KESHA LA ASUBUHI IJUMA 6/4/2018 _KUTAFUTA HAZINA_ ✍*Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. Mathayo 13:44.*Kwa kiasi kikubwa, katika siku zetu hizi, kanisa limekuwa likiridhishwa na ukweli wa ufunuo unaoonekana juu juu, ambao umefanywa kuwa wazi na rahisi kueleweka kiasi ambacho wengi wamedhani huu umeshaeleza yote yaliyokuwa muhimu, na katika kuukubali wameridhika. Lakini Roho Mtakatifu, anapotenda kazi moyoni, hatauruhusu utulie katika uvivu. ✍Huwa anaamsha shauku ya dhati kwa ajili ya ukweli usiochafuliwa kwa makosa na mafundisho ya uongo. Ukweli wa mbinguni utamtuza mtafutaji wa kweli. Moyo ambao una shauku ya kweli ya kujua kweli ni nini, hauwezi kuridhika katika uvivu. ✍?Ufalme wa mbinguni umefananishwa na hazina iliyofichwa shambani, “ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.” Anainunua ili apate kuifanyia kazi, analima kila sehemu yake na kuchukua vile vilivyo katika hazina yake. Kuongoza utafiti huu na kuutuza ni huduma ifanywayo na Roho Mtakatifu. ✍?Mtafiti, anapokuwa akililima shamba anakutana na mkondo wa madini ya thamani ambayo anajaribu kukadiria thamani yake, naye hudidimiza mtarimbo chini zaidi, kwa ajili ya hazina zaidi yenye thamani. Kwa namna hiyo tabaka kubwa zaidi la madini hugunduliwa. Maeneo ya dhahabu ardhini hayakusokotana na mikanda ya mawe ya thamani kama lilivyo shamba la ufunuo lenye mikanda inayodhihirisha utajiri wa Kristo usiochunguzika. ??♂ ```Ni shauku ya Bwana kwamba kila mmoja wa watoto wake wanaoamini awe tajiri katika imani; nalo hili ni tunda la utendaji wa Roho Mtakatifu moyoni. Kutokea moyoni, Roho hutenda kazi akielekea nje, akiendeleza tabia ambayo Mungu ataikubali.``` ??♂ ``` Shamba la hazina za ile kweli ambazo Kristo aliongeza kwenye milki ya imani ili wanafunzi wapate kujitwalia ni kubwa kiasi cha ajabu! Tunahitaji imani kubwa zaidi kama tunahitaji kuwa na ufahamu bora wa Neno. Kizuizi kikubwa zaidi katika upokeaji wetu wa nuru ya mbinguni ni kwamba hatutegemei ufanisi wa Roho Mtakatifu. – Ellen G. White 1888 Materials, uk. 1537, 1538.``` *MUNGU AWABARIKI MUWE NA SIKU NJEMA.*KESHA LA ASUBUHI
Category Archives: Spirituality
Kesha la asubuhi: Kwenda kwenye chanzo cha Nuru
*KESHA,,, LA,, ASUBUHI "* Jumatano. *04/04/2018* *"Kwenda Kwenye Chanzo cha Nuru ?"* ?... ? *"""Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga. Zaburi 119:130."""* ✍??...Nyakati fulani imekuwa kwamba watu wenye uwezo mkubwa kiakili, walioendelea kielimu na kwa ustaarabu, hushindwa kuelewa aya fulani za Maandiko, wakati wale wengine ambao hawajafunzwa, hupata maana, wakipata nguvu na faraja katika kile ambacho walioelimika wanasema ni fumbo au kukiacha kama kisicho cha muhimu. Kwanini iwe hivi? Nimeelezwa kwamba kundi hili la wasio na elimu kubwa hawategemei ufahamu wao. Hawa huenda kwenye Chanzo cha nuru, Yeye ambaye ndiye aliyevuvia Maandiko na kwa unyenyekevu wa moyo humwomba Mungu hekima na huwa wanaipokea. Yapo machimbo ya ukweli ambayo bado hayajagunduliwa na mwenye kutafuta kwa dhati. ✍??......Kristo aliwakilisha ukweli kama hazina iliyofichwa shambani. Haikai juu tu kwenye uso wa nchi; ni lazima tuichimbue. Hata hivyo, mafanikio yetu katika kuipata, hayategemei sana uwezo wetu wa kiakili bali unyenyekevu wa moyo na imani inayoshikilia msaada wa Mungu. ✍??..Bila uongozi wa Roho Mtakatifu itaendelea kuwa rahisi kwetu kulazimisha Maandiko au kuyatafsiri vibaya. Upo usomaji mwingi wa Biblia usio na faida na mara nyingi hujeruhi kwa hakika. Pale Neno la Mungu linapofunguliwa bila kicho na wala ombi; wakati mawazo na matashi yasipoelekezwa kwa Mungu au katika upatanifu na mapenzi yake, moyo huwa katika giza la mashaka; na katika somo lile lile la Biblia, hali ya kuwa na shaka huimarika. Adui hutawala mawazo na hupendekeza fasiri zisizo sahihi. ✍??.....Wakati wowote watu wasipotafuta, kwa neno na kwa tendo, kuwa katika upatanifu na Mungu, hata wawe wameelimika kiasi gani, inawezekana sana kwa hao kukosea katika uelewa wa Maandiko na sio salama kutumainia maelezo yao. Tunapotaka kutenda mapenzi ya Mungu kweli, Roho Mtakatifu huchukua kanuni za Neno lake na kuzifanya kuwa kanuni za maisha, huku akiziandika kwenye bamba za moyo. Na ni wale tu wanaoifuata nuru ambayo imekwisha tolewa wanaoweza kutumaini kupokea nuru ya ziada ya Roho. – Testimonies, vol. 5, uk. 704, 705.
