Hongera sana mdogo wangu Davis Kateti na wifi yangu Ester Kateti kwa kula kiapo KITAKATIFU. Mungu awaongoze katika kila jambo jema mlitendalo! Akapate kuwa ngao na kimbilio lenu wakati wote siku zote katika nyakati zote za raha na tabu! Akabariki uzao wenu hata kizazi cha tatu na cha Nne! Nyumba yenu ikawe hekalu ndogo; amani, upendo, furaha vikadumu ndani yenu! Hongereni sana wapendwa!
Kwa faida ya wengi, bwana harusi ni mtoto wa mama yangu mdogo. Mama yake (pichani juu ☝) anamfuata mama yangu mara ya 6 katika kuzaliwa. Mama yangu ni mama yake mlezi. Harusi ilifungwa katika kanisa la Wasabato Ukonga, na sherehe ilifanyika ukumbi wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es salaam siku ya JumaPili, tarehe 07/ 09/2017.
Harusi ilishuhudiwa na babu mzaa baba mzee Kateti ambaye alitoka kijijini Utegi na ndugu wengine wengi toka Utegi, Musoma, na Arusha ambapo wazazi wa bwana harusi wanaishi! mawifi wa bibi harusi katika nyuso za furaha mama mlezi mama Igogo na babu wa bwana harusi mzee Kateti Shangazi wa bwana harusi upande wa baba (kati kati) pamoja na maharusi wanandugu ndugu na jamaa pamoja na marafiki wazazi na maharusi mama wa bwana harusi na mkamwana wake! Mama mkubwa / mama mlezi mama Igogo akiwapiga picha wanawe mabinamu / dada wa bwana harusi Magreth na mama Ngosha Kwamara nyingi tena, hongereni sana. Mbarikiwe wote! ?❤