Category Archives: Tanzia

Tanzia: pumzika kwa amani ya Bwana baba mkubwa mzee John Obure!

Marehemu mzee John Obure enzi za uhai wake

Kwaniaba ya familia ya Mr and Mrs O.O Igogo naomba kuchukua nafasi hii kutoa salamu zetu za pole kwa familia ya marehemu mzee John Obure na Mwalimu Anna Cornel Awiti a.k.a Mrs John Obure, kilichotokea alfajiri ya leo huko Mwanza, Tanzania. Tunawaombea utulivu na amani wakati wote wa maombolezo wa msiba huu wa baba na Mungu akaendelee kuwa nguzo imara na kimbilio lenu wakati wote. Mwenyezi Mungu akawe mfariji wenu siku zote. Sisi sote tu mavumbi na mavumbini tutarudi!

Kwa faida ya wasomaji wangu, marehemu mzee John Obure ni baba yangu mkubwa. Yeye alimuoa mama yangu mkubwa ajulikanaye kama Mwalimu Anna Cornel Awiti. Wao maisha yao yote yalikuwa Musoma, na miaka ya hivi karibuni walihamia kijiji cha Shirati kilichopo wilaya ya Rorya mkoa wa Mara. Mzee John Obure yeye ni mzaliwa wa Shirati, na alioa mrembo toka kijiji cha Kowak wote ni wana Rorya kwa asilimia 100%!

Mr and Mrs John Obure wakiteta!

Kama wanavyo onekana pichani ni marehemu akiwa na mkewe wakiteta jambo fulani wakati wa msiba wa baba yangu mkubwa mzee Joseph Musira (soma ?) Tanzia: Pumzika kwa amani baba yetu mzee Joseph Musira ….. Marehemu Mzee Joseph Musira alioa first born (mtoto wa kwanza) na Marehemu mzee John Obure alioa second born (mtoto wa pili).

Mama zangu wakubwa mtoto wa kwanza na wapili katika pozi nyumbani kwa Mr and Mrs Musira. Wote ni wakazi wa kudumu hapo Musoma, hivyo ni majirani.

Mama zangu, mabinti wa mzee Cornel Awiti na Valeria Awiti

Pichani ni mama zangu wote 6 kwa ujumla wao. Mwenye nguo ya Orange (rangi ya chungwa) ndio mke wa marehemu mzee John Obure. Bibi yangu mzaa mama alizaa watoto 12 ambao walikuwa mpaka utuuzima! Sita (6 ) wakiume na sita (6) wakike. Wakike wote wapo hai, twamshukuru Mungu kwa hilo. Lakini wakiume wamebaki watatu (3) na watatu wengine wamesha lala usingizi wa mauti. Lakini kiuhalisia bibi yangu alizaa watoto 14! Uzao mmoja ulikuwa pacha (twins) wao walikufa siku waliozaliwa. Twamshukuru Mungu kwa yote.

Pichani juu nikiwa na mama yangu mzazi pamoja na mmoja wa watoto wa marehemu ajulikanaye kama Dr. Joseph John Obure. Hapo ilikuwa ni 2018 Washington DC. Kaka yangu huyu yeye anaishi North Carolina na familia yake.

R.I.E.P baba mkubwa!

Kwa mara nyingine tunatoa pole zetu za dhati kabisa kwa familia ya marehemu mzee John Obure.

“Kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa; maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.” *** Mwanzo 3.19

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. ????

Siku ya mazishi

Mke wa marehemu

Dada wa marehemu!
Dada mkubwa wa marehemu

Wajukuu!

mtoto wa marehemu (watatu kuzaliwa) Dr Joseph Obure
Mtoto wa marehemu (wapili kuzaliwa) Deus Obure

Pumzika kwa amani ya Bwana mtoto wa dada yangu!

Kutoka kushoto: Alpha mkubwa, Alpha mdogo (R.I.P) na dada Pendo Igogo (mama Alpha).

Pumzika kwa amani ya Bwana wajina wangu Alpha! Ilikuwa heshima kubwa sana pale ulipo zaliwa, dada yangu Pendo Igogo akasema huyu mwanangu nampa jina Alpha kumuenzi mdogo wangu anipendaye sana. Ilikuwa ndio njia pekee ya yeye kunionyesha upendo wake kwangu na jinsi anavyo shukuru kwa upendo wetu kama madada.

