Category Archives: Uncategorized

Ni ujinga zaidi kutegemea pesa za misaada!

FB_IMG_1459455577520

Hot Shot of the day

FB_IMG_1459426513052Lilian looking beautiful! Kapendeza sana, pia rangi ya nguo is one of my favorites. Ubarikiwe sana.

Watoto wengine ni majanga!

FB_IMG_1459386353030Jamani, hivi vitu huwa vinatokea kweli japo vina chekesha. Kuna watu kadhaa ambao nawafahamu walikuwa na majina makubwa mjini, pesa za kumwaga (mafisadi wa Serikalini), watu wana wanyenyekea kama Mungu vile lakini kwao wazazi wanaishi kwenye nyumba ya udongo ??  Siku moja akafiwa na baba yake mzazi mmh! Kaenda kwenye msiba aibu tupu, yani hata yeye mwenyewe pakulala alikuwa hana ikabidi awe ana lala ndani ya gari! ??

Kuna mwingine yani yeye sasa alikuwa akija kwenye misiba ndo sehemu yake ya kutoa mashauzi na michango mikubwa kwa dharau ya kuwa yeye ndo ana pesa zaidi. Basi siku moja watu fulani (kumbe walimpania) waka ‘mnywea’ pombe. Basi alipo anza mashauzi yake tuu wale wababa wakasimama na kuanza kumzodoa. “Unajifanya unapesa hapa mjini wakati mama yako anaishi kwenye nyumba ya udongo iliyo ezekwa kwa manyasi! Ipo siku moto utashika nyumba na kumkaanga mama yako kama ngenge (sato)!!” ??? yani walimchambua kama karanga hadi yule baba alilia. Baada ya hapo mbona alienda mjengea mama yake nyumba nzuri yenye paa ya mabati ?? chezea vichambo vya wajaluo wewe??  Yani alimtoa mkewe aende kijijini kusimamia ujenzi kwa miezi 3 nyumba ikasimama ?

Kuna mwingine huyu ni kizazi cha “.com”! Kutwa yupo busy kupost picha za kwenye Facebook, na Instagram yupo kila kona ya dunia hii anakula na kulala kwenye mahotel makubwa na mume wa kizungu. Kuvaa expensive designers cloth. Wakati wazazi wake maisha yao mmh! Yeye akija TZ anafikia hotelini na familia yake. Wazazi ndo wanaenda kumsalia hotelini. Zinapigwa picha za kumwaga zina rushwa mtandaoni ??? Hawa ni watoto walilelewa katika maisha mazuri kweli kweli enzi hizo. Lakini wazazi wao hawakujali kabisa maisha ya wazazi wao kijijini watoto wakike ndo walio simama na wazazi wao!

Ujumbe: Tuwajali wazazi wetu. Na pia wazazi wakumbuke kuwa watoto hujifunza kwa kuangalia wazazi wao. Kama wewe mzazi humjali mzazi wako basi tegemea hayo hayo kutoka kwa watoto wako.

Sasa ngoja niwaulize nyie Wahaya mlioko kwa Obama, je wazazi wenu wana nyumba au mnaleta ubishoo tuu hapa ???

Hakuna Matata Kitchen

Screenshot_2016-03-31-08-57-05-1Wapendwa wasomaji wangu mlipo pande za kwa Obama, kuna dada yetu huyu amefungua home business yake ya kupika ambayo inaitwa Hakuna Matata Kitchen, yenye makao makuu yake mjini Austin, TX, USA Screenshot_2016-03-31-08-56-28-1Basi naomba wapendwa tu ‘like’ page yake kwa Facebook. Napia tumuungishe mkono mwenzetu. Binasfi bado sijakula vyakula vyake kwani nilikuwa simfahamu. Usihofie sana kuhusu utamu wa vyakula kwani vitu vizuri vinaonekana hata kwa macho tuu! Mpangilio (presentation) yake yatosha kutoa ushuhuda. Nipo jiani ku order vitu tofauti halafu nje nitowe hushuhuda wangu humu. Simnajua mie sipendi kutowa hushuhuda wa uwongo?? Screenshot_2016-03-31-08-56-47-1Wenyewe wana safirisha order yako popote pale ndani ya America. Japo sina huwakika kama unaweza kukaa na kula hapo kwake. Mfatilie kwa ukurasa wake wa Facebook kujua mengi.Screenshot_2016-03-31-09-00-39-1

Kutoka Facebook

FB_IMG_1459448207019-1Leo nimependa picha hii ya my schoolmate kutoka Kowak Girls Secondary school.  Yeye anaitwa Angela anaishi Musoma, Mara……… Angela pole sana kwa msiba wa baba. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele. Na baba aendelee kupumzika katika amani ya Bwana ?

