Reposted from @dinamarious – Leo nimeamka kichwa kiko mbio maana zimebaki siku 4 tu niwe nawe katika Maisha Class Seminar.
Lakini nimemkumbuka rafiki yangu mmoja wa toka udogoni.Hatuonani sanaa ila tunaongea sana kwenye simu.Nikakumbuka namna walivyokuwa wakiishi maisha mazuri sana.Wao ni miongoni mwa watu wa kwanza wazazi kuporomosha mijengo huku Mbezi beach.Miaka ya 90 wana hadi boat ya kucruz kwenda visiwa hivyo vya bongoyo sijui mbudya ambavyo sie ndio twaenda leo.
Mama yao aliwazaa mapema sana na baba yao akafariki mapema pia.So walilelewa zaidi na mama.Mama alikuwa na pesaa alikuwa mrembo sanaa na alikuwa na marafiki wengiii mno.Na pia alikuwa mzuri wa sura na wa roho kujitolea kwa marafiki na ndugu sanaa.Wadogo zake kama watatu aliwawezesha kwenda kuishi nje.Yeye safari za nje ya nchi kama sijui kitu gani.Party za babakyu na marafiki safari na marafiki za kula bata nyumbani kwake palikuwa hawakauki watu.
Yule mama alikuja akaanza kuishiwa akaanza pia kuumwa aliugua kwa muda kidogo na kwa wakati huo rafiki yangu na mimi tupo kidato cha pili.Ndugu walikula kona,marafiki ndio usiseme.Alibaki yeye na watoto wake tu na hadi anafariki alimfia mwanae huyo shoga angu mikononi hivi akimhudumia maana ndio wa kwanza.
Kuna mengi yalitokea sanaa lakini hili jambo huwa silisahau.Maana mie ndio nilikuwa shoga ake namna ndugu zake walikuwa wakimfanyia nilishuhudia kwa macho.Na huwa namkumbuka sana huyo mama na sasa nimekuwa mtu mzima ishu hiyo huzunguka sana kichwani kwangu.
Je marafiki waliotuzunguka ni wa aina gani?una marafiki kweli au una wapambe?Ni wangapi katika mafanikio tunakuwa na marafiki wengiii ambao kiukweli wapo hapo kwa manufaa yao?Wapo na wewe sababu una nafasi fulani,wadhifa fulani kupitia wewe mambo yao yatanyooka?Kwa sababu una mkono wa kutoa labda utatatua shida zao,utasikiliza hofu na nyakati ngumu wanazopitia. Utawalisha,utawanywesha,utawapa pesa,nguo,viatu inshort unarahisisha maisha yao.Ngoja pesa ikate ndio wa kwanza kukusema umefulia na kukukimbia.
Ngoja cheo/nafasi uliyonayo ipotee ndio utawajua walimwengu au wali nyama!Sitasema sana ila Mungu atujaalie watu sahihi katika maisha yetu.
MaishaClass #NenoLangu – #regrann
**Imeandikwa na Dina Marious**