Namshukuru Mungu kwa mambo mengi sana! Na moja ya vitu au mambo ambayo siku zote huwa nashukuru ni hii zawadi ya mtoto ambayo alinipatia, sina lugha yakuelezea ni jinsi gani huwa namshukuru Mungu sanaaaaa!
Mungu alinizawadia zawadi ya mtoto katika umri ambao sikujua vizuri thamani yake au umuhimu wa uwepo wake katika maisha yangu lakini nilijua kuwa its worthy to keep her alive! Na leo hii ndiyo naelewa haswa thamani halisi na umihimu wa mwanangu kwa maisha yangu! Sitachoka kumshukuru Mungu siku zangu zote!
Kwa maneno naweza sema mwanangu ni rafiki yangu mkuu, lakini kimatendo au kiuhalisia mimi ni mama yake na ndingependa siku zote bond ambayo nitakuwa nayo ni bond ya mama na mwana na wala si bond ya best friend! Yeye anamarafiki zake ambao anawa consider kama best friends zake, na mimi ni mama yake ambaye uhusiano wetu ni wakaribu na uwazi kiasi ya kwamba yupo huru kuongea nami kitu chochote! Best friends sometime can’t tell you the truth but your mother always will!
Najua kuna wamama wengi ambao wako single (not married) ambao mara nyingi huwa wanapenda kusema “mimi ndio mama, na mimi ndio baba!” Kwakweli mimi binafsi huwa sipendi huo msemo hata kama I’m a single mother, kwani naamini baba yake siku zote ataendelea kuwa baba yake na hata siku moja mimi kama mama siwezi kuchukua nafasi ya baba yake maishani mwake! Yote yale mazuri ambayo ninamfanyia mwanangu mimi nafanya kama mama ambaye anamapenzi ya dhati na mwanae na si kwamba nafanya kwa niaba ya baba yake!
Sasa basi ni influence ya kiasi gani ambayo baba mzazi anaweza kuwa nayo kwa mtoto hapo inategemea na kiasi gani huyo baba alijihusisha na maisha ya mwanae. Na hapo ndipo kunakitu kinaitwa “father figure” au “mother figure.” Yani hawa ni walezi walio simama kama wazazi katika maisha ya mtoto.
Kuzaa kunakufanya kuwa baba au mama lakini haikufanyi kuwa mzazi! Mzazi is earned not given!! Those who nurtured and inspired you to be the person whom you’re today hao ndio wazazi wako. Kwa maana hiyo tunapo sherekea au kufurahi baba zetu katika mwezi huu wa Sita kama ilivyo desturi ya hii dunia; basi napenda kumshukuru sana baba yangu mzazi si tuu kwa kanilea mimi bali pia kwa kusimama kama baba mlezi wa binti yangu (father figure). Niukweli usio pingika kuwa kupata baba mwenye roho ya utu, hekima, busara, na upendo kama alio kuwa nao baba yangu ni nadra sana katika jamii ya Waafrika haswa Tanzania. I’m more than blessed!! Asante sana baba yangu. Mungu azidi kukubariki sanaaaaa mpaka ushangae hahaha!
Kama una picha yako na baba yako ungependa kushare nasi basi kuwa huru na tutumie kwa [email protected]
Asante sana.