Category Archives: Uncategorized

Birthday wishes

FB_IMG_1441031960530Kheri ya siku ya kuzaliwa kaka yangu kipenzi Noah Manongi! Niseme nini mimi Alpha?! Baba wa Mbinguni anajua yote yaliyopo ndani wa moyo wangu jinsi ninavyo kushukushuru kwa uwepo wako katika maisha yangu huku nilipo mbali na familia yangu! Umekuwa Nami kaka yangu katika tabu na raha, umekuwa nami hata pale ambapo mimi  mwenyewe nilikuwa sina imani nawe. Umesimama nami bila kutetereka hata pale baadhi ya marafiki zako walipo geuka na kunijengea chuki ambazo hazielezeki! Kaka yangu wewe hukuniacha kwani wanijua mimi jinsi nilivyo  na hukuogopa wala kuona haya kusimamia ukweli! Niseme nini kaka yangu? Kwakweli sina cha kusema zaidi ya Asante! FB_IMG_1441031782827Katika siku hii ya leo, siku ya kuzaliwa kwako kaka yangu, namwomba Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema azidi kukulinda, siyo akubariki bali azidi kukubariki kwani wewe teyari ulisha barikiwa! Mungu akupe afya bora, amani, furaha, na upendo ndani yako na ndani ya familia yako. Hekima yako na upendo  wako vikapate kuongezeka maradufu! Ukaguse na kubariki maisha ya watu wengine kama ulivyo fanya kwangu mimi. Happy birthday my brother. Love you deep!

Hot shot of the day

FB_IMG_1440626325986Mwajuma a.k.a Mwaju! Looking hot like never before! FB_IMG_1440625506263After 3 kids and still flying like this?! What else do you want ma dear ?? just beautiful!


 

 

 

 

 

 

#TBS

FB_IMG_1440913223538-1My brother Noah Manongi! Sina huwakika na mwaka ila ni kati ya 2006 au 2007  summer time. Hapa ilikuwa siku ya Send-off party ya Regina Mugetta, Benton Habour, Michigan.  Pembeni nilikuwa mimi sema nimejitowa sikupenda nilivyo toka nilikuwa nimeshangaa sana ??

Hotuba ya Mwalimu Nyerere kuhusu vyama vingi

Embu msikilize marehemu Mwl. Nyerere halafu wewe mwenyewe utafakari na kutafsiri ulivyo elewa!

“Double Life”

imagesWatu ambao wamesomea na wanafanya kazi za upelelezi wa hali ya juu ndio tumezoea kusikia au kuwaona wakiishi maisha ya siri ambayo hayatoi huwasilia wa yeye ni nani. Hii nikutoka na sababu za kiusala wa maisha yao pamoja na kupata ukweli halisi wa jambo wengi inabidi wa-prented maisha yao. Kwamfano; mtu anaweza akaishi maisha ya chini sana (low profile) siyo kwamba hana uwezo ila nikwasababu hatakiwi kuwapa watu matamanio ya kumjua na kuanza kumfuatilia; hivyo hawa tunasema wanaishi “double life.” Lakini vile vile kuna watu ambao wanaishi “double life” siyo kwasababu ya kazi wanazo zifanya bali wanakuwa na maisha fulani ambayo si mazuri labda kwa familia yake, marafiki, ndugu, wafanyakazi, na jamii inayomzunguka. Maisha ya “double life” siyo tatizo la njisia moja tu, la hasha! Ni tatizo kubwa ambalo lipo kote kwa wanaume na wanawake hambao huficha siri za ajabu kutoka kwa wake walio karibu nao. Katika kundi hili tunaweza kuligawa katika sehemu kuu tatu:-are-you-living-a-double-life Continue reading “Double Life”

Kutoka Facebook

image-1Nimependa sana hii picha ya Tabu Obago. Huyu ni binamu yangu binti wa marehemu shangazi yangu. Navivile tuliishi wote ndani ya himaya ya mzee Igogo. Nampenda sanaaaaaa!

Usije ukakosea ukanichokoza nitakusemea kwake atakukuchambuaje sasaa? ?? Yani atakunyambua kama mchicha vile utajuta kwanini ulinichokoza?? halafu yeye anachanganya Kiswahili, Kijaluo, na English mtamkoma ???

Jana tulikuwa tuna text akaniambia kuna “house gal mmoja kwenye Facebook ananiudhii” (Akimaanisha Joyce Kiria) yani hii sentence hadi leo bado nacheka ??? Mambo ya team Magufuli na team Lowassa hayo

Mother and Son moment

FB_IMG_1439831575519Lovely pic of Mwaju and his son all the way from the ‘Queen’s land” Mmependeza sana, mbarikiwe.

Manhood

FB_IMG_1440250271729Love this pic and the message!

