Category Archives: Uncategorized

is always the woman’s fault when the man cheats!

We need to stop this nonsense that, it is always a woman’s fault that their husbands/bf cheat because of them.

A friend of mine posted a blog saying, after a woman gets married, she stops caring about herself, gains 100lbs, bluh bluh…. That’s why the husband will go look for side dishes who are slimmer etc.

What about men who look like they swallowed the biggest Abs ball when they get married?? So we are allowed to go look for 6 packed men? Let’s stop this BS that it is always the woman’s fault when the man cheats.

You can marry Miss. Universe and still cheat. Once a cheater always a cheater. Stop this nonsense of hormones. So the ones that don’t cheat are women in men’s clothing ??????   #WomenPower

Faith Mbori
Faith Mbori

My attitude today: keep your nose where it belongs!

2016-06-04 15.08.37

Matukio katika picha

FB_IMG_1465300493686Hawa Gwao (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye meza kuu kama mmoja wa majaji katika show ijulikanayo kama The West Midlands Talent show iliyopo United Kingdom FB_IMG_1465300454708Hawa pamoja na mmoja wa majaji  FB_IMG_1465300465341Hongera sana Hawa

#Hoja: ACHA KUFANYA MAMBO HAYA NA UTAFANIKIWA 100%

1. ACHA KUWA NA MARAFIKI WANOKUPOTEZEA MUDA:

Watu wengi tumekuwa na marafiki wengi sana na marafiki ni mhimu sana katika maisha yetu haya wapo wanaotufaa na wasiotufaa kuwa na marafiki wanao weza kukusaidia na kukupa hamasa ya kimaendeleo ,malengo yako na kuwa na maisha Fulani. Hivyo achana na marafiki wasio kuwa na msaada kwako.

2. ACHA KUKIMBIA MATATIZO YAKO

Waswahili wanasema kuwa “kukimbia tatizo si kutatua tatizo” Hivyo basi kama tatizo umekutananalo basi tafuta njia ya kulitatua tatizo hilo kwani matatizo hayaji kuisha katika dunia hii kama unakimbia utakimbia mangapi ? unatatizo la pesa kwanini usitafute pesa ila kama hufanyi kazi unategemea kupata pesa huwezi. Matatizo hayaepukiki komaa na ulitatue utajikuta kama uko peke yako katika hii dunia lakini kuna watu wana matatizo zaidi yako na wanahangaika kuyatatua.

3. ACHA KUJIDANGANYA MWENYEWE

Katika maisha ya sasahivi unaweza kumdanya mtu yoyote yule lakini ogopa sana kujidanganya. Vijana wengi tumekuwa tukijivuna mbele za watu kuwa tuna hili mara lile ili mradi tu tuonekane ni watu wazuri kwa watu wanao tusikiliza.

4. ACHA KUIGA MAISHA YA WATU WENGINE

Vijana wengi hili kwetu limekuwa janga kubwa sana maisha yetu yamekuwa yakuigiza sana (copy and paste) hasa hasa tunapenda kuonekana ni watu Fulani wenye maisha mazuri, hatuzijui shida ni watu wakula bata wakati si kweli. Maisha yetu yamekuwa magumu na yatakuwa magumu kwasababu ya kuiga maisha ya watu wengine ishi maisha harisi uliyonayo watu wakujua asili yako siyo kuigiza unaweza kosa kusaidiwa na watu.

5. ACHA KUKUMBUKA YALIYOPITA

Hapa kuna mambo mengi tunajifunza wengi hukumbuka yaliyopita hasa waliyo shindwa kuyafanya au yaliyowaumiza kwa kukumbuka yaliyopita haiwezi kukusaidia kwani kila tuamkapo asubuhi ni kama tumezaliwa upya na siku ni nyingine,tarehe na mambo utakayoyafanya ni mengine si sawa na jana. Waswahili wanasema “Tusahau yaliyopita tugange yajayo” hii ina maana kuwa wewe si wa kipindi kile bali ni mwingine na akili ni mpya.

