Napenda salamu hizi za kheri ya siku ya kuzaliwa zimfikie mama yangu mkubwa Mrs. Musira, aishie pale maadadui wa Kamnyonge, ndani ya jiji la Musoma. Miaka 72 katika duniani hii ya Musa si mchezo ati! Mungu aendelee kukulinda, akupe nguvu, afya tele, na furaha moyoni mwako. Happy 72nd birhday to you! Ubarikiwe sana mama!
Category Archives: Uncategorized
Family time-sisters sisters!
Hongera sana Bernard Chisumo!
Hongera sanaaaaaa Bernard Chisumo kwa kwa kimaliza masomo yako ya degree ya kwanza na pass with flying colors “Honors” Mungu azidi kukubariki sana wewe na familia yako, akakujalie zile ndoto zako zote zitimie . Amani, upendo, na furaha vikatawale nyumba yenu siku zote. Hongera sana shemeji yake na mimi ?? Bernard amehitimu degree yake ya Computer Science in Software Engineering kutoka katika chuo kikuu cha Surrey kilichopo katika inchi ya Malkia Elizabeth! Familia yake nao walikuwa kumpa hongera baba kwa hatua aliopiga kama wanavyo onekana kwenye picha. Kwenye picha ni Bernard, mke mwema, na watoto wake Bernard. Binti kipenzi, naye alifuraha sana, kwa kusema ‘congrats dad, you made me proud’! Like father like son! Naye ametoa ahadi za kufuata nyao za baba yake. Kwamba nayeye lazima siku moja alivae hilo John na kofia kama baba alivyofanya. Hongera sana shemeji yangu, ubarikiwe sanaaaaaa milele zote!
Family time-the Mabadas’
Happy birthday Mama Ngonyani!
Kheri ya siku ya kuzaliwa kwako dada yangu mama Ngonyani. Mungu akulinde, akupe afya njema, upendo, amani, na furaha nyingi mno. Ukaishi maisha marefu, ufanikiwe kuwaona wajukuu na vitukuu vyako! Upendo na Amani vizidi kutawala katika ndoa yenu. Mimi nashukuru sana kwa Mungu kwa kuniwezesha kufahamiana na nyinyi. Upendo wenu kwangu mimi na mwanangu ni mkubwa sana. Na nasema asante kwa upendo wenu mbarikiwe mara dufu! Mkabarikiwa sana nyinyi na uzao wenu wote. Happy birthday Mama Magreth and Cynthia. Enjoy your day!
Hot shot of the day
A million dollar smile!
Mjane wa Deo Filikunjombe awashukuru Watanzania!
Kwakupitia account yake ya IG mjane wa Filikunjombe ametoa shukran zake za dhati kwa Watanzania wote walioguswa (kuna wengine hawakuguswa kama Joyce Kiria) na msiba wa mumewe. Amesema yeye hana chakuwalipa kwa upendo na ukarimu walio muonyesha. Pia wale ambao hawakuguswa na kifo cha mumewe nao amewashukuru. Na wale ambao hawakuguswa nawakaona njia pekee ya kumfariji ni kumuongezea machungu kwa kumuongelea mme wake vibaya nao amewashukuru kwa kusema amemuachia Mungu! Soma ujumbe wake hapa chini ? Mjane wa Filikunjombe ameumizwa sana na maneno ambayo Joyce Kiria wa Wanawake Live Show aliyasema kwenye social media kuhusu nyumba ya marehemu. Joyce bila huruma wakati watu wakiwa wanakusanyika kwa msiba wa Deo pale nyumbani kwake Mtomi Kijichi aliandika post ambayo ilikuwa ikionyesha nyumba ya marehemu na nyumba mbovu ya manyasi kama mfano wa maisha ya mwanasiasa wa CCM na maisha ya Mtanzania wa kawaida! Hiyo post aliandika kama ifuatavyo:- ? Joyce Kiria, wewe unajiita “Super Woman” kwakweli mimi nakuita ‘Super Mchawi!!’ kwani uliyo yatenda ni uchawi mtupu!! Yani wewe mwenzako kafiwa na mumewe katika ajali mbaya namna ile, kaachwa mjane wakati angali “mdada mbichi” kabisa na watoto wadogo watatu wote wakiwa chini ya miaka kumi na nane!! Lakini hayo yote hukuona cha kuongelea isipokuwa nyumba yao?! Kweli?? Unajua mchawi si lazima atembee na hirizi na tunguli shingoni bali matendo na maneno yake yanatosha kuwa mchawi!! Na wewe ume-qualify kuitwa Mchawi!! Jifunze kufurahia maendeleo ya wengine, bariki wengine nawe utabarikiwa. Kila mtu anafungu lake ambalo Mungu amemuandalia; lini na wapi atakupa hiyo ni siri yake Muumba! Kwahiyo usiumie sana kuona wenzako wamebarikiwa sasa kama nawewe ungeacha roho ya kichawi labda Mungu naye angekubariki wakati huu. Lakini kwa roho hii utangoja sanaaa!! Halafu hujui watu wamepitia wapi mpaka kufika hapo walipo ‘when you see the glory ask for their story!’ Shame on you!!
