Regrann from @farajanyalandu - Oprah Winfrey amefanya interview na marais, waimbaji, wanamichezo na mashujaa wa matukio mbalimbali. Kila mmoja akiwa ni mtu aliyefanikiwa katika eneo fulani. Hawa ni watu walioenda mbele zaidi na kujitofautisha na wengi. Lakini wote wakimaliza mahojiano, camera zikizimwa, huwa wana swali moja kwa Oprah. How did I do? Sina tafsiri ya moja kwa moja lakini ni swali ambalo wanataka kujua iwapo walipatia au walikosea. Sana sana wakitamani kusikia walifanya vizuri na interview yao ilikuwa bora. Huu ni uhitaji ambao kila binadamu anao. Si udhaifu kwasababu ni katika harakati za kujitambua. Ni vile tunataka kufanya vizuri na tungependa kupewa feedback na wakati mwingine kupewa moyo kuwa tunaenda sawa. Ni muhimu kuwa na neno la upendo kwa wengine. Tusione watu wanatembea ni wazima kumbe ndani wana vidonda. Pengine wewe ndio utakuwa wa kwanza na pengine utamuwahi kabla hajakata tamaa na kudhani hana thamani. Tutibiane vidonda. Tuthaminishane. Tukubaliane tofauti zetu. Tukosoane kwa upendo. Sisi ni watoto wa Mungu na Mungu ni pendo. Let's validate each other! #WeekendWisdom ? - #regrann
Related