Here are some of the experiences that are worth sampling while you practicing #TheWait – what would you add?
Category Archives: Uncategorized
Autism is not a disease, it’s a condition!
Kwanza naomba nianze kwa kumpongeza sana wifi yangu Veneranda Obure na binamu yangu Dr. Joseph Obure pamoja na wazazi wote wenye watoto wanao sumbuliwa na Autism inchini Tanzania kwa ujasiri wao wa kuweza kutoka mbele ya public na kueleza dunia kuwa watoto wao wanasumbuliwa na ugonjwa ujulikana kama Autism. Sio wazazi wengi wanaweza kujitokeza hadharani namna hii kwasababu ya kuogopa kauli za watu na stigma zao zilizo jaa ufinyu wa fikra!! Hongereni sana.
Nakumbuka mara ya mwisho nilipokuwa nyumbani. Rafiki / jirani yetu wa zamani alinisihi sana kuwa nisiondoke bila kumuona. Basi nami nilifanikiwa kwenda kuwasalimia. Katika kuongea ndipo akaamua ku-share nasi (nilikuwa na mdogo wangu Magreth) kuwa kwa muda mrefu ameangaika na mwanae na alipo mpeleka Nairobi kwa uchunguzi zaidi, doctor akamwambia kuwa mtoto wako ni autistic! Yani kwa Africa huu ugonjwa ndiyo sasa hivi wanaanza kuelewa tofauti na nchi zilizo endelea. Hivyo doctor akikwambia kitu kama hicho kwakweli kwa mzazi inakuwa ngumu sana kuelewa na hujui jinsi gani uchukulie. Hivyo nikitu ambacho rafiki yangu huyu kimemuadhiri sana. Na matatizo yanaongezeka zaidi haswa pale mzazi mmoja anapo kuwa hatoi ushirikiano katika kumuangalia mtoto.
Naomba Mungu ampe nguvu huyu rafiki yangu ili siku moja naye awe jasiri zaidi ya alivyo sasa, aweze kutoka mbele za watu na kushiriki na wazazi wenzie ambao wana watoto wanao sumbuliwa na Autism. What is Autism!
Kuna huyu mwana mama ajulikanaye kama Holly Robinson Peete yeye ni mmoja wa wamama ambao watoto wao wana sumbuliwa na Autism. Kwakweli napenda sana jinsi wanavyo handle hii situation ampaka imemsaidia sana ukuwaji wa mtoto wao tofauti kabisa na doctors walivyo sema. Na kitu cha kwanza wanasema ni wazazi kukubaliana na hali halisi. Halafu kuweza kuwa wazi kwa mtoto toka akiwa mdogo. (Tazama baadhi ya video ?)
Mungu akinijalia uzima mwakani nitashiriki nanyi katika movement hii. I will walk for my darling nephew, mtoto wa rafiki yangu, na kwaajili ya watoto wengine wote wanao sumbuliwa na Autism hapa duniani. Mungu awape mwangaza doctors wanaofanya uchunguzi juu ya ugonjwa huu waweze kupata tiba haraka ?
Hot shot of the day
Natural Hair Movement
https://youtu.be/kURnxOHii7A
June 2015, Bethel and I in Kalamazoo, Michigan. Bethel is rocking her own natural hair ? I am very proud of you all young ladies! Keep up the good work, and let us all embrace the all authentic us!! #NaturalHairMovement
Nunua nguo kwa bei nafuu!
Wapendwa, naomba mtembelee Facebook na Instagram ya Zawadi Kakoschke upate kujichagulia nguo nzuri sana kwa bei nafuu. Ni nguo ambazo ni zake mwenyewe lakini zipo kwenye hali nzuri kabisa kwani hazijavaliwa sana. Muungishe mkono kwani 50% ya mauzo I nakwenda kwenye kutoa msaada ?
Get your ticket!
IT’S OFFICIAL THE MOST ELECTRIFYING SHOW TO HIT THE EAST COAST FEAT. AFRICA’S ARTIST OF THE YEAR -DIAMOND PLATNUMZ LIVE CONCERT IN WASHINGTON DC THIS MEMORIAL WEEKEND SUNDAY MAY 29 @ COCO CABANA CLUB ……… THIS IS THE BIGGEST SHOW TO EVER HIT THE DMV, TICKET LEVELS OUT NOW ? WWW.DIAMONDDC.EVENTBRITE.COM
#AfricasArtistOfTheYear #MTVAwardWinner#BETNominee #AfrimmaWinner #AEAU.S.AWinner#ChannelOWinner #KilimanjaroAwardsWinner #ThisIsIt
Birthday girl night-out with her friends
Someone was feelin’ #22! Get together and had fun with her friends, Kalamazoo, Michigan………Enjoy the pictures
Cyber crime law!
