Leo asubuhi muigizaji wa muda mrefu Charlie Sheen ametangazia dunia kuwa yeye ni muathirika wa HIV kwa muda wa miaka minne sasa. Alisema hayo wakati wa mahojiano maalum kati yake na Matt Lauer wa Today’s show katika channel ya NBC.
Wapendwa wasomaji, mkiona mtu ana fanya mambo ambayo ni tofauti kabisa na mlivyo mzowea; embu jaribu kumchunguza kwa karibu au tafuta nia ya kuwa naye karibu ili ujuwe nini haswa kinacho msibu. Watu wengi hufanya vitu ambavyo vitawatowa katika uwalisia watatizo walilonalo haswa likiwa nikitu ambacho hawana uwezo wa kuki control. Utakuta mtu anaingia kwenye ulevi ulio pindukia, au uwongo usio na mbele wa nyuma, au anakuwa mtu wa starehe 24/7 na kupoteza focus ya maisha, au anaingia kwenye madawa ya kulevya, au ghafla anaingia kwenye ulokole usio elezeka (haijalishi wa thehebu gani), au anakua muislamu yule wa siasa kali (udini ulio pitiliza), au anafanya mambo ya ajabu ajabu yasio eleweka wala elezeka, au anajenga chuki na mtu pasipo sababu yoyote hata kama huyo mtu anamaisha duni kuliko yeye, au anakonda kupita kiasi kwa madai ya “diet”, au anakuwa na uncontrollable waight gain, na mambo mengine kama hayo. Tusiwe wepesi wa kucheka na kuhukumu watu bila kujua ukweli wa jambo. Wengi huwa wana go through stuff and they don’t what to share with people for the fair of being judged or because they have trust issues!
Kwanini nimesema hayo? Kwa miaka kadhaa sasa dunia immeshudia jinsi Charlie Sheen alivyo ingia kwenye ulevi usio elezeka, drug use, na tabia nyingine nyingi zisizo elezeka. Watu waka m-judge na kusema maneno yote mabovu juu yake bila kujua ukweli kuwa anamatatizo ambayo yame mu-affect psychologically (ni baada ya kujua ana HIV+)! Basi wapendwa muwe na roho ya kiubinadamu japo najua ‘vidudu watu’ pua wapo humu duniani, lakini inawezekani tukawa wakarimu kwa wengine!