Watu ambao wamesomea na wanafanya kazi za upelelezi wa hali ya juu ndio tumezoea kusikia au kuwaona wakiishi maisha ya siri ambayo hayatoi huwasilia wa yeye ni nani. Hii nikutoka na sababu za kiusala wa maisha yao pamoja na kupata ukweli halisi wa jambo wengi inabidi wa-prented maisha yao. Kwamfano; mtu anaweza akaishi maisha ya chini sana (low profile) siyo kwamba hana uwezo ila nikwasababu hatakiwi kuwapa watu matamanio ya kumjua na kuanza kumfuatilia; hivyo hawa tunasema wanaishi “double life.” Lakini vile vile kuna watu ambao wanaishi “double life” siyo kwasababu ya kazi wanazo zifanya bali wanakuwa na maisha fulani ambayo si mazuri labda kwa familia yake, marafiki, ndugu, wafanyakazi, na jamii inayomzunguka. Maisha ya “double life” siyo tatizo la njisia moja tu, la hasha! Ni tatizo kubwa ambalo lipo kote kwa wanaume na wanawake hambao huficha siri za ajabu kutoka kwa wake walio karibu nao. Katika kundi hili tunaweza kuligawa katika sehemu kuu tatu:-
Sehemu ya kwanza ni group la watu ambao ni hatari sana kwa jamii. Hawa ni watu ambao atafanya kila njia ku-gain public trust (waaminike kwenye jamii) kuwa wao ni watu wema, mara nyingi watatumia elimu yao, au utaalamu fulani walio nao, au cheo chao kama mapadri au wachungali ili kujenga imani kwenye jamii lakini wakati huo huo hawapendi watu wawajue maisha yao kiundani. Siku zote hawa ni wale watu wanaodai “privacy” ili kuficha maisha yao ya siri. Yani hawa huwa hatakama anajiusisha na social media utakuta anaweka picha au vitu vinavyo husiana na kazi anayofanya tuu au haweki kitu chochote kwa madai ya “privacy.” Sababu ya kusema hili group ni la watu hatari ni kwasababu wengi ni wasomi wenye familia zao na wanahela hivyo ni rahisi kwao kuaminika kwenye jamii bila shinda. Lakini vile vile ni hatari kwa jamii kwasababu ya mambo wanayo yafanya; hapa wengi wao ni wale ambao wanafanya biashara za human-trafficking, ubakaji wa watoto, wateja wakubwa wa child-pornography, kufanya mapenzi na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane, na pia wauza madawa ya kulevya wakubwa. Katika group hili la kwanza wanaume ni wengi zaidi kuliko wanawake kwasababu ya aina ya uwalifu unaofanyika. Mfano mzuri wa group hili la kwanza, ni hii habari ambayo zimetanda kwenye television kwa muda sasa the Subway guy-Jared Fogle (pichani juu). Unaweza soma na kusikiliza habari zake kwa kubonyeza (HAPA). Labda kwa faida ya wasiojua hiyo lugha niseme kwa ufipi kuwa huyu mtu alipata kuaminika kwa jamii yake inayo mzunguka na kwa wamarekani wote kutokana na hadithi yake ya kuweza kupungua zaidi ya pound 100 kwa kula Subway sandwich. Alijipatia umaharufu mkubwa sana na kutengeza hela nyingi sana kwakuingia mkataba na Subway wa kutangaza chakula chao ambacho kilimsaidia kupunguza unene ambayo ikapelekea watu kumuita “the Subway guy.” Jared au the Subway guy alikuwa mtu mwenye familia (mke, watoto wakike wawili na wakiume mmoja) walikuwa wanaishi maisha yao mazuri sana hapa U.S.A katika State ya Indiana. Lakini Jared alikuwa anaishi “double life.” Alikua anamisha yake ya siri ambayo hata mkewe wazaidi ya miaka kumi halikuwa hayajui mapaka siku FBI walipo vamia nyumba yao na kuanza kuchunguza vitu na wengine wakifanya doria kwa juu kwa muda wa masaa kadhaa kisha kuondoka na mumewe! Yeye alikuwa mteja mkubwa wa picha za ngono za watoto (children pornography) pamoja na kufanya mapenzi na watoto wa chini ya miaka kumi na nane. Just imagine sikuzote anamuaga mkewe kwenda New York City kikazi kumbe hii ndiyo ilikuwa kazi yake huko New York. Msaidizi wake wa kazi katika business zake ndiye aliyekuwa natengeneza hizo picha za ngono za watoto na kumuuzia pia kumfanyia mipango yote ya kufanya mapenzi na watoto!! Embu jaribu kuvaa viatu vya mke wa Jered Fogle, ungeweza? Mie nimejaribu nimeshindwa vimenibana mnoo! Sijui ningefanyaje na hivi nilivyo mwepesi wa ku-panic naona “ningechungulia kaburi!” Embu msikilize hapa akimsifia mumewe (HAPA) Sasa hivi mkewe ameamua ku-file divorce na kutaka custody ya watoto wao wote. Binafsi nimebaki nimejiuliza usalama wa watoto wake tena ukizingatia wa wili ni wakike! Kama mama lazima utajiuliza je alishawahi kuwafanyia kitu wanangu au la? Maana tunaona yeye anadili na watoto, very scary! Pia katika group hili ndo anakuta wale wachungaji ambao wameowa kumbe ni ma-gay mpaka siku wakikamatwa ndiyo huwa wana kiri. Au wake za watu ambao ni lesbian wa kisiri siri!