Happy belated birthday Vivian

Screenshot_2016-03-31-13-22-03-1Happy belated birthday to darling niece Vivian. So sorry I missed your big day but you know I love you and wishing you the best of all that your heart desires. May you grow older to conquer the world! Happy birthday gorgeous. We all love you ?❤❤❤

What’s the best time to see the doctor?

Alot of times I hear  people says , they are students or don’t have money or still in debt  , so  they can’t see  financial advisor! My response is, what’s the best time to see the doctor?  When sick or when well? You talk to us when you are sick, broke, in debt, no saving, confused, …… coz we can help you get out of that but of you keep ignoring or assuming things will change without seeking help? …... Goodluck. 

MS. Betty Achapa-Financial and Tax expert in Houston, Texas
MS. Betty Achapa-Financial and Tax expert in Houston, Texas

THIS IS MS. B, INBOX ME FOR FREE ONE ONE ONE, WEBCAST OR PERSONAL

“Kilimo na ufugajI kwanza”

 

Screenshot_2016-03-31-07-52-23-1

MUONGOZO WA UZALISHAJI WA PAPAI UTANGULIZI

Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.

Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.

KUHUSU MPAPAI: Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu

i) Mpapai wenye maua kiume tu ii) Mpapai wenye maua kike tu iii) Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya)

Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.

Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.

UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI

Miche ya mpapaiKatika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika: –

1. Mbegu za Kawaida (Local seeds)

Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote. Hivyo itakulazimu kung’oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.

2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)

Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaoja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1, MALAIKA F1 n.k.

Upandaji

Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.

Mbegu ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.

Kitalu cha mipapai

BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI

Mpapai upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5.

yInapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi.

Kiaisi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda. Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yalioja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu.

Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.

UANDAAJI WA SHAMBA

Njia ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba.

Nafasi

Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.

Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba shimo.

NB: Kiasi cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekari ( 400 hadi 800 kwa ekari)

Kupanda mimea shambani

Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.

shamba la mipapai

Uwekaji wa mbolea.

Zuia matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbole gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phospate kwa kaisi kikubwa. Mfano; – 12:24:12. (NPK)

Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK)

Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.

UmwagiliajiMaji ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji niya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.

Magugu

Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.

HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI

Kitalu – Wiki 1 – 6

Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa shamba – wiki 7 -16

Maua na kuweka matunda – wiki 17 – 21

Kukua kwa matunda – 22 – 26

Mavuno ya kwanza – Wiki 37 nakuendelea ……………..Screenshot_2016-03-31-07-54-03-1-1Wapendwa wasomaji wangu, kama wewe ni mpenzi wa kilimo, ufugaji, au unapenda kununua / kuuza vitu organic toka shambani, basi unga na na hili group ☝ huko Facebook ili uweze kujiona mambo mbali mbali yanayo fanywa  na wengine.

Lilian katika harakati za kupungua!

2016-03-31 08.52.42Lilian katika harakati za kupunguza mafuta na maji mwilini. Najua kuna mtu atawaza eti “maji mwilini”! Yes! Siyo kila mtu mnene anamafuta mengi mwilini mwake. Wengine ni wanakuwa wana maji zaidi kuliko kiwango cha kawaida ambacho mwili utakiwa kubeba! FB_IMG_1459426856621FB_IMG_1459426830073Hizo picha hapo juu ☝ ni picha za mwaka jana (2015)  na hivyo ndivyo alivyo kuwa. FB_IMG_1459426625020-1Hii ? alipiga mwanzo mwa mwaka huu (2016) . Kapendeza sanaFB_IMG_1459426505974-1hapa ni picha yake ya sasa FB_IMG_1459426351487Yeye amekakazania sana mazoezi ya nguvu pamoja na diet. Screenshot_2016-03-31-07-14-17-1Naona ana ruka kamba, anaogelea sana, ana kimbia, pamoja na mazoezi mengine kama kuendesha bicycle………. Hongera sana Lilian.

#TBT

FB_IMG_1459433658131#TBT #Home #KekoJuu

….. Nimesahau mwaka lakini ni kati ya mwaka 88 na 89. Mmh! Nilikuwa “kipotabo” lol!