(audio): “Muumbaji wa ndoa ni Mungu peke yake…..Hakuna mwalimu wa ndoa hapa duniani” – Tumaini Kilangwa

2015-08-22 12.59.00

Tumaini Kilangwa au da Tuma, yeye ni mama wa watoto wawili, mke, na mfanyabiashara. Katika mahojiano haya ambayo yote amerekodi na unaweza sikiliza ameongelea mambo mabali mbali kuanzia alipotokea, maisha yake ya elimu, maisha kama mama, maisha kama mke, na maisha kama mfanyabiashara. Ni mahojiano mazuri sana ambayo yanafundisha na kutia moyo kuwa hakuna lisilo wezekana kwa Mungu (kama unaamini kuna Mungu). Tafadhali chukua muda wako umsikilize wala hutojutia kamwe!2015-03-25 05.57.39Elimu na kazi alizofanya

2015-08-22 17.42.52Dada Tuma kwa sasa ameamua kuachana na kazi za kuajiri hivyo yeye ni mfanya biashara anaye miliki mgahawa ujulikanao kama Eastern Cuisine. Uliopo Wichita Kansas.

2015-08-22 17.38.15Pichani ☝ ni watoto wa da Tuma wakiwa wamevalia Tshirt za mgahawa huo….

FB_IMG_1431827984235Katika swala la uzazi na malezi ya watoto wake mpaka hapa walipofika japo safari bado inaendelea Tumaini anashuhudia kwa kusema “tumeuona  mkono wa Mungu na tunaendelea kuuona ukuu wake siku hadi siku.” Ni ushuhuda wa kusisimua na unatoa faraja kwa wale ambao wanapitia changamoto kama hizi katika malezi au jambo lolote lile. Embu msikilize wewe wenyewe…….

FB_IMG_1431828022321 Kuna changamoto nyingi katika malezi haswa ukizingatia tupo katika inchi ya ugenini ambapo mila na desturi zetu nitofauti na tulizo lelewa ameeleza da Tuma……

2015-04-22 21.29.44Dada Tuma ametoa ushauri au ujumbe kwa Watanzania wote waishio nje ya Tanzania na hata wale waliopo nyumbani kwamba  wawe na moyo wa kupenda kujaribu vitu na wasikate tamaa, kuwa na plan na mipango kwenye maisha. Utambuwe karama yako ili uweze kuweka mipango yako vizuri. Pia ameshauri watu kumtegemea Mungu sana kwani Mungu wetu ni Mungu wa upendo na anasikia sala za watu wote!

2015-08-23 17.58.59Maisha ya ndoa yanahitaji uvumilivu na maombi ya kila siku. Da Tuma amewasihi wanandoa haswa wadada kuacha tabia ya kuiga iga mambo ambayo wanayaona au kusikia kutoka kwa watu wengine hususani kwenye “kitchen parties” kwani kitu ambacho kimewezekana kwenye ndoa ya mwenzako siyo lazima kifae kwenye ndoa yako! Hakuna Mwalimu wa ndoa hapa duniani ni Mungu peke yake……!

Napenda kutoa shukran zangu za dhati kabisa kwa dada Tumaini, pamoja na kubanwa sana na kazi na misha ya familia lakini kwa upendo kabisa ameweza kuchukua muda wake wa pekee na kukubali kufanya mahojiano haya na mimi. Ubarikiwe sana da Tuma.

Pia shukran kwa wote ambao wamejitolea kwa njia ya pekee kabisa kuweza kushare picha zao, mawazo yao, na pia ku-share maisha yao kwa njia ya mahojiano na hii blog. Wote naomba Mwenyezi Mungu awabariki sana kwani mimi binafsi sina cha kuwalipa!

N.B: Kama unataka ku-share nasi kitu chochote au unaswali wasiliana nami kwa [email protected] Pia naomba nikumbushie kuwa huitaji kuweka email wala jina lako unapotaka ku-comment japo fomu ya comment inaonyesha hivyo lakini si lazima. Asanteni wote!

Mahojiano haya yameandaliwa na Alpha Igogo

 

Family time

FB_IMG_1438805635414Familia ya mama na baba watatu. Hapa walikuwa kwenye state fair (ni kama saba saba in Bongoland). FB_IMG_1438805621313Jeshi la mutu 3 pamoja na Chief Comonder  (daddy yao)…..wamependeza sana  FB_IMG_1438805611600MaWatatu umependeza mno! Ubarikiwe sana pamoja na familia yako.

Hot shot of the day

FB_IMG_1440181860328Mr President!  Safi sanaaaaaa, sio kama wakina “fulani” wakienda likizo wanaishi Dar hawakumbuki hata bibi na babu zao kijijini eti kisa wanakaa sijui U.S.A au Ulaya kha! Kuishi nje ya Tanzania sio sababu ya kutokuthamini wakwenu hata kama ni masikini kiasi gani!

Wengine mpaka wanatafuta mama / baba na ndugu wa bandia, wanajiona hawawezi kuwa na undugu na wakwao kisa wanaishi majuu!! Mmmh! Halafu sasa wakitokea kwenda kusalimia huko vijijini  au “uswahili” (kama waitavyo) wanakaa kwa masaa machache hawasaidii kazi yoyote ile; hata kuosha vyombo hawasaidi ?? jamani tujifunze kutoka  kwa watu kama Mr. President! Ubarikiwe sana.

Kwa faida ya wasomaji huyu ni Iddi Sandaly maarufu kama Mr President. Ni President wa jumuiya ya Watanzania wa DMV.