*”TAFAKARI,,, NJEMA,,, “*
Kesha la asubuhi: UTAKATIFU
*Kesha la Asubuhi* *J, tano Tarehe 28/3/2018* *UTAKATIFU* ?? *Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. Waebrania* *12:14* ??Tangu milele, Mungu alichagua watu wawe watakatifu. “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu” (1 Wathesalonike 4:3). Mwangwi wa sauti yake unatujia, daima ukisema, “Utakatifu zaidi, Utakatifu zaidi.” Na jibu letu daima yafaa liwe, “Ndiyo Bwana, watakatifu.” ??Hakuna mtu anayepokea utakatifu kama haki ya kuzaliwa, au kama zawadi kutoka mwanadamu mwingine yeyote. Utakatifu ni zawadi ya Mungu kupitia kwa Kristo. Wale wanaompokea Mwokozi wanakuwa wana wa Mungu. Hawa ndio watoto wake wa kiroho, waliozaliwa upya, waliofanywa upya katika haki na utakatifu wa kweli. Nia zao zimebadilishwa. Wanaona mambo halisi ya milele kwa maono yaliyo wazi zaidi. Hawa wamefanywa kuwa sehemu ya familia ya Mungu nao wanapatanishwa na sura yake, wanabadilishwa na Roho wake kutoka utukufu hadi utukufu. Kutoka katika kufurahia hali ya kupenda nafsi katika viwango vya juu sana, wanafikia hatua ya kufurahia upendo wa juu kwa Mungu na kwa Kristo. “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo” (Warumi 5:1). Kuhesabiwa haki kunamaanisha msamaha. Kunamaanisha kwamba moyo, ukiwa umesafishwa na kuondolewa matendo yaletayo mauti, umeandaliwa kupokea baraka ya utakaso. Mungu ametuambia kile ambacho ni lazima tufanye ili tupokee baraka hii. “Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu” (Wafilipi 2:12-15). ??Upendo wa Mungu, ukihifadhiwa moyoni na kudhihirishwa katika maneno na matendo, utafanya sehemu kubwa ya kujenga na kuadilisha wanadamu kuliko jambo lingine lolote lile. Katika maisha ya Kristo, upendo huu uliweza kuonekana kikamilifu na bila upungufu. Msalabani pa Kristo, Mwokozi alifanya upatanisho kwa ajili ya jamii ya watu iliyokuwa imeanguka dhambini. Utakatifu ni tunda la kafara hii. Ni kwa sababu alikufa kwa ajili yetu ndiyo maana tunaahidiwa karama hii kuu. Hivyo ni shauku ya Kristo kutupatia karama hii. Ni shauku yake kwamba tuweze kuwa washirika wa tabia yake. Ni shauku yake kuokoa wale ambao kutokana na dhambi wamejitenga na Mungu. Yeye anawaita wachague huduma yake, wajitoe wenyewe kikamilifu kuwa chini ya utawala wake, wajifunze kutoka kwake namna ya kufanya mapenzi ya Mungu. – Signs of the Times, Des. 17, 1902. *MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Kesha la asubuhi: Ujasiri
```KESHA LA ASUBUHI``` *JUMATATU MACHI 26, 2018* *Ujasiri* _Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Waebrania 10:35._ ? Yohana anasema, “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:14, 15). Hebu tudumishe zaidi wazo hili kwa watu, ili mawazo yao yapate kupanuliwa, imani yao iongezeke. ? Hebu watiwe moyo kuomba kwa upana zaidi na kutegemea bila mashaka utajiri wa neema yake; kwani kupitia kwa Yesu tunaweza kuja kwenye chumba cha kuzungumza naye Aliye Juu. Kupitia kwa stahili zake tunayo fursa ya kumfikia Baba kupitia kwa Roho huyu mmoja. ? Laiti tungekuwa na uzoefu mkubwa zaidi katika maombi! Tunaweza kumjia Mungu kwa ujasiri, tukijua maana ya kuwepo kwa Roho Mtakatifu na nguvu yake. Tunaweza kuungama dhambi zetu na pale pale, huku tukiomba, tujue kwamba Yeye anasamehe makosa yetu, kwani ameahidi kusamehe. Ni lazima tuiweke imani katika matendo na kudhihirisha uaminifu wa kweli na unyenyekevu. ? Kamwe hatuwezi kufanya hivi bila neema ya Roho Mtakatifu. Ni lazima tulale chini miguuni pa Yesu na tusiendekeze ubinafsi, tusioneshe namna yoyote ya kuiinua nafsi, lakini tumtafute Bwana kwa namna iliyo sahili, tukimwomba Roho wake Mtakatifu kama mtoto mdogo aombavyo mkate kutoka kwa wazazi wake. Ni lazima tufanye sehemu yetu, tumchukue Kristo kama Mwokozi wetu binafsi, nasi, huku tukisimama chini ya msalaba wa Kalvari, “Tutazame na tuishi.” ? Mungu anajitengea watoto wake kwa ajili yake