Happy birthday Mercy!

Leo ni siku ambayo mwanangu kipenzi cha roho yangu amezaliwa. Katika kuadhimisha siku hii nimeamua kuweka kumbu kumbu ya post zote za birthday wishes ambazo Niliwahi kuandika huko Facebook. Japo nikawaida yangu kupost siku za birthday yake lakini sijui bbn kwanini nimejikuta nimewaza kama Facebook ikafutika ghalafa hizi kumbu kumbu zote zitapotea. ?‍♀️?‍♀️?‍♀️ Nilipokuwa naziandika niliandika hisia zangu halisi, niliandika vitu ambavyo sio tu vilitoka moyoni bali ninaviamini, hivyo vinabeba uzito mkubwa sana kwangu. Na nilipokua nazisoma tena leo yani mwili unanisiaimka kwa furaha na tabasamu la amani moyoni. ?? Ninawatoto wengi lakini aliyekaa tumboni mwangu na kunifanya ni experience uchungu wa kuzaa ni huyu mmoja tu! Hivyo ana Extra special place in my heart and life!

Mimi huwa nikiandika kitu chochote ambacho kinagusa hisia zangu huwa sirudii kukisoma mpaka muda upite sanaaaa! Yani huwa napenda ku-present my raw feelings! Napenda mtu apate ujumbe kwa jinsi nilivyo jisikia mara ya kwanza. Ndio maana hata kama kuna makosa ya kiherufi (spelling error) huwa naacha hivyo hivyo mpaka nitakapo jiona nipo tayari kusoma hisia zangu katika maandishi ya uhalisia wake! Haya ngoja nitiririke kama ifuatavyo ??






https://www.alphaigogo.com/ni-kwa-neema-tu/

Haya yani hapa nimesha weka kumbu kumbu sawa za toka akiwa na miaka 18 mpaka leo ??? Yani hii hata siku Mungu akinijalia wajukuu basi watakuja ona jinsi nilivyo mpenda mama yao nao itabidi wampende hivyo hivyo, sitaki utani na mwanangu mie ??

Happy birthday Mercy, mjukuu number moja, ubarikiwe sana. Nakupenda leo, nitakupenda zaidi kesho, na milele nitazidi kukupenda.

Leave a Reply