 Apr 2018 *_KUTAKASWA kWA NJIA YA NENO_* ? *Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Yohana 17:17.* ✍?Mzigo wa ombi la Yesu ulikuwa kwamba wale waliomwamini Yeye waweze kulindwa dhidi ya uovu wa dunia na kutakaswa kwa njia ya ile kweli. Yeye huwa hatuachi katika hali ya kubuni kusiko na uhakika kama ukweli ni nini, bali huongezea, “Neno lako ndiyo kweli.” ✍? Neno la Mungu ni njia ambayo kwayo utakaso wetu ni lazima ukamilishwe. Kwa hiyo, ni jambo la muhimu sana, kwamba tujifahamishe maelekezo matakatifu ya Biblia. Ni jambo la muhimu kwetu kuelewa maneno ya uzima kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa awali kufahamishwa kuhusu mpango wa wokovu. ✍?Hatutakuwa na udhuru ikiwa, kutokana na uzembe wetu wenyewe, hatutajua madai ya Neno la Mungu. Mungu ametupatia Neno lake, udhihirisho wa mapenzi yake naye amewaahidi Roho Mtakatifu wale wanaomwomba, ili awaongoze kwenye kweli yote; na kila nafsi ambayo kwa uaminifu inatamani kufanya mapenzi ya Mungu itayajua mafundisho. ✍?Dunia imejazwa na mafundisho ya uongo; na tusipochunguza Maandiko kwa ajili yetu wenyewe kwa makusudi, tutakubali makosa yake kana kwamba ndio ukweli, tutakubali mila zake na kudanganya mioyo yetu wenyewe. ✍? Mafundisho na desturi za dunia vinatofautiana na ukweli wa Mungu. Wale wanaokusudia kugeuka kutoka katika kuitumikia dunia ili wamtumikie Mungu watahitaji msaada wa kimbingu. Itawapasa kukaza nyuso zao kama chuma kuelekea Sayuni. Watahisi upinzani wa dunia, mwili na mwovu, nao itawapasa waende kinyume cha roho na mivuto ya dunia. ✍?Tangu nyakati Mwana wa Mungu alipokabiliana na chuki zisizo na sababu na majivuno na hali ya kutokuamini ya watu, hakujawa na badiliko katika mtazamo wa dunia kwa dini ya Yesu. Watumishi wa Kristo ni lazima wakutane na roho ile ile ya upinzani na shutuma na ni lazima kwenda “nje ya kambi, tukichukua shutumu lake” (Waebrania 13:13). ??♂```Utume wa Yesu ulidhihirishwa kwa miujiza ambayo haikuwa na mashaka. Mafundisho yake yaliwashangaza watu. Mafundisho yake hayakuwa lugha za kitaalamu zilizokinzana za waandishi, zilizokuwa zimejawa na imani za mafumbo, ambazo zilikuwa na mizigo ya mifumo ya kipuuzi na ulazimishaji usio na maana; ??♂ lakini ni mfumo wa ile kweli ambao ndio uliokutana na mahitaji ya moyo. Mafundisho yake yalikuwa wazi, bayana na yenye upana. Ukweli halisi aliousema ulikuwa na uwezo wa kusadikisha, nao ulivutia usikivu wa watu. – Review and Herald, Feb. 7, 1888.``` *MUNGU AWABARIKI NYOTE MNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*
Kesha la asubuhi: Kufurahi katika neno
*Kesha la asubuhi* _Jumanne Aprili 17, 2018_ *_Kufurahi Katika neno_* _Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi. Yeremia 15:16._ ? Katika kutekeleza dini ya Biblia, kuna hitaji la subira, uungwana, kujikana nafsi na kujinyima. Lakini, kama Neno la Mungu litafanywa kuwa kanuni inayodumu maishani mwetu, kila linachotwambia inatupasa kufanya, kila neno, kila tendo lililo dogo, litadhihirisha kuwa sisi ni raia wa Yesu Kristo, kwamba hata mawazo yetu yamewekwa kwenye kifungo chake. Neno la Mungu likipokelewa moyoni, litaondoa nafsini hali ya kujitosheleza nafsi na kuitegemea nafsi. ? Maisha yetu yatakuwa nguvu kwa ajili ya kutenda mema, kwa sababu Roho Mtakatifu atajaza mioyo yetu kwa mambo ya Mungu. Dini ya Kristo itatekelezwa nasi; kwani nia zetu zipo katika upatanifu kamili na mapenzi ya Mungu. Baadhi ya wale wanaodai kuwa na dini ya kweli inasikitisha kwamba huwa wanapuuzia Kitabu kilicho Mwongozo utokao kwa Mungu ili kuelekeza kwenye njia ya mbinguni. Wanaweza kusoma Biblia, lakini kusoma tu Neno