Are you a magician?
Huu ujumbe toka kwa Mombobied umenichekesha sana nikaona ni share nanyi ?? kuna kitu cha kujifunza!……… swali are you a magician? ??? Lakini watu wengi ambao tuna hela ya ‘kuunga unga’ ndio huwa tuna matatizo kama haya!! Haya sasa tujifunze na tubadilike!
Kumbukumbu binafsi!
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Muheshimiwa Samia Suluhu na Mr. Otieno O. Igogo wakipeana mikono baada ya mazungumzo kwenye ofisi ya Muheshimiwa Makamu wa Rais iliyopo ndani ya Ikulu ya Dar es salaam, Tanzania siku ya Ijumaa, tarehe 04 / 01/ 2016Nimeziweka hizi picha humu kwasababu ya kumbukumbu zangu binafsi na pia kwasababu nawapenda watu walioko kwenye hizi picha. Hakuna la zaidi.
Si vibaya kuanza upya-Dina Marios
Wakati na join Efm @efm_93.7 nilipata support ya watu wengi na pia nakumbuka watu wengi zaidi walinicheka na kunong’onezana amepotea, amefulia ni ndio basi tena. Ametoka radio inasikika mikoa mingi Tanzania kaenda karedio kidogo kanasikika Dar tu na Pwani. Na inawezekana hadi leo bado wanacheka na kuponda.
Kwenye list zilikuwepo radio kubwa tu zilizopenda kufanya kazi na mimi. Kwa hali niliyokuwa nayo nilikaa kwa Kina na kufanya maamuzi. Nilishaanza kuboreka na redio lakini Nilifanya research zangu kitaa na uongozi wa Efm93.7 @efm_93.7 nilishakutana nao mara kadhaa kisha nikafanya maamuzi.
Nikasema Yes naanza upya tena kwenye radio ndogo na mpya na nina ona bright future ahead. Sio vibaya kuanza upya kwenye maisha na sio lazima kukariri formula ile ile au wasemavyo watu angeenda BBC sijui safari ya maisha yako ipo mikononi mwako.
Kuna ndege anaitwa Tai ndege huyu huruka juu sana, ana nguvu sana na akiwa juu anaweza kuona hadi chini. Ndege huyo kuna wakati manyoya yake na mabawa huzeeka anakuwa hawezi kuruka tena vizuri yaani anakuwa fala tu. Anachofanya anajificha kwenye mapango anajipiga piga mpaka manyoya yote yanatoka mwilini kisha yanaanza kuota upya. Yakisha jaa anatoka mapangoni akiwa kazaliwa upya na anaruka tena juu zaidi mabawa yakiwa na nguvu zaidi.
Kuna wakati kwenye maisha inabidi uwe kama Tai. Anza upya, tafuta nguvu mpya, unakubali umepigika then unaanza upya. Efm nimekutana na vijana bado wana nguvu, ari na kiu ya kufanikisha nimejifunza kutoka kwao na wanajifunza kutoka kwangu. Ni miezi 7 sasa toka nimeanza hapo I feel new, spirit yangu imeamka upya kama wakati ule naanza 2005_2006
Leo Efm 93.7 @efm_93.7 imetimiza miaka 2 na bado mambo mazuri na makubwa yanakuja my big boss @majizzo na vijana wake hawataki utani TUNALISONGESHA
#tunalisongesha HAPPY BIRTHDAY EFM
Mr and Mrs Odinga ndani ya Chato!
Mr. Raila Odinga akitua kwenye Helicopter ndani ya mji wa Chato kwa Rais Dr. Magufuli. Ukweli: ukiwa na mtu mmeshibana kwa miaka mingi halafu hata wazazi wako hawajui au hajawahi fika kwenu. Basi huyo si rafiki ni “shoga” yako tu wa kusaidia maisha ‘kimujini mujini’ Rafiki lazima atajua kwenu na wakwenu watamjua!! Karibu Chato shemeji, hapa ndiyo kwetu. Jisikie hupo nyumbani ?urafiki wa Dr. Magufuli na Mzee Odinga ni wa miaka mingi sana. Na leo hii amekuwa mtu wa kwanza (kwa viongozi / politicians) kutembelea Chato akiwa kwenye likizo yake ya kwanza. Hii inamaanisha kuwa Mzee Raila Odinga ni rafiki wakaribu sana na Dr. Magufuli au naweza sema ni ‘mabest friend’ kwa lugha ya kimujini mujini ?Raha sana kuwa na rafiki mliye shibana namna hii! Mama Magufuli anakula matunda ya uzao wake japo umri umekwenda. Lakini lazima atakuwa anamshukuru Mungu kwani kamuwezesha kuyaona matunda ya uzao wake kwa macho yake yeye mwenyewe na si kwa kusimuliwa. Hongera sana bibi. Na urafiki wa watoto zako udumu mileleWalitoa heshima zao kwa kaburi la baba mzazi wa Dr. Magufuli……kwaheri ya kuonana. Karibuni tena
Meet Ninon Marapachi: Tanzanian ‘gemstone’ shinning brightly in America!