Pole sana mjane na watoto wako, pamoja na ndugu, jamaa, marafiki, na Watanzania wote. Mungu awape faraja na nguvu ya kuhimili kipindi hiki kigumu. R.I.P Mh. Deo Filikunjombe.
Mrs Nyongo!
Happy 66th birthday Mama Kachare
Kheri ya siku ya kuzaliwa mama yetu kipenzi, wajina wa mama yangu. Hongera sana kwa kutimiza miaka 66 ya kuishi katika dunia hii. Unapongezwa sana na pia wanamshukuru Mungu sana kwa uwepo wako katika maisha yao kutoka kwa watoto na wajukuu zako wote. Sote tunakuombea maisha marefu zaidi, yalio jaa amani, furaha, na upendo. Ubarikiwa sana. Happy birthday mama!
our very first female Vise President!!
What a joy! Watanzania kwa mara ya kwanza wamemchagua Makamu wa Rais mwanamke! Hili nitukio la kihistoria katika nchi yetu ambayo hajawahi kuwa hata na Waziri Mkuu mwanamke!! Hii ni ishara ya ukombozi wa fikra kwa jamii yetu kuwa wanawake nao wanaweza! Hongera sanaaaaaa Mh. Samia, najua utalitumikia vyema taifa letu.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa na watu wake.
Tanzanians have spoken, let everyone say Amen!
Well, well! It wasn’t an easy race, but finally the people of United Republic of Tanzania have loudly and clearly spoken! Let everyone say Amen! Congratulations to the President elect Dr John Pombe Magufuli. People of Tanzania have so much faith and believe in you. You are the change they sincerely need. I hope you will never let us down as you have said before. Many God guide you in every step of the way.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa na watu wake.
Furaha ya dunia
The Kakoschkes’
Kwanza nianze kwa kusema happy belated birthday baba Amika. Mr Kakoschke alisherekea birthday yake siku chache zilizopita. Alixungwa na familia yake ambao anawapenda sana na yeye anawapenda sana. Naona Malaika yeye kajichokea na kujilaza kabisa. Hapa walikuwa ndani ya treni wakielekea sijui wapi, nimesahau ?? Hawa watu wanasafiri sana. Wanapenda kusafiri na all outdoor adventures. Tembelea blog yao kuona picha nyingi nzuri sana na kujua maisha yao. Nenda wwww.maisafari.com ukaone dunia japo kwa picha. This Velvet Strawberry cake looks delicious! Yummy!
Hot shot of the day
This is too cute, hot indeed! Mh. ShyRose Bhanji akiruka toka kwenye boti wakati wakitokea maeneo ya Musoma vijikini wakati wa campaign. Naamini kwasababu sasa kampeni zimeisha basi haita kuwa mbaya kwa mimi kuweka picha kama hii. Kwani hii natambua na ludhamini wasomaji wangu wote bila kujali dini zao, kabila, wala itikadi zao.
Mother and daughter moment
Hot shot of the day
My cutest babysister!
Alicia 4th birthday party
Princess Alicia akiwa anameremeta teyari kwa kusherekea birthday yake siku ya Juma Mosi. Alicia birthday yake ni 10/08/ lakini party yake ilifanyika siku ya Saturday kwasababu birthday iliangukia katikati ya wiki. Kusoma post ya birthday wishes yake bonyeza ? theme ya birthday ilikuwa ni mambo ya ‘princess’ party ! Pendeza sana
Alicia you are too cute! Eddah Gachuma na princess wake. Mziwanda huyu kipenzi cha mama. Princess Alicia na daddy ake. Hongera Vincent ila hapa “Germany shepherd” itahusu sana na fancy ya umeme ?? Mamkubwa naye hakubaki nyuma. Gatty Gachuma na niece yake. Mmependeza sana. Mama na wanawe, mmependeza sana Hongera da Eddah, umekuza haswa Hongera sana wazazi kwa kumuandalia binti party nzuri sanaaaaaa…………..Happy 4th birthday Princess Alicia. God bless you.