mwenyewe. Nao wanapounganika Naye, wanakuwa na nguvu pamoja na Mungu na kushinda. Kwa uwezo wetu hatuwezi kufanya lolote; bali kupitia kwa neema ya Roho wake Mtakatifu, tunapewa uzima na nuru, nayo nafsi hujazwa na shauku ya dhati na hamu ya Mungu, na ya utakatifu. Hapo ndipo Kristo anapotuongoza kwenye kiti cha enzi cha neema na kutuvisha kwa haki yake; kwani Bwana Mungu wa mbinguni anatupenda. ? Kuwa na wakaidi na wenye mashaka kwa makusudi ndiko kunakoweza kutufanya kuwa na mashaka kwamba moyo wake huwa unatuelekea sisi. Wakati Yesu, Mpatanishi wetu, anapotuombea mbinguni, Roho Mtakatifu huwa anafanya kazi ndani yetu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Mbingu zote huwa zinapendezwa na wokovu wa roho moja. Sasa, tunayo sababu gani ya kuwa na mashaka kwamba Bwana anatusaidia na atatusaidia? –Signs of the Times, Okt. 3, 1892. ```MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI UJUMBE WA LEO```
Kesha la asubuhi: Utii
*KESHA LA ASUBUHI* ```JUMAPILI MACHI 25, 2018``` *UTII* _Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. 1 Petro 1:14, 15._ ? Mungu anahitaji nini? Ukamilifu, ukamilifu usio na upungufu wowote. Lakini ikiwa tunataka kuwa wakamilifu, ni lazima tusiweke imani yetu katika nafsi. Kila siku ni lazima tujue na kuelewa kwamba haifai kuitumainia nafsi. Tunahitajika kushikilia ahadi za Mungu kwa imani thabiti. Tunahitajika kuomba kupewa Roho Mtakatifu huku tukitambua kikamilifu hali yetu ya kutojiweza. Kisha, Roho Mtakatifu akitenda kazi hatutaipa nafsi utukufu. ? Kwa uzuri, Roho Mtakatifu atauchukua moyo katika hifadhi yake, huku akiuletea mionzi angavu ya Jua la haki. Tutatunzwa na nguvu ya Mungu kwa njia ya imani. Tukiwa chini ya utawala wa Roho wa Mungu kila siku, tutakuwa watu wenye kuzishika amri. Tunaweza kuionesha dunia kwamba utii wa amri za Mungu unakuja na thawabu yake, hata katika maisha haya na katika maisha yajayo baraka za milele. ? Bila kujali kukiri kwetu imani, Bwana ambaye anapima matendo yetu, anaona jinsi tulivyopungua katika kumwakilisha Kristo. Ametangaza kwamba hali ya namna hiyo ya mambo haiwezi kumtukuza.Kuamua kukabidhi nafsi kwa Mungu kuna maana kubwa. Inamaanisha kwamba inatupasa tuishi na kutembea kwa imani, siyo kwa kuitumainia au kuitukuza nafsi, bali kumtazama Yesu kama Wakili wetu, kama mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu. ? Roho Mtakatifu atafanya kazi yake kwenye moyo uliotubu, lakini kamwe hatafanya kazi kwenye moyo unaoweka umuhimu katika nafsi, unaojitafutia haki yake. Katika hekima yake mwenyewe, mtu wa namna hiyo hujaribu kujirekebisha mwenyewe. Huwa anakuwa akiingilia kati ya nafsi na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu atafanya kazi kama nafsi haitaingilia kati. ? Tunaegemea wapi? Msaada wetu uko wapi? Neno la Mungu linatuambia: “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana 14:26). Roho Mtakatifu yuko tayari kushirikiana na wale wote watakaompokea na kufundishwa naYeye. Wale wote wanaoishikilia ile kweli na kutakaswa kupitia katika ile kweli huwa wanakuwa wameunganishwa vizuri na Kristo kiasi kwamba wanaweza kumwakilisha Yeye katika maneno na matendo. – Manuscript Releases, kit. 12, uk. 52, 53. *MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MFALME*
Kesha la asubuhi: Umaridadi wa nje
*KESHA LA ASUBUHI*
“`JUMAMOSI MACHI 24, 2018“`
*Umaridadi wa Nje*Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mithali 31:21, 22._
✍? Elimisha, elimisha, elimisha. Wazazi wanaopokea ile kweli yapasa wapatanishe mazoea na desturi zao na maelekezo ambayo Mungu ameyatoa. Ni shauku ya Mungu kwamba wote wakumbuke kwamba utumishi wa Mungu ni msafi na mtakatifu na kwamba wale wanaopokea ile kweli ni lazima wasafishwe katika mielekeo, tabia, mioyo, mazungumzo, katika mavazi, na nyumbani, ili malaika wa Mungu ambao hawawaoni, wapate kuja na kuhudumia wale watakaokuwa warithi wa wokovu.
