Category Archives: Uncategorized

Hongera sana LB

IMG-20160412-WA0010

Many congratulations to Missy LB for being honored the 2016 Fashion Design Award by the Black Women In Jazz & The Arts Awards 2016. Personally I am truly proud of you keep representing our country so wel! IMG-20160412-WA0009

Tukio hili la kufurahisha lili tokea mnamo tarehe April 10, 2016, katika hotel ya Marriott mjini Atlanta, Georgia IMG-20160412-WA0005

Baadhi ya watu maarufu ambao walitunukiwa tunzo hiyo siku hiyo ni Legend Ms. Cicely Tyson na Melba Joyce na wengine wengi! IMG-20160412-WA0008

Missy LB akiwa anaingia ukumbini huku akiwa amevalia vazi aliyo buni na kushona yeye mwenyewe IMG-20160412-WA0002Pendeza sana IMG-20160412-WA0001LB alifurahiya tuzo na binti yake Brenda, wote wakiwa wamevalia mavazi ya LBIMG-20160412-WA0003mlipendeza mno! IMG-20160412-WA0006Kwa mara nyingine tena hongera sana Linda Bezuidenhout. Nakutakia mafanikio makubwa zaidi ya haya ?

“changamoto nyingi hapa duniani ukigeuza upande wa pili utagundua ni fursa” -Dina Marios

Baba mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti chake chini ya mti anasoma gazeti. Pembeni yake alikuwepo mtoto wa miaka 6 ambaye alikuwa akimsonga kwa maana nae alikuwa anataka kuangalia kilichomo ndani ya gazeti.

Baba huyu ili kuondoa usumbufu akaona ni vema achane ukurasa mmoja ili ampatie mwanae. Ukurasa huu ulikuwa na ramani ya dunia, akamuonesha “unaiona hii ramani eh? baba  yake akaichana ile ramani vipande vidogo vidogo kama kumi na tano. Akamwambia mwanangu nenda ukavipange hivi vikaratasi mpaka iwe ramani kama ilivyokuwa, ntakupa booonge la zawadi. Hii yote ikiwa ni katika kuondoa usumbufu.

Mtoto akaenda kujifungia baada ya dakika chache akarudi akiwa amevipanga kwa usahihi kabisa. Kwamshangao haaaaaa!! Umewezaje kufanya haraka hivyo? mtoto akajibu nyuma ya vikaratsi hivi  ilikuwepo picha ya sura ya mtu hivyo nilivipanga kwa kukufuta sura hiyo. 

Oooh!  Unajua maishani suala si kukutana na changamoto bali ni jinsi gani unazichukulia changamoto hizo. Ukikutana na changamoto yoyote tuliza akili na utapata mlango wa kutokea changamoto nyingi hapa duniani ukigeuza upande wa pili utagundua ni FURSA. Fanya hivyo utashanga mambo yanavyokuwa rahisi kwako. Ila ukiwa kipofu wa kuitazama ile changamoto kwa hisia za itakuwaje utabaki hapo hapo.

Good Morning! FB_IMG_1460529725619

Father and son moment

FB_IMG_1460541857129-1Ain’t they cute!  Wamependeza sana, great picture and happy  belated birthday Dr. Martin Sarungi. Live long!

Hot shot of the day

Screenshot_2016-04-11-09-13-33-1I loved this! Cute! Cute! Mr and Mrs Dangote na Queen Latifah………… Pendeza sana. Screenshot_2016-04-11-09-13-43-1beautiful!

“Sijawahi kuishi kwa kumtegemea mtu ila ninaishi kwa kumtegemea Mungu”Le mutuz

Screenshot_2016-04-11-09-03-38-1

Motherhood

Screenshot_2016-04-11-09-10-23-1I love this pic. Zari na wanae wamependeza sana. Kuwa mama ni kazi ya kishujaa sana, nikazi ambayo unatakiwa ujitolee kwa asilimia zote si tu kifedha bali pia kwa matendo yako, na kwa mawazo yako! Wabarikiwe wamama wote!

Our humble beggings!

2016-03-27 13.16.40Sikutegemea kuweka hapa hii picha siku ya leo. Lakini nimeona moyo wangu umenisukuma kuweka basi ngoja nifanye kile kitu roho napenda! Hii picha tulipigia tukiwa kijijini Utegi, Rorya, Mara mwaka 1987. Tulienda kusherekea siku kuu ya Christmas. Katika hii picha kuna watu wawili ambao hawapo nasi tena.

