Ujumbe wa leo ni kwamba mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako ukiwa bado unanguvu na muda mwingi sana. Usisubiri mpaka majanga yakukute au use kwenye near death situation ndo uwanze kumtumikia Mungu. Ni jumbe kwetu wote, nashukuru dada yeti kipenzi Shy-Rose ameweza kutukumbusha kwa kutokujikweza mfanikio.
Mh. Shy-Rose aliudhuria ibada ya Ijumaa iliyopita alipokuwa mjini Mwanza kwa shughuli za kichama. Ubarikiwe sana dada yetu.
Kama mmoja ya wazazi walio zaliwa na kukulia katika mazingira ya kiafrica ambapo wengi wazazi wengi miaka ya nyumba hawakuwapa watoto wao uhuru wa kukuza vipaji vyao. Wazazi wengi walikuwa na mtazamo yao ya ni nini wanataka watoto wao wawe wanafanya wanapo kuwa wakubwa. Basi nami kwakweli nilijikuta nikiwa na mtazamo huo huo wakumnyima mwanangu uhuru wa kupata full “exposure” ya vitu vile alivyokuwa akionyesha kuvipenda au niseme kuwa talented navyo kwani nilikuwa teyari nina picha ya ni nini mwanangu anatakiwa kufanya au kuwa.
Mwanangu ni anapenda sana basketball, mwanzoni nilimuacha ashiri mchezo huo alipokuwa elementary school. Alicheza mpaka darasa la saba lakini baadaye nilimzuia. Sababu haswa nilitaka a-constraint kwenye masomo zaidi kuliko michezo. Kitu ambacho kwa upande mmoja au mwingine hakikuwa kizuri kwani nili mnyima haki yake ya kuendeleza kile kitu ambacho roho uake inapenda sana.
Najua kuna wazazi wengi ambao bado wana mtazamo kama wangu, basi ngoja nikushauri kama utapenda. Ukiona mtoto wako anapenda kitu fulani au anaonyesha uwezo wa kitu fulani basi usidharau au kukatisha tamaa unless iwe ni kitu ambacho si kizuri kama kudokoa n.k Usiweke nguvu myingi (pressure) kumuhiza akazanie no-no! Ila muonyeshe kuwa unam-support kile anacho kifanya. Nasema usitumie nguvu sana kwani kama ni kipaji chake basi utazidi kuiona, na kama ni kitu cha mpito tuu basi baada ya muda atapoteza interest ya hicho kitu.
Dunia ya leo ni vizuri mtoto akiwa malt-talented. Dunia ya sasa si kama ile ya wazazi wetu ambapo kama mtu ni Manager wa kapuni basi utakuta ana kuwa na ma secretary wawili, leo hii wanataka Manager ambaye ajua kutype na basic computer skills kwa kwasababu ya mambo ya confidentiality makampuni mengi wanapenda Managers wa type na kuhifadhi baru wenyewe ili kupunguza risk za kuvuja kwa siri za kampuni.
Nimependa sana hii picha ya Bella Ayugi-Twaakyondo. Kwakweli kapendeza sana, uzuri wa asili, na lipstick ya rangi iliyo tulia vinavutia. Inaaonyesha ni jinsi gani Bella anajikubali na kujiamini ndiyo maana hajaangaika na makoro koro mengi usoni. Big up Bella.
Jamani hakuna kitu kina nikera na ninaweza kusema sikipendi kabisa kama ninavyo ona watu wako busy wakati wa mambo ya muhimu kama hapo kwenye picha chini!!
Mwanzoni nilifikiri ni mwanangu tuu ndo anahii tabia mbovu laakini kumbe watu wengi tuu; inawezekana hili likawa “janga la dunia.” Kwani si watoo, si vijana, na wala si watu wazima yani wote wana hili tatizo. Najiuliza why? Ndo madhara ya technology au ni watu tuu kujiendekeza? Mie sielewi kwani hii tabia sina, labda kutoka na field niliosoma imenifanya kidogo niwe mwangalifu sana wa tabia kama hizi.