6. ACHA KUOGOPA KUFANYA MAKOSA

Makosa ndiyo walimu wetu mkubwa sana katika maisha yetu na kila binadamu si mkamilifu toka uzaliwe mpaka sasa kuna makosa mengi uliyoyafanya na kupitia makosa hayo umejifunza kutorudia makosa tena na makosa hutujenga zaidi na kuwa makini zaidi kama ukifanya kosa huna haja ya kujilaum chukua muda kujilekebisha na kusonga mbele kosa lisiwe tatizo la kukukatisha tamaa.

7. ACHA KUNUNUA FURAHA

Vitu vingi tunavyo vihitaji vinagharama kubwa sana na vitu hivyo si kwamba tuna vipenda bali ni tamaa tu tuliyonayo na hiyo yote ni kuamini kuwa furaha ya maisha tutaipata huko si kweli. Mungu alitupatia furaha, na upendo bure ni vitu unavyozaliwa navyo fikiria kama vingekuwa vinauzwa wangapi? Wangapi tungekuwa hatuna furaha. Hivyo basi anza kuyafurahia maisha yako hivyo vingine vitakufuata.

8. ACHA KUSHINDANA NA MTU KIMAISHA

Acha kushindana na mtu kimaisha haitakusaidia huwezi jua yeye anafanya nini kuzipata pesa zake au mali zake na wewe unazipataje ushindani mzuri katika maisha ni ule wa kwako na mafanikio yako jiangalie kile unachokifanya na matokeo yake unapata nini? huo ndio ushindani mzuri kuliko wote sio kushindana na mtu kimaisha acha.

9. ACHA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO YASIYO SAHIHI

Katika mahusiano si kitu cha kujiingiza tu au kama unaoa si kuoa tu kwasabu Fulani kaoa basi na mimi nioe, si kudai kuwa nimechoka kufua ngoja nioe sasa ndiyo maana karne hii inaongoza kwa wanandoa kuachana na ndoa za utotoni kwasababu watu hawajipangi ni kuiga tu. Mahusiano au ndoa ni kitu kikubwa sana na kama umempenda mtu onyesha kuwa unampenda kweli mtangulize mbele yako kuwa ndiyo kila kitu kwako/ kila kitu kinaenda kwa ajiri yake. Kama unaingia katika mahusiano mheshimu mwenzako na kumpenda mpe nafasi kubwa katika maisha yako.

10. ACHA KUJILAUMU

Kuacha kujilaumu ni njia mojawapo ya kufanikiwa katiaka maisha yako unapo kosea amini kuwa wewe si mkamilifu na hakuna binadamu aliyekamilika jipange songa mbele. Wagunduzi wa vifaa mbalimbali vinavyotumika kama vya umeme na vinginevyo si kwamba hawa kufanya makosa walikosea sana mpaka kutoa kitu sahihi .

11. ACHA KUONGELEA YAWATU FULANI

Kuzungumzia maisha ya mtu Fulani haikusaidii ni kupoteza muda tu kwanini usiwaze maisha yako unatakiwa kufika wapi na ufanye nini kuishi maisha mazuri unakaa na kuanza kuzungumzia mtu Fulani yupo hivi mara hivi wakati huo huyo mtu unaemsema yeye yupo kazini we upo kijiweni mtalingana kweli? Acha kuzungumzia maisha ya watu fanya yako ufurahie maisha.

By Mike Mwakatundu MP2020

Source: Change Tanzania

You can’t stop water from flowing!

2016-06-07 07.03.33

A word of wisdom

Hold on to your faith even when things look hopeless. Faith is the substance of the things we hope for, and when you have God in your life, you have hope no matter what the circumstances look like.~~~~~~~ Victoria Osteen

Ramadhan Mubarak

IMG-20160605-WA0002jamani si ndo ule umeandama eeh! Haya nawatakieni Ramadhan njema wapendwa wasomaji wangu, ndugu, jamaa, na marafiki. Mtukumbuke katika dua zenu FB_IMG_1465210863756Happy holy month to all Muslims around the world ?

