“HILI ALILOSEMA MBOWE BUNGENI JUU YA UTAWALA NA WABUNGE WA CCM LINAHITAJI KUTHIBITISHWA UKWELI WAKE.”-Peter Sarungi

Katika kipindi cha maswali na majibu ya hapo kwa hapo kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Chini ya mwamvuli wa UKAWA Mh. Freeman Mbowe alitaka kujua ukweli wa taarifa ya kufanyika kwa kikao cha wabunge wa CCM chini ya mwenyekiti wao Mh. Kassim Majaliwa Ambaye pia ni Waziri Mkuu. Katika kikao hicho kulikuwa na ajenda ikiwemo kujadili Mswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari na upashaji wa habari pamoja kujadili mpango wa bajeti ya mwaka ujao ambazo kwa pamoja zinakwenda kujadiliwa katika bunge la sasa na ikiaezekana kupitishwa. Lakini Mh. Mbowe amekwenda mbali zaidi katika taarifa alizopata na kusema kwamba ” Wabunge wa CCM wamepewa Zawadi ya sh. milioni kumi (10M) kila mmoja na shuguli hiyo ikiratibiwa katika ofisi za CCM Lumumba.

Taarifa hizi zina mshitua mwananchi yoyote ambaye ni mzalendo na makini na nchi yake bila kujali itikadi za kisiasa na mwenye imani na utawala huu wa JPM kwa juhudi zake za kubana matumizi na kutumbua majipu kama njia ya kupambana na Rushwa. kwa taarifa hizi zisipo elezwa ukweli wake basi wananchi watabaki njia panda juu ya imani kwa serikali yao pendwa.

Kama Taarifa hizi ni za kweli basi zitakuwa zina tafsiri yafuatayo:…..

1. Serikali ya awamu hii imezidiwa katika kuibua, kusimamia na kutetea hoja hadi kufikia kutoa zawadi ya 10M ambayo ni rushwa kwa wabunge ili kuweka mazingira mazuri katika ajenda zake bungeni

2. Kuna dalili za serikali ya JPM kutoungwa mkono na wabunge hadi wa chama kinacho tawala. Na inaonesha hata wabunge wa ccm wanasoma namba za kisiasa na za utawala huu.

3. Ile kauli ya kupambana na rushwa ina ubaguzi katika utekelezaji maana haiwezekani ukatumbua majipu kwingine halafu kwako ukatekeleza ufugaji wa majipu.

4. Inawezekana huu Mswada wa sheria ya vyombo vya Habari una matatizo ya mbeleni ama una nia ovu ya kukandamiza uhuru wa habari kama wahariri wengi wanavyo lalamika na ndio maana Waziri Mkuu ameamua kutumia nguvu ya pesa katika kulainisha koo za wabunge na kupata kuungwa mkono

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

#Mytake
Kuna haja ya Waziri Mkuu kujitathimini kama kweli kikao hicho kilifanyika na mlungura ukatolewa kwa wabunge ili kama hana uwezo wa kuongoza baraza la mawaziri katika kutetea hoja na mipango inayotazamiwa kufanywa na serikali. Kama hawezi basi akae pembeni kupisha nguvu mpya yenye kuendana na kasi ya JPM na wenye ushawishi wa hoja bila kutumia Zawadi.
JPM akilifumbia macho taarifa hii na matendo kama haya yanayo fanywa na watendaji na viongozi wasaidizi alio wateua, atakuwa anafifisha juhudi alizo anzisha za kupambana na Rushwa na tutakuwa na tafsiri mbaya juu ya ndoto alizo nazo kwa nchi.

Tunaiomba serikali isikae kimya kwa tuhuma hizi na ikiwezekana itoe maelezo ya kina na kueleweka juu ya kikao hicho kama kilifanyika kwa kubagua wabunge tu na posho nono kama zawadi.

asanteni sana

Leave a Reply