Hakuna dhambi kuwa wa tofauti na wengine. Dhambi nikulazimisha kuwa kama wengine! Kuna watu ambao maisha yao binafsi yanawapita au wanajikuta kwenye matatizo kila siku iyendayo kwa Mungu kisa na mkasa ni kulazimisha kukubalika kuwa mmoja wa “nyumbu” wa kundi fulani! Nimewaita “Nyumbu” kwasababu Nyumbu ndio wanatabia ya kufata mkumbo wa wengine ili akubalike! Trying so hard to “fit in”! Na saa nyingine hata kama una fit-in kwenye group fulani haimaanishi kuwa hapo ni mahali pako stahiki! Kuna watu wanashindwa kupata mibaraka yao mikubwa ambayo Mungu amewaandalia kwasababu ya kulazimisha kuwa kwenye group fulani!
Mibaraka ya Mungu ni mitakatifu hawezi kupa kama hauko teyari! Hivyo nilazima uwe umeandaa sehemu au umejiandaa kwa kujisafisha / fanya matengenezo ya njia zako ndipo anakumiminia!
Vijana wengi wa kike hata wanawake wazima wasiku hizi wanapenda sana maisha ya kuiga na kufata mkumbo kwasababu hawajui thamani yakuwa mtu ‘Huru’! Mtu mwenye mtazamo na maamuzi yako binafsi ambayo hayavunji sheria wala kuingilia haki na uhuru wa mtu mwingine! Why trying so hard to fit in when you were born to stand out! #BeYou
Kama picha zinavyo onekana, mimi naamini ni mtu huru! Basi weekend hii na week hii yote nimejisikia na nimeamua ku-rock mabutu hair style! Kwani kuna dhambi gani mtu kusuka mabutu? Yani kuna joto kiasi kwamba sitaki kusuka rasta, na mawigi yananiwasha kwa hili joto! Nasema hivi, hakuna dhambi kuwa wa tofauti, dhambi nikulazimisha kufanana na kila mtu! In a world full of Kardashians be Princess Diana!………..Btw, Sijajichubua, ni makeup na reflection ya miyonzi ya jua! #AlphaBeingAlpha Hii picha ☝ nilipiga Summer 2015, one week baada ya kuhamia Texas! Hapa sikupaka makeup ?