Nimetafakari sana suala la simu FAKE nchini Tanzania. Nimetafakari sana uamuzi wa kuzizima simu FAKE hizo mwaka huu. Nimejiuliza maswali mengi sana, simu FAKE hizo zimeingiaje Tanzania? Zimeingia kupitia mlango gani? Hayo maduka yanayouza yameruhusiwa na nani? Mwananchi mnyonge anayenunua kwenye duka la simu kosa lake Nini? Nani katufikisha hapa kiasi cha kuwatia hasara wananchi wetu? Hatua gani zimechukuliwa dhidi yao?
Simu bandia na vifaa bandia vya electronics vimeleta maafa makubwa sana, nyumba nyingi zimeungua, watu wamedhurika hata kupoteza viungo vya miiko yao. Uhalifu unaongezeka. Nani alaumiwe? Wako wanaozitaka hizo feki kwa matumizi maalumu (uhalifu)! Wananchi wengi wanapoteza fedha, serikali inapoteza mapato (hazipitishwi njia halali hivyo hazilipiwi kodi)!
Tunahitaji kuwa salama, tunahitaji kuepuka madhara tusiuoyajua kwani hazijulikani zinatengenezwa na nini!Simu feki sio za kutoka China, yako Mataifa sugu kwa kutengeneza simu bandia! Hakiki yako sasa, huwezi kujua umebeba nini na unakaa nayo 24%! Serikali imefanya uamuzi huu baada ya kutoa tahadhari tangu 2010 na kutoa miezi 6 ya kuelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia 16/6/2016 Kweli? Wananchi wsmetahadharishwa tangu Juni 2010! Taarifa zimetolewa kwa njia mbalimbali zaidi ya miaka 5! Wakati Kenya ikizima simu bandia serikali ililaumiwa kwa nini hamfanyi kama Kenya! Makampuni ya simu yametuma text message kwa kila mwenye simu kuhakiki simu yake kabla ya kununua! Wajibu wa TBS tunaujua? Kazi yao sio kuzuia vitu bandia bali kuweka viwango na kuthibitisha ubora wa bidhaa (Angalia Mandate Yao kwenye sheria iliyoanzisha Shirika).
TCRA haina mamlaka ya kusaka wala kuzuia bali kusaidia soko kujua na kutambua vifaa vya mawasiliano vyenye kukidhi viwango vilivyowekwa na ITU na WHO na kutoa leseni kwa waagizaji na wasambazaji wa vifaa vya mawasiliano. Iko maabara ya kukagua vifaa kuanzia minara, vifaa vya utangazaji na vyote vya mawasiliano.
FCC ndio wenye dhamana ya kukagua, kusaka na kuharibu bidhaa bandia kwa ujumla. Wanafanya kazi yao vizuri. Tatizo ni kuwa bidhaa bandia ni uhalifu wa kimataifa na zinatumika mbinu mbalimbali kuziingiza nchini. Ilichofanya TCRA ni kuleta teknolojia ya kuzitambua simu bandia kuunga mkono jitihada za kimataifa kukabiliana na tatizo hili.
Vitu bandia ni vingi, unahitajika ushirikiano wa wananchi kuisaidia serikali kupambana na uhalifu huu badala ya kufikiria “kutumbua” tu. Tuwatumbue kina nani kuhusu fedha bandia? cheni bandia? Tushirikiane kuzuia Tanzania kuwa soko la bidhaa bandia. Chukua hatua, hakiki simu yako leo, usinunue simu bandia.