la Mungu, kama mtu asomaye maneno yaliyoandikwa kwa kalamu ya mwanadamu, kutampa mtu ujuzi wa juu juu tu. ? Kuuzungumza ukweli hakutatakasa wapokeaji. Wanaweza kudai kufanya kazi ya Mungu, wakati ambapo, kama Kristo angekuwa kati yao, sauti yake ingesikika, akisema, “Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu” (Mathayo 22:29). Watu wa namna hiyo hawataweza kujua kile dini ya kweli inachokimaanisha. ? Kristo alisema, “Maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima” (Yohana 6:63). Yeremia anashuhudia juu ya Neno la Mungu akisema, “Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu.” Kuna uponyaji wa kimbingu katika Neno la Mungu, ambao wale waitwao wenye hekima na busara hawawezi kuupata, lakini ambao unadhihirishwa kwa watoto. ? “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga” (Zaburi 119:130). Kama Neno hili litahifadhiwa moyoni, litakuwa ni hazina ya moyo, ambako vitatoka ndani yake vitu vipya na vya kale. Hatutaendelea kufurahia kufikiria mambo duni ya dunia, bali tutasema, “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu” (aya ya 105). – Review and Herald, Mei 4, Mei 4, 1897. _TAFAKARI NJEMA MWANA WA MUNGU_
Yes! Zari goes to church!
Regrann from @zarithebosslady – All my days are for God, but Sunday I go all out…. #Church – #regrann
Hayo ni maneno yake Zari Hassan the Bosslady kupitia Instagram page yake. I am happy for you Zari keep that spirit God is everything! I hope one day you will warship on Sabbath with me here in Houston or you want me to come to South Africa? I can ??…. Bwt, you look Amazing! ? Be blessed mama Tee ?❤
Kesha la asubuhi: Tukiwa na vyombo vitupu
KESHA LA ASUBUHI ALHAMISI 12-04-2018 *TUKIWA NA* *VYOMBO VITUPU.* ? *Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu. 2 Wakorintho 4:7.* ✍? _Swali hili limeulizwa, “Ni aina gani ya vyombo ambavyo Roho huvitumia?” Kristo anasema nini? – “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11:28-30). Ni aina gani ya vyombo vinavyofaa kwa ajili ya matumizi yake Bwana? – Vyombo vitupu. Tunapotoa kila uchafu moyoni, tunakuwa tayari kutumiwa._ ✍? _Je nafsi yetu tumeitoa? Je, tumeponywa kutokana na kupanga kibinafsi? Ah, natamani tungepunguza kuitumikia nafsi! Hebu Bwana asafishe watu wake, walimu na makanisa._ ✍? _Yeye ametoa kanuni iwe mwongozo kwa wote na katika hii hapatakiwi kuwa na namna yoyote ya kuiacha njia kizembe. Lakini huwa kumekuwa, na bado hili lipo, hali ya kuyumba kutoka kwenye kanuni za haki. Hali hii ya mambo itadumu kwa muda gani? Bwana atawezaje kututumia kama vyombo kwa ajili ya utumishi mtakatifu tusipoondoa vyote ndani yetu wenyewe na kutoa nafasi kwa ajili ya ya utendakazi wa Roho wake?_ ✍? _Mungu anawaita watu wake wamdhihirishe. Je, dunia itaonesha kanuni za uadilifu ambazo kanisa halishikilii? Tamaa binafsi za kuwa wa kwanza vitaendelea kuoneshwa na wafuasi wa Kristo? Kanuni zinazopendwa nao hazitawekwa kwenye msingi wa kweli, yaani Kristo Yesu? Ni vitu gani tutakavyoweka kwenye msingi, ili pasiendelee kuwa na uhasama, badala yake umoja, ndani ya kanisa?_ ✍? _Tutaweka kwenye msingi mbao, nyasi kavu au mabua? Je, badala yake si tulete vitu vya thamani - dhahabu, fedha, vito vya thamani? Hatutatofautisha kwa namna iliyo dhahiri kabisa kati ya makapi na ngano? Hatutatambua kwamba ni lazima tupokee Roho Mtakatifu mioyoni mwetu, kwamba anaweza kutuumba na kutengeneza maisha?_ ```Tunaishi nyakati za hatari. Kwa kumuogopa Mungu naweza kusema kwamba ufafanuzi wa kweli wa Maandiko ni wa muhimu kwa ajili ya maendeleo sahihi ya kimaadili kwa ajili ya tabia zetu.``` ```Mioyo na roho vinapokuwa vimefanyiwa kazi na Roho, nafsi inapokufa, ukweli una uwezo wa kudumu kupanuka na kuwa na maendeleo mapya. Ukweli unapoumba tabia zetu, utaonekana kuwa ukweli hasa. – Review and Herald, Feb. 28, 1899.``` *MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI*