Kundi la pili, ni kundi la wale wanaopenda ku-cheat au maisha ya kihuni wakati wanafalimia zao. Hili kundi si hatari sana kwa jamii lakini madhara yake huwa ni makubwa sana kwasababu wengi huishia kupoteza maisha yao au maisha ya familia yao yote. Kwamfano baba mwenye familia mbili tofauti na hazijuwani, au housewife ambaye nafanya uhuni wakati mumewe yupo kazini, au mume / mke mwenye huusiano mwingine bila mwenzie kujua. Mfano wa muda kidogo ni Tiger Woods au mfano wa karibu ni huyu police mkuu aliyejiuwa baada ya information za Ashley Madison kutoka hadharani kimakosa na kugundulika kuwa alikuwa akiishi maisha mengine ambayo familia na jamii haikujua. Unaweza soma habari zake (HAPA). Ashley Madison ni mtandao ambao unawakutanisha watu ambao wanataka kufanya mapenzi bila kuwa na commitment yoyote. Wana slogan yao isemayo “Life is too short have an affair!” Kuvuja kwa information za watu wanao tumia mtandao huo kisiri kumeumbua watu wengi sana, wenye nyathifa za juu mbali mbali haswa hapa U.S.A na Canada. Hili kundi la pili mara nyingi ni watu ambao kwababu fulani hawataki kuacha familia walizo zianzisha ila wanaamua kuwa na mahusiano na watu wengine kwa siri na unaweza usiamini huu ukweli kuwa wanawake wanaongoza kwa hili group! Nimesema hapo mwanzo kuwa madhara la hili kundi ni makubwa sana japo si hatari kwa jamii kwasababu matukio mengi ya kutisha na kusikitisha watu hawa husababisha uhalifu, vurugu, na mara nyingi vifo kwa wahusika. Nimeshaona story kwenye Oprah show ambapo wanawake zaidi ya sita waliambukiza HIV na mtu ambaye kila mtu aliamini kuwa ni boyfriend wake. Pia nilishaona kwenye forencic TV mwanamke aliye amua kutuma watu kumuuwa mpenzi wake wa inje ya ndoa baada ya kumtishia kutoa siri yao kwa mumewe na pia kutaka ajue kuwa mtoto wao wa kati (3) siyo wake. Huyu mwanamke alitaka kuachana na huyo “serengi boy” wake na ndio hapo mambo yakawa si mambo! Pia kuna show fulani inaitwa “who did I F’n married to” ambapo mwanume mmoja alikuwa na familia 4 kwenye inchi nne tofauti. Yani hii dunia ni kichwa cha mwandawazimu! Katika kundi hili la tatu ni lawatu ambao nao pia wanataka kuaminiwa na kuheshimika katika jamii kuwa ni watu wema, waungwa, na wenye tabia nzuri lakini wakiwa ndani ya nyumba zao zile tabia anazo zionyesha nje kwenye jamii ni tofauti kabisa. Hawa ni watu ambao wakiwa nje ya nyumba zao ni wakarimu, wampendao Mungu, na tabia nyingine kama hizo lakini wakirudi nyumbani ni moto wa kuotea mbali! Ni wanyanyasaji wa hali ya juu, na siku zote amani haiko ndani ya nyumba zao. Hili group ni la watu wengi sana ambao limejumuisha watu wa hali tofauti, masikini, matajiri, wasomi, na wenye elimu ya chini lakini mara nyingi halina madhara makubwa kwa jamii zaidi ya wale wanao wazunguka kama wake / waume zao na watoto wao au saa nyingine wafanyakazi walio chini yao. Kundi hili wanaume ni wengi zaidi kuliko wanawake. Hapa naweza nikatoa mfano wa mke wa Pastor mmoja hivi ambaye alizidiwa na siku hiyo akasema basi liwalo na liwe akachukua bunduki na kumuua mume wake! Huyo Pastor ambaye alikuwa anaaminika sana kwenye jumuiya na kuonekana muungwana lakini akirudi nyumbani alikuwa ana sexually abusing mkewe. Ana m-treat mkewe kama “striper” (yani wale wanawake wanaocheza uchi kwenye striper’s clubs). Huwezi amini mwanamke alikamatwa na kushinda kesi baada ya kutowa ushahidi ya jinsi mumewe alivyokuwa akimfanyia pamoja nakuwa alikuwa ni Pastor na wamezaa watoto watatu. Alikaa jela kwa miaka 3 tuu na kutoka. Tazama sehemu ya mahojiano yake kwenye hii video
