Hongera sana Mr Bilton kwa kuamua kufanya ‘maamuzi magumu’ ya kuachana na maisha ya u-single na kufunga ndoa, kuanza maisha mapya ya familia. Hongera sana! Harusi yao ilifungwa katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurios, Kurasini na kufanyika Marantha Hall, Msimbazi CenterMrs Lulu Otto, amependeza sana. Hakuna ajuae kuumba kama Mungu! wifi yangu kaumbwa na akaumbika kweli kweli ? Mungu awabariki sana upendo wenu ukadumu milele Naomba niwakumbushe tena wale walevi kuwa huyu mrembo si Lulu Andrea Nyigo tena bali NI MKE HALALI Wa NDOA WA BILTON TOBIAS OTTO! Heshima inahusu sana, wajaluo huwa hawataki matani na wakezao ooooh! Usijesema sijakwambia. Hongera sana Bilton, umepata mke mwema mpende na umtunze vyema kama utunzavyo mboni ya jicho lako. Mawifi naona wao walivaa “dark-red” mmependeza sana. Haya kaka kesha owa mumshike wifi yenu kwa mikono yenu yote miwili lasivyo itakuwa “imekula” kwenu ??
Safi sana. Mmependeza mno?? Hongera sana Mr and Mrs Bilton Otto ❤❤