(1) aliyevaa sandals nyeupe. Yeye alikuwa mama yangu mkubwa mke wa marehemu baba yangu mkubwa mzee alijulikana kama Mama January

(2) Shangazi yangu kipenzi cha roho yangu. Theresia Obuoro Igogo. Ambaye amekaa karibu na mimi. Alikuwa msichana mmoja tu kwenye tumbo la bibi yangu mzaa baba. Yeye ndo mwanangu amepewa jina lake (Theresia a.k.a Teddy) in honoring of her. Ipo siku nitamuongelea kwa kirefu zaidi kwani yeye ndio chanzo cha mibaraka yote ambayo watu wanaiyona katika familia yetu!!

Wengine ni:- mama yangu mzazi? 

2016-04-10 12.13.10

dada yangu ambaye ninamfuata ? 2016-04-10 12.16.06mdogo wangu anaye nifuata kwa mara ya pili 2016-04-10 12.11.32 na mimi mwenyewe ? ??? what a massive #ThrowBackSunday..! 2016-04-10 09.41.02Hilo “banda” la udongo kwa upande wa kushoto lilikuwa ndiyo jiko la marehemu bibi yetu nyakati hizo (baadaye alijengewa lingine). Na kwa upande wa kulia ilikuwa ni sehemu wanalala mbuzi.

Everyone starts from somewhere! Hakuna kitu kinacho onekana hapa duniani ambacho hakina mwanzo wake au chanzo chake! #TheRoots Na huwa nikikumbuka tulipo toka then unakuta mtu anataka kuingilia mambo ya familia usizozijua chanzo chake!! I swear, naweza toa mtu ng’eo ya macho! Kama wewe hukuwepo nasi nyakati hizi then keep your nose where it belongs!!

Nilimtumia mdogo wangu na baba yangu hii picha. Wakashangaa sana. Mdogo wangu alikuwa hajawahi kuona hii picha vile vile maisha yao walivyo kuwa ni tofauti na sisi tulivyo kuwa wadogo. Hivyo hana kumbukumbu ya maisha haya ya hali ya chini. Hapo kwenye picha alikuwa na miaka mitatu  (3yrs). Basi hivi ndivyo alivyo sema ? 2016-04-10 09.46.05

 Na baba yangu yeye nilimtumia muda kidogo na hivi ndivyo alivyo sema ?  (Samahani kwa some typos) Screenshot_2016-04-10-13-10-38-1Anyway! That’s our humble beggings. I’m glad nime share nanyi kidogo ?

A word of Wisdom

FB_IMG_1460236077765Yes! Only God sits that High! Kuna “watu” wanajiona wao ni Mungu! Yani bila uwepo wao kwenye maisha yako au kwenye jambo lolote unalotaka kufanya kuwa huta weza songa mbele bila wao! Yani watafanya kila njia kukufanya uwamini kweli bila wao wewe huwezi songa mbele. Bila wao wewe hauna dhamani yoyote ile mbele za watu! SMH! Kuna mtu ambaye alishawahi kunuambia hivi karibuni “kama umeshindwa kupatana na basi hutoweza patana na mtu yoyote yule.” In my mind I was like ‘really’!! Who made you God!! Yani from their heshima yangu kwake imeshuka mno! I mean imeshuka sana! Kwani hawa ndio wale “watu” niliokuwa nawaongelea kwenye post iliyopita!

Watu wanafiki, wanacheka na wewe usoni kumbe nyuma yako wao ndio wanao suka na kusambaza majungu! Too bad, at this age and stage in my life I HAVE ZERO TOLERANCE NA WANAFIKI!……. anyway, mpendwa msomaji wangu nakusihi sana usimdharau binadamu mwenzio haswa usiye mjua. Huwezi jua huyo unayemdharau na kumdhihaki ndiye atakaye kuwa mkombozi wako! Only God sits that High! !