Utakuta mtu kaalikwa kwenye sherehe, lakini yupo busy na simu it’s just so rude! Wewe umealikwa kwenye sherehe ya mwenzio kwanini usiweke mawazo pale, onyesha heshima kwa wenye shughuli. Na kama unaona ina ku bore si uondoke kimya kimya?
Wengine bila aibu wala hofu ya Mungu utakuta kanisani (not sure about Msikitini) yupo busy na simu utafikiri ni standby surgeon!! Na wengine hata kwenye ibada za mazishi wao wapo busy, yani roho ngumu kama kazaliwa na Farao!!
Embu kama unaweza badilika basi jitahidi ubadilike. Mie hapa napiga kelele sikuhizi amepunguza kidogo ila sito nyamaza mpaka atakapo acha 😉 😉
Shout out to my cute cousin-sister Lisa Makoyo. Kwa kweli si tu kapendeza bali uzuri wake wa asili na rangi yake ya chocolate inavutia sana.
Kuna baadhi ya wanawake ambao wanafikiria kupendeza ni lazima uvae nguo za expensive designers na upake poda, na marangi rangi mengi usoni, kumbe wala si kweli. Hivi hujawahi ona watu wanavaa vitu vya pesa nyingi nabado wanaonekana “kituko” bara barani? Yani utakuta mtu kapaka heavy makeup, aye shadow za rangi za kung’aa, bangili, hereni yani makoro koro kibao usoni. Basi hapo ndo mkute ana nguo yake ya sijui designer gani na lipstick juu, ukimwangalia utazani yule ndege mwenye mdomo mrefu aitwae Kasuku!!
Halafu pia kupendeza siyo lazima uvae nguo za bei ya ghali. Kinachotakiwa kikubwa ni usafi wa mwili na mavazi. Unaweza ukavaa nguo yako uliyo ishona kwa fundi “Chochote” na bado ukapendeza zaidi ya yule aliye vaa nguo ya bei “chafu.” Kupendeza ni muhimu sana kwa kila mwanamke lakini kujiweka mapambo mengi inaonyesha kuwa ni mwanamke mwenye low-selfesteem (hujiamini).
Jamani kwa kifupi, simplicity is always the best, and too much of anything is harmful!! Tuige mfano wa Lisa Makoyo.
Kwa usafi na mahitaji yako ya nywele basi fika Cecilia Hairdressing Salon iliyopo Temeke hospital, mtaa wa Wailes. Nyumba no. 74, opposite na showroom ya magari makubwa. Aksante sana!
Hivi ndivyo baadhi ya wasomaji wetu walivyo shereke siku kuu ya kufufuka kwa Bwana Yesu (Pasaka).
Mambo yalikuwa kama ifuatavyo pande za Atlanta, Georgia kwa designer maharufu Linda Bezuidenhout(owner of Lb apparel). Linda kama kawaida yake amevaa vazi la ubunifu wake yeye mwenyewe.
Na hivi ndivyo ilivyokuwa pande za Mbagala, Dar es salaam. “Undugu ndo hazina yetu” hayo maneno aliyo sema Felister Sarungi wakati akisherekea ufufuo wa Mfalme Yesu pamoja na shangazi yake Tabu Obago pamoja na Jack na Juliet (binti wa Tabu).
Mbarikiwe wote na muendelee kufurahi katika Bwana.
Wow! Love this so much, my darling brother Noah Manongi preaching for the very first time yesterday April 4, 2015. May God keep blessing you and your family. Thank you for being a good symbol of a good father, husband, brother, and a friend!
Just love this father and daughter moment. That’s my darling babysister Blessing and our father, early today in Dar es salaam, Tanzania. Father is always girl’s best friend! God bless all fathers!
