Hata Kama Mambo Yanakwenda Vibaya, Fanya Hivi
Ni rahisi sana kuwa na hasira, kukatishwa tamaa na hata msongo wa mawazo. Hiki ni kiu ambacho kila mtu anaweza akawa nacho kwenye maisha yake.
Nikiwa na maana kila mtu akikasirishwa, anaweza akakasirika sana au mtu akikatishwa tamaa anaweza akakata tamaa pia sana.
Lakini yote hiyo haiwezi kusaidia kitu. Busara na ukomavu wako wa kimaisha unakuja pale hasa unapokwenda kinyume na mambo hayo.
Ni kweli unaweza ukawa umekasirishwa na ukatamani upige mtu sana, sasa je, kwani ni lazima ifike mahali ukakakasirika kwa kiasi hicho?
Ni kweli unaweza ukawa umekatishwa tamaa, lakini kwa wewe haina haja kuendelea kufanya mambo ambayo yanakukatisha tamaa zaidi.
Unachotakiwa kufanya au kujifunza ni kuweza kugeuza mambo ya hovyo na yakawa bora zaidi hata kama imetokea hali ya kukasirishwa au kukatishwa tamaa.
Kufanya hali mbaya ambayo tayari naweza kusema umeshapewa na ikawa ni nzuri, huo ni ukomavu wa hali ya juu utakaokufanya uishi vizuri sana duniani.
Mtu amekuuzi sana na wewe huhitaji kuendelea kufoka au kuumia zaidi. Unatakiwa kutuliza akili yako na kufanya mambo ili yawe mazuri.
Kufanya mambo yawe mazuri hasa pale yanapokuwa yameharibika ni kitu ambacho unatakiwa ujifunze nacho sana karibu kila siku.
Kila siku na kila wakati endelea kuweka juhudi za kuwa mtu chanya, mpaka maisha yako yalete utofauti mkubwa na kwa wengine.
Ni watu wachache sana ambao wako tayari kubadilisha hali mbaya ya msongo wa mawazo walionayo, kukatishwa tamaa na kukasirishwa kuwa nzuri.
Wengi wakikasirishwa na wengine hukasirika na kukasirisha zaidi. Hivyo, unatakiwa usiwe miongoni mwao. Unatakiwa uwe mtu wa kubadilisha hali.
Kufanya hali yoyote iwe bora ni zoezi ambalo unaweza ukalifanya karibu kila siku kwenye maisha yako pale ambapo unakuwa unaona mambo hayajakwenda sawa.
Unatakiwa uelewe hili, pale mambo yako yanapokwenda hovyo, fanya mambo hayo yawe bora. Jitahidi kubadili hali hiyo kwa busara na ikawa bora.
**By Mapigano**
Related