Kesha la asubuhi: Kwa Mioyo Minyenyekevu
*Kesha la asubuhi* _Kwa Mioyo Minyenyekevu_ *Jumanne Aprili 10, 2018* Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu. Isaya 57:15. ? Wale wote watakaolijia Neno la Mungu ili kupata mwongozo, wakiwa na akili za unyenyekevu zenye kupenda kujua, wakidhamiria kujua masharti ya wokovu, wataelewa kile yanachosema Maandiko. Lakini wale wanaokuja katika uchunguzi wa Neno wakiwa na roho isiyokubaliwa nalo, watachukua kwenye uchunguzi mwelekeo ambao uchunguzi huo haukuuweka. Bwana hatanena na akili ambayo haijali. Huwa hapotezi maelekezo yake kwa mtu ambaye kwa kukusudia kabisa hana kicho na amechafuka. ? Lakini mjaribu huwa anaelekeza kila akili inayokubaliana na mapendekezo yake, naye yuko tayari kuifanya sheria takatifu ya Mungu kuwa kama vile haina maana. Inatupasa kunyenyekeza mioyo yetu, tena kwa uaminifu na kicho tuchunguze Neno la uzima; kwani moyo ulio mnyenyekevu na wenye toba ambao ndio tu uwezao kuiona nuru. Akili, moyo, nafsi, ni lazima viandaliwe kuipokea nuru. Ni lazima pawepo ukimya moyoni. Ni lazima mawazo yasalimishwe na kuwekwa kwenye kifungo cha Yesu Kristo. ? Hali ya kujivunia ujuaji ya nafsi na kujitosheleza nafsi lazima vikemewe mbele za Neno la Mungu. Bwana huwa ananena na moyo unaojinyenyekeza mbele zake. Kwenye madhabahu ya sala, kiti cha enzi cha neema kinapoguswa kwa imani, huwa tunapokea mwenge wa kimbingu kutoka mkononi mwa Mungu unaoangazia giza letu na kutusadikisha juu ya umuhimu wetu kiroho. ? Roho Mtakatifu huchukua mambo ya Mungu na kumfunulia yeye aliye mwaminifu katika kuitafuta hazina ya kimbingu. Tukikubali uongozi wake, yeye hutuongoza kwenye nuru yote. Tunapotazama utukufu wa Kristo, tunabadilishwa na kufanana naye. Tunakuwa na ile imani inayotenda kazi kutokana na upendo na kusafisha moyo. Mioyo yetu hufanywa upya tena, nasi tunafanywa kuwa tayari kumtii Mungu katika mambo yote. –Review and Herald. *MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MFALME*
Kesha la asubuhi: Kuchimba Ndani Zaidi Kwenye Machimbo
*KESHA LA ASUBUHI* *JUMATATU APRILI 9, 2018* *Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Matendo 17:11.* ?Ni sawa na sahihi kuisoma Biblia; lakini wajibu wako haukomei hapo; kwani inakupasa uchunguze kurasa zake wewe mwenyewe. Elimu ya Mungu haipasi ipatikane bila jitihada ya akili, bila maombi kwa ajili ya hekima ili upate kutenga nafaka ya kweli kutoka kwenye makapi ambayo watu na Shetani wamewasilisha mafundisho ya ile kweli visivyo. Shetani na muungano wake wa mawakala wa kibinadamu wamenuia kuchanganya makapi ya uongo na ngano ya ile kweli. Inatupasa tuchunguze kwa bidii hazina iliyofichwa na kutafuta hekima kutoka mbinguni ili tuweze kutenganisha uvumbuzi wa kibinadamu na maagizo ya Mungu. ? Roho Mtakatifu atamsaidia mtafutaji wa ukweli mkuu na wa thamani ambao unahusiana na mpango wa ukombozi. Ninawasisitizia wote ukweli kwamba kusoma Maandiko juu juu hakutoshi. Ni lazima tuchunguze na hii maana yake ni kutenda yale yote Neno linayomaanisha. Kama vile mchimbaji wa madini anavyochimbua ardhi ili kugundua mikanda yake ya dhahabu, wewe pia inakupasa uchunguze Neno la Mungu ili kupata hazina iliyofichika ambayo kwa muda mrefu Shetani amekuwa akitafuta kumficha mwanadamu. Bwana anasema, “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo” (Yohana 7:17). ? Neno