Katika pita pita yangu huko Facebook nikachungulia kwa mama wa “Wanawake Live” a.k.a “Mwanamke piga kazi” a.k.a “Super woman”……….. Nilipochungulia nikaona post ambayo chanzo chake ni Jamii Forum! Post hiyo ilikuwa inamuhusu yeye Joyce Kiria kuwa kwanini havai pete ya ndoa? Embu soma hiyo post hapa chini kabla ya kusoma maoni yangu Mimi naamini kuwa kuna umuhimu wa kuvaa pete ya ndoa lakini si lazima kwasababu zifuatazo:- (1) kama wewe ni mtu upo kwa macho ya jamii kila wakati basi ni muhimu watu wakajua your identification ya mambo ya msingi kama marriage status yako. Lakini si lazima! Yani nisawa na kusema wakristo wabebe Biblia mikononi au vichwani muda wote ndio tuamini kuwa ni wakristo! Hapana! (2) Kuvaa pete ya ndoa 24/7 haichangii kuongeza wala kupunguza upendo kati yenu nyie wawili kama kweli mna mapenzi ya dhati! Upendo wa kweli hutoka moyoni nasio kwenye pete! (3) Sio wote waitao Bwana Bwana watakao uona ufalme wa Mungu! Basi ndivyo ilivyo kwa wanandoa; sio wote wavaao pete ya ndoa 24/7 ni waaminifu katika viapo vyao! Tabia ya mtu haibadilishwi na pete! Rejea scandal ya Bill Clinton na Monica Lewinsky au Tiger Woods (4) Kuvaa pete siyo guarantee ya kupata heshima. Heshima ya mtu hujengwa na mtu mwenyewe! Mfano Oprah Winfrey na Stedman (5) Pete ya ndoa haiongezi wala kupunguza amani ndani ya ndoa. Kuna mifano hai ambayo nimeona japo siwezi zisema hapa. (6) Furaha ya ndoa hailetwi na pete ya ndoa. Kuna wanadoa wengi tu hawavai pete ya ndoa na wanapenda na furaha tele. Mfano hai ni Wasabato hatuamini kuwa pete ni sehemu muhimu ya ndoa. Hivyo kuvaa au kutokuvaa ni maamuzi yenu nyie wawili. (7) Kuvaa pete ya ndoa 24/7 doesn’t validate your marriage! Kuna watu wana vaa pete ya ndoa 24/7 lakini hata “kiss” tu hawapeani ?? ndoa za maigizo ??? (8) Jamani hata Yesu alifunga kwa siku arobaini na si mwaka mzima. Hivyo saa nyingine acha kidole kipumbue kidogo kha! (9) Thamani ya ndoa yako haitokani na pete bali inatokana na nyie wawili jinsi mnavyo heshimiana, thaminiana, na kupendana ndani ya nyumba na nje ya nyumba! (10) Adamu na Eva hawakuvaa pete ya ndoa ??