Mother and daughter moment:The Obamas’

FB_IMG_1440250199992Beautiful pictures of Mrs Obama and her gorgeous daughters. FB_IMG_1440250313993

ujumbe huu uwafikie Wahaya wote duniani

FB_IMG_1440260252629??????

Nawatakieni weekend njema

IMG-20150626-WA0027Leo nimeamua kujiweka mie mwenyewe mzima mzima ?? picha hii nilipiga June 26, 2015 Kalamazoo, Michigan ila kuna some changes nikiangalia na nilivyo sasa? nimenuna kwasababu nilikuwa na njaa halafu mtu fidenge alikuwa anachelewa kutoka ndani na yeye ndo alikuwa driver. Kana kwamba haitoshi katoka nje ya mlango na kunipiga picha ??………….. Haya nawatakieni weekend njema. Mbarikiwe wote.

 

N.B: Hauwitaji kuweka email wala jina lako kwenye comment box! Najua inasema hivyo lakini si lazima. Unaweza acha wazi na bado nitaipata. Asanteni.

Hot shot of the day

2015-08-21 09.55.54Lisa Makoyo kutoka Bongoland, ndani ya jiji la Dar. Just beautiful!

Manhood

2015-08-21 09.58.17Mzee William looking great! Huyu mdogo wangu ndo anayeniweka mjini hapa, kwahiyo huwa namuheshimu sana maana nisije jikuta napewa eviction notice kwa  kushindwa  kulipa kodi ya “banda” langu buree ?

Father and daughters moment

20150712_201949Wow! Nani kama baba?! Mzee Ngonyani na binti zake warembo sana Cynthia(kushoto) na Magreth 20150712_201949-1Mmependeza sana. Mbarikiwe sana wapendwa.

Unyanyasaji wa kiroho

gun-on-bible-spritual-abuseKatika mfumo wa unyanyasaji au aina za unyanyasaji kuna unyasaji wa aina nyingi kwamfano physical abuse, sexual abuse, emotional / psychological abuse, gender abuse, financial abuse, power / position abuse na vile vile kuna “spiritual abuse” au kwa lugha ya Kiswahili unaweza sema ni unyanyasaji wa kiroho! Dini ni imani, na imani huwa kila mtu anauwamuzi wake wakuamini au kuto kuamini dini au maandiko bila kulazimishwa au kushurutishwa na mtu yoyote yule. Hii ni kwa dini zote waislamu kwa wakristo, sisi wajibu wetu ni kuwafundisha watu neno la Mungu lakini hatuna haki ya kuwalazimisha au kushurutisha mtu aamini kile wewe unacho kiamini hata kama wote ni wa dini na dhehebu moja. Wokovu ni wa mtu mmoja mmoja na kila mtu kwa wakati wake. Kama mtu hajaamini kile kitu ambacho wewe unadhani ni sahii na anahitaji kuamini basi muache, wewe bado utahesabiwa thawabu Mbinguni kwani umefanya sehemu yako. Ipo siku katika njia ya pekee roho atamwingia na kuamini (kama kweli ni sahii hicho unachotaka aamini) lakini siyo kwa kulazimishwa. Continue reading Unyanyasaji wa kiroho

Blessing 1st day of school

2015-08-18 09.35.54Wow! Kweli siku hazigandi! My babysister jana ameanza nursery school. Yani hata sitaki a mini maana ni juzi tuu ndo kazaliwa leo hii huyo anaenda shule, na wakati bado nashangaa nitashtukia ananiambia  “dada nakuja college U.S.A” ?? 2015-08-18 09.34.01Nimeambiwa jana alilia sana alipo achwa, lakini leo (in Tanzania’ time) ameamka hasubuhi akawa anasema “school time” kwahiyo alikuwa yupo okay na anaanza kupenda ??? Good job Blessing ………….(pichani ni Blessing, mama Blessing, na cousin-sister Rhoda Igogo).2015-08-18 08.32.29Hapa unapo muona anamtaka 2 na miezi 8 lakini  IQ yake utafikiri mtoto wa miaka 7 au 8 ndo maana wameona bora aanze shule. Yeye ajapelekwa daycare kabisa, alikuwa anafundishwa nyumbani na mama yake kabla ya kuanza shule.  Mungu azidi kumbariki, akashike sana elimu na awe nuru mbele za watu! Proud of you babysister! Love you deep!

Dondoo 10 muhimu kwa wazazi na watarajiwa

Habari zenu wapendwa……… Nadhani wengi watu humu ndani ni wazazi au Wazazi watarajiwa.. So si vibaya kama tutasoma hapa na kuzingatia dondoo 10 muhimu sana kwa wazazi na wazazi watarajiwa wote

1. Mkanye mtoto wako wa kike na hata wa kiume kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.

2. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.

3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao “Mchumba”, “Mke wangu” au “Mme wangu.”

4. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu na wengine wana maambukizi.

5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda kwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.

6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.

7. Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za siri mwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.

8. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.

9. Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.

10. Usipende kumruhusu mwanao kulala na housegirl au houseboy au mgeni. Huwezi jua tabia za watu na wanayomtendea usiku!!!