la Mungu ni ukweli na nuru na yapasa liwe taa miguuni pako, kukuongoza katika kila hatua kwenye njia iendayo kwenye malango ya mji wa Mungu. Ni kwa sababu hii, Shetani amekuwa akiweka jitihada za hali ya juu kuzuia njia ambayo imewekwa kwa ajili ya waliokombolewa na Bwana kuipitia. Haipasi uingie kwenye Biblia na dhana zako na kufanya mitazamo yako kuwa kiini ambacho kwa hicho ukweli yapasa uzungukie. ? Inakupasa uweke pembeni fikra zako kwenye mlango wa uchunguzi nawe ukiwa na moyo mnyenyekevu, nafsi iliyofichwa katika Kristo, na maombi ya dhati, inakupasa utafute hekima kutoka kwa Mungu. Inakupasa ujisikie kwamba ni lazima ujue mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa, kwa sababu yanahusu ustawi wako binafsi, wa milele. Biblia ni mwongozo ambao kupitia kwa huo unaweza kujua njia ya kufikia uzima wa milele. Kupita mambo yote, inakupasa ujue mapenzi na njia za Bwana. – Fundamentals of Christian Education, uk. 307, 308. *TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*
Pastor Caleb Migombo: Tunapokuwa watoto, mawazo yetu na kufikiri kwetu vinapangiliwa kutokana na uzoefu wa maisha tunayoishi
Kwa kiasi fulani, wewe na mimi tumepangiliwa (programmed). Tunapokuwa watoto, mawazo yetu na kufikiri kwetu vinapangiliwa kutokana na uzoefu wa maisha tunayoishi. Mpangilio huo wa namna ya kufikiri na kuishi hutokea kwa kila mmoja wetu. Lakini kama vitu ambavyo vimewekwa katika ubongo wetu na kumbukumbu za vichwa vyetu ni vibaya au si vya kweli, basi matokeo yake tunaweza kupata matatizo baadaye katika Maisha.
Kwa maana hiyo basi, kufikiri kwetu na mioyo yetu vinahitaji kupangilia upya; tunahitaji kuweka vitu vipya vizuri na vya kweli pale palipokuwa vitu vibaya amabavyo vimeeota mizizi ndani yetu…Na hapo bila shaka yoyote tunapohitaji msaada wa Mungu. Katika neno lake Mungu anatupatia ukweli unaofaa kuchukua nafasi ya uongo ambao umekuwa ukiuamini sikuzote kuhusu wewe na maisha yako.
“Wewe ni wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; …” ISAYA 43:4 In a sense, you and I get programmed. When we are young, our minds are constantly being programmed by the experiences we have. This programming happens to all of us. But when the things that have been put into our memories are bad and untrue, we will have problems later in life.
In that case, we need to reprogram our mind and hearts; we need to replace the bad things that has taken root there with good and true things. And that is where God can help. In His word, He provides truths to replace the lies you have believed about yourself.
“Since You are precious and honored in my sight, …I love you”. ISAIAH 43:4
Kesha la asubuhi: Kujua yasiyo julikana
*KESHA LA ASUBUHI*
*JUMAPILI 8/4/2018*
*KUJUA YASIYO JULIKANA*
*_ Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 1 Wakorintho 2:11._*
?Ufunuo sio uumbaji au ugunduzi wa kitu kipya, bali dhihirisho la kile kilichokuwepo, ambacho hadi kilipofunuliwa, hakikuwa kikifahamika kwa wanadamu. Ukweli ulio mkuu na wa milele uliomo kwenye injili hufunuliwa kwa njia ya bidii katika kuchunguza na kujinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu. Mwalimu wa mbinguni huwa anaongoza akili ya mtafutaji wa ukweli aliye mnyenyekevu; na kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, ukweli wa Neno hujulikana kwake. Tena, hapawezi kuwa na njia iliyo wazi na stadi zaidi ya ujuzi kuliko ya kuongozwa kwa namna hiyo. Ahadi ya Mwokozi ilikuwa, “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yohana 16:13). Ni kwa njia ya namna Roho Mtakatifu anavyopasha habari ndivyo tunavyowezeshwa kulielewa Neno la Mungu.