✍? Wale wote wanaojiunga na kanisa sharti wadhihirishe badiliko la tabia inayoonesha kicho chao kwa mambo matakatifu. Sharti maisha yao yote yajengwe kulingana na uzuri wa Kristo Yesu. Wale wanaojiunga na kanisa yapasa wawe wanyenyekevu kiasi cha kutosha kupokea maelekezo katika maeneo ambayo hawajawa makini kwayo na ambayo wanaweza na ni lazima wabadilike katika hayo.
✍? Ni lazima waoneshe mvuto wa Kikristo. Wale wasiofanya mabadiliko katika maneno au mwenendo, katika namna yao ya kuvaa au katika nyumba zao, huwa wanaishi kwa ajili yao wenyewe na sio kwa ajili ya Kristo. Hawajaumbwa upya katika Kristo Yesu, hata kufikia usafi wa moyo na mazingira ya nje. Wakristo watatambuliwa kutokana na tunda wanalolionesha katika kazi ya matengenezo. Kila Mkristo wa kweli ataonesha kile ambacho ukweli wa injili umekifanya kwake. Yeye ambaye amefanywa kuwa mwana wa Mungu ni lazima awe na mazoea ya kutenda kwa unadhifu na usafi.
✍? Kila tendo, hata liwe dogo kiasi gani, lina mvuto wake. Bwana anatamani kumfanya kila mtu kuwa wakala ambaye kupitia kwake Kristo anaweza kudhihirisha Roho wake Mtakatifu. Kwa namna yoyote haipasi Wakristo wawe wazembe au wasiojali suala la mwonekano wao wa nje. Inapasa wawe maridadi, japo bila mapambo. Inapasa wawe wasafi ndani na nje. – Testimonies to Southern Africa, uk. 87.
*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI SOMO LA LEO*
Kesha la asubuhi: Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu
*KESHA LA ASUBUHI* ijumaa. *23/03/2018* *Usafi* ? *Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu. Mathayo 5:8.* ??. Mtu akiwa ameondolewa ubinafsi kabisa, wakati kila mungu wa uongo anapoondolewa kutoka moyoni, ombwe hujazwa kwa mtiririko wa Roho wa Kristo. Mtu wa namna hiyo huwa anayo imani itendayo kazi kwa upendo na kusafisha moyo kutokana na kila uchafu wa kimaadili na kiroho. Roho Mtakatifu, Mfariji, anaweza kufanya kazi moyoni, akiweka mvuto na kuongoza, kiasi cha mtu huyo kufurahia mambo ya kiroho. Mtu huyo anakuwa “aifuataye Roho” (Warumi 8:5), naye huyafikiri mambo ya Roho. Huyu anakuwa haweki tumaini katika nafsi; Kristo ndiye yote katika yote. Bila kukoma, ukweli unakuwa ukifunguliwa na Roho Mtakatifu; naye hupokea kwa upole neno linalopandikizwa na kumpa Bwana utukufu wote, akisema, “Mungu ametufunulia sisi kwa Roho” (1 Wakorintho 2:10). “Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu” (aya 12). ??. Roho anayefunua pia hutenda kazi ndani yake katika kutoa matunda ya haki. Kristo anakuwa ndani yake, “chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele” (Yohana 4:14). Yeye ni tawi la Mzabibu wa Kweli nalo huzaa vishada vilivyosheheni vya matunda kwa utukufu wa Mungu. Matunda yanayozaliwa yana tabia gani? “Tunda la Roho ni upendo.” Zingatia maneno haya – upendo, siyo chuki; ni furaha, siyo hali ya kutoridhika na kuomboleza; amani, siyo harara, fadhaa, majaribu yaliyotengenezwa. Ni “uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria” (Wagalatia 5:22, 23). ?? Wale wenye Roho huyu watakuwa watendakazi wenye bidii pamoja na Mungu; wajumbe wa mbinguni watashirikiana nao na wanakwenda wakiwa na uzito wa Roho mwenye ujumbe wa kweli ambao wanaubeba. Hawa wanakuwa tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa watu. Hawa wanakuwa wameadilishwa, wametakaswa, kupitia kwa utakaso wa Roho na imani ya ile kweli. Hawa hawajaleta kwenye hazina ya nafsi; kuni, majani, visiki, bali dhahabu, fedha na mawe ya thamani. Hawa hunena maneno yenye uzito wa maana na kutoka kwenye hazina za moyo huleta mambo safi na matakatifu kulingana na mfano wa Kristo. – Home Missionary, Nov. 1, 1893. *tafakari... Njema*""" . .