Kutoka kushoto: Janeth Igogo, Alpha mkubwa, dada Pendo, Alpha mdogo, na nyuma ni mama yake Pendo mke wa marehemu baba yangu mkubwa.

Alpha, kifo kimeumbiwa mwanadamu lakini sikutegemea maisha yako yangekuwa mafupi namna hii! Leo hii umemuacha dada yangu akiwa si tu mlemavu wa viungo bali moyo uliyojaa maumivu makali sana. The only child she had! Ulizaliwa kama miujiza kwani wengi hata madaktari hawakuweza kuwamini mwanamke mwenye ulemavu wa viungo aina ya mama yako angeweza kubeba mimba kwa miezi tisa na kujifungua mtoto! Na sasa umemuacha mama mkiwa!

Kutoka kushoto: Magreth Igogo, Alpha mkubwa, dada Pendo, Alpha mdogo, na nyuma ni mama yake Pendo mke wa marehemu baba yangu mkubwa.

Baba yako ndie mwanaume aliyempenda dada yangu na akamuoa na Mungu akaibariki familia yao kwa kuwapa mtoto Alpha. Leo hii wote wewe na baba hamponae tena mmemuacha kama alivyo! Kweli maisha ni fumbo na Mungu mwenyewe ndio mwenye kuweza kulifumbua! Nasikiaga wakisema kuwa “ng’ombe wa masikini hazai” na leo umenifanya niamini huu msemo kwa viwango vingine kabisa!

Pumzika kwa amani mrembo, tutakutana asubuhi njema!

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake litukuzwe milele! ????

Tanzia: Pumzika kwa amani baba yetu mzee Joseph Musira

Mr and Mrs Musira

Ni miaka 59 ya kujuana kwao na September 12, 2020 walitakiwa kufikisha miaka 56 tangu wale kiapo kitakatifu cha ndoa yakwamba “MPAKA KIFO KIWATENGANISHE”! Kiapo chao kitakatifu aliapa katika kanisa la Roman Catholic lillopo katika kijiji cha Kowak, wilaya ya Rorya mkoa wa Mara. Siku ya leo tarehe 06 / 05 / 2020 Mungu aliamua kuitimiliza ahadi walio iweka mbele zake. Mnamo majira ya saa kumi na moja alfajiri saa za Africa Mashariki baba yetu kipenzi mzee Joseph Musira alilala usingizi wa mauti katika hospital kuu Musoma alipokuwa akipatiwa matibabu!

Tunahuzunika kwasababu sisi ni wanadamu tulioumbwa kwa hisia. Tulikua bado tunampenda sana. Rafiki yake (Mke wake) bado alikua anamuhitaji sana. Lakini mapenzi ya Mungu yametimia nasi tunasema Amen!

Pumzika kwa amani ya Bwana baba yetu, ulitupenda nasi tunafarijika kujua yakwamba umelala ukitambua upendo wetu kwako. Maisha uliyo ishi ni mfano wa kuigwa kwa watu wengi sana. Umeishika imani na kuiishi kwa vitendo mpaka mwisho wa safari yako. Ulikuwa Mwalimu ulielimisha jamii nyingi sasa. Mchango wa elimu kama Mkurungenzi wa elimu wa mkoa katika Diocese ya Mkoa wa Mara kwa zaidi ya miaka 25+ kamwe hauta sahaulika. Hata baada ya kustahafu walikuhitaji wakati wote nawe hukusita kwenda kusaidia. Kazi zako za kujitolea katika mambo mbali mbali ya jamii zimeacha alama kubwa kwa vizazi vya sasa na hata vijavyo.

Asante kwa kuwa baba mlezi wa mama yangu wakati akisoma Secondary. Kazi ambayo hukusita kuifanya tena kwangu mimi nilipokuwa mwanafunzi pale Kowak Girls Secondary school. Umeishi maisha vyema nasi tutayasherekea kwani unastahili! Pumzika kwa amani, tukutane asubuhi njema. ????

“Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” ** 2Timothy 4: 6-8

  • “Leo ngoja niandike kidogo. Mwl. Joseph Musira alikuwa baba kwangu, alikuwa Mwl. wangu wa hesabu na Jografia nikiwa nikiishi nao ni mshauri. Alinilea kwa upendo usio mfano akiniita “rafiki yangu” Halafu ananitania “Susilia” kisha anacheka wote familia ni kicheko. Jamani na umri niliyo nao nikimsalimia Mwl. kwenye simu napiga magoti hadi chini, watu hunicheka kwa kupiga magoti kwa mtu nisiyemuona lakini upendo wake ulinikaa katika akili mimi nashtukia nimeshapiga magoti nikisikia sauti yake. Mzee Musira, ameniinua kutoka msingi, amenifanya nimefikia hapa kwa kunisaidia na kunitia moyo nikiwa darasa la saba hadi nikafanya vizuri na kujiunga na Rugambwa Sekondari School enzi hizo. Mara ya mwisho nilikwenda kuwasalimia akiwa ameanza kuumwa nikampelekea Rozari nzuri kutoka Jerusalem akafurahi sana kwa maana Wimbo wake ulikuwa sala. Lakini safari imefika hatungeweza kuongeza dakika wala nukta. Amepiga vita vilivyo vizuri vya upendo akiwa ni mkwe wa kwanza kwa Baba yangu na mama yangu Marehemu Mzee Cornel Awiti Oyata na mama Valeria (Mareh.) Maishao yao ni hubiri tosha kiasi kwamba mabinti na wajukuu wa Mzee Awiti wangeiga mfano wao hakika kifo ndicho kingetutenganisha na wenzi wetu. Baba wa mfano na kila mara mimi na mzee wangu O.O Igogo tunawataja kwa maisha matulivu, furaha na amani waliyonayo. Familia hii ninawaombea faraja peke yake Bwana awatie nguvu ni maumivu makali lakini ni lazima tushukuru kwa kila japo. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake litukuzwe.” *** Shemeji wa marehemu Mama Igogo pichani juu ????

Till we meet again baba yangu, tutakukumbuka daima!

LifeWellLived #ManOfGod #ManOfIntegrity #HusbandOfOneWifeOnly #FamilyMan #GrandFatherToMany #Educator #Trustworthy #GoodCitizen #CommunityAsset #Patriot

Baadhi ya picha za msiba:

Wakili Jacob Sarungi kuagwa kesho!

*OBITUARY*

*ADVOCATE JACOB EMMANUEL SARUNGi

*Dear Member,It is with deep regret that we inform you of the untimely death of TLS member Advocate Jacob Emmanuel Sarungi , Roll Number 4666 who passed away on Friday 15th May 2020 in Morogoro *after being involved in car accident*

*Last respects* for the late Advocate Jacob Emmanuel Sarungi will be held on *Monday 18th May, 2020 from 1700hrs at his residence, Mbagala Majimatitu Saku street , Dar es Salaam* Thereafter the *burial services will take place at Rorya Utegi village, Mara region on Wednesday , 20th May, 2020*Members who wish to attend the last respects and burial in honor of our dearly departed friend and colleague, should dressed in bibs and robes.

*MAY THE ALMIGHTY GOD REST HIS SOUL IN ETERNAL PEACE* Regards, |Tanganyika Law Society Secretariat

  • Kwa taharifa kutoka ndani ya familia na kama ilivyo andikwa na jumuiya ya wanasheria wa Tanzania yakwa Wakili Jacob Sarungi ataagwa kesho mchana masaa ya Africa mashariki kisha mwili wake kusafirishwa kwenda kijijini Utegi, wilaya ya Rorya, mkoa wa Mara ambapo atalazwa katika nyumba yake ya milele katika makaburi ya familia. Nitaendelea kuweka kumbukumbu hizi kadri nitavyokuwa nazipata. Asanteni.

Tanzia: Pumzika kwa amani Advocate Jacob Sarungi!

