Tanzania ni inchi iliyo jaliwa kuwa na makabila mengi sana, nafikiri (sina huwakika) ndoyo inchi inayo ongoza kuwa na makabila mengi dunia. Na kitu kinachofanya Tanzania ionekane unique mbele ya uso wa dunia, ni kotoka na ukweli ya kwamba pamoja na wingi wa makabila yaliyomo ndani ya inchi; hakuna kabila lenye nguvu kuizidi nyingine. Kitu hichi nitafauti sana na mataifa mengine barani Africa, ambapo utakuta kuna kabila moja au mawili uanajiona ‘superior’ kuliko mengine, na hivyo husababisha migongano na migogoro mingi ndani ya inchi husika.
Lakini kwa leo nataka niseme hili kuhusu kabila la waluo au wajaluo kama wengi waitavyo. katika kila kabila kuna mila na desturi zake, basi baadhi ya desturi ya Mluo ni kuto kuvaa khanga, kuto kupiga magoti wakati wa kusalimu, na kuvaa vizuri siku ya mazishi hasa kama wewe ndiye muhusika mkuu kwenye msiba huo.
Mimi kwakweli kama ningeolewa kwenye makabila ambayo culture zao ni zile za kupoga magoti; basi mie naona ningeachika 🙂 🙂  Yani ni kitu ambacho siwezi kabisa, na naogopa kuiga nisije siku nikaanguka bure mbele za watu.
Pia si desturi ya Mluo kwa wanawake kuvaa khanga. Sema sikuhizi mambo yanaingilia unaweza kuta baadhi ya wamama wakijaluo wakivaa khanga hata kwenye misiba. Khanga kwa desturi ya mluo huwa inatumika kama pambo fulani ambalo huvaliwa kwa kuwekwa begani. Lakini kama nilivyo sema sikuhizi kuna vitu vingine ambavyo huko juma vilikuwa vinatendwa na specific tribe lakini leo hii vipo common katika makabila mengi-na khanga ni moja ya mfano huo.
Kitu kingine ambacho ni sehemu ya culture ya Mluo, ni kuvaa vizuri na kusherekea baada ya mazishi. Mila na desturi za mluo zina amini kifo ni sherehe ya mwisho ya kila binadamu hivyo inafaa kuaherekewa kama ilivyo katika sherehe zingine kama kuzaliwa, na kuoa / kuolewa. Waluo ni watu ambao siku ya mazishi watu wata vaa vizuri sana na baada tuu ya mwili kuwekwa kaburini basi kiyakacho fuata ni kula, kunywa, na kucheza. Nakama ikatokea aliye fariki ni mtu aliyekuwa akiheahimiwa sana hapo anapoishi basi sherehe itakuwa kubwa sana na mbwembwe za kifahari nyingi sanaaa, kama vile kuvyatua risasi angani, kuchinja ng’ombe zaidi ya wawili ili watu wale na kusaza, na mambo mengine mengi sana.
Picha hapo chini ni za wiki iliyo pita ambapo mama yangu pamoja na shangazi yangu-Theresia Nyobuya walienda huko Karungu, Kenya kwenye msiba wa mme wa bibi yetu mdogo (Mwenye nguo nyeupe. Marehemu bibi yetu mzaa baba (Rhoda Igogo) yeye alitokea maeneo ya Kenya. Na huyu mjane ni mdogo wake pekee ambaye yu hai. Hivyo basi baba yetu anamchukulia kama mama yake mzazi  kwa sasa, kwani mama yake alisha fariki. Pole sana bibi  yetu, and R.I.P babu yetu.
Kitu kingine ambacho nilimwambia mtu hakashangaa, ni kwamba wajaluo hawajui kitu matembele wala kisamvu. Na mkowa wa Mara huwa hatupiki kwa kutumia nazi na wala sijawahi ona nazi mkowa wa Mara, wanapika na maziwa au organic cheese  (jibini).