Nakumbuka wakati naanza kazi 2005 nilifanya kazi kama miezi minne bila kulipwa mshahara wala chochote. Nilikuwa natembea umbali mrefu sana wakati mwingine sababu ya kukosa nauli ili kwenda kazini. Na hata nilipoanza kulipwa nakumbuka mshahara wangu ulikuwa 45,000 ulikuwa mdogo sana na hautoshi.Ila niliridhika kwa sababu nilikuwa najua ni mwanzo wa safari yangu na bado sina ujuzi kivile wala uwezo mkubwa.
Leo hii vijana wengi ninaokutana nao kutafuta ajira swala la kujitolea ni gumu kwao?kusubiri ni ngumu kwao kwanza wengi wavivu na bado wanataka kufanikiwa na kupata pesa.Mtu hafanyi kitu bila kuuliza nitapata nini???
Katika kutafuta kufanikiwa wakati mwingine fanya kazi hata za kujitolea usitangulize malipo.Hili litakupa nafasi ya kujijengea uwezo na kukupa wasifu utakaokusaidia kujipanga vizuri na pengine ukawa mwanga wa ajira ya malipo hapo baadae.
Mdogo wangu Mimi alonifatia alipomaliza chuo sehemu alikuwa anafanyia field waliona uwezo wake wakampa ajira lakini sababu alikuwa bado mdogo wakawa wanamlipa kidogo sana akawafanyia kazi miaka 4 bila mshahara kupanda. Kila siku ananiambia sister mshahara mdogo sana mie nataka kuacha kazi.
Nikamwambia usijihisi upo kazini fanya kazi kama vile upo chuoni chukua ujuzi na mafunzo. Fanya kazi kwa bidii am sure siku ukitoka hapo basi uwe umepata sehemu yenye kukulipa vyema na waseme wamepata jembe haswaaa. Mwaka mmoja baadae akapata kazi tena kwa kufuatwa sio yeye kuomba ambayo wanamlipa vizuri sanaaa na ameweza kutimiza malengo yake mengi sana.
Jiwekee malengo na mikakati hata malengo makubwa huanza kwa udogo. Sawa una elimu kijana na pengine ulihisi ukimaliza chuo tu utapata kazi ya ndoto yako na mshahara mnono. Ukija kwenye ukweli mambo wakati mwingine hayaendagi hivyo.
Ukipata sehemu hata kama wanakwambia fanya bila malipo......fanya huo ndio mwanzo wako.Jijengee maarifa na uwezo.Jamani acheni uvivu.......acheni kutaka ghafla uwe una mihela unalipwa vizuri.Jitumeni mie nawaona wengi humu makazini wavivu. Na usigelezee mwingine alianzaje ukadhani mna safari moja hapa duniani.
Good Morning!
Related