International Day ni siku ambayo makanisa ya Wasabato hapa Marekani wanasherekea au unawezasema wana enzi uwepo wa "diversity" (uwepo wa mataifa mbali mbali na tamamaduni zao) ndani ya makanisa na haswa ndani ya nchi. International Day haifanyiki siku moja yani hakuna siku maalumu iliyotengwa kuwa leo ni International Day bali husherekewa kuanzia mwezi wa Nne mpaka mwishoni mwa mwezi wa Tano, anywhere kabla ya sherehe za makambi. International Day nikama siku ya wageni inavyofanyika Tanzania, wale Wasabato wenzangu waliopo Tanzania wananielewa. Tofauti huko Tanzania naona mnasahau kuwa siyo wageni wote ni Watanzania (hawaongei Kiswahili) hivyo kungekuwa na umuhimu wa kuwatambua kwa mataifa yao.Anyway, siku hii kwa hapa kwetu ilifanyika jana May 5th, 2018. Tulifurahi sana kwa kula vyakula vya mataifa tofauti tofauti. Haya nawe enjoy picha hizo na ubarikiwe sana. Pichani ni First Lady wa kanisa letu (Mke wachungaji wetu) pamoja na mama yangu mzazi. Mtanzania mwenzangu na mshiriki wa kanisa letu pamoja na mama yangu. A sister from Kenya and our church members Another sister from Kenya, I real do love Kenyans! Ni watu ambao wako straight to the point kama hataki kitu anasema wazi kuwa sikitaki kwasababu hii! Ule unafiki wa "Kibongo" kwakweli hawana au mimi sijakutana na Wakenya wenye unafiki wa level yetu sisi Wabongo! Napia wanaelewa kuwa to agree to disagree ni jambo lakawaida siyo chuki! Mimi ninaugonjwa wa kuchukia WANAFIKI NA WAONGO!! Jamani siwape watu wenye tabia hizo!! mniombee tu kwakweli maana only God knows how much I hate watu wa sampuli hiyo!! Anyway, tuendelee na story yetu ??? Wanawake wa Kitanzania wakiwakilisha ?