Jamani, hivi vitu huwa vinatokea kweli japo vina chekesha. Kuna watu kadhaa ambao nawafahamu walikuwa na majina makubwa mjini, pesa za kumwaga (mafisadi wa Serikalini), watu wana wanyenyekea kama Mungu vile lakini kwao wazazi wanaishi kwenye nyumba ya udongo ?? Siku moja akafiwa na baba yake mzazi mmh! Kaenda kwenye msiba aibu tupu, yani hata yeye mwenyewe pakulala alikuwa hana ikabidi awe ana lala ndani ya gari! ??
Kuna mwingine yani yeye sasa alikuwa akija kwenye misiba ndo sehemu yake ya kutoa mashauzi na michango mikubwa kwa dharau ya kuwa yeye ndo ana pesa zaidi. Basi siku moja watu fulani (kumbe walimpania) waka ‘mnywea’ pombe. Basi alipo anza mashauzi yake tuu wale wababa wakasimama na kuanza kumzodoa. “Unajifanya unapesa hapa mjini wakati mama yako anaishi kwenye nyumba ya udongo iliyo ezekwa kwa manyasi! Ipo siku moto utashika nyumba na kumkaanga mama yako kama ngenge (sato)!!” ??? yani walimchambua kama karanga hadi yule baba alilia. Baada ya hapo mbona alienda mjengea mama yake nyumba nzuri yenye paa ya mabati ?? chezea vichambo vya wajaluo wewe?? Yani alimtoa mkewe aende kijijini kusimamia ujenzi kwa miezi 3 nyumba ikasimama ?
Kuna mwingine huyu ni kizazi cha “.com”! Kutwa yupo busy kupost picha za kwenye Facebook, na Instagram yupo kila kona ya dunia hii anakula na kulala kwenye mahotel makubwa na mume wa kizungu. Kuvaa expensive designers cloth. Wakati wazazi wake maisha yao mmh! Yeye akija TZ anafikia hotelini na familia yake. Wazazi ndo wanaenda kumsalia hotelini. Zinapigwa picha za kumwaga zina rushwa mtandaoni ??? Hawa ni watoto walilelewa katika maisha mazuri kweli kweli enzi hizo. Lakini wazazi wao hawakujali kabisa maisha ya wazazi wao kijijini watoto wakike ndo walio simama na wazazi wao!
Ujumbe: Tuwajali wazazi wetu. Na pia wazazi wakumbuke kuwa watoto hujifunza kwa kuangalia wazazi wao. Kama wewe mzazi humjali mzazi wako basi tegemea hayo hayo kutoka kwa watoto wako.
Sasa ngoja niwaulize nyie Wahaya mlioko kwa Obama, je wazazi wenu wana nyumba au mnaleta ubishoo tuu hapa ???