Wapendwa hii Foster Collection itakuwa inachanganya viwalo / mavazi tofauti ya Foster na mambo mengine ambayo yeye Foster anayapenda na angependa kushea nanyi. Kama mmeona jana Jokate Mwegelo kasema Diva2006 ndio mahala pake pakuchagua viwalo basi hivyo ndivyo nitakavyo fanya kwa Foster. Nitawaletea mambo tofauti na recommendation zake Mimi binafsi sitakuwa na specific place; bali kama nikitaka kununua bidhaa au kushona nguo hapo Bongoland basi nitakwenda kwenye maduka ambayo yatakuwa recommended na hawa wadau wangu halafu nita share nanyi. Uwamuzi wa wapi kwenda utafanya wewe mwenyewe. Mimi kazi yangu ni kukuonyesha sehemu utapata vitu vyenye ubora wa kimataifa kutoka kwa watu nilio waamini na hawata niangusha Huu upendeleo ni kwa watu wachache sana lakini ni muhimu kwa hii blog. Niwatu ambao siyo tu nimewachagua kiholela holela hapana! Yani hata wewe utawakubali. Sitaji majina yao lakini utawajua tu siku zinavyo kwenda….. Hili zoezi nitafanya hata kwa wauza maandazi, vitumbua, na chapati hapo Bongoland yani wale mama ntilie ili ujue ukiwa mjini na hauna hela ya kula 5*hotel wapi pakwenda. Kama unataka viwalo vizuri wapi pakwenda. Basi siku si nyingi nitawaambia ni wapi Foster ananunua vitenge vyake na nani huwa anamshonea. Hata kama wako kumi nitaweka list yao hapa wewe ndio utachagua wapi pa kwenda.