Nimependa sana hii picha ya waheshimiwa hawa wawili Mh. Vincent Nyerere and Mh. Shy-Rose Bhanji, ni viongozi ambao nawakubali sana, haswa kwa ile mañana ya kutokujikweza! Yani hawa viongozi hawana dharau ya kujiona kuwa wao ni watu wa level fulani tofauti na watu wengine. Wanakula na kushiriki na watu wa level zote za maisha bila matatizo kabisa, na sio ile yakupata “kodak” moments za Facebook na IG. Mbarikiwe sana!
Kwanini unamkatisha mwenzio tamaa? Wewe Kama haukubaliani na ndoto za mtu mwingine, basi pale anapo amua ku share na wewe badala ya kumkatisha tamaa ni vyema ukanyamaza’ If you don’t have any positive thing to say to someone just “shut your front door!”
Tujifunze kupenda kubari wengine nasi tutabarikiwa tena zaidi. Mtu anapo share na wewe mawazo yake au mipango yake inamaana amekuamini, kama upendi aendelee kukuamini basi nyamaza! Hivyo itakuwa umetumia busara zaidi kuliko kuanza kumtolea maneno ya kukatisha tamaa kama vile; “sidhani kama utafanikiwa”, au “mh! Jitahidi mwanzo mugumu.”
Okay, mtu kufuata ndoto zake sio lazima afanikiwe kama wewe unavyotaka au unavyo fikiria kwani kitendo cha mtu kujaribu teyari ni mafanikio tosha! na wewe ni nani haswa mpaka ujue what the future holds of your fella? Unajua aliye tengeneza bulb alijaribu mara ngapi kabla ya kufanikiwa? Bill Gate alishawahi kusema kuwa yeye huwa haajiri mtu ambaye hajawahi ku fail! Na hawa ni watu ambao leo hii dunia inawatazama kama baadhi ya watu ambao ni the most achievers in the world!
“Mwanzo mugumu” oh! well, who doesn’t know that?! Why uone umuhimu wa kumguna mtu ili umwambie mwanzo mugumu? Au Wenzetu wanasema “talking / saying with attitude” hivi unajua Billoner Mr. Trump amewahi ku file bankruptcies mara ngapi? na ni nani asiye jua kuwa Rome haikujengwa ndani ya masaa 24?! Hakuna ubaya kumkumbusha mtu kitu au kumpa mtu tahadhari. Tatizo ni jinsi unavyo sema na mahala unapo semea ndiyo huleta shida! Pia tabia ya kurudia rudia moja kila wakati it becomes annoying! Namwishoe mtu anaanza kulichukulia hilo neno in a negative way hata kama ulilisema kwa nia nzuri.
Be a blessing to people hata kama your personal life haipo sawa!
Wishing my lovely daughter a very Happy 21st Birthday! It’s sad to see you helpless sick in bed while its time to celebrate your big day! I wish you a speedy recovery and much love. Happy birthday my queen!
Nimependa sana huu ujumbe kutoka kwa mama yake Essy na Evin “Punda alipoona wametandika nguo na akapita juu ya hizo nguo na watu wanashangilia, alijisifu sana, hakujua ni kwa sababu alimbeba YESU. Siku moja aliamua kwenda Yerusalem peke yake bila kumbeba Yesu, alishangaa! Njia haikutandikwa wala hakushangiliwa, na alipoingia Hekaluni alikimbizwa kwa viboko. SOMO: Fahari na heshima yako ni kumbeba YESU, ukimtua Utafedheheka. Wakumbushe uwapendao.”
Kuna Punda wengi na waina nyingi na huu ujumbe unawahusu au unatuhusu sana, Tafakari!
Napenda kumtakia uponyaji wa haraka dada yetu kipenzi cha wengi Shy-Rose Bhanji. Shy-Rose amekua akiugua tangia mwanzoni mwa wiki hii, amelazwa katika hospitali ya Agha Khan. Kwa neema za Mungu anategemea kutoka kesho na kurudi nyumbani. Mkono wa Mungu unaponya magonjwa yote uwe naye, ukamtibu maradhi yanayo msumbua, Amen!
Picha ni rafiki yake mkuu mwanamuziki Lady Jaydee alipokwenda kumuona hospitalini leo. Ubarikiwe Jaydee.