Awii! Aren’t they cute! Dr. Mengi na vijana wake. Wapendezaje sasa, usinicheke hata majina yao siyajui ?? lakini hiyo haitoi ukweli kwamba ni ma-handsome wa nguvu! Mungu awabariki.
Ngoja nitumie nafasi hii kuongelea jambo fulani ambalo nililiandika humu wakati fulani mwaka jana. Niswala ambalo lilikuwa linahusu family ya Dr. Mengi haswa kuhusu ndoa yake na K-Lynn These boys are adorable! Super cute!…. anyway tuendelee na story yetu ? Basi katika kujifanya mimi ni mmoja wa wanaojua kutoa kasoro na ushauri kuhusu familia za watu sinikaandika kuhusu habari ya K-Lynn na Dr Mengi! ?? mbona nilikoma!! Mara naangalia simu nakuta missed calls kibao kutoka home kwa mama Igogo. Watsup msgs ndo usiseme! Akasema nifute haraka sana hiyo post na hata mtu aki Google asiipate! ???
Mbona ilikuwa balaa! Mdogo wangu Magreth toba! Yeye ndo alikuja juu kweli kweli utadhani Dr Mengi ni baba yake mzazi ??? Anyway to make a long story short, Mama yangu alicho nisisitizia ni kuwa hata siku moja nisije weka post humu kuhusu matatizo ya familia ambazo hazinihusu!! Niache mara moja, na kama nikitaka kuandika basi niandike matatizo ya familia yetu na si zawatu wengine!!……. yani nilikosa raha nika muandikia my cousin-sister Sophia Makoyo msg (inbox) kwa Facebook, soma ? Tokea siku hiyo sijawahi kuandika kitu chochote kile juu ya K-Lynn na Dr. Mengi mpaka hivi leo. Nawala sito kaa tena kuzungumzia matatizo ya familia yoyote ile ambayo hainihusu unless nimeitwa mahakamani kutoa ushahidi!! Haha! Nilijikuta nime ‘kula’ block kwa Instagram ya K-Lynn lakini naelewa na hivyo mbele yenu nyinyi wasomaji wangu, na mbele za Mungu naomba leo niwaombe rasmi msamaha K-Lynn na Dr. Mengi’s family kwa ujumla wao. Naomba mnisamehe sana for my lack of wisdom and respect to your family. Nilikosea sana kuingilia maswala ya familia yenu wakati hayanihusu hata chembe! Natoa ahadi, sito rudia tena. Na si kwenu tuu bali kwa mtu yoyote yule. I hope you will find a place in your heart to forgive me. ?
Ushauri wangu kwa wasomaji wangu wote ni kwamba; maswala ya familia ni maswala sensitive sana, ni maswala personal, ni maswala ambayo yapo very complicated. Hivyo kama wewe si muhusika wa moja kwa moja wa hiyo familia basi keep your nose out of it!! Tujifunze kuheshimu na kulinda familia zetu. Hata kama hiyo familia ipo machoni kwetu 24/7 hiyo haitupi huwalali wa sisi kuingilia na kutoa ushauri wa nini kifanyike katika hiyo familia, kwani “kitanda usicho kilalia hujui kunguni wake.”!! Halafu sisi tunapo ziongelea hizo familia hakuna tunalo saidia zaidi ya kuongeza matatizo, chuki, na kuumiza wahusika zaidi. Matatizo ya familia yatatatuliwa ndani ya familia na wana familia wenyewe.
Kila familia hapa duniani ina matatizo yake! Sasa sisi ni akina nani hata tunyooshee familia zingine vidole wakati matatizo ya familia zetu wenyewe yanatushinda?! Hata mimi mwenyewe nipo over protective when comes to my child, parents, and family. Yani dare not to mess up with my family! Kwanza nitakuuliza who the heck are you!! If you’ve never walked even a single mile in my shoes, you have no say in my world!! Just find a seat somewhere on the corner and zip it!!
Mungu azidi kuzibariki na kuzilinda familia zote hapa duniani ? much love to K-Lynn and Dr. Mengi’s family ?❤