Hapa duniani naweza sema 99% tumezaliwa kwa mfumo mmoja tuu (1% nimeacha kwa wale wanao pandikiza mimba kutumia utaalamu wa kisasa). Lakini kwa 100% bila shaka yoyote nasema kuwa wote tumekuja hapa dunia kwa kutumia mwili wa mwanamke! Hivyo kama ni mtu mwenye akili timamu unaweza ona ni jinsi gani mwanake anaumuhimu sana katika dunia hii! Yani hata kama technology itakuwa advanced kiasi gani katika maswala ya uzazi lakini bado mwanamke atahitajika tuu!! Na ndio maana inchi zinazo litambua hilo wanaweka sheria kali za kumlinda na kuheshimu mwanamke.
Kwanini nimesema haya; nikutokana na kile nilicho kiona baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema kujitoa katika madalaka yake na watu haswa haswa wananachama wa Chadema walivyo amua kumtusi na kumshtumu mke wa Dr. Slaa. “Lakini huyu mzee Slaa ni mzigo kwakweli, mzee mzima kama huyu kushikwa akili na mwanamke ni aibu sana, hivi kweli huyu urais angeuweza kweli, kiongozi wa chama mkubwa unalipwa zaidi ya 7 per monthly bado posho na marupu rupu kibao lakini week sasa inaisha umefungiwa ndani na janamke kazini huendi? Hivi kweli unadiriki kumpa mwanamke password za social networks, aiseee huyu mzee mi nimemshusha sana thamani,” hiyo ni moja tuu ya baadhi ya maoni mengi ambayo yametolewa na watu juu ya huyu mama. Mengine siwezi hata andika humu kwasababu ya ukali wa lugha walizo tumia.
Ngoja nianze kwa kusema kwanza yeye mwenyewe amekanusha hizo shtuma na kusema ni uwongo na uwonevu! Sasa nyie mbuluraz mliomtukana mlitumia kigezo kipi? Au kama kwaida yenu sikuzote mnamtupia lawama mwanamke? Si ndio tatizo la mfumo dume wa Tanzania ambao wanawake wa Tanzania na wengine duniani wanaupiga vita?! Kumkandamiza mwanamke na kumuonea bila sababu tena katika karne hii 21 halafu mnasema manataka mtawale inchi? Ni inchi hipi hiyo? Inaama Chadema ikichukua inchi haitawasikiliza wanawake katika kufanya maamuzi magumu ya inchi? Are you guys serious?! Au ni inchi nyingine wezetu mnaongelea ambayo haina wanawake? SMH!
Halafu embu tuwe wakweli, mnasema eti Dr. Slaa hana maana kwasababu anamsikiliza mkewe?! Really? Nyie militaka amsikilize nani wakati huyo ndiye ambaye kila siku wako naye kwenye mabomu ya machozi? Mbona hata sikumoja hatujawahi kumuona mke wa Mwenyekiti wenu (Mrs. Freeman Mbowe) kava gwanda yupo jukwaani kwenye jua kali akinadi sera za Chadema kama kweli anapenda maendeleo ya inchi hii ambayo mume wake anayapigania? Hatujawahi ona hata watoto wa Mbowe kwenye magwana wapo jukwaani halafu leo hii mnasema Dr. Slaa asimsikile mkewe? Inapanda akili hii kweli? Shame on you all! Kama mkeo hajawahi kupigwa kama mke wa Dr. Slaa kwa kutete chama chake basi nyamaza na mumuache Dr. na mkewe huyo huyo ambaye nyinyi mmemuona hakufaa kuwa first lady wenu yeye ndo kesha muona na anajua she’ll always be his first lady! Kama vipi kumywa vinegar changanya na tangawizi!
Bila hata aibu mnasema amechukia kwasababu amekosa nafasi ya u-first lady! Siwezi mshangaa hata kido, kwani hata ingekuwa mimi ningechuki tena ninge mwaga siri zote za Chadema nje! Kupigwa kote kule mpaka na mimba ikatoka kwa ajili ya Chadema halafu leo hii mnamuona hafai na kumuweka mtu mwingine? Halafu eti mnamlaani? Hiyo laana itawajia nyinyi Chadema kwani machozi ya mwanamke hayaendi bure!! Wakezenu mmewafungia ndani wanakula raha tuu kwajasho la mwanamke mwenzao halafu mnaona sawa? Dah! Mnabahati sana maana natamani nimuweke kristo pembeni niwatukane kidogo nyie mbuluraz sema nashindwa! Uchugu na utamu wa ndoa ya Dr. Slaa wanaijua wao wawili, nawamesha fanya maamuzi yao basi nyie nao make na hizo ndoa zenu za kidikteta ambazo mwanamke si kitu mbele ya mwanaume! SMH!
Wanaawake ndiyo dira ya ulimwengu huu. Kama sio kwa uvumili, busara, na ufanyaji kazi bila kipimo cha mama zenu wengi wenu hata shule msinge kanyaga; kwani baba zenu wengi walikuwa wanashinda kwenye vilabu vya pombe na kuangaika na starehe zisizokuwa na kichwa wala mguu! Hao wanawake ambao mnawadhara ndio walivumilia upuuzi wote ili kuwafichia baba zenu aibu japo nao waonekane wana familia! Halafu leo hii mnatumia hiyo hiyo elimu ambayo imeipata kwa nguvu na jasho la mwanamke kuwadhalilisha mwanamke?! Mbuluraz nyie!
Inchi zote zilizo endelea zinathamini sana mwanamke kwani wanaelewa uhumimu wa mwanake katika jamii, si tuu kwa kuzaa watoto bali hata kwa kujenga jamii iliyo bora! Kama umeshawahi kuchunguza mataifa yenye shida sana ni yale yasio kuwa na maadili ya kuheshimu na kumlinda mwanamke. Wanyewe wanaziita “Third World countries!.” Na Tanzania nimoja ya hizo inchi za “Third World Countrie.” Ni wakati muwafaka wa tasisi zote za serika na watu binafsi beba jukumu la kufundisha watoto zao wakiume hata wakike umuhimu wa mwanamke katika jamii. Kuna mibaraka siyo tuu nyumbani bali hata kwa jamii inapo mjali na kumuheshimu mwanamke! Katika uchaguzi huu nawasii wanawake wenzangu wasichague chama chochote kile chenye misingi ya kunyanya na kuto kuheshimu wanawake.