Marehemu Jacob Emmanuel Sarungi enzi za uhai wake

Kwamasikitiko makubwa sana naomba kuweka kumbukumbu hii ya kifo cha kaka yangu (first cousin brother) Advocate Jacob Emmanuel Sarungi kilichotokea siku ya Ijumaa tarehe 15, May; 2020 kwa ajali ya gari maeneo ya kona ya Mikese, Morogoro, Tanzania. Marehemu alikua akielekea Dodoma kikazi ndipo mauti ilipo mkuta. Marehemu ameacha mke na watoto, wazazi, pamoja na kaka na dada zake.

Kuna vitu vya kuandika lakini sio kifo cha mtu yoyote yule! Ni ngumu sana, haswa unapoona kijana ambaye ana maono makubwa, nguzo imara ya familia, moja ya watu ambao anategemewe katika kuongoza ukoo fulani, na nguvu kazi ya taifa inaondoka wakati ndio kwanza ameanza mwendo, amewasha mshumaa wake teyari kuimulika dunia halafu ghafla unazimika! Unajikuta unamaswali mengi sana lakini kwakua tunaimani katika Mungu hivyo tunaamini kazi ya Mungu haina makosa!

Natoa pole zangu za dhati kabisa kwa mke wa farehemu, watoto, wazazi, ndugu, marafiki, wanasheria wenzake wote walioguswa na msiba huu haswa chama cha wanasheria (Tanganyika Law society), wafanyakazi wenzake, pamoja na ukoo wote wa Chief Sarungi Igogo.

2 Timoth 4: 7-8 …. “7Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.”.

R.I.P brother! Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote ????

Watu wengi wameguswa na msiba huu, na zifuatazo ni baadhi tu ya jumbe zilizo andikwa na ndugu pamoja na mara fiki

  • ???? Huo ulikua ni ujumbe wa masikitiko toka Mwanasheria mwenzake, na dada yake Janeth Igogo ambao aliuandika kupitia account yake ya WhatsApp
  • Naye dada wa marehemu Maria Sarungi-Tsehai kwa kupitia account zake ya Instagram na Facebook aliandika ujumbe huo ? hapo akionyesha ishara ya kuguswa na kusikitishwa na msiba huu.
Kwa kweli, kwa masikitiko makubwa sana nimepokea taarifa ya kifo cha kaka, ndugu, jamaa, rafiki  na mwanasheria msomi mzuri kijana wetu damu ya Rorya Jacob Sarungi (Adv).Moyo wangu umeugua sana. Najikongoja kifikra kukubali kuwa Adv Jacob Sarungi ameaga dunia.Jacob alikuwa ni kijana mweye ndoto nzuri na pevu sana kwa ujenzi wa Rorya Mpya.Jacob ameacha familia changa sana nyuma yake na vijana waliomtegemea sana kujifunza katika tasnia ya sheria.Imeniuma sana. Jacob alitegemea njonzi yake ingekuwa angavu kwa maisha ya familia yake,  wanarorya, jumuiya ya wanasheria na watanzania kwa ujumla.Tumbo la dunia lihifadhi mwili wake kwa amani. Namuomba Mungu mwingi wa rehema aipokee roho yake ikisubiri parapanda ya mwisho.Bwana alitoa, Ndiye ametwaa.Jina lake lihimidiwe.  ??????                                                                                                                                 Maina Ang'iela Owino.©2020. 
  • REST IN PEACE BROTHER JACOB SARUNGI.Ni Mapema sana kuamini kwamba umerudi kwa Muumba wetu. Mungu akupe kauli thabiti huko uendako, nasi atupe uvumilivu wa kustahimili maumivu haya sisi tuliobaki.
  • Ujumbe huu ulitoka kwa mdogo wa marehemu Mwanasheria na mpatanishi wa serikali (government Arbitrator) Magreth Igogo ambao aliandika katika kupitia account yake ya WhatsApp

Kama ilivyo semwa na wengi kua ni ngumu kuamini lakini hatuna budi kukubali kuwa hiyo ndio hali halisi. Mungu awe nanyi wakati wote haswa katika kipindi hichi cha maombolezo.

Rest easy brother you are gone but you will never be forgotten ????

