Na Peter Sarungi (Next Speaker)
Kila mtu hapa duniani ana mapungufu yake, inawezekana mtu akayajua hayo mapungufu ama laa asiyajue mpaka aambiwe. Kuwa na mapungufu ni sehemu ya uumbaji wa Mungu maana Mungu hakupi vyote vilivyokamilika na ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kibinadamu wa kukosoana, kuelekezana, kusifiana na hata kupingana katika maswala mbalimbali. Sio jambo la ajabu kukubali unapoambiwa mapungufu yako maana huo ndio mwanzo wa kutibu udhaifu unasababishwa na mapungufu yako, lakini ni jambo la ajabu na lililokosa busara na hekima kukataa kushauriwa ama kupinga uwepo wa mapungufu yako pale unapo ambiwa.
Kuna tukio linalozungumzwa sana na makundi mengi ya kijamii Tanzania, UKUTA. UKUTA inaratibiwa na chama cha upinzani Chadema Tanzania katika kufikisha ujumbe ya madai yao, lakini pia serikali ya awamu ya tano kupitia Chama cha Mapinduzi nao wanaratibu operation ya KUVUNJA UKUTA chini ya idara ya ulinzi n usalama wa nchi. Pande zote mbili zimekuwa na matamko mbalimbali yenye kuonesha ubabe, vitisho, dhihaka, chuki, na hali ya kutokubali kurudi nyuma. Kwa historia za mambo ya kisiasa hali hii ya sasa ni hatari sana kwa usatawi wa nchi ki uchumi, siasa na jamii nzima.
UKUTA na VUNJA UKUTA ni majina tu ya operation zinazoratibiwa lakini utekelezaji wake unabeba matendo na matukio makubwa yanayozaa mbegu ya chuki itakayopandikizwa kwa wananchi na serikali yao kwa vizazi vya sasa na vinavyokuja. Hali kama hii ilianza miaka ya 90+ nchini burundi na watawala wakashindwa kisoma alama za nyakati kwa kujivunia dola wanayo miliki bila kujua kuwa dola huletwa na wananchi, matokeo yake nchi ilipata hasara na pigo kubwa linalosumbua mpaka leo.
Viongozi wetu wanahitaji kutumia meza ya mazungumzo zaidi katika kufikia makubaliano mbalimbali kuliko kutumia operation za UKUTA na VUNJA UKUTA. Mazungumzo ni busara yenye nguvu ya Mungu kuliko operation za kibinadamu zinazotumia mabomu, mawe na vurugu. Hivyo nawaomba viongozi wa pande zote mbili kujadili kwa kutumia meza badala ya nguvu. Hii ndio busara na hekima zinazohitajika kutoka kwa viongozi wetu. Mfano: video hii ya chini
inatafsiri hali halisi ya viongozi wetu wengi tunaowapa dhamani ya kulinda maslahi ya nchi na wananchi wake wanavyokosa lugha yenye matamshi ya kuleta nchi pamoja na badala yake wanatoa matamshi ya kugawanya wananchi na kushauri wajenge UKUTA mwingine maana huu wamesha ubomoa tayari, matamko kama haya yanaishi vichwani mwa wananchi kwa muda mrefu na wengine hufika mbele zaidi katika kufikiri jinsi ya kukabiliana na VUNJA UKUTA zingine zitakazo kuja mbeleni.
#My_Take Tutumie taratibu za kisiasa katika kutatua migogoro ya kisiasa balada ya nguvu za dola, migomo na maandamano.
Naipenda Tanzania kuliko chama na mwanasiasa.