Source click here
Usiamini katika wakati
Usiamini katika Wakati kwani Wakati waweza kukudanganya… Wakati waweza kukufanya ukawa mpumbavu… Wakati waweza kukurudisha nyuma… Wakati waweza kukufungia milango ya Baraka…. Wakati waweza kukupotezea muda….
Usiamini kwamba ukiishi na MTU miaka 20 ukampa moyo na mwili wako wote ukaongeza na maini na wakati wako wote basi ndio wako milele na hatakutenda….
Usiamini ukimzalisha /ukimzalia watoto 10 ndio wako wa maisha… Na Hata akikunyanyasa na kukutenda uendelee kumpa muda na kumuamini ukiamini atabadilika….
Usiamini katika wakati kwani wakati hauna fursa… Binadamu tunazo fursa…. Usiamini katika wakati kwani wakati haufi… Binadamu tunakufa… Usiamini katika wakati kwani wakati hauzeeki… Binadamu tunazeeka (japo najua wengi hatupendi uzee?)…
Usiamini katika Wakati… KAMATA FURSA pale ulipo… Usiamini katika wakati LIVE YOUR LIFE we just live once…. Usiamini katika wakati JIAMINI MWENYEWE…..
Hot shot of the day
My darling daughter, looking HOTTy ❤❤❤
Birthday girl katika mapozi:Happy 22nd birthday mwanangu mimi!
#MyDaughter #MyOnlyOneChild#MyNumberOne #MyFirstBorn #MyLastBorn #MyHeartBeat #UzaoWaTumboLangu #MtotoWaUjanaWangu
She is all grown and classy! Hey! Always remember money doesn’t buy class you got to learn it from someone! better tell em you learned it from your mama ?? You made me experience the joy of motherhood! Asante sana, nakupenda sana.you are gorgeous my darling daughter ❤❤ ??? Awiiii! ? Mwanangu mzurijee!! ? you God! Happy birthday gorgeous! I love you uuuuuu!
❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤
The Lyimos
Familia ya Lyimo katika mapumziko nchini Canada. Jamani kazi na dawa eeh! Si mmeona hata Dr. Magufuli kaenda vacation Chato ?? ndio maana yake! Mtu ukisha fanya kazi sana sharti upumzishe mwili na akili. Pia ndo muda muafa wa ku spend quality time na familia. Mjifunze jamani kutoka kwa wenzenu, family is everything! Hapana chezea musichana toka kanda ya ziwa wee! Kitu kutoka Majita hiki ? when mama is happy, family is happy too! Always make sure mama yupo happy in the house! #MkeMwema #MamaMwema ubarikiwe milele zote ? Prince Amani na wazazi wake. Safi sana. Nice family. Mfano nzuri sana wa kuigwa haswa familia hizi za ‘majuu’ ambapo naona wakaka wengi wa Kibongo hawajui what does it mean to be a family man and does it take to be one!! ?? Pendeza sana kaka na dada. Mbarikiwe sana The girls themselves! Pendeza sana mama na mwana. Mnafanana hadi mapozi Asante sana familia ya Lyimo. Enjoy your vacation, na mrudi nyumbani salama. Mbarikiwe sana
Blessing katika ubora wake!
Mwe! Blessing kwa raha zako binti wa O.O Igogo ? haya bwana wee kula raha acha siye wengine tubebe “mabox” kwani mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe ??wacha wee! Pendeza sana ? taratibu Blessing, Usije ukajikuta na wewe ni “jipu” unaitaji kutumbuliwa ???? haya bwana ??
Kutoka Facebook
Leo kutoka Facebook nimependa hizi picha za mtani wangu! Katufanyia surprise ya mwaka?? yani huyu Muhaya kaenda nyumbani kwetu Utegi, Rorya, Mara akapiga na picha mbele ya nyumba yetu halafu akaja kuzirusha Facebook! Kweli wewe Muhaya kiboko!!! Au ndo una nyemelea ‘makaratasi’ ya Utegi??Mtani asante sana kwa kufika nyumbani kwetu. That place is so dear to my heart! That is where I call it home! Hapo ndipo nyumbani my friend huko mjini mie nimeenda kufanya shopping tu kidogo nitarudi ?? ubarikiwe sanaaaaaa mpaka ushangae ?
Jumaa Mubarak
Jumaa Kareem wapendwa, Sabato njema, na JumaPili njema. Mbarikiwe wote. …….Keep love around you all the time! ❤❤