Kesha la asubuhi: UKARIMU
*KESHA LA ASUBUHI* _JUMATANO MACHI 21, 2018_ *Ukarimu* ```Maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. 2 Wakorintho 8:2.``` ? Ni pale tu makusudi ya Mkristo yanapotambulika kikamilifu na dhamiri inapoamshwa kwa ajili ya wajibu, ambapo nuru ya Mungu huweka mguso kwenye moyo na tabia, huo ubinafsi unashindwa na nia ya Kristo inadhihirishwa. Roho Mtakatifu, akifanya kazi mioyoni mwa watu na tabia zao, ataondolea mbali mielekeo yote ya tamaa, mielekeo ya kufanya mambo kwa udanganyifu. ? Mjumbe wa Bwana anapokuwa akiuleta ujumbe kanisani, Mungu ananena kwa watu, akiamsha dhamiri zao zione kwamba hawajaleta zaka kwa uaminifu kwa Bwana, na kwamba pale ambapo haikuonekana kuwa muda unaofaa kutoa, wameshindwa kumletea sadaka yao. Wametumia pesa iliyo mali ya Bwana kwa ajili yao wenyewe, katika kujenga majumba, katika kununua farasi, vyombo vya usafiri, au ardhi. Huwa wanafanya hili wakitumaini kupata mapato makubwa na kila mwaka udhuru wao ni huo huo. “Je, mwanadamu atamwibia Mungu?” (Malaki 3:8). Kwa kweli, amekuwa akilifanya hili mara nyingi, kwa sababu hajawa mtu wa kiroho, kuweza kuona mambo ya kiroho. ? Kwa wapenda dunia, wabinafsi, Bwana amekuwa akitenda nyakati fulani, kwa namna iliyo wazi kabisa. Akili zao ziliangazwa kwa Roho Mtakatifu, mioyo yao ikahisi mguso wake unaolainisha na kunyenyekeza. Kutokana na utambuzi wa wingi wa rehema na neema ya Mungu, walijisikia kuwa ni wajibu wao kuhimiza mpango wake, kuujenga ufalme wake. Walikumbuka sharti, “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi” (Mathayo 6:19, 20). ? Walijisikia kuwa na shauku ya kuwa na sehemu kwenye ufalme wa Mungu, nao wakaahidi kutoa pesa zao kwa ajili ya baadhi ya shughuli mbalimbali katika kazi ya Mungu. Ahadi hiyo haikutolewa kwa mwanadamu, bali kwa Mungu mbele za malaika zake, ambao walikuwa wakipita mioyoni mwa hawa watu wabinafsi, wapendao pesa. – Review and Herald, Mei 23, 1893. *MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MFALME*
Kesha la asubuhi: Upendano wa ndugu
*KESHA LA ASUBUHI* ```JUMANNE MACHI 20, 2018``` *Upendano wa Ndugu* Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu. Warumi 12:10. ✍? Roho Mtakatifu anapoingia kwenye mawazo ya mtu, malalamiko na mashtaka madogo madogo baina ya mtu na watu wenzake yatatupiliwa mbali. Mionzi angavu ya Jua la Haki itang’aa kwenye vyumba vya moyo na akili. Katika ibada yetu kwa Mungu hakutakuwa na kutofautisha kati ya matajiri na maskini, weupe na weusi. Ubaguzi wote utayeyuka. Tunapomkaribia Mungu, itakuwa kama undugu mmoja. Sisi sote ni wasafiri na wageni, tunaoelekea kwenye nchi iliyo bora, ile ya mbinguni. Pale, kiburi chote, mashtaka yote, hali yote ya kujidanganya, vitakuwa vimekoma milele. Kila namna ya kificho kitaondolewa nasi “tutamwona kama alivyo” (1 Yohana 3:2). Pale nyimbo zetu zitachukua mada yenye kutia moyo nazo sifa na shukrani zitapanda kwake Mungu. – Review and Herald, Okt. 24, 1899. ✍? Bwana Yesu alikuja katika dunia yetu ili aokoe wanaume na wanawake wa mataifa yote… Yesu alikuja kueneza nuru kwa ulimwengu wote. Mwanzoni mwa huduma yake aliitamka nia yake: “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Luka 4:18, 19)… ✍? Jicho la Bwana li juu ya viumbe wake wote; anawapenda wote naye haweki tofauti kati ya weupe na weusi, isipokuwa kwamba Yeye huwa ana huruma maalumu kwa ajili ya wale walioitwa kuchukua mizigo mizito zaidi kuliko wengine. Wale wampendao Mungu na kumwamini Kristo kama Mkombozi wao, huku wakilazimika kukabiliana na majaribu na matatizo yanayokuwa njiani mwao, bado yawapasa wakubaliane na maisha kama yalivyo kwa moyo uliochangamka, wakikumbuka kwamba Mungu mbinguni anaona mambo haya, na kwa yale ambayo dunia inapuuzia kuwapa, Yeye atawalipa kwa fadhila zilizo bora zaidi. – Selected Messages, kit. 2, uk. 487, 488. *UBARIKIWE MWANA WA MFALME*
Kesha la hasubuhi: Umoja
KESHA LA ASUBUHI
JUMAPILI- MARCH 18, 2018
UMOJA
“Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” Yohana 17:20, 21.
