Nikiwa kama mwanaharakati wa kutetea haki na kukuza utu wa watu wenye ulemavu, jukumu langu kubwa ni kukusogeza karibu na jamii hii ili sote tujue mazingira ya watu wenye ulemavu kwa kukuonesha changamoto na mafanikio yetu katika kuchangia maendeleo ya jamii. Tunaamini ushirikiano wako kwetu utaongezwa ikiwa utajua mazingira yetu.
Leo natumia jumapili hii kupongeza mafanikio aliyoyapata dada yangu Sophey Mbeyela baada ya kutwaa Tunzo ya Malkia wa Nguvu kwa mwaka 2017 kutoka Clouds Media kupitia kampeni yao ya kuwatafuta Malkia wa Nguvu kila mwaka. Anapenda aitwe Madam Sophey, ni moja kati ya akina dada shupavu, asiye kata tamaa na mwenye kufuata ndoto yake kutoka katika kundi la watu wenye ulemavu. Kazi yake kubwa ni mwalimu lakini pia ni mwamasijashi (Motivator) mzuri sana anaye warudisha vijana walio kata tamaa katika msitari, pia amekuwa akiamini katika kutoa na hivyo ameendelea kutoa misaada mbalimbali kwa jamii yenye mahitaji maalum kama vile watoto na watu wenye ulemavu hasa wanafunzi. Record yake ni nzuri sana kwa jamii yetu ya walemavu na amekuwa akichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha jamii inapata ustawi.
Nichukue fursa hii kumpongeza sana kwa mafanikio anayo endelea kuyapata na nimtie moyo kwa kusema HAKIKA HIYO NDIO DUNIA YAKE ALIYOPEWA NA MUNGU, ASITAFUTE DUNIA NYINGINE..
Tafadhali kama unapendezwa na mafanikio haya kutoka katika jamii ya watu weye ulemavu basi andika chochote cha kumpa nguvu Madam azidi kutoa mchango kwa jamii.