Tanzia: Pumzika kwa amani mama Guka

Kwamasikitiko kwa niaba ya familia ya mzee Otieno Igogo tunatoa pole kwa mtoto / mdogo wetu Guka Otieno Igogo na familia ya mama yake kwa kufikwa na msiba mzito sana wa mama yao mzazi. Kama familia naomba mtambue kuwa tumeguswa sana ma msiba huu na dua na sala zetu zipo pamoja nanyi siku zote haswa wakati huu wa maombolezo. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. Kwafaida ya wasomaji wangu, marehemu ni mama yake na mdogo wangu Guka (pichani hapo akiwa na mimi kwa nyuma). Tumawaombea faraja toka kwa Mungu wakati huu wa msiba na siku zote. ??

Rais Magufuli: Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria

In God we trust!  R.I.P Aquilina  ??

Jokate Mwegelo: Hukustahili kufa kwa namna ulivyouawa

Regrann from @jokatemwegelo - Such a beautiful innocent young woman. ??❤ Aquilina Akwilini Baftaha, umefariki ukiwa kijana mdogo sana, kwa wakati ambao ndiyo haswa unatakiwa katika Jamii. Kifo chako kimetushtua na kimetugusa. Inawezekana tumeguswa kwa sababu mbali mbali na tofauti, ila tu uhakika ni kuwa imetuuma. Wengi tulikuwa hatukufahamu, lakini leo hii unawakilisha kundi kubwa la vijana wadogo kama wewe walio chuoni, na katika mioyo yetu tunajua inavyouma kumpoteza mtu wa hivyo. Haswa kwa namna ambayo umepoteza maisha kama mshumaa uliozimwa ghafla. Hukustahili kufa kwa namna ulivyouawa. Mwenyezi Mungu awape nguvu, imani na amani ndugu na jamaa wako wa karibu na kila aliyeguswa kwa kifo hiki cha kusikitisha. 
R.I.P Aqualina ❤ - #regrann

Aquilina, pumzika kwa amani ya Bwana Mungu!

Nashindwa niandikaje kwa jinsi nilivyo umizwa na kifo cha huyu binti! This is too painful, inhumanity, and wrong in all levels!! Siwezi kunyamaza kwani mimi ni Mtanzania! Siwezi kunyamaza kwani mimi ni mama! Siwezi kunyamaza kwani mimi ni mwanamke!! Nimekataa kunyamaza kwa hili!!!  Baba yangu Dr John Pombe Magufuli nakuomba ukemee huu unyama hadharani!!!   This has everything to do with humanity  and leadership. As a leader of our country you should condemn these kind of acts!! As a father of many, this beautiful, precious soul could have been one of yours!! You need to take action ASAP!! This should have never happened, it's scary that it is a fact its happening in Tanzania right in front our very own eyes!! That is not the Tanzania we want!! Mambo kama haya siyo ya kuyanyamazia hata kidogo!! .... Rest in eternal peace Aquilina, justice we surely be done!!

Mpaka kifo kitakapo tutenganisha!…….. R.I.P Mr and Mrs Ngombale Mwiru!

 Pichani hapo juu ni sura ambazo naamini zinafahamika na watu wengi kwenye jamii ya taifa la Tanzania. Ni  marehemu mzee Kinguge Ngombale Mwiru na mkewe marehemu Peras Ngombale Mwiru! Wanandoa hawa walianza maisha ya ndoa wakiwa vijana na wamedumu kwenye ndoa yao mpaka kifo kilipo watenganisha kwa jumla ya siku 28! Sasa wote wapo kaburini wamelala usingizi wa mauti! What a journey! What a lovely love story to tell! Naamini hawa wazee wetu walifunga ndoa ya serikali kwani watu wanao wafahamu wanasema mzee Kinguge Ngombale Mwiru alikuwa hana dini! Sina huwakika kama alikua ANAAMINI MUNGU!? Kuna watu wanaamini Mungu yupo lakini hawana dini! Sasa Sina huwakika na hilo, japo mama yeye inaelekea alikuwa muumini mzuri wa dini ya Kikristu wa thehebu la Katoliki! ....... Natamani tungekuwa na video ambazo hawa wazee wanatueleza maisha yao ya ndoa yalikuaje, na nini walifanya  kuhakikisha ndoa yao inadumu haswa ukizingatia mmoja alikuwa hana dini napia mwanasiasa! Wakati mama yeye ni muumini wa Katoliki na ameishi maisha yake pretty much privately! ...... Yani tungetamani  kujua when things got heated in the house what did they do?! Walipiga magoti wakasali, au walimuita mganga wa kienyeji, au walitafuta cancellers?! ......... Hapa ndipo wenzetu wa nchi zilizoendelea  walipo tupiga bao! Wazee kama hawa wenye vitu fulani ambavyo jamii ingeweza kujionea na kujifunza toka kwao wangekuwa wamesha fanyiwa interviews kibao kuhusu maisha yao ya ndoa na familia mbali na siasa ili jamii inufaike! Marehemu naamini walibahatika kupata mtoto moja aitwae Kinjekitile kama mnavyo waona hapo pichani! ........ Poleni sana wanafamilia na wafiwa wote! Poleni sana Watanzania!  Bwana alitoa na Bwana ametwaa sifa na utukufu ni zake milele zote, Amen!