“Suala la mshahara si issue sana”- Mh. ShyRose Bhanji

FB_IMG_1460290692526Wakati niko Dawasco mwaka 2005 kuna makampuni makubwa kama 6 walinipa job offers ikiwemo NMB. Hata hivo NMB ndio walikuwa na mshahara mdogo kuliko wote…… nikaona si issue so nikachagua NMB kwa vile ilikuwa haijulikani kabisa na haikuwa kwenye soko. Nikajipangia malengo kwamba (yaliyoambatana na malengo ya NMB) ndani ya miaka 5 benki hiyo lazima ikue, iskike na iwe benki kubwa hapa nchini. Bahati nzuri benki tayari ilikuwa na mtaji mkubwa wa mtandao wa matawi almost nchi nzima…… kwa ushirikiano na wafanyakazi wenzangu tukaipaisha……. mshahara nilionza nao uliendelea kupanda kadri siku zilivokuwa zikienda……. lengo la post hii ni kuwashauri wale wote wanaotafuta kazi: suala la mshahara si issue sana ila pata kazi then onyesha maujuzi then kiwango chako kikionekana mshahara utapanda tu…

Hata shetani naye ni mtu!

Screenshot_2016-04-10-07-04-54-1Jana huyu mtani wangu aliandika hii “status” yake kwa Facebook kama inavyo someka hapo juu ☝. Sasa mie nilimjibu kwenye comment kama inavyosomeka hapo chini ?. Nashukuru kuna binadamu ambao nao wanaelewa kile ambacho mimi naye nakielewa na kuamini kuwa si kila mtu ni mtu kwani hata shetani naye ni mtu!

Sasa ngoja nitolee maelezo. Hata shetani naye ni mtu kama walivyo watu wengine hivyo kuwa muangalifu sana na “watu”! Tafuta kuzungukwa na watu wenye UTU ambao ndiyo wanaitwa “binadamu” lakini kama wewe unataka kuzungukwa na watu? Ndugu yangu nakupa pole sana kwani unaweza ukajikuta umezungukwa na kundi la mashetani au mapepo wewe ukidhani. ni watu!

Kuna na “watu” wenye roho za shetani ambao ukiwaona utadhani ni binadamu! Wanavaa vizuri,  wengine wana elimu nzuri, wana sura na sauti za upole mfano wa malaika, wengine ni warembo sana, wengine wapo mbele  kuwa wanataka kusaidia “watu”. Lakini kaa nao karibu wow! Utajikuta unajiuliza hivi huyu ni mtu au shetani! Kuna watu waongo mfano hakuna, kuna watu ni wataalam wa kusuka na kusamba majungu ambayo yanaweza yakafanya mtu akauliwa  (I’m a living testimony),  watu ambao wana roho mbaya hujawai ona, kuna watu ambao ni serial killers, wachonganishi, etc!

Wapendwa wasomaji wangu, kuweni waangalifu na “watu” siyo kila mtu ni binadamu! Shetani na wafuasi wake wapo hapa duniani nao ni “WATU”! Na anaweza kuwa mtu yoyote yule; ndugu, rafiki, jirani n.k 2016-04-10 07.08.04Mungu atupe uwezo wa kuwatambua hawa “watu” ili ukae nao mbali sana!

TANZIA

 

Ndugu  Wanajumuiya,

Tunasikitika kuwataarifu  juu ya mauti yaliyomkuta mwanajuiya mwenzetu hapa Houston Marehemu Henry Kiherile.  IMG-20160408-WA0022Marehemu alikumbwa na mauti na kuaga dunia jana-April/ 06/2016 usiku saa tano na nusu kwa kupigwa risasi mbili na kuporwa gari lake. Mwili wa marehemu uko chini ya uchunguzi ukisubiri kupelekwa Funeral Home.

Ndugu Wanajumuiya tutakuwa na MKUTANO kwa ajili ya huu MSIBA siku ya Ijumaa (04/08/2016 ) katika anuani hii hapa chini :

Anuani   :    8107  Meadows Pond DR

   Missouri City, TX, 77459

Tarehe   :    April /08/2016 { FRIDAY }

Muda     :    6 PM

Henry ni  Mtanzania mwenzetu hapa Houston na ana Family members hapa.  Marehemu ni mpwa wa Lucy Tenende, na pia ni mpwa wa  Mathew Mohono.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na: 

Lennard Tenende (713) 540-6355

Lucy Tenende (832) 338-7222

Matthew Mohono (281) 804-6478

Imetolewa na : THC Spokesman

*Kwa masikitiko makubwa sana, natoa salamu zangu za rambi rambi kwa wana familia wote, ndugu, jamaa, marafiki, pamoja na Attachmentjumuiya ya Watanzania wote waishio Houston, Texas kwa msiba huu. Ni kifo cha kuhuzunisha sana! Mungu awe nanyi nyote katika kipindi hichi cha maombolezo. Apumzike katika amani ya Bwana kaka Henry….. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote ?* 

Kusoma juu ya habari ya kifo cha Henry Kiherile  bonyeza hapa.