Hot shot of the day

Screenshot_2016-03-29-13-09-55-1Wee Zari weee! Jamani hizo sasa sifa kha! Si kwa uzuri huo jamani ?? em legs gal! Awiw! Too cute for a word ?? ………… Enjoy your tour mama Tee, waiting to see you in Dallas ??

Mother and daughter moment

FB_IMG_1459292116133-1Nimependa sana hizi picha za Sandra Mushi na mama yake. #NaniKamaMama Pendeza sana  FB_IMG_1459292101845-1wazurije sasa. Too cute! mbarikiwe sana

A word of wisdom

Not everything that happens to you is bad. Maybe God allows some things to happen because of the good He is trying to do in your life! You might be going through a difficult time right now but TAKE HEART – God will lead you THROUGH IT! #DeVonFranklin #motivation #inspiration #takeheart FB_IMG_1459292361302

Special edition: Mr and Mrs Dangotes katika ubora wao!

Screenshot_2016-03-29-13-10-50-1Awii! Aren’t they cute! wamependeza sanaaaaaa!Screenshot_2016-03-29-13-11-14-1 ??? si kwa mapozi haya jamani kha! Screenshot_2016-03-29-13-11-42-1Sasa hapo ulikuwa unaimba ‘Zari lala’ badala ya “Latty lala” lol! Screenshot_2016-03-29-13-11-06-1Pendeza sana baba Tee na mama Tee wa ukweli ❤❤

Jamani ratiba ya tour si mmeiyona? Kama bado tazama hapa ? hutakiwi kupitwa na hii history ? Screenshot_2016-03-29-13-25-32-1

Father and daughter moment

Screenshot_2016-03-29-18-27-39-1Precious little girl how cute you are!!  Wow! Huyu mtoto ni mzurijee jamani! Naona aliumbwa asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma baada ya mapumziko ya Sabato. Yani Mungu akiwa fresh hajachoka ?? really cute! Mbarikiwe sana wazazi wake. Na Mungu awalindie mwanenu ?

 btw huyu kaka ndiyo promoter anaye mletea Diamond na ma super star wengine hapa USA

Father and twins moment

Screenshot_2016-03-29-13-13-03-1Awii! Aren’t they cute! Dr. Mengi na vijana wake. Wapendezaje sasa, usinicheke hata majina yao siyajui ?? lakini hiyo haitoi ukweli kwamba ni ma-handsome wa nguvu! Mungu awabariki.

Ngoja nitumie nafasi hii kuongelea jambo fulani ambalo nililiandika humu wakati fulani mwaka jana. Niswala ambalo lilikuwa linahusu family ya Dr. Mengi haswa kuhusu ndoa yake na K-Lynn Screenshot_2016-03-29-18-29-43-1These boys are adorable! Super cute!…. anyway tuendelee na story yetu ? Basi katika kujifanya mimi ni mmoja wa wanaojua kutoa kasoro na ushauri kuhusu familia za watu sinikaandika kuhusu habari ya K-Lynn na Dr Mengi! ?? mbona nilikoma!! Mara naangalia simu nakuta missed calls kibao kutoka home kwa mama Igogo. Watsup msgs ndo usiseme! Akasema nifute haraka sana hiyo post na hata mtu aki  Google asiipate! ???

Mbona ilikuwa balaa! Mdogo wangu Magreth toba! Yeye ndo alikuja juu kweli kweli utadhani Dr Mengi ni baba yake mzazi ??? Anyway to make a long story short, Mama yangu alicho nisisitizia ni kuwa hata siku moja nisije weka  post humu kuhusu matatizo ya familia ambazo hazinihusu!! Niache mara moja, na kama nikitaka kuandika basi niandike matatizo ya familia yetu na si zawatu  wengine!!……. yani nilikosa raha nika muandikia my cousin-sister Sophia Makoyo msg (inbox) kwa Facebook, soma ? Screenshot_2016-03-29-08-27-32-1Tokea siku hiyo sijawahi kuandika kitu chochote kile juu ya K-Lynn na Dr. Mengi mpaka hivi leo. Nawala sito kaa tena kuzungumzia matatizo ya familia yoyote ile ambayo hainihusu unless nimeitwa mahakamani kutoa ushahidi!! Screenshot_2016-03-29-13-13-27-1Haha! Nilijikuta nime ‘kula’ block kwa Instagram ya K-Lynn lakini naelewa na hivyo mbele yenu nyinyi wasomaji wangu, na mbele za Mungu naomba leo niwaombe rasmi msamaha K-Lynn na Dr. Mengi’s family kwa ujumla wao. Naomba mnisamehe sana for my lack of wisdom and respect to your family. Nilikosea sana kuingilia maswala ya familia yenu wakati hayanihusu hata chembe! Natoa ahadi, sito rudia tena. Na si kwenu tuu bali kwa mtu yoyote yule. I hope you will find a place in your heart to forgive me. ?

