Hakuna hatua ambayo unaweza kupiga halafu ukasema hiyo hatua ni ndogo hivyo haistahili kujipongeza au kupongezwa, kwani hakuna mtu alianza kusimama na kutembea bila kutambaa angalau kwa siku kadhaa! Japo najua baba yangu kuna mambo mengi na makubwa amefanya na amepongezwa sana si tu ndani ya Tanzania bali hata inchi za ugenini, lakini kama nilivyo wahi kusema huko nyuma moja ya nia kuu ya hii blog ni ku inspire watu kwa kutumia mifano halisi (real life experience / stories) ili iwasaidie kwa njia moja ama nyingine kutokukata tamaa na kuona kuwa hakuna lisilowezekana! Basi kwa maana hiyo naomba nitumie mwanya huu kumpongeza baba yangu. Hongera kwa kuteuliwa kwake kuwa Makamu Mwenyekiti wa World Green Design Organization upande wa Tanzania. Hii sasa ni kwa mara ya pili kwa nonprofit organizations kubwa duniani kumteuwa kuwakilisha Tanzania. Zaidi ya miaka 17 iliyopita chama cha walipa kodi duniani (World Tax Payers Association) kilimteuwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Tanzania ambapo mpaka leo hii bado ni mwanachama wao na ni mmoja wa Board of Directors wa chama hicho.
Hongera sana Sir. Otty, sky’s the limit!
hongera Uncle