“A heartfelt thank you to all fabulous men who support women in their lives, starting with the DSM Regional Commissioner, we appreciate you” Janeth Igogo Janeth Igogo (Mrs) akiwa Mlimani City wakati wa sherehe ya kufurahia siku ya wanawake duniani!
Category Archives: Women’s Day
Janeth Igogo: Whatever a man can do, a woman can do it better
Kheri ya siku ya Wanawake duniani kote!
“Strategic plan yako unaijua? Ipoje?” -Dr Blandina
Hii ni very late post, lakini mtaniwiya radhi kwani I only blog at my spare time! Wenzetu wanasema “better late than never”! Nitukio ambalo lilikuwa limeandaliwa na organization ya Vital Voices wakishirikiana na Dare To Dream foundation! Kiongozi wa shughuli yote alikuwa ni Emelda Mwamanga (Mrs) ? ambaye ndie Mkurugenzi Mkuu wa Dare To Dream foundation, Bang Magazine, na pia ni “mshika bendera” a.k.a Ambassador wa Vital Voices Tanzania! Mgeni rasmi alikuwa ni Mh. Devota Likolola (Mbunge viti maalum)
Tukio zima lilifanyika siku ya Jumamosi, tarehe 08, March, 2017 katika ukumbi wa Danken Hall pale Mikocheni. Ambapo yalianza kwa kutembea kidogo huku wanawake wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kuwakilisha sauti ya vilio vya wanawake wote inchini Tanzania na dunia kote!
Dhumuni haswa la hii shughuli ilikuwa kuwakutanisha wanawake wote ili kuadhimisha siku ya Wanawake duniani na pia kujifunza mambo mbali mbali toka kwa wanawake ambao wamethubutu kufata ndoto zao na kufanikiwa japo kwa changamoto mbalimbali ambazo zingewafanya wakate tamaa! Pia kulikuwa na mambo mengine ya kujifunza kutoka kwa wanawake wengine katika makundi yao kama VIKOBA! Katika shughuli hiyo kulikuwa na baadhi ya Motivational speakers ambao waliongea mambo mbali mbali yanayo husu nafasi ya mwanamke katika kuendeleza uchumi wa familia na jamii kwa ujumla. Waongeaji hao alikuwepo Mh. Devota Likolola, Dr. Blandina, Chris Mauki, Mkandarasi bora wa kike-2017 Ms Waziri (Nimesahau jina la kwanza) na wengine wengi!
Waongeaji wote waliongea vizuri sana na ifuatavyo ni sehemu ndogo ya maongezi ya Dr. Blandina ambapo aliwasihii sana wanawake kuwa na tabia ya kujifanyia tathimini wao wenyewe badala ya kufanya vitu kwa kufata mkumbo wa marafiki / mashoga! Pia aliwataka wawe na tabia ya kujiwekea malengo na strategy plan ya maisha yao kama kweli wanataka kuingia kwenye dunia ya kujenga viwanda kama wanaume! Na zaidi aliwasihii kutokuogopa kutumia neno HAPANA pale panapo bidi kutumia neno hilo! Tafadhali msikilize mwenyewe. ….?
Shughuli hii kwakweli ilikuwa nzuri sana! Binafsi nilijifunza mengi, tulifurahi na kuburudika. Ngoja nikuonjeshe kidogo ?
Asante sana Emelda Mwamanga na timu yako yote! Salome thank you much! Be blessed!
Malkia wa nguvu 2017: Hongera sana Mwanaidi Mayowela, pongezi kwa Clouds TV!
Nilikuwa sijapata muda wa kuwapongeza washindi na waandaaji wa sherehe za “Malkia wa nguvu” hivyo naomba nichukue muda huu kuwapongeza!…………Kwakweli kama kuna kitu ambacho kimenivutia sana na kunigusa kwenye TV za Bongoland; basi ni hii sherehe ya Malkia wa nguvu. Sababu kuu yakunivutia nikuona kuwa waandaaji walichukua muda wao kufanya kazi ya kujua nani anastahili kupewa tuzo hiyo ambapo imekuwa tofauti sana na events /awards nyingi sana za “Wabongo” wengi kwani mara nyingi ni zakujuana juana. Yani authentication ya awards inakuwa haipo kabisa!!
https://youtu.be/LVNGUI6vtAQ
Hongera sanaaaaaa Clouds TV mmenifanya niangalie hii event mara zote mlikuwa mkiirusha hewani! Natumaini na wengine wataiga mfano wenu. Pia hongera sana dada Mwanaidi Mayowela kwa kulitwaa taji kwani unastahili kwakweli! Ubarikiwe sanaaaaaa wewe na familia yako! Nawashindi wengine wote pia nanyi nawapongeza sana. Mungu azidi wabariki.