Ushauri wangu kwa wasomaji wangu wote ni kwamba; maswala ya familia ni maswala sensitive sana, ni maswala personal, ni maswala ambayo yapo very complicated. Hivyo kama wewe si muhusika wa moja kwa moja wa hiyo familia basi keep your nose out of it!! Tujifunze kuheshimu na kulinda familia zetu. Hata kama hiyo familia ipo machoni kwetu 24/7 hiyo haitupi huwalali wa sisi kuingilia na kutoa ushauri wa nini kifanyike katika hiyo familia, kwani “kitanda usicho kilalia hujui kunguni wake.”!! Halafu sisi tunapo ziongelea hizo familia hakuna tunalo saidia zaidi ya kuongeza matatizo, chuki, na kuumiza wahusika zaidi. Matatizo ya familia yatatatuliwa ndani ya familia na wana familia wenyewe.

Kila familia hapa duniani ina matatizo yake! Sasa sisi ni akina nani hata tunyooshee familia zingine vidole wakati matatizo ya familia zetu wenyewe yanatushinda?! Hata mimi mwenyewe nipo over protective when comes to my child, parents, and family. Yani dare not to mess up with my family! Kwanza nitakuuliza who the heck are you!!  If you’ve never walked even a single mile in my shoes, you have no say in my world!! Just find a seat somewhere on the corner and zip it!!

Mungu azidi kuzibariki na kuzilinda familia zote hapa duniani ? much love to K-Lynn and Dr. Mengi’s family ?❤

Mother and son moment

Screenshot_2016-03-29-08-25-27-1Mama Dangote na Dangote kwa raha zao ati ndani ya mitaa ya Europe . Mmependeza sana. Mbarikiwe mno

Mother and daughter moment

Screenshot_2016-03-28-22-15-49-1Mwamvita Makamba na binti yake Malaika. Wamependeza sanaaaaaa! Hii ilikuwa juzi kati siku ya 10th birthday ya Malaika.  Walinoga mno!………..jamani mimi ukija kwenye mambo ya ‘theme’ za birthday za watoto ni sijui kabisa! Nafikiri pia mimi kutokuwa mtu wa party-party imechangia zaidi. Basi hapa idea tu sina kuwa hii ilikuwa theme ipi ?? ngoja ni confess ??sijawahi kumfanyia mwanangu birthday party ??yani siku zote nitampeleka dinner yeye na marafiki zake pamoja na baadhi ya marafiki zangu, lakini si party.  Na hii tabia naona nimeitowa kwetu. Sisi huwa tunapenda kwenda dinner as family au saa nyingine tunatoa order ya catering wanatuletea nyumbani…………… anyway, mbarikiwe sana

Wapendwa, Mwamvita pia ana blog inakwenda kwa jina la www.mwamvitamakamba.com pita uione.

Hongera sana Flaviana Matata Foundation

Screenshot_2016-03-29-08-22-17-1Screenshot_2016-03-29-08-21-29-1Screenshot_2016-03-29-08-21-42-1

Wapendwa wasomaji wangu, naomba wote mlioko Bongo kama una mtoto na anakwenda shule. Basi ukitaka kununuliwa vifaa vya shule na pamoja na madaftari na school bags, tafadhali tafuta ambavyo vinywa na Flaviana Matata. Vile vyenye logo ya Flaviana kwani kwa kufanya hivyo tunasaidia kutunisha mfuko wa Flaviana Matata ambao inasaidia ndugu zetu walioko kwenye mazingira magumu.  FB_IMG_1458142752494

Hongera sana Flaviana Matata Foundation kwa kazi nzuri mnayo ifanya ya kusaidia jamani yetu haswa wasichana. Mfano mzuri sana wa kuigwa.

Mother and sons moment

Screenshot_2016-03-29-13-06-44-1Kiki Zimba na vijana wake. Priceless! Mbarikiwe sana