?Mtunga zaburi anaandika, Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. “Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, usiniache nipotee mbali na maagizo yako….Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zaburi 119:9-18).
?Tunaaswa kuutafuta ukweli kama kutafuta hazina iliyofichwa. Bwana huwa anafungua ufahamu wa mtafutaji wa dhati wa ukweli; naye Roho Mtakatifu anamwezesha kuelewa ukweli wa ufunuo. Hiki ndicho mtunga zaburi anachomaanisha anapoomba macho yake yafunguliwe apate kuona maajabu kutoka kwenye ile sheria. Nafsi inapoonea shauku ubora wa Yesu Kristo, moyo unawezeshwa kushika utukufu wa dunia iliyo bora. Tunaweza tu kuelewa ukweli wa Neno la Mungu kutokana na msaada wa Mwalimu wa mbinguni. Kwenye shule ya Kristo, huwa tunajifunza kuwa wapole na wanyenyekevu kwa sababu tumepewa ufahamu wa siri za utauwa.
? Yeye aliyelivuvia Neno ndiye mfafanuzi wa kweli wa Neno. Kristo alionesha kielelezo cha mafundisho yake kwa kuvutia usikivu wa wasikilizaji wake kuelekea kwenye kanuni za viumbe asili na kwenye vitu vinavyofahamika ambavyo waliviona kila siku na kuvishughulikia. Kwa namna hiyo aliongoza mioyo yao kutoka kwenye vile vilivyo vya asili kwenda kwa vile vya kiroho. – Sabbath School Worker, Dec. 1, 1909.
*MUNGU AKUBARIKI NA UWE NA SIKU NJEMA*
ULIMI UNA NGUVU YA AJABU…..! Our Tongues has enormous power….. !
Our Tongues has enormous power
Our tongues have enormous power-both for good and for evil. Indeed, with our tongue we can build healthy relationships, and with it we can destroy people’s lives…including our own. How do you use your own tongue?
The Apostle James put it this way: “The tongue also is a fire, a world of evil among the parts of the body…with the tongue we praise our Lord and father, and with it we curse men, who have been made in God’s likeness” (James 3:6,9).
Commit your tongue to God. Beyond that, commit your whole inner being to Christ, and ask Him to cleanse you of anger and hate, and fill you instead with His love and patience.
A gentle answer turns away wrath, but harsh word stirs up anger. Proverbs 15:1
ULIMI UNA NGUVU YA AJABU
Hakuna kiungo cha mwili kilicho na nguvu ya kujenga au kubomoa mahusiano yetu kama Ulimi…Hakika ndimi zetu zina nguvu ya ajabu – ya kutenda mema au mabaya. Kwa kutumia ulimi (maneno yetu) tunaweza kutengeneza mahusiano mazuri au kuharibu maisha ya watu wengine -na kuua mahusiano yetu wenyewe. Je Unautumiaje Ulimi wako?
Yakobo katika waraka wake anauelezea Ulimi hivi: “Ulimi nao ni kiungo kidogo sana lakini hujivunia mambo makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! Ulimi pia ni kama moto. Ulimi ni ulimwengu wa uovu kati ya viungo vyetu. Humchafua mtu nafsi nzima na kuwasha moto maisha yake yote, nao ulimi huwashwa moto wa kuzimu… Kwa kutumia ulimi tunamsifu Bwana na Baba yetu na kwa ulimi huo huo tunawalaani watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa hicho hicho hutoka sifa na laana. Ndugu zangu, haipaswi kuwa hivyo. [Yakobo 3: 5-6, 9-10]
Usalimishe Ulimi wako kwa Mungu. Zaidi ya hapo salimisha maisha yako yote na moyo wako kwa Kristo, na muombe akutakase na kukuondolea hasira, chuki, na roho ya kisasi — badala yake akujaze upendo wake na uvumilivu.
“Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu” [Mithali 15:1].
***Imeandikwa na Pastor Caleb Migombo***