▶Upatanifu na umoja unapokuwepo kati ya watu wenye tabia mbalimbali ni ushuhuda wenye nguvu zaidi uwezao kuonesha kwamba Mungu alimtuma Mwana Wake duniani kuokoa wenye dhambi. Ni fursa ya pekee ambayo tumepewa kudhihirisha hili. Lakini, ili tulifanye hili, ni lazima sisi wenyewe tujiweke chini ya agizo la Kristo. Ni lazima tabia zetu zitengenezwe kuwa katika upatanifu na tabia yake, nia zetu ni lazima zisalimishwe kwa nia Yake. Hapo tutatenda kazi pamoja bila hata wazo la kugombana.
▶Kudumu katika tofauti ndogo ndogo kutatufikisha katika kutenda yale yatakayoharibu ushirika wa Kikristo. Tusimruhusu adui apate nafasi dhidi yetu kwa namna hiyo. Hebu na tudumu kumkaribia Mungu na kukaribiana sisi kwa sisi. Ndipo tutakapokuwa kama miti ya haki, iliyopandwa na Bwana na kumwagiliwa na mto wa uzima. Nasi tutaweza kuzaa ajabu! Je, Kristo hakusema; “Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana” (Yohana 15:8)?
▶Moyo wa Mwokozi umeelekezwa kwa utimilifu wa kusudi la Mungu unaofanywa na wafuasi wake katika urefu wake na upana wake wote. Inawapasa wawe wamoja na Mungu, japo wawe wameenea duniani kote. Lakini Mungu hawezi kuwafanya kuwa wamoja katika Kristo wasipokuwa tayari kuchukua njia yake badala ya njia yao.
▶Sala ya Kristo itakapokuwa imeaminiwa kikamilifu, maelekezo yake yatakapokuwa yameingizwa katika maisha ya kila siku ya watu wa Mungu, umoja katika matendo utaonekana katika jamii zetu. Mtu atashikamanishwa na mwingine kwa kamba za dhahabu za upendo wa Kristo. Roho wa Mungu pekee ndiye awezaye kuleta umoja huu. Yeye aliyejitakasa mwenyewe, anaweza kutakasa wanafunzi wake. Wakiwa wameunganishwa naye, wataunganishwa kila mmoja na mwingine katika imani iliyo takatifu sana. Tunapopambana kwa ajili ya umoja huu kama ilivyo shauku ya Mungu kwamba tuutafute, utatujia. – Testimonies, kit cha 8, uk. 242,243.
My times are in Your hand!
*MORNING TEA ☕?*
SATURDAY, 17TH MARCH 2018
*ACCELERATE*
TODAY’S SCRIPTURE
*”My times are in Your hand…” (Psalm 31:15, NASB)*
*TODAY’S WORD*
One thing I’ve learned is that God doesn’t always work on our timetable. In fact, He rarely does. But in a single moment, God can change your life! All throughout Scripture, we see examples of how God was working behind the scenes and instantly turned things around for His people. Scripture tells us He is the same yesterday, today and forever which means He can instantly turn things around for you, too!
You may be going through some difficulty today, but be encouraged because your times are in God’s hands. He wants to accelerate things in your favor. He wants to take you further than you dreamed possible and work in your life in ways beyond what you have ever imagined.
Let this truth sink down into your heart today. Resist discouragement by speaking His Word over your future. Keep standing. Keep hoping; keep believing because He is working behind the scenes. He’s going to accelerate your times and lead you into the life of victory He has for you!
*A PRAYER FOR TODAY*
“Father, today I humbly come before You giving You all that I am. I trust that my times are in Your hands. I trust that You are working things out in my favor. I set my focus on You knowing that You are working things out for my good in Jesus’ name. Amen.”
