Jana katika jiji la Dar kulikuwa na mpambano wa jadi kati ya Yanga na Simba. Mpambano ulikuwa na mbwembwe nyingi na mwisho wa siku ikawa 1-1. Kilichonifurahisha ni Goli linalioitwa la Mkono alilolipata Tambwe. Mimi ni yanga na kweli furaha yangu ni ushindi tu iwe ni kwa mafigisu ama kwa halali. Goli hili nalifananisha na Goli la Mkono katika siasa, kuna mwanasiasa mmoja aliwahi kusema kuwa watashinda hata kwa bao la mkono…..Magoli kama haya ni adimu sana na ndio yanaleta furaha/huzuni na utamu/uchungu wa mpira kama ilivyo mafigisu ya siasa wakati wa uchaguzi. Goli ni goli tu ikiwa limekubaliwa na mwamuzi.
Hongereni watani wangu wa Jadi kwa kurudisha kwa Goli zuri la Kichuya. Ila hamkuonesha ustaharabu katika mchezo baada ya kuharibu viti na miundo mbinu mingine. Mkiendelea na ushabiki huo wa vurugu kutakuwa na haja ya anko Magu kuwafundisha adabu ili mje mumuite Dikteta kama kawaida ya wabongo wengi.
Tukutane tena Round ya Pili.