Huwa sipendi kuingilia siasa za ndani za vyama vingine lakini huwa inanilazimu kwa sababu chama kama cha ccm kinatawala serikali hivyo maamuzi yake yana athari kwa uendeshaji wa serikali na Taifa kwa ujumla.
Nimeona mjadala wa wafuasi wengi wa upinzani wakilalamika juu ya maamuzi ya fukuza fukuza ya wanachama wa ccm wanao itwa wasaliti. Wanapinga na kulaani maamuzi halali yaliyotewa kutokana na vikao halali.
Mimi naunga mkono maamuzi hayo maana watu walio fukuzwa wamepatwa na mazingira ya kusaliti chama. Ni kama Mh. Zitto alivyo vuliwa uana chama wa Chadema Tanzania kwa tuhuma za usaliti ulio elezewa na viongozi wa kushirikiana na chama tawala. Walio fukuzwa wana mazingira ya kusaport harakati za Lowasa Edward kushika dola kupitia vyama vya upinzani wakati wao wakiwa na vyeo katika chama cha ccm, huu ni usaliti usio takiwa kufumbiwa macho.
Fukuza, fukuza, fukuza hadi wale wote karibia 75% ya wajumbe wa almashauri kuu ya NEC walio imba wimbo wa kuwa na imani na Lowasa wafutike katika vyeo vyao ndani ya ccm, mkìweza wafukuzeni na wabunge ambao bado ni waumini wa Lowasa.
Mkiamua kujenga safu ya mwenyekiti wenu kwa mgongo wa kusafisha chama, nawashauri mfanye kwa uhakika na asibaki hata mmoja aneyeweza kuhoji na hata kusema tofauti na mkuu. Hilo ni jambo lenu la ndani na wala sisi tusio wanachama hatupaswi kuingilia na ndio maana nina pinga kwa nguvu zote wanao laani na kubeza maamuzi haya.
Nawatakia mkutano mwema katika kujenga ccm mpya na kuiacha ccm ya Nyerere, ccm ya mwinyi, ccm ya mkapa na hata ccm ya Jk.