Wapo watu wenye tabia za Chatu huyu

Ilikuwa kawaida yake kulala na nyoka wake, na haya ndiyo yaliyomkuta. FB_IMG_1465163970073Hii ni hadithi ya kweli kuhusu mwanamke aliyekuwa na nyoka wake aina ya chatu aliyempenda sana. Nyoka alikuwa na urefu wa mita 4, aliishi naye kwa muda mrefu na siku zote nyoka yule alionekana mwenye afya. Hata hivyo, nyoka alianza kukosa hamu ya kula kwa wiki kadhaa jambo lililomnyima raha mama yule kwani alihisi nyoka wake ni mgonjwa. Mama alijaribu kumpa kila kitu alichoweza ambacho nyoka wangependa kula lakini haikusaidia kitu, mama yule alikata tamaa na aliumia zaidi kwakuwa alimpenda sana nyoka wake. Hatimaye mama yule aliamua kumpeleka nyoka wake kwa daktari wa mifugo. Daktari alimsikiliza yule mama kwa makini kisha akamuuliza , ” Je, unalala na nyoka wako wakati wa usiku? anapenda kulala karibu zaidi na wewe na kujipimisha urefu wake na wako? “

Mama kwa matumaini makubwa alisema, “Ndiyo! Ndiyo! anafanya hivyo kila siku na inanipa huzuni kwa sababu nahisi kuna kitu anatamani kuniambia lakini hawezi na Mimi pia nashindwa kumuelewa hivyo nakosa namna ya kumsaidia ili ajisikie vizuri kama siku zote “

Daktari akampa jibu la kushtusha moyo ” Mama, chatu wako si mgonjwa ; … “Ndiyo, chatu hakuwa mgonjwa, amekuwa katika maandalizi ya kumla mama yule. Daktari akaendelea, “Kila wakati anataka kukaa karibu na wewe, kujikunjakunja mwilini mwako na kukutambaa kila muda, lengo lake ni kupima ukubwa wako na kuangalia namna gani utakuwa mzuri mlo wake. anajilinganisha kujua jinsi gani utawa mlo mkubwa kwake hivyo anajipanga kwa mashambulizi. Na ndio maana hataki kula sasa ili kulipa tumbo lake nafasi ya kutosha kwaajili yako pindi atakapokugeuza kitoweo chake “.

FUNDISHOWatu wako wa karibu zaidi unaowaamini, wapole na wanaoonyesha kukupenda wanaweza kuwa wabaya zaidi kwako. Upendo wa dhati na dhamira nzuri haitokani na namna watu wanavyo Kukumbatia na kukuchekea. Unafiki huambatana na Upendo wa kujilazimisha. Usiogope mashambulizi yanayopangwa na maadui zako juu yako Bali ogopa rafiki mnafiki anayekukumbatia na kukuchekea huku anakumwagia sumu kali. Adui wa MTU ni wa nyumbani mwake.

Mbarikiwe.

Source: Unknown 

Asie na kasoro ni Mungu pekee -Dina Marios

Alikuwepo mfalme mmoja ambaye yeye alikuwa na tatizo katika jicho lake moja la kushoto na mguu mmoja alikuwa hawezi kusimama akiwa ameunyoosha. Jicho la kushoto limefumba halioni. Siku moja akahitaji wataalamu wa kuchora wa mchore kwa umahiri mkubwa picha yake ipendeze iwe na mvuto wa ajabu pamoja na madhaifu yake.

Wachoraji mbali mbali walijitahidi kufanya walichoweza kuhakikisha hili linawezekana maana waliahidiwa dau kubwa kutoka kwa mfalme. Walichora lakini bado ule udhaifu ulionekana wazi na hazikuwa na mvuto kama yeye alivyotaka.

Basi alitokea kijana mmoja ambaye yeye alimchora mfalme kama “muwindaji flani ambaye amefumba jicho moja na amekunja mguu mmoja akilenga shabaha kukipata kile anachokiwinda. Mfalme alifurahishwa sana na picha ile na kijana akashinda.

Katika maisha ni vema tujitahidi kuficha madhaifu ya wenzetu na kuchochea yale wanayoyaweza katika maisha ili kila mtu awe na furaha siku zote bila kujali muonekano na mapungufu yake.