KUWA NA SHUKRAN
KESHA LA ASUBUHI IJUMAA 16/03/2018 *KUWA NA SHUKRANI* ? _Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 1 Wathesalonike 5:18._ ✍?Kuna mashaka mengi sana yasiyo ya muhimu, wasiwasi mwingi kwenye akili za watu, juu ya mambo ambayo mtu hawezi kuyabadilisha. Bwana anatamani watoto wake wamtumainie Yeye kikamilifu. Bwana wetu ni Mungu mwenye haki na mwaminifu. Yapasa watoto wake watambue wema na haki yake katika mambo makubwa na madogo ya maisha. ✍?Wale wanaoendekeza roho ya wasiwasi na manung’uniko huwa wanakataa kutambua mkono wake unaoongoza. Wasiwasi usiohitajika ni jambo la kipumbavu; nalo hutuzuia tusisimame katika nafasi zetu halisi mbele za Mungu. ✍?Roho Mtakatifu anapotujia moyoni, hatutakuwa na hamu ya kulalamika na kunung’unika kwa sababu ya kutokuwa na kila kitu tunachokitaka; badala yake, tutampa Mungu shukrani inayotoka kwenye mioyo iliyojaa kwa sababu ya baraka tulizo nazo. Kati ya wafanyakazi wetu leo, lipo hitaji kubwa la kuwa na shukrani zaidi; na wasipofikia hatua ya kuwa na roho hii watakuwa hawajajiandaa kuwa na nafasi kwenye ufalme wa mbinguni. ✍?Kazi kubwa yapasa ifanyike kwa ajili ya kila mmoja wetu. Huwa tunaelewa kidogo sana kile Mungu anachokusudia kufanya kupitia kwetu. Inatupasa tujitahidi kutambua upana wa mipango yake na tufaidike kutokana na kila fundisho ambalo Yeye amekuwa akijaribu kutufundisha. ``` ??♀Hali ya kudhamiria mabaya ipo kwa wingi mawazoni mwa mioyo na akili zetu tunapojitahidi kuenenda kwa namna yetu wenyewe kinyume na sheria ya wema. Hapa ndipo wengi wanaposhindwa. Huwa hatujengi welekeo wa wema; tunataka kila kitu kitujie kwa namna iliyo rahisi.``` ```??♀ Lakini swali lenye umuhimu mkubwa zaidi kwa kila mmoja wetu haipasi liwe juu ya namna tunavyotekeleza mipango yetu wenyewe dhidi ya mipango ya wengine, lakini namna tunavyoweza kupata uwezo wa kuishi kwa ajili ya Kristo kila siku. Kristo alikuja duniani na kutoa uhai wake ili tupate wokovu wa milele. Anataka amzingire kila mmoja wetu kwa angahewa la mbinguni, ili tuweze kuupatia ulimwengu mfano utakaoiheshimu dini ya Kristo. – Loma Linda Messages, uk. 602.```
Seek God first!
@Regranned from @cheyennebbostock - The reason a lot of folks can’t find love is because they are looking in the wrong places. The fastest way to find a husband/wife is to find God. Once God fixes you up to be the man/woman God wants you to be, you won’t have the desire to go looking for Love because Love dwells inside of you. He will make you whole. Now here is where I’m about to help someone. >>> Too many people are looking to go out on a date, be in a relationship, or jump into a marriage and they haven’t been made whole. They are broken vessels trying to become whole through the help of a man/woman, then wonder why it doesn’t work out. When you get right with God, your thirst level will go down, you won’t be as eager and impatient to get into a relationship or marriage. You’ll notice your friendships and your network will change, the way you dress will change, everything about you will change... and then finally... your relationship status will change, but this time it will be with God’s help. If you’re looking for love, you’re doing it wrong! Seek God first! ?? ***My picture has nothing to do with the story ***
Pastor Caleb Migombo: It’s not wrong to enjoy something, as long as it’s good and honorable
How do you draw the line between your own desires and God’s will for you? It
isn’t always easy. The question of our motives-why we do what we do-is always with us.
It’s not wrong to enjoy something, as long as it’s good and honorable. God may even have gifted you in certain ways, and it would be wrong to deny those gifts. But always commit your motives to God and seek His will in everything-even in things you enjoy.
Delight yourself in the Lord and He will give you the desire of your heart. Psalms 37:4
Edwin Kihore: KEEP YOUR CROWN
KEEP YOUR CROWN
You are a person of great value! In fact, God has crowned you with his glory and honor.
REVELATION 3:11 “Tells us to hold fast to what we have and not let anyone take our crown. Our Crown represents our destiny, dream, goal, talents, authority in Christ and God’s blessings and favor in our life. Yet, many people have let other’s words or unfair situation knock off their crown. Jesus says JOHN 5:41 “Your approval or disapproval means nothing to me.” He was saying that it doesn’t matter what other people say, or think or do, He has give is approval and bless. Start build you confidence back. So, you can do everything through Christ.