Ijumaa Kareem

FB_IMG_1460124592020Jumaa Mubarak. Sabato njema. JumaPili njema………sorround yourself with greatness ?❤❤❤

Halotel inawatakieni mapumziko mema

FB_IMG_1460123889165Nimejikuta nime miss matangazo yangu ya Halotel ? lakini lazima ni keep ahadi yangu mpaka mwezi wa tano……..Basi ngoja ni kukumbushe kuwa Halotel bado ndiyo habari ya mujini na vijijini! Nunua Halotel kwa mawasiliano yako yote kwani wana network nzuri, Internet ya uwakika kabisa, na HaloPesa kwa huduma za kifedha za haraka!

Hot shot of the day

FB_IMG_1460124700563-1Gorgeous! Kitu uzuri wa asili ‘no chemical added’, organic from Kanda ya ziwa ?? pendeza sana mrembo. Tafadhali, huyu ni mke wa mtu hivyo tazama hii picha kwa heshima zote! Ubarikiwe sana Anna.

“You will never walk alone”

You Will Never Walk Alone!

When you walk through a storm, hold your head up high

 And don’t be afraid of the dark

At the end of the storm, there’s a golden sky

And the sweet, silver song of a lark

Walk on through the wind 

Walk on through the rain

Though your dreams be tossed and blown

Walk on, walk on

With hope in your heart

And you’ll never walk alone

You’ll never walk alone

Walk on, walk on

With hope in your heart

And you’ll never walk alone

You’ll never walk alone

 

Source: one of Facebook friends

#TBT

2016-04-07 09.31.35Me, myself,  and I #TBT  #1996  #TemekeSDA

Kwenye maisha hakuna hali ya kudumu -Dina Marios

Nimejifunza kwenye haya maisha hakuna hali ya kudumu.Kufumba na kufumbua mambo yanaweza kubadilika. Kufumba na kufumbua uelekeo wako wa maisha unaweza kubadilika kwa uamuzi utakaoufanya. Uelekeo utakaochukua unaweza kukupa neema au kukupa majuto baadae. Hayo ndio maisha full of surprises.

Watu tusiowatarajia wanaweza kutokea na kututengeneza kuwa kile tunachotamani kuwa au kile tunachotaka kuwa. Hayo ndio maisha full of suprises.

Kufumba na kufumbua unaweza kujikuta kwenye hali mbaya sana kama binadamu. Kuna kaka nilikutana nae kama mara mbili hivi mara ya tatu naambiwa yule kaka amepata matatizo ya akili amechanganyikiwa ni kufumba na kufumbua.

Kufumba na kufumbua watu uliokuwa unahisi unawajua sanaa kutokana na ukaribu mliokuwa nao utagundua kumbe ulikuwa huwajui hata chembe… ndio maisha full of surprises.

Hayo ndio maisha kufumba na kufumbua kila kitu kinaweza kubadilika hali kuwa nzuri au mbaya…… good morning! FB_IMG_1460010305974

Nani anastahili kula matunda?

Nataka wewe leo uwe hakimu (Judge), tena si wa mahakama ndogo. Hapa, wewe leo ni jaji wa mahakama ya rufaa. Na unatakiwa kufanya maamuzi juu ya kesi hii na maamuzi yako ni ya mwisho hakuna wakupinga. Nakuletea hawa watu wawili ambao wote wanataka haki itendeke bila kumuonea mtu yoyote kwani “mnyonge mnyongeni haki yake mpeni”!  c870acd11ac7f72e26d3e44fe6221a1e17fe5673e3e9db547ed6ee9a777e8d5b_1Mtu wa kwanza tutampa jina la Sikudhani. Na mtu wa pili tutampa jina la Sikujua. Sasa Sikudhani na Sikujua wao wenyewe kwa hiyari yao wakaamua kununua shamba pamoja. Wote walitoa kiasi sawa cha fedha kilichohitajika kununua shamba. Wakagawana katika ili kila mtu alime sawa bila ‘kumyonya’ mwenzake. Sikujua hakuwa na pesa za ziada hivyo alitegemea wangesaidiana na rafiki yake ili waweze kutafuta pesa pamoja kwa kuuza mazao watakayo lima. Sasa katika harakati za kuanza kuandaa shamba ili wapande mazao ilikuwa kama ifuatavyo -:

