Napenda kuwatakia mama yangu mkubwa pamoja na baba yangu kheri na furaha ya miaka 51 ya ndoa yao. Mungu azidi kuwalinda, kuwabariki sana, upendo, furaha na amani vizidi kutawala maisha yenu na nyumba yenu. Mmekuwa mfano nzuri si kwetu sisi watoto wenu hata kwa watu wengine. Mbarikiwe sana. Kwa faida ya wengi; mama Musira au Mrs Musira ni dada yake mkubwa na mama yangu mzazi. Yeye ndiyo mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya mama yangu. Pia alikuwa mlezi wa mama yangu wakati anasoma secondary huko nyumbani kwa watani zangu Rugambwa Secondary. Vile vile walikuwa ni walezi wangu mimi wakati nasoma Kowak Girls Secondary school. Mzee Musira ndiyo alikuwa akija kwa mikutano ya wazazi pale wazazi wangu walipo shindwa fika, kwani ilikuwa ni rahisi kwa mzee Musira kufika si tuu kutokana na ukaribu wa wanapoishi bali pia alikuwa Mkurugenzi wa Elimu wa diocese ya Musoma (kwa kanisa la Catholic) hivyo kila mkutano lazima anakuwepo. Asante sana baba na mama. Hapa ni mwaka jana waliokuwa wanasherekea Jubilee ya ndoa yao. Atukuzwe Baba Mungu aishie mahali pa juu Mbinguni. Hapa ni mimi na wadogo zangu Janeth na Magreth pamoja na mama mkubwa. Tulienda wasalimia huko Kamnyonge, Musoma mwaka 2013.
Kwenye picha hizi ☝ ni mimi na wadogo zangu pamoja na baadhi ya watoto wa mama mkubwa Neema (mwenye top nyeupe na nyeusi) pamoja na Yacinta (mwenye pink na black)…………Happy 51st Wedding Anniversary wazazi wetu. Tunawapenda sana.