Familia tatu kwa pamoja wakifurahia siku kuu! Aliye kati kati ndio kiungo kikuu cha hizi familia tatu! Huyo ni shemeji mkubwa kutoka familia ya Lyimo. Na kulia ni Dennis Rweikiza ambaye amemuoa dada wa Jackson Lyimo. Mnakumbuka niliwapaga story yangu na Dennis Rweikiza? Soma ?? (MrAndMrsRweikiza). Na upande wa kushoto ni John Adhero ambaye pia amemuoa mdogo wake Jackson Lyimo. Na hao ni watoto wao! Hata kama utakuwa na marafiki milioni moja lakini familia bado ni muhimu zaidi ya vyote! Everyone needs a family! Marafiki wanakuja na kuondoka lakini family will always be there! Udugu haufutiki hata kwa bleach isipokuwa KIFO! Blood is thicker than water! Hata kama mtakuwa na mahusiano mabaya but that "bloodely thing" will always find a way kuwaweka pamoja! Marafiki ambao watakuwepo na wewe siku zote, wakati wa raha na shida, wakati unapitia misuko suko ya maisha na kila mtu anakuona haufai mbele ya macho yao, wakati wengine wanakukimbia lakini hao wachache au mmoja atakaa na kusimama na wewe mpaka mwisho basi naomba ujue huyo SI RAFIKI BALI NI NDUGU YAKO! Tofauti ya rafiki mwema na ndugu ni kwamba ndugu anaweza asiwe nawe wakati wote lakini ndio hivyo huwezi kumkana!! Ile damu iliyowaunganisha ndio itasimama siku zote! Lakini rafiki mwema lazima aonyeshe kuwa yeye ni rafiki mwema ili muwe na kitu kilicho waunganisha!! Ndugu yako anaweza asiwe rafiki yako lakini bado atabaki kuwa ndugu yako! Ili udugu ukolee na upendeze zaidi lazima kuwe na urafiki kama mnavyoona hizi familia tatu! Wameweza kuacha kazi zao na kukaa pamoja wakati huu wa siku kuu! Kama wangekuwa hawana urafiki hata kama ni ndugu usingeona haya yakitokea! Upendo hupo ndani yao, na Mungu ni pendo! Familia zilizo jaliwa kumjua na kumwamini Mungu utaziona tu! Kwenye Mungu kuna upendo, kwenye Mungu siku zote ni furaha na amani tele hata sura zao zitaonyesha zinakuwa na mvuto wa "Kimungu Mungu" tu ??......Pichani ni Jackson Lyimo na wadogo zake. Anita Lyimo Rweikiza upande wa kulia na Linda Lyimo Adhero upande kushoto What a family reunion!! Mtu kati hapo ndio wifi mkubwa mke wa Jackson Lyimo pamoja na wadogo zake Lyimo! ....wazurije sasa ???? .....Jamani nawatakieni kheri na baraka zote za kufunga mwaka 2017 ziambatane nanyi pia mwaka 2018! Mzidi kubarikiwa zaidi ya hapo na upendo wenu udumu siku zote!