Malkia wa nguvu; Mchapa Kazi, Mbunifu, Jasiri!
HATA KWETU TUNAO MALKIA WA NGUVU. HONGERA SANA MADAM SOPHEY MBEYELA. -Peter Sarungi
Nikiwa kama mwanaharakati wa kutetea haki na kukuza utu wa watu wenye ulemavu, jukumu langu kubwa ni kukusogeza karibu na jamii hii ili sote tujue mazingira ya watu wenye ulemavu kwa kukuonesha changamoto na mafanikio yetu katika kuchangia maendeleo ya jamii. Tunaamini ushirikiano wako kwetu utaongezwa ikiwa utajua mazingira yetu.
Leo natumia jumapili hii kupongeza mafanikio aliyoyapata dada yangu Sophey Mbeyela baada ya kutwaa Tunzo ya Malkia wa Nguvu kwa mwaka 2017 kutoka Clouds Media kupitia kampeni yao ya kuwatafuta Malkia wa Nguvu kila mwaka. Anapenda aitwe Madam Sophey, ni moja kati ya akina dada shupavu, asiye kata tamaa na mwenye kufuata ndoto yake kutoka katika kundi la watu wenye ulemavu. Kazi yake kubwa ni mwalimu lakini pia ni mwamasijashi (Motivator) mzuri sana anaye warudisha vijana walio kata tamaa katika msitari, pia amekuwa akiamini katika kutoa na hivyo ameendelea kutoa misaada mbalimbali kwa jamii yenye mahitaji maalum kama vile watoto na watu wenye ulemavu hasa wanafunzi. Record yake ni nzuri sana kwa jamii yetu ya walemavu na amekuwa akichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha jamii inapata ustawi.
Nichukue fursa hii kumpongeza sana kwa mafanikio anayo endelea kuyapata na nimtie moyo kwa kusema HAKIKA HIYO NDIO DUNIA YAKE ALIYOPEWA NA MUNGU, ASITAFUTE DUNIA NYINGINE..
Tafadhali kama unapendezwa na mafanikio haya kutoka katika jamii ya watu weye ulemavu basi andika chochote cha kumpa nguvu Madam azidi kutoa mchango kwa jamii.
I got my ticket ready! What about you?! Please order it today!
HAPPY WOMEN’S DAY 2017- Peter Sarungi
Nitumie siku hii ya leo kuwatakia heri wanawake wote duniani kwa mchango wao mkubwa na wa kutukuka katika kuendeleza dunia.
Kipekee nimshukuru Mama yangu kipenzi Bi. Martina Sarungi kwa kuendelea kuwa mama bora kwa watoto wake. Nimtakie maisha marefu na yenye furaha na afya tele ili hata wajukuu na vitukuu waje wafaidike kwa busara na maombi yake.
Pia nimpongeze Mama fidel kwa kuchagua kuwa mama mwema na mwenye malezi yenye maadili, nampongeza kwa kuitwa mama na akumbuke kwamba mafunzo yake kwa mtoto wakati wa malezi ndio nguzo kwa mtoto ukubwani. Sipati picha maisha yangekuwaje bila wanawake, fikiria na wewe alafu naamini utajifunza umuhimu wa wanawake duniani.
Leo natoa dedication ya wimbo wa “power of the women” kwa wanawake wote wanao itwa Grace au Neema maana majina hayo yamebeba historia kubwa sana kwangu. Awe ni bibi, mama, dada, mke, mchepuko ama binti yote hayo ni majini lakini yanasimama kwa wanawake. Nawapenda sana na Mungu azidi kuwapa nguvu katika kutimiza majukumu yenu.