“We all, like sheep, have gone astray, each of us has turned to his own way”
“When we go a wrong path in life, God grieves over our foolishness, because He knows we are only hurting ourselves. He also knows that this is our natural tendency, because we
-like sheep-easily wonder and stray from the only Shepherd who can guide us and keep us safe.
What decision are you facing today? Don’t rely only on your own wisdom, or even on the wisdom of others. Instead, seek God’s will, and ask Him to guide you and show you His will.
Remember: His way is always best-always. We all, like sheep, have gone astray,
each of us has turned to his own way [Isaiah 53:6]” Yani Mungu huyu!! Nilikuwa Facebook kabla sijafunga nakutana na ☝ hilo hubiri toka kwa Pastor Caleb Migombo, nikajikuta ghafla nimekuwa mpole. Unajua maybe because I love Zari so I put my emotions to her situation nakusahau kuwa kuna Mungu! Eeh, Mungu nisamehe! And let me withdraw my words about the Zari situation: Zari whatever God tells you to do, you follow Him! Mlilie Mungu akupe hekima ya uwamuzi wa kufanya not us human being for we all are sinners in God’s eyes! …….As I said whatever decision you make I will respect you. But seek God’s wisdom only!! Be blessed
“Keep on believing in God. God is the referee of all referees until He says it is over.”~~~ Zari the BossLady
“Half time is not full time and HIS calendar for your life is not man’s calendar. BE ENCOURAGED! DON’T GIVE UP. With God all things are still possible!” Everyday is a fresh start with potentials. .. keep the faith…. keep on believing in God. God is the referee of all referees until He says it is over. Have a blessed week ahead….”~~~~~ Zari the BossLady
Eli baptism
Waacheni watoto wote waje kwangu kwakuwa ufalme wa Mbinguni ni wao; hayo ni maneno yake Mungu mwenyewe alitusihi tuwapeleke watoto kwake kwani ndipo wanapostahili kuwepo kwa usalama zaidi! Basi siku ya jana mtoto Eli alipelekwa mbele za Mbingu na kupokea upako mtakatifu wa kumkabidhi maisha yake kwa Yesu! Eli ni mtoto wa my brother Kevin and Laura from Wichita, KS. Huyu ni mtoto wao wa pili. Mungu awakuzie, awalinde, na kuwabariki watoto wenu na familia yenu kwa ujumla! Kevin akiwa amembeba mtoto Eli!.....Kwafaida ya wasomaji wangu, huyu kaka yangu Kevin a.k.a KB (Kevin Bwahama) ndio alikuwa my very first neighbor hapa Marekani, in Wichita, Kansas. Nyumba zetu zilikuwa zinatizamana, alikuwa ananijali as his little sister tumeishi kwa upendo sana. Namshukuru sana Mungu kwa kunipa some few good friends ambao hata mida ambayo nakuwa sina imani na Wabongo nikiwaona watu kama akina brother Kevin napata a little bit of hope to try to trust again! Asante sana kaka yangu for being there for me. Mungu azidi kukubariki sana. I'm sure your wife got the best man, such humble caring man! Japo kishingo upande lakini inanibidi niseme Yes! Is another good Muhaya ?? ......Btw, kwa wale mnajua story ya Notorius BTK leader miaka kama mitatu hivi baada ya kuhama Wichita aligundulika kuwa alikuwa anakaa mtaa wa pili toka kwenye nyumba zetu ??? Scary! Nafikiri ulikuwa inaitwa Hydraulic / Douglas Mbarikiwe sana wapendwa! Ngoja nifurahie baby Eli na huu wimbo
Tumkumbuke mama yake Zari katika dua na sala zetu!
Tafadhali popote pale ulipo unaposema dua au unapotuma maombi yako kwa Mwenyezi Mungu basi mkumbuke na mama yake mzazi Zarinna Hassan a.k.a The Bosslady! Naona hali yake si nzuri na Zari ameomba tumsaidie kuomba! Pia muwaombee family yao yote katika haya majaribu wanayopitia!......Mungu asikie na kujibu sala zote kulingana na mapenzi yake! Amen!
TAUS retreat, July 12 – 16, 2017
Nawasalimu wote katika jina la Bwana! ……. Naomba uweke hii event kwa calendar yako ya mwaka huu! Never too late for spiritual revival so please add it! Ni TAUS retreat itakayofanyika tarehe July 12 -16, 2017 huko Wisconsin, U.S.A! Hii ni retreat ambayo inafanyika kila mwaka na huwa inaandaliwa na umoja wa Tanzania wa dhehebu la Wasabato hapa Marekani (TAUS) lakini huwa wanakaribisha watu wote wa madhehebu yote kwa dini zote na hata wale ambao hawana dini wanakaribishwa! …….kusoma zaidi na uweze kujiandikisha basi fungua hii link ? Emailing DOC-20170531-WA0005
WOTE MNAKARIBISHWA!