Katika kuitafuta furaha usimuumize mtu mwingine ili wewe uwe na furaha.Kila lililopangwa kuja kwako litakuja tu kama Mungu amelipanga kuja. Huwa nayatazama maua yakiwa bustanini.Ni maua ya aina tofauti lakini hupokezana kuchanua.Hili litakaa miezi hata tisa bila kuchanua lakini siku likichanua linapendeza kweli kweli,lingine huwa limechanua mara zote,lingine huitaji jua kali ili lichanue na kupendeza.Ndivyo hata sisi tulivyo hatufanani na kila mmoja ana wakati wake wa kuchanua…wakati wake wa kufanikiwa.Sidhani kama yale maua huwa yanaoneana wivu mbona yule kachanua mimi sijachanua?Usiitazame furaha ya mwenzako ukateseka nayo,mafanikio yake ukateseka nayo na wewe ukaitaka pengine na yeye ni kama lile ua linalokaa miezi tisa ndio lichanue.Itazame safari yako na wewe wakati wako ukifika utachanua Utang’ara.
Katika  kuitafuta furaha na mafanikio njiani usimkanyage mtu,usimuumize mtu.Unaweza kufanikiwa leo lakini sio milele.Kufumba na kufumbua mambo yanaweza kubadilika.Unaweza kuwa kwenye nguvu na control leo lakini huwezi kuushinda muda…muda hubadilika….Good morning!