Je ulishapata kusikia life story ya ndugu yetu (Mtanzania mwenzetu) Fortunata Kasega ambaye aligundulika akiwa na HIV akiwa na umri wa miaka 22? tena baada tu ya kuolewa na kupata ujauzito? Alikuja Marekani na ndipo walipo ngundua kuwa ana HIV!
Ni kisa cha kusisimua lakini kinafaraja ndani yake. Binafsi naweza shuhudia kuwa nimeona ndugu, jamaa, na marafiki ambao wapatwa na majanga kama hili la Fortunata, kuna wengine wamesha tangulia mbele za haki, lakini watoto wao mpaka leo bado wanaishi pamoja na watoto zao. Kuna mmoja wa my nephew ambaye kwasasa yupo secondary lakini wazazi wake wote walishatanguli.
Basi, naweza sema hata nyumbani siku hizi elimu ya kuishi na HIV na kuwa na watoto wako imekuwa sana. Yani sasa hivi wapo wengi wenye HIV lakini wanazaa watoto. Tatizo la nyumbani ni jinsi ya ku-control watu wenye HIV wasiambukize wengine kwasababu hakuna legal consequences ambazo zinamfunga huyu muathirika kama akiambukiza mtu mwingine kwa makusudi; hivyo watu wenye roho za kishetani hutumia mwanya huu kuambukiza wengine.
Watu au jamii hujifunza kutoka na makosa. Lakini nashangaa kwanini taasisi ya fya ya Tanzania hajajifunza kuhusu kuzuia maambukizo ya HIV kwa uzembe. Kwanfano state nyingi hapa U.S.A wame weka mkataba wa ku-share infos za mtu akisha gundulika kuwa ana HIV taharifa ya majibu yake yatasambazwa kwa vituo vyote vya afya ndani ya U.S.A ambavyo wame signed huo mkataba ili wajue na waweze kum-monitor (inaitwa duty to warn). Kwasababu mtu anaweza akahama state moja kwenda nyingine nakuanza kuambukiza watu kwa makusudi. Hivyo kwa jina lake kuwa kwa database inasaidia sana kani wanaweka haina ya HIV aliyonayo (yani aina ya vijidudu) hivyo ukimwambukiza mtu ni rahisi kujua ni nani amekuambukiza.
Napenda kuipongeza mamlaka ya kanisa la Waadnevtista Wasabato Tanzania kwa kuliona hili mwanzoni kabisa HIV ilipokuwa ni tishio kubwa sana. Kama nilivyosema jamii hujifunza kutokana na makosa, basi wao walijifunza kutokana na makosa yaliyotendeka na kuweka sheria ya kupima kwa lazima kabla ya ndoa siku ya ndoa. Yani bila majibu ya HIV hakuna ndoa tena nilazima ya pimwe Muhimbili siyo hospitali nyingine za private. Sisemi hii inazuia kwa asilimia 100% kwasababu wapo ambao wanaambukizwa HIV baada ya ndoa lakini angalau kama kanisa inakuwa imefanya sehemu yake katika kuokowa maisha ya wale walio waaminifu. Nafikiri kuna baadhi ya madhehebu nayo yana hii sheria sina huwakika na ndigi zetu ambao ni waislamu.
Habari hii ya Fortunata Kasega nimeitowa kwa blog ya nesiwangu.com, nawe waweza soma habarii kwa kina kabisa kwa kubonyeza link hii NESI WANGU