Jana huyu mtani wangu aliandika hii “status” yake kwa Facebook kama inavyo someka hapo juu ☝. Sasa mie nilimjibu kwenye comment kama inavyosomeka hapo chini ?. Nashukuru kuna binadamu ambao nao wanaelewa kile ambacho mimi naye nakielewa na kuamini kuwa si kila mtu ni mtu kwani hata shetani naye ni mtu!
Sasa ngoja nitolee maelezo. Hata shetani naye ni mtu kama walivyo watu wengine hivyo kuwa muangalifu sana na “watu”! Tafuta kuzungukwa na watu wenye UTU ambao ndiyo wanaitwa “binadamu” lakini kama wewe unataka kuzungukwa na watu? Ndugu yangu nakupa pole sana kwani unaweza ukajikuta umezungukwa na kundi la mashetani au mapepo wewe ukidhani. ni watu!
Kuna na “watu” wenye roho za shetani ambao ukiwaona utadhani ni binadamu! Wanavaa vizuri, wengine wana elimu nzuri, wana sura na sauti za upole mfano wa malaika, wengine ni warembo sana, wengine wapo mbele kuwa wanataka kusaidia “watu”. Lakini kaa nao karibu wow! Utajikuta unajiuliza hivi huyu ni mtu au shetani! Kuna watu waongo mfano hakuna, kuna watu ni wataalam wa kusuka na kusamba majungu ambayo yanaweza yakafanya mtu akauliwa (I’m a living testimony), watu ambao wana roho mbaya hujawai ona, kuna watu ambao ni serial killers, wachonganishi, etc!
Wapendwa wasomaji wangu, kuweni waangalifu na “watu” siyo kila mtu ni binadamu! Shetani na wafuasi wake wapo hapa duniani nao ni “WATU”! Na anaweza kuwa mtu yoyote yule; ndugu, rafiki, jirani n.k Mungu atupe uwezo wa kuwatambua hawa “watu” ili ukae nao mbali sana!