Muda mwingi tunanyoosha vidole kudhihaki na kutangaza mapungufu ya wenzetu, maumbile n.k Tunajifunza kuwapenda watu ndugu zetu, jamaa, wapenzi, marafiki kwa kuyapa kipaumbele yale mazuri waliyonayo ukizitafuta kasoro za mwanadamu hutazikosa ni nyingi kweli na asie na kasoro ni Mungu pekee. FB_IMG_1465217175783Dina Marios!

A word of wisdom!

The Creator of the universe has equipped you, empowered you, and put seeds of greatness inside of you. He says, “You’re one of a kind, a masterpiece; you’ve got what it takes.” He’s qualified you, so don’t disqualify yourself.

Source: one of THC members 

Ijumaa Kareem

2016-06-03 10.30.36Ijumaa Kareem kwenu wote……Sabato njema. …….Tumsifu Yesu Kristo. ……Sorround yourself with ❤❤❤

“Watanzania wanataka maisha ya kisasa lakini wengine hawataki kulipia gharama ya maisha hayo ya kisasa”

Neno la Leo: Watanzania wanataka maisha ya kisasa lakini wengine hawataki kulipia gharama ya maisha hayo ya kisasa. Wanataka wawe kama Marekani, Japan, China, Ulaya lakini wakiambiwa walipe hiyo gharama wanakuja juu! Sasa kwani Marekani, Japan, China, Ulaya zilishushwa toka Mbinguni zikimeremeta? Au wanafikiria haya mabarabara, mabasi na matreni yanayokimbia kama yanafukuzwa na radi yalikuja tu ghafla bin vuup! Kwamba, vyuo vyao vikuu vimeweza kufikia kutoa wataalamu wenye ubunifu wa kila namna kwa sababu Mungu anawapenda saaana hao na anatuchukia sisi?

Au watu wanafikiri – na nimeshawahi kukutana na watu wa aina yao – kwamba Mzungu kapendelewa saaana kwa sababu mweupe!? Au ni kweli tunaamini maneno tunayoambizana “Waafrika sisi tumelaaniwa” halafu tunaishi kama watu waliolaaniwa kutimiza unabii wetu wenyewe?

Nilisema juzi kuishi kwa njia ya mkato kuna raha yake hasa kama njia ya mkato haikufanyi utoke jasho! Hatuwezi kuwa na maisha ya kisasa na kujenga jamii ya kisasa yenye ubora wa maisha kwa kila namna bila kulipa gharama ya kufanya hivyo. Nje ya hapo tutaendelea kutamani tu samaki wa picha na mchuzi wa jirani!

MMM

Usajili wa vitambulisho kwa diasporas

IMG-20160603-WA0000

Manhood

FB_IMG_1464961059928Ngoja leo ni watambulisha kwenu shemeji yangu aitwaye Michael Owino! Yeye ni muandishi wa vitabu kama mnavyo ona!……… sisi wajaluo tumeendelea tunao ndugu zetu wazungu ??? FB_IMG_1464961142924Please follow him on Facebook, he goes by his name  Michael Owino

Ukiniuliza tatizo KUU sio serikali kuingilia biashara bali ni biashara kuingilia serikali na siasa

NAAMKA HIVI –FB_IMG_1464959113521Ukiniuliza tatizo KUU sio serikali kuingilia biashara bali ni biashara kuingilia serikali na siasa kwa ujumla kwa takribani miaka 20 sasa.

Hapa tulipofika ni zao la siasa kutumikia wafanyabiashara wachache wenye nia ya kulinda maslai binafsi hata kwa kuigarimu serikali na taifa letu.

Hatuwezi rekebisha hii hali bila kupitia mkondo huo huo uliotufikisha hapa. Naamini hapa ndio tutaona tofauti ya siasa za kusaka dola na utawala baada ya kuikamata dola.

Tukisha chagua viongozi tunategemea waunde serikali na kutawala/kudhibiti nchi sio kupiga siasa tu siku ziende tu bila suluhisho.