SIKUDHANI: Sikudhani yeye hakudhania kuwa lile shamba lina ubora na virutubisho vyoyote ambavyo vingewezesha kuzaa matunda au mazao. Hakuona kama kuna umuhimu wa kutumia nguvu na pesa zake kuwekeza kwenye hilo shamba kwani halina thamani hiyo. Hakudhania kuwa kuchukua pesa zake na kutafuta watu wa kulimaa na kuongeza mbole kwenye hilo shamba ni wazo la busara. Hivyo aliachana na hilo shamba bila kujali chochote. Hata pale Sikujua alipo msihi kuwa jaribu hata mara moja kabla ya kusema haifai, lakini Sikudhani alikataa kata kata tena kwa dharau na dhihaka nyingi; “shamba lenyewe lipo sehemu kavu. Hakuna hata maji pamekauka kama jangwani nitapata nini hapo! Angalia lipo kwenye muinuko mvua ikija mazao yote yatachukuliwa na mvua. Sina shida nao, hela ya kununua vyakula ninayo mpaka siku nakufa.”!

SIKUJUA: Yeye alikuwa na imani kuwa anaweza kupata kitu katika shamba lile japo hakujua ni kwa kiasi gani. Alijua kuwa linadhamani yakutosha kuwekeza nguvu zake hapo kwani ametumia pesa yake kulinunua. Sikujua yeye alikuwa mtu mwenye hali duni hivyo shamba ndiyo ilikuwa tuamini lake!

Basi, Sikujua alianza kuandaa shamba kwa jembe lake dogo la mkono. Kila siku anaamka hasubuhi na mapema, anaandaa chakula na maji ya kunywa anaenda shambani kuanzia saa kumi na moja (5am) asubuhi mpaka saa kumi na moja (5pm) jioni. Akatoa magugu yote, upande wake na upande wa Sikudhani. Kwasababu alikuwa hana pesa, hivyo akamwambia Sikudhani kuwa; nimetoa magugu na nyasi zote shambani  naomba unisaidie hela kidogo ya kununua mbegu ili nipande mazao. Nitapanda hata upande wako. Kwa kuzuiya mmonyoko ningependa kuanza kwa kupanda miti ya maembe pembezoni mwa shamba kwanza. Sikudhani akamjibu kwa dhiaka; “nipishe huko wewe mjinga, sina pesa za kupoteza mimi.”! Sikujua kwa upole na unyonge mwingi akaondoka huku akisema “asante Sikudhani.” mangosmtree2-1Sikujua akatafuta pesa za kununua mbegu kutoka kwa mama yake mzazi akampatia. Japo mama yake alikuwa na shida nyingi lakini hakuweza kumtupa mwanae kwani naye kama ilivyo kuwa kwa Sikujua aliamini kuwa mwanaye atapata kitu kwenye lile shamba na hato hitajika kumsaidia tena. Sikujua alimshukuru sana mama yake si tu kwa msaada wa pesa aliyompatia bali kwa kumsaidia kujihifadhi pamoja na wanawe kwenye kibanda alichokuwa anaishi.

unnamedSikujua akapanda mbegu 20 za mti wa maembe kuzunguka eneo lake tu. Hakupanda hata mbegu moja kwenye eneo la Sikudhani! Kwasababu pale ni pakavu sana basi ilimbidi aende mbali kuchota maji ya kumwagilia ili mbegu zake zisikauke. Sikujua alitembea peku peku kwani alikuwa hana uwezo wa kununua viatu. Pesa alizokuanazo kidogo alinunua mbolea akamwagia kwenye mbegu. Mvua ikaanza kunyesha.

Kwakuwa mvua ilikuwa inanyesha kubwa akahofia mbegu zake kuchukuliwa na maji kwani pale kulikuwa na mteremko. Basi akaamua kwenda kusomba mawe ili aweke pembezoni mwa shamba kuzuiya madhara ya mvua kwa mbegu zake. wakati anarudi kutoka kutafuta mawe akiwa njiani mvua ikaanza kunyesha. Pale hapakuwa na sehemu ya kujihifadhi hivyo ilimbidi aendelee na safari. Aliloana sana.