Wataalamu wanasema watu wengi wanao ishi maisha ya double life huwa kunakitu ambacho psychologically kinawasumbua ndani ya miyoyo yao hivyo jufanya hivyo kukidhi haja ya lile pengo “void” walilonao. Inawezekana ni power-struggle, abandonment walio pata wakiwa wadogo kwani wengi huwa wanabeba hizo hasira mpaka ukubwani, au ni watu wasio jiamini (low self-esteem), au ni watu tuu wamezaliwa na roho ya shetani na Mungu pekee ndiye anayeweza kuwaponya! Wengine inatoka na maisha aliyokulia labda yalikuwa ni maisha ya kunyanyasika / kikatili sana japo hao walikuwa ni wazazi wake hivyo anajikuta anaiga tabia zile zile na kumalizia hasira kwa mkewe au watoto wake. Nakumbuka ilikuwa mwezi wa sita mwaka huu mida ya saa 5 na dakika kadhaa usiku nilikuwa naendesha gari kulekea nyumbani (kwenye gari nilikuwa na binti yangu) nikaona kabinti kadogo dogo hivi nikamwambia mwanangu huyu mtoto anatoka wapi saa hii? Kumbuka kalamazoo, Michigan ni mji mgodo sana hivyo saa 5 za usiku ni kupo kimya. Basi nikaamua kutoka barabarani na kum-block kwa mbele yake. Nikamuuliza anatoka wapi na anakwenda wapi? Akasema anatoka kazini na anaenda nyumbani (na nikweli alikuwa amevaa uniform za Lee’s Kitchen). Nikamuuliza kama anaishi karibu akasema hapa, anatumia masaa 3 mpaka kufika kwao (Gull road). Nikamwambia aingie kwenye gari nitampeleka. Basi akapanda, nikamuuliza anaishi na nani akasema anaishi na mama yake mzazi. Nikamuuliza kuhusu baba yake akasema hataki hata kusia habari zake, “he’s just useless.” Akanieleza amemaliza High School April 2015, na anasubiri kuanza college in September hivyo imembidi atafute kazi kwani mama yake anasema she’s 18 yrs inabidi wa share bills!! Kwakweli baada ya sentence hizo mie sikutaka tena kumuuliza kitu kwani sikutaka agundue kuwa machozi yalikuwa yakinitoka!! Wondering how can a mother be so rude to her only one child / daughter? Na nashukuru nilikuwa na mwanangu kwenye gari kwani ilimfanya azidi kunipenda sana! Basi yule binti akasema mama yake huwa anamuhaidi kumfata halafu hatokei hivyo inambidi kutembea, hata wakati wa mvua!! Fikiria anatoka kazini saa 5 atembee masaa 3 inamaana anifika nyumbani kwao majira ya saa 8 usiku!! And she’s only 18 yrs old! Kitu ambacho kiliniuumiza zaidi nipale alipo malizia kwa kusema “I want to be a Child Psycologist. I can’t wait to finish college and have a nice job and my own place I will be very selfish just like them!” Nilisikitika sana! Unaona jinsi wazazi wanafanya watoto wao wawe na hasira za milele na kuishi maisha ya chuki kwasababu ya kukosa upendo nyumbani?!!
Mwisho, nawasihi wazazi muwe makini sana na watu wanao wazunguka watoto wenu. Usiamini mtu yoyote hata siku moja. Treat everyone like a suspect kwani hii dunia imeisha! Hawa watoto wanaofanyiwa ukatili huu (child pornography na under age sex) wanafanyiwa nawatu ambao wanaaminiwa sana kwenye familia, ndugu, jamaa na marafiki. Je mtoto wako anapokuwa uchi ni nani huwa anakuwa karibu yake? Je umemfundisha mtoto kuhusu good touching na bad touching? Hii si tuu kwa watoto wakike hata wakiume pia ni janga la dunia. Mungu alinde na kuwabariki watoto wote!
I like this post, enjoyed this one appreciate it for putting up.
Hello. remarkable job….touchy stories. Thanks!
Very interesting topic, thank you for putting up.