Hongera sana Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwa kazi nzuri sana ya kujali elimu kwa watoto wanaosoma katika mazingira duni. Hakuna kitu ambacho cha furaha ambacho hata Mungu anafurahia kama mtu anayetoa sehemu ya jasho lake na kuwapa watu ambao hawawezi kumlipa na bila kuhitaji fadhila yoyote ile toka kwao. Mrs Mengi SIYO mkazi wa wilaya ya Temeke, wala SIYO mwanasiasa kusema labda ipo siku ataomba kura. Na wala haitakaa hata siku moja watoto wake wasome katika wilaya ya Temeke! Hello!! Can we talk? Am keeping it real! Hata kama wakifirisika leo sana sana wataishia kusoma labda South Africa au India ?? No shade people! Kwa mfano my feature babies nani alikwambia watasoma Bongoland?! Subutuuu! Watasoma hapa hapa kwa Trump Bongoland wataenda kutembea tu ?? anyway back to our story…. Ninachotaka kusema ni kwamba Jacqueline kwa kupitia mfuko wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation hawakuwa na ulazima wa kukanyaga wilaya ya Temeke, hivyo kwa wao kuifikiria wilaya hiyo ambayo hawana faida nayo yoyote inaonyesha jinsi gani wanaguswa na maisha ya Mtanzania wa hali ya chini bila kujali wanatoka sehemu gani!! Kwamaana hiyo, watu wa Wilaya ya Temeke ambao mpo jirani na shule ya Muungano ikifika siku ya Ijumaa mjitokeze kwa wingi kuwashukuru na kuwaomba waendelee kuikumbuka wilaya hiyo! Wapi Juma Nature na wanaume TMK?! ? Please show some love to Dr. Ntuyabaliwe Foundation on Friday! “Today in celebrating Universal Children’s Day I had the pleasure of visiting Muungano Primary School as the chairman of @drntuyabaliwe_foundation and got a chance to talk with the children there. I was happy to see how confident and smart these kids were and can’t wait for Friday when we will launch a new library and donate books to them.” Jacqueline N. Mengi