R.I.P Leo Mapunda Mwakitalu

screenshot_2016-12-05-09-05-05-1screenshot_2016-12-05-09-09-33-1screenshot_2016-12-05-09-09-44-1

Naomba niungane na Watanzania wote waishio Marekani na nyumbani Tanzania katika kuomboleza kifo cha ndugu yetu Leo Mapunda Mwakitalu. Binafsi sikubahatika kumfahamu marehemu wala kumuona lakini pamoja na hayo naomba nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa familia ya marehemu, ndugu wote, marafiki, jamaa, na Watanzania wote……….Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. R.I.P Leo!

R.I.P Fidel Castrol!

screenshot_2016-11-27-08-41-49-1May your soul R.I.P comrade, your good deeds will forever live!?

Pumzika kwa amani Mzee Samwel Sitta!

screenshot_2016-11-07-09-01-56-1Mchango wako kama Mtanzania mzalendo na kiongozi hauta futika kamwe kwenye historia ya taifa la Tanzania!……Enenda kwa amani ya Bwana wetu. Poleni sana wafiwa wote; familia ya marehemu, ndugu, marafiki, na taifa la Tanzania kwa ujumla!…….. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe siku zote ??

Pumzika kwa amani ya Bwana mpendwa Juliana

screenshot_2016-11-03-17-13-01-1Jamani what a sad story!!! Nimesikitika sanaaaa! What a loss! Jamani binti mdogo hivi watu wanamtenda unyama huu jamani! Ee Mungu tusaidie hii dunia imejaa laana isiyo elezeka! screenshot_2016-11-03-17-07-26-1Halafu hapa sikujua kuwa ni Mtanzania, nilifikiri ni South Africa! Nimeguswa sana na kifo chake. So painful!……… Wazazi wako wapi taifa linawalilia!! Watoto wanalelewa bila maadili wala upendo, shetani ameshika roho za wazazi kuzaa siku hizi ni FASHION SHOW tu! Wazazi wengi hawana muda wa kulea watoto wao matokeo yake watoto wanalelewa na TV and social media!! And all they can see, hear, and learn is nothing but violence!! ……… Where are the fathers jamani!!! Fathers are supposed to be PROTECTORS for their girls where are they??? Watoto wakike wanalia kwa uchungu lakini baba zao wahajali!!! watoto wakike wanajiona hawana thamani!! Wanatafuta baba zao kwenye vitanda na wanaume wengine! They are crying out for help but their fathers have turned def!! they care less about them!! This is too painful! Oo’good Lord hear our humble cry!………Enenda kwa amani ya Bwana mpendwa wetu Juliana, tutaonaa katika hasubuhi ile ya fahari!!……. Now #Salome is no longer fun to watch, gosh!! What a  talent! What a loss! R.I.P

Dr. Magufuli baba unatumbua majipu mpaka kwenye misiba?!

fb_img_1472436063790Mmmh! “Amefunga ndoa na Janet Massaburi”, Okay! Yes!  “Na ameacha wajane”? Uncle Foo! Are you okay! Hao wajane ni wakina nani, kwanini hukuwataja watu wakawasikia?? Na idadi yao!! Mbona mnafanya mambo ya aibu namna hii!….. Hata nyie wenyewe dhamira zinawasuta! Nampenda sana aunt Janet Massaburi lakini ukweli ni kwamba Ashura Massaburi ndio mke mkubwa wa marehemu! Kila mtu analijua hilo hata marehemu anajua hivyo! Yes! Alifunga ndoa na aunt Janet but tell people the truth the Real story behind hiyo ndoa ya kanisani! Mmh! Hapana, msifanye hivyo siyo vizuri kabisa!