Tukubaliane ‘kibongo bongo’ hakuna anaeTAKA mabadiliko ya kweli pamoja na kuyaHITAJI. Kwa wengi ‘mabadiliko’ ni kauli mbiu tu. Ukiwa kiongozi Tz lazima uwe mnafiki aka roho mbaya au kauzu aka roho ngumu.

Siasa mwisho chalinze, HAPA KAZI TU! ?

A word of wisdom

Proverbs 20:3 says, “Avoiding a fight is a mark of honor.” A lot of times, we think winning a fight is a mark of honor. That’s not really winning. You make yourself feel good, but it doesn’t strengthen the relationship. The real way to win is to walk away, to take the high road. That’s a mark of honor.

Source: One of THC members

 

DICOTA’s statement on misrepresented facts made by Mb. Joseph Mbilinyi

Screenshot_2016-06-02-14-13-38-1Screenshot_2016-06-02-14-10-52-1Screenshot_2016-06-02-14-10-52-1Screenshot_2016-06-02-14-10-40-1

To read in pdf file click ? DICOTAToJosephMbilinyiLetter

To read through DICOTA’s website ? DICOTAToJosephMbilinyi

 

 

Mnada mkubwa kutoka ubalozi wa Marekani!

IMG-20160602-WA0003Ubalozi wa Marekani unapenda kukujulisha mnada mwingine mkubwa wa Magari, Mafridge pamoja na Furniture mbalimbali za nyumbani. Universal Auction Centre kwa idhini tuliyopewa tutauza kwa mnada Magari, Mafridge na Furniture jumamosi ya wiki hii 04.06.16 kuanzia saa 4 asubuhi, Golden Resort, Sinza, jirani na Lion Hotel. Mali zote zinaweza kukaguliwa kuanzia kesho mpaka ijumaa.

Kwa mawasiliano nasi tupigie +255754284926

 

Katika kukua kwetu huwa tunakua huku tukijitafuta sisi ni kina nani?-Dinna Marios

Utajitafuta katika muonekano unapenda uonekanaje? Mavazi yako yakutambulishe vipi?sauti yako iweje? tembea yako iweje utembee vipi? ucheke vipi? nakumbuka nikiwa nakua nimekuwa na mapenzi ya kuangalia movie basi nilikuwa napenda sana sehemu inayomuonyesha mtu akitembea kwa slow motion au kukimbia nilikuwa napenda nitembee mwendo huo wa slow motion kama kwenye movie ???? nilihisi ni nzuri sana Katika kujitafuta huko wakati mwingine tunajikuta tunaiga/kucopy mambo hasa muonekano na tabia kutoka kwa wanaotuzunguka. Kama ni sauti Utapenda uongee kama fulani anaekuvutia, kutembea kama fulani anaekuvutia, kuvaa,kujidai, kucheka  n.k

Sasa katika kuiga au kucopy huko je unamcopy nani? Je unachocopy kinakujenga au kubomoa? Wakati unaiga muonekano, tabia, tembea, ongea kama unamuiga mtu anaeendana na unachotamani kuwa itapendeza sanaa katika kukujenga na kujitafuta.

Lakini angalia usiwe mtu unaeiga vitu visivyofaa ambavyo vitakufanya ujichimbie shimo. Unaiga wale watu wako wa karibu ambao ni walevi nawe unaanza ulevi, uzinzi, utapeli, kuvuta bangi, kula unga, kuvaa uchi uchi, kujichetua, umarioo, uhuni wa kijinga, uongo na umbea inshort tabia zote mbovu unaziiga kutoka kwa wanaokuzunguka. Kwako kijana ambae bado unaendelea kujitafuta wewe ni nani hakikisha haupotei. Wakati unajua unataka kuwa mtu wa aina gani basi angalia mtu wa mfano unaoutaka haukupotoshi! FB_IMG_1464870072403By Dina Marios!

Africa produces 75% of World’s Cocoa. And receives only 2% of the $100 Billion industry?!

Screenshot_2016-06-02-07-20-40-1What a shame! Hili ni jipu kubwa sana!!…… Who’s fault is this?  Please  visit changeTanzania page to read what other people have to say!

Source: face2faceAfrica.com