Akafika shambani na kuweka mawe huku mvua ikiendelea kunyesha lakini hakuacha kwani mbegu zile zilikuwa muhimu sana kwake kuliko kuloana na mvua haswa akikumbuka kuwa pesa alizo nunulia mbegu amepewa na mama yake mzazi ambaye ni mzee na masikini kama yeye! Mvua ilikuwa ni kubwa sana, mbegu 19 kati ya ishirini zilisombwa na maji. Ikabakia moja tu ambayo ilikuwa katikati ambapo ndipo panagawa mpaka wa eneo lake na eneo la Sikudhani. Sikujua hakukata tamaa. Akalinda mbegu hiyo moja. Mti ukawa mkubwa. Sikudhani alipo ona mti unakuwa mkubwa kama ilivyo kawaida yake na dharau nyingi. Akawa anasema “huo wala hauto toa maembe. Huo mti ni tasa hauzai unajisumbua tu!”  

Screenshot_2016-03-31-00-57-12-1Baada ya muda kidogo, mti ule ukaanza kuota maembe. Ukatoa maembe makubwa sana tena maembe “dodo”! Maembe yalikuwa mengi sana na matawi yalikuwa marefu hivyo yalipo anguka chini mengine yaliangukia upande wa Sikudhani! Sikujua akayakusanya maembe akapeleka sokoni akauza akapata pesa za kujikimu.  Mti unaendelea kutoa maembe na Sikujua anafurahia faida anayo pata kutokanana jasho lake. Ameweza kununua ng’ombe anapata mbolea na kuuza maziwa pia anatumia ng’ombe kulimia. Sikujua sasa amejenga na nyumba anaishi na wanawe! IMG_20160406_155652Bahati mbaya mama yake mzazi Sikujua aliugua na kufariki kabla ya mti kuanza kutoa matunda. Alibahatika kuuona ulivyo kuwa mkubwa lakini hakuona matunda yalivyo toka. Hii inamsikitisha sana Sikujua na baadhi ya ndugu zake kwani wanatamani sana mama yao angeona na kuonja matunda angalau kidogo. Mungu si Athumani, Sikujua amebahatika kupata wajukuu. Nao wanapenda sana maembe. Wanafurahiya kunywa maji ya maembe kila siku!  Screenshot_2016-04-06-15-44-08-1Chakushangaza, Sikudhani sasa naye ananyemelea maembe ya Sikujua! Anasema yale yanayo angukia upande wake ni yakwake! Sikujua hataki hata kusikia habari hiyo! Sasa hivi Sikudhani anaumwa anahitaji hela za matibabu matokeo yake anataka achukuwe maembe aende kuuza ili apate pesa za matibabu. Lakini Sikujua hataki kusikia habari hiyo kwani bado anakumbuka matusi, dharau, na dhihaka alizo mfanyia!  Gold+Mangoes+4.JPG-1Siku moja, Sikudhani akamwambia Sikujua kwa sauti ya ukali kuwa; hata kama hilo shamba tuligawana katikati kwaajili ya kulima, lakini hati miliki ya shamba inaonyesha wote wawili ni wamiliki wa hilo shamba. Hivyo nayeye anastahili kupata maembe yaliyopo shambani hapo! Sikujua amekataa na sasa amekimbilia mahakamani kupata haki yake!Screenshot_2016-03-29-08-25-27-1Ni nani haswa anastahili kula matunda kati ya Sikudhani na Sikujua? Na kuna ubaya wowote Sikujua kumkatalia Sikudhani kuchukua maembe? Tafakari kwa kina toa hukumu ya haki na sahii!

Tafadhali: picha zilizo tumika hazina huusiano wa moja kwa moja na hadithi hii.

 

Hot shot of the day

FB_IMG_1459874496611Mr and Mrs Baraka Kissa ndani ya Rock city! Nafikiri hapa ni Tilapia Hotel kama sijakosea. Enjoy your vacation wapendwa ❤❤❤ FB_IMG_1459874517218

Kutoka Facebook

FB_IMG_1459973264324-1Nimependa sana hii picha ya Mwajuma na wanawe. Hawa wanaishi kwa Malkia Elizabeth. Mbarikiwe sana wapendwa