c5Rais akiwa na mkewe wakati akitoa pole kwa wake za marehemu. Hapo kwa upande wa kulia ni mke mkubwa wa marehemu Ashura Massaburi a.k.a NyarKigoma (maana yake ni binti wa Kigoma), na kushoto ni Janet Massaburi a.k.a NyarMajita (binti kutoka Majita) ambaye ni mke wa tatu!

fb_img_1472436063790Dr Magufuli baba umenichekeshaje?! Unatumbua “majipu” mpaka msibani ??? But huo ndio ukweli wenyewe!…………. Kwa kweli mimi sitaki ongea mengi kwa leo ngoja niwaache ndugu zangu waomboleze kwa amani! Lakini haya mambo ya kuoa wake wengi mmh! Nishida tupu! Mnatesa watoto na ndugu wa karibu bila sababu ya msingi! Mambo ya ukewenza yalikuwa zamani hizooo! siku hizi ni matatizo tu haswa pale unapokuta the so called “step mother” ana roho ya kichawi halafu unalazimishwa undugu naye ?? Ngoja ninyamaze mie ?? …………. Mimi naona kama watu mmechokana ni bora kila mtu achukue hamsini zake kuliko hii fedheha!…….. Anyway, hekima na upendo wa Mungu ukawatawale na shetani asipate nafasi! ??c2 Wake za marehemu Dr Didas Massaburi wakiwa wamekaa mstari wa mbele. c1Rais Maagufuli akitoa neno, pembeni yake mwenye suti ya dark maroon ni mzee O.O Igogo

Picha zote nimetoa kwa ? Michuzi

Kwa picha zaidi ? Vijimambo

“Yusta wangu, rafiki yangu hivi ni kweli umetuacha au naota” Janeth O.O Igogo

screenshot_2016-10-14-15-36-54-1R.I.P Yusta!

“Nimepokea habari za kifo cha ndugu yetu Dkt Masaburi kwa mshtuko na masikitiko sana” Mh. ShyRose Bhanji

screenshot_2016-10-14-15-38-53-1

Pumzika kwa amani dada Yusta Msoka!

screenshot_2016-10-13-10-17-48-1Too young, too beautiful to departure at this age; but who knows the best time more than our Creator! May your lovely soul Rest In Peace!fb_img_1476371988149 Mungu awape uvumilivu katika kipindi hichi kigumu watoto wa marehemu, wazazi, na wana familia wotefb_img_1476371873526I’ve never met you but very touched by your death!You will surely be missed by so many…….Till we meet again, R.I.P Yusta.

“Rest In Peace Comrade” -Lemutuz

screenshot_2016-10-12-18-39-37-1

“ENENDA KWA AMANI BOSS D.J. MASSABURI, MUNGU AKUPE PUMZIKO LA AMANI.”- Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
 Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

Kwa mara nyingine tena ndani ya mwaka, moyo wangu unapata sikitiko na jaribu kwa kuondokewa na Bossi wangu niliefanya naye kazi Chuo cha IPS.

Nimesikitika sana kwa jinsi nilivyomfahamu na kuishi naye kwa miaka 5 ya ajira. Kwa kweli Dunia, Afrika Mashariki, Tanzani, Taaluma ya Procurement, wana Mara, Ukoo wa Ojambi pamoja na ndugu jamaa na marafiki tumepata pigo na pengo ambalo halitazibika kamwe.

Binafsi nimepata kujifunza Ujasiri, Uthubutu, Umakini, Uwezo wa kujenga na kutete hoja kutoka kwake. Nakuombea Heri na naamini muda utafika na sisi tutakufuata huko ulikokwenda.

Pole sana Familia ya Massaburi na Mungu awape nguvu kwa kipindi hiki kigumu cha huzuni.fb_img_1